Mchanganuo wa Biashara (Business Plan) - REQUESTS

Mkuu Nashukuru sana kwa msaada wako hasa katika link ambayo umenipatia.
Hata mimi niko kwenye biashara ya mafuta ya alizeti, lakini ni kwa level ya uuzaji wa rejareja. tumekua tukichukua mafuta viwandani Dodoma kwa jumla kuanzia dumu 50 na kuyapaki upya kwenye vyombo vya lita moja na lita tano na kuyauza hapa mjini Dar.

lakini kila tukienda kuchukua mafuta nimekua nikitamani sana ku grow katika hii industry hata nikafikia hatua ya kumiliki kiwanda na kuanza kukamua mwenyewe kwani kule viwndani bei zao haziko stable.

Elimu yangu ni kidato cha sita sina uzoefu sana katika kuandaa na kuandika mchanganuo ndo maana nimejitokeza ili niweze kupata mwanga kwa ambao mna uzoefu juu ya maswala kama hayo. ili nijiandae kutafuta source of funds. -Ahsanteni
Habari mkuu unaweza kunipa ABC za hii biashara jinsi ulivyokuwa unafanya...na mm nitumbukie humo
 
Back
Top Bottom