STREET SMART
JF-Expert Member
- Feb 19, 2010
- 807
- 622
Soma hapa chini manabii wa ukweli !
..........(Nabii Ibrahim alimuonya Baba yake Mzazi aache kuabudu Masanamu, Baba yake akamfukuza. Ibrahim akaamua.........) Basi alipojitenga nao na yale waliyokuwa wakiyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, tulimpa Is-haq (Isaka) na Yaakub (Yakobo) na kila mmoja tukamfanya Nabii. Na tukawapa rehema zetu na tukawajaalia kupewa sifa za kweli na tukufu.
Na mtaje Mussa (Moses) katika kitabu (Quran). Hakika Yeye alikuwa ni mwenye kuchaguliwa, na alikuwa Mtume, Nabii. Na tulimwita upande wa kulia wa mlima (Sinai) na tukamsogeza kunong'ona naye.
Nasi kwa rehema zetu tukampa nduguye, Harun, awe Nabii.
Na mtaje katika Kitabu (Quran) Ismail. Bila shaka Yeye alikuwa wa ahadi, na alikuwa Mtume, Nabii. Na alikuwa akiamrisha watu wake sala na kutoa Zaka, na alikuwa mbele ya Mola wake Mwenye kuridhiwa.
Na mtaje katika Kitabu (Quran) Idris. Hakika yeye alikuwa Mkweli, Nabii. Na tulimuinua daraja ya juu.
Hao ndio aliowaneemesha Mwenyezi Mungu, miongoni mwa manabii katika uzao wa Adam, na katika uzao wa wale tuliowapandisha pamoja na Nuhu (katika Safina) na katika uzao wa Ibrahim na Israil na katika wale tuliowaongoa na tukawateuwa (watu wema). Wanaposomewa Aya za Mwingi wa Rehma huanguka kusujudu na kulia. Quran: Maryam:48-58.
Walio haribu dini ni hawa:
..........Lakini wakaja baada yao walio wabaya, wakaacha sala, na wakafuata matamanio (ya kilimwengu). Basi watakuja kupata malipo ya ubaya. Quran: Maryam: 59.
...........Hao Manabii (Mwingira, JKB, Ndege, Kakabe, Vernon, TB Joshua na wengineo), sie Waislaam tunawaona "ZE COMEDY"
Waswahili tuna msemo wetu " WAJINGA NDIO WALIWAO" waache wamchangie jamaa yuko smart anajua kuwa BRAIN WASH: siku hizi kuna MTUME FLORA kaibuka anali promote kanisa lake ktk magazeti ya shigongo anakula vichwa kama hana akili nzuri, kajichubua huyo yuko materialistic kinoma yani. waswahili husema " HAMJUI KUSOMA HATA PICHA HAMUELEWI. WAACHE WALIWE MKUU