Mch. Mhe. Dr. Getrude Lwakatare achunguzwe!

kama wamekosa watu wa kuwachukua na ndugu zao hawajaja na kusema walikufaje mnaaminije ni misukule?
 
soma 1Corithians 14 32-39. na maandiko hayo yanasema kama ifutavyo:
Kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu ni lazima kitawaliwe na huyo mwenye hicho kipaji. 33Maana Mungu si Mungu wa fujo, ila wa amani. 34Kama ilivyo desturi katika makanisa yote ya watu wa Mungu, wanawake wakae kimya katika mikutano ya waumini. Hawana ruhusa kusema; ila wawe watii kama isemavyo Sheria. 35Ikiwa wanayo maswali ya kuuliza, wawaulize waume zao nyumbani, maana ni aibu kwa mwanamke kusema katika mikutano ya waumini. 36Je, mnadhani neno la Mungu limetoka kwenu ninyi au kwamba limewajieni ninyi peke yenu? na biblia yenyewe inakataza tena kwa laana kwa mtu kupunguza au kuongeza neno. soma Revelation 22 18-19, pia Galatians 1 6-14
sasa je; mamlaka ya mwanamke kutangaza injili ya Bwana anayapata wapi?
 
Mkuu tusihamie kwenye gender bias as in who is best or more suited for the gospel between a man and a woman.
Hiyo si topic...Ofcourse nilikuwa nimeuliza swali.....JE MISUKULE NI WAFU?
 
Misukule ni wafu?
ndo maana nikasema utawaitaje misukule kabla ya kuwaona ndugu zao wadhihirishe kweli walikufa na walikufa je? kumbuka mpaka sasa hivi wako kanisani kisa ndugu zao hawajaonekana
 
Ochu, the Holy book is a complicated text, one needs to read between the lines otherwise you wil mutilate your whole body if you take every word as it is written.
 
mkuu mbona "umepiga" kote, sasa tukimbilie wapi? Kazi kweli kweli!

Huo ndio ukweli kaka, la muhimu tukisha jua ukweli, tunakaa humo humo kwenye makanisa yetu, hali ukijua kuna swala fulani personally hukubaliani nayo! Bible tells us tukiujua ukweli utatuweka huru.Kuna vitu vingi haviko sawa ukivijua hata siku kama kuna mtu anachokonoa imani yako, you just keep quiet, hakuna haja ya hasira,DINI HIZI ZINA WENYEWE. Our task ni kumwabudu Mungu, other politics ni kuwaachia wenyewe.

wapo mkuu, kasome vizuri biblia "yako"

Nisaidie ndugu, nimesoma bible cover t0 cover, sijakutana na hiyo cases.Cases zilizopo za wafu ni nyingi , ila sio misukule-Nipe kipande

Kuna swala la Yesu kuwa transfigureed mlimani, wale wanafunzi wakawaona Musa na Eliya.Kuna swala

Lipo la Lazaro, mtoto wa Binti yairo , na mtoto wa mwanamke mjane kufufuliwa but was not misukule

Kuna wafu walionekana na wakapotea at the time Yesu anafufuka!

Nasubiri ipande cha misukule, kindly weka pia kwenye PM yangu

Waberoya
 
Mkishanipa jibu kama misukule ni wafu ama la...Then tunaweza ku conclude....Kama ifuatavyo either way...
Kama misukule ni wafu...Then ushahidi unahitajika kwasababu mfu ni mfu na kabla ya kusema mtu amekufa ushahidi lazima uwepo(kiutaratibu wa kawaida) kuwa kweli binadamu huyo amekufa....Ni wakati wa kuwapa wananchi elimujamani ili haya mazingira ya ujima yaishe...Na tuikumbatie sayansi kama wenzetu..

Tunaishi karne ya kwanza(Karne aliyoishi Yesu)....Kwani wakati huo hata dawa hazikuwepo na watu ni umasikini na njaa na magonjwa huku mafarisayo na watoza kodi(mafisadi)wakila kuku na sadaka zao.

Dhehebu la wakristo limetekwa...Jesus christ was for the poor na sasa matajiri wameiteka dini na kui manipulate...Wananchi wapewe na elimu na UCHAWI UMALIZWE ONCE AND FOR ALL.

Kama misukule si wafu...Then wabadili usemi na waseme misukule ni watu waliohamishwa kiushirikina....

Ama iwekwe wazi kabisa kuwa kuchukuliwa msukule ni kufa...Kama thats not the case then usiwaaminishe watu kuwa eti wakifa utawafufua....Bali uwaambie kuwa ukichukuliwa msukule tutakurudisha.
 
Inakuwa hawajafa....Ila wanakuwa wamekufa msukule...Sasa hapo ndio utata ulipo...Kwamba wanakuwa wamekufa msukule lakini bado hawajafa(kisayansi?) Kwasababu inasemekana hata huko walipo bado wanakuja kufa kikweli kweli?!
Hapo ndio shida...Labda waseme tu kuwa wamewatoa huko porini baada ya kuhamishwa kichawi/kishirikina....Hapo ita make sense...Lakini madai kuwa wamekufa....Hapo kuna shida.

Nakubaliana na wew ekaka, SWALA NI KUWA WAKATI HAWA WATU 'WANAKUFA' MUNGU ALIKUWEPO NA ALIWAONA! HAKUWASAIDIA.LEO HII ANAKUJA BINADAMU MWINGINE ANAMWOMBA MUNGU 'WASIFE -WAFUFUKE' MUNGU HAJICHANGANYI KIIVYO, HAWAKUFA(Hapo sawa) na kama ni kweli she still have opportunity akawaombee wafu wote pale kinondoni wafufuke. wengine waliuawa, walibakwa n.k..

Waberoya
 
Nikisema ni "usanii" najua nitashambuliwa sana lakini nasema hivi: Yesu alifanya miujiza mingi km kufufua (Lazaro), kutembea juu ya maji, kuponya wagonjwa (ukoma, upofu), kulisha watu wengi (mikate 5 wakashiba watu 5,000), kutoa pepo na mingine mingi. Leo hii tunaona maigizo kama:
1. Uponyaji feki: Watu wanadai kuponesha viwete, vipofu nk, lakini sijawahi kushuhudia wala kusikia mtu anayefahamika kuwa kiwete wa polio ambaye sasa anatembea, au kiwete ambae sasa anaona kwa miujiza hii, ingawa wanatangaza kila kukicha. Hebu anayejua atutajie japo jina la mtu mmoja tu aliyekutana na miujiza hii. Wale walioandikwa kwenye biblia walijulikana kabisa kwa majina na wanakotoka. Nawachagiza wanaoshabikia haya mambo ya miujiza ya kina Lwakatare na wengine kama hawa, waje hapa na majina halisi na anwani (au angalao taja anakaa wapi au ilitokea wapi) ya watu waliopata miujiza hii.
2.Kunena kwa lugha "feki" kama "ooooh rrroboshankaraktsika rraboshhhh". Lugha zilizonenwa katika biblia zilieleweka kwa waliosikia, kwani walizisikia katika lugha zao wenyewe tofautitofauti. Mbona hii "ooooh rrrobosshhhh" haieleweki ni kitu gani?
3. Kufufua "misukule" feki. Hii ni tofauti sana na Yesu ambaye alimfufua Lazaro "live" kutoka kaburini, mtu aliyejulikana kabisa.

Na mengine mengi ya ajabu. Sasa hii "miujiza" kweli ni ya Mungu au ndiyo ibilisi mwenyewe?

Naunga mkono kuwa huyo Mch Lwakatare na wenzie wa namna hiyo wachunguzwe, tutajua zaidi.
 
Uchunguzi uliofanywa na waandishi wetu katika kanisa hilo, unaonyesha kuwa kati ya watu hao Misukule nane waliopatikana katika misitu hiyo baada ya waliowachukua kimazingira kumrudia Mungu, watano wameshachukuliwa na ndugu zao ambapo watatu bado wanaendelea kutunzwa na kusali katika kanisa hilo, hali iliyowafanya baadhi ya waunimi kusema kuwa ndugu zao watakuwa wamewasusa.

Baadhi ya waumini waliozungumza na waandishi wetu kwa sharti la kutoandikwa majina yao gazetini kwa kuwa si wasemaji wa kanisa, walidai kuwa wanaamini kwamba vijana hao watatu ambao ndugu zao hawajajitokeza licha ya habari zao kutangazwa katika vyombo mbalimbali vya habari, inawafanya waamini kuwa jamaa zao bado wana imani kuwa wamekwisha fariki dunia.
1217917692_mfuhai2eweb.gif

Hata hivyo, uchunguzi unaonesha kuwa baadhi ya waumini walikuwa na mawazo tofauti kwa kusema kwamba uwenda ndugu zao hawajapata taarifa kuhusiana na vijana wao kwa kuwa wengi walipoteza kumbukumbu na endapo wangepatiwa taarifa wangeweza kujitokeza.

Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu jana, Mchungaji Lwakatare alikiri kuendelea kuwa na misukule hao katika kanisa lake.

“Hata kama ndugu zao watawasusa nitaendelea kuwalea na baadaye wakiwa na akili safi nitawapa ajira,” alisema mchungaji huyo.
1217917692_msukuleweb.gif

Akifafanua zaidi, Mchungaji Lwakatare alisema kuwa watu hao wengi wao awali walikuwa wamepoteza kumbukumbu kabisa lakini sasa wana afadhali kwa kuwa wanaanza kuelewa mambo.

Hivi karibuni gazeti hili na vyombo vingine vya habari viliripoti kukamatwa kwa misukule katika Kanisa la Mikocheni B Assemblies of God na kusababisha wasomaji wetu wengi kutaka kujua kinachoendelea, hivyo kuanzisha uchunguzi kujua kama bado wapo au la.
1219302231_jenifaweb00.jpg

My Take:
Kanisa la huyu mama naamini linaeneza one of the most elaborated scheme of deception a.k.a a hoax! Inanikumbusha kisa cha Mchungaji Gilbert Deya wa Uingereza (raia wa Kenya) ambaye alikuwa amedai yeye na mke wake kuwa wanauwezo wa kuombea wa kina mama na wakapata mimba na kuzaa watoto hata kama kina mama hao walishapita uwezo wao wa kuzaa n.k

Ingawa mwanzoni mambo hayo yaliweza kuonekana ni miujiza, utaalamu wa kisayansi ulionesha kuwa mke wa mchungaji huyo na washirika wao kule Kenya walikuwa wananunua watoto wadogo na kuwapa kina mama wengine na kwa kufanya hivyo kufanya biashara ya watoto lakini wakati huo huo kulifanya kanisa la Mchungaji huyo kukua zaidi na kuwa na ujiko usio kifani kutokana na kazi ya "Mchungaji huyo".

Mwishoni, sheria ikakutana naye, mke wake akaswekwa jela na yeye mwenyewe mchungaji kutakiwa kurudishwa Kenya kukabiliana na mashtaka ya usafirishaji haramu wa watoto.

Naamini, kama kuna mtu ana ujasiri wa kuchunguza hii "misukule" na kanisa hilo kutaonekana pasipo shaka jinsi gani this hoax was propagated and carried out na hivyo kumpa mama Lwakatare ujiko na kumuongezea sadaka.Natoa hoja, kanisa lake na yeye mwenyewe achunguzwe pamoja na hao "misukule" kwani anachezea imani za watu na hasa hofu yao ya mambo ya kishirikina.

Kwa vile tuna utaalamu wa DNA, basi misukule hao na "familia" zao na hata makaburi wanayodaiwa kuzikwa yachunguzwe ili wananchi wetu wasitekwe na ulaghai wa kidini unaoendeshwa kwa jina la dini.

Endapo uchunguzi wa kisayansi utaonesha kuwa kweli hawa watu walikufa, wakazikwa na baadaye kukutwa porini wakiwa wamechukuliwa misukule nitamwomba radhi; Lakini nasimamia kusema this is a HOAX inayofanywa na Mbunge Mchungaji!

Mwanakijiji nashukuru kwa thread hii yenye changamoto

Hata hivyo ninapata shida sana na mtizamo wako ktk hili la misukule Mikocheni B Assemblies of God.

Umeonesha msismamo wako kuwa unaamini anachofanya Mch.Lwakatare ni uongo (deception/hoax).Hilo umelionesha bila wasiwasi wowote.

Hata hivyo umeshauri kuwa uchunguzi ufanywe na mwenye ujasiri lakini kabla ya kusubiri uchunguzi wenyewe tayari umeshatoa matokeo ya uchunguzi kwa kusema kuwa ndipo "...kutaonekana pasipo shaka jinsi gani this hoax was propagated and carried out na hivyo kumpa mama Lwakatare ujiko na kumuongezea sadaka".

Naamini kuwa suala uliloliwaslisha hapa jukwaani ni critical kwa kuwa linagusa zaidi imani ambayo kwayo kila mwanajamii anajipambanua kivyake.Kwa mantiki hii nilitarajia wewe uweke jukwaani mawazo dadisi na kutoa mtizamo usiokuwa na hitimisho linalohitilafiana na nia shabaha nzuri uliyokuwa nayo.

Kama mawazo yako yangekuwa kupendekeza uchunguzi juu ya hili suala la misukule ingekuwa vizuri kwa wewe kutokutoa msimamo wako ambao unajitanabaisha kuwa matokeo ya uchunguzi ulioupendekeza.

Je kama ikigundulika kuwa matendo ya kanisani kwa Mch.Lwakatare siyo uongo kama ulivyouita msimamo utabaki kama ulivyo au?.
Pengine Mwanakijiji hukuwa unashauri uchunguzi bali matokeo ya uchunguzi ambayo unayafahamu tayari?
 
Ni dini hizi hizi zilizowagawanya waafrika kama watumwa makahaba.
Kwasababu si ndio dini hiyo hiyo wazungu waliyoitumia kuwaweka utumwani waafrika na hata kuendelea kuwabaguwa hata sasa?
Kama Ochu analeta ubaguzi wa kijinsia kama inavyoonekana kuwa biblia inaruhusu...Then kwanini wakristo hao hao kina Palin bado wanakuwa kama hawawependi watu weusi?
Ama kwanini dunia hii igawanywe kwa misingi ya imani za kidini?
Kwanini hatuoni jinsi dini imekuwa ikitumika vibaya karne baada ya karne?
Na mwarabu na yeye si anakubaliana na agano la kale?
Na mwarabu huyo huyo na yeye si ndiye aliuza mwafrika kwa mzungu?
Waafrika tuwe makini sana...Na inasikitisha sana kuona mijitu ikipigania maslahi ya kidini kwenye issue za Taifa lenye kila aina ya wananchi wa makabila na dini tofauti.
 
Ukianza kufikiria sayansi za kiafrica wakuu zinaumiza kichwa sana kwa maana hakuna scientific test mtu anaweza akafanya na tukashuhudia.....yaani zinachanganya sana...
Hao wenyewe walio rudi kundini na kuamua kuokoka ukimuuliza au ukimwomba afanye experiment ya kuchukua watu na kuwa msukule sijui kama atakubali..zaidi zaidi atakwambia mimi saizi nimemwangukia Mungu.Lakini alipo kuwa anajulikana mchawi ukimfaata adhihilishe lazima atakataa kuwa mimi si mchawi yaani hizi sayansi za kiafrica ni kama za kusadikika tu.

Na swala la imani nalo linachanganya sana watu yaani nguvu ya Mungu...utasikia mtu anaponya wagonjwa vilema wanatembea,maneno chungu nzima lakini ukimpeleka mgonjwa wako unakuta ziiiiiiiii nimeshuhudia kuna mchungaji kasema anaponya vipofu na vilema hawa walienda kwa wakati mmoja nipo karibu nao lakini jamaa alichemka kuwaponya na kuishia kusema hawana imani....
Turudi kwenye biblia ni wapi panapo onyesha Yesu alichemka kumponya mtu au kufanya muujiza wowote ule?Utakuta hakuna .

Mwisho ndugu zangu dini sasa hivi imegeuka kuwa dili watu wanafanya biashara kupitia dini sadaka sadaka tunazo changa pamoja na mafungu ya 10 ni neema kwa watu flani flani kanisani....Unaambiwa biashara inayo lipa sasa hivi ni kanisa na shule.....ni wewe tu kujitangaza kwa kutumia mbinu mbali mbali....Mnaona lile kanisa la pale Ubungo juu ya mitambo ya Richmondo na dowans linavyo sheheni watu?Jamaa alianza gia ya misukule hii hii kama ya Mama mheshimiwa akaja gia ya kumwona Amina Chifupa Kibaha akasema anauwezo wa kumrudisha lakini kimyaaaaaaaaaaaaaaaa mpaka leo kachemka na sasa anavuna kondoo balaa pita juma pili magari yamejaa hadi packing inakuwa ndogo watu wanafulika balaa na jamaa anaunga unga ujenzi kulipanua kanisa limekuwa dogo....baadae ataanzisha nae Television yake na kujenga kanisa kubwaa kuliko lile....Kanisa linalipa.
 
Poor Tanzanians! Kwa imani hii ya kufufua waliochukuliwa misukule, tunathibitisha kwa mara nyingine kuwa tunakaribiana zaidi na nyani hayawani kuliko binadamu wa kawaida.
 
Tatizo wananchi wengi hawana kazi,elimu na ni wajinga.
Ni kama Obama alivyowaambia huko PA...Kuwa wana cling on something kwasababu life is tough.
Wananchi hao wakiwa na kazi basi jamii zinakuja pamoja na kufanya shughuli za kimaendeleo za kuutokomeza uamsikini,Ujinga na Maradhi..Lakini serikali inayategemea makanisa na misikiti ili wananchi waendelee kuwa kama mkoloni alivyokuwa akitaka(ufahamu mdogo)...Tatizo mkoloni wetu sasa ni FISADI MWENYEWE.
 
cha kushangaza wazungu ndio walituletea dini zao wakatuachia wao hawana tena muda nazo.na wao hawakuwahi kufufua wafu
 
Nikisema ni "usanii" najua nitashambuliwa sana lakini nasema hivi: Yesu alifanya miujiza mingi km kufufua (Lazaro), kutembea juu ya maji, kuponya wagonjwa (ukoma, upofu), kulisha watu wengi (mikate 5 wakashiba watu 5,000), kutoa pepo na mingine mingi. Leo hii tunaona maigizo kama:1. Uponyaji feki: Watu wanadai kuponesha viwete, vipofu nk, lakini sijawahi kushuhudia wala kusikia mtu anayefahamika kuwa kiwete wa polio ambaye sasa anatembea, au kiwete ambae sasa anaona kwa miujiza hii, ingawa wanatangaza kila kukicha. Hebu anayejua atutajie japo jina la mtu mmoja tu aliyekutana na miujiza hii. Wale walioandikwa kwenye biblia walijulikana kabisa kwa majina na wanakotoka. Nawachagiza wanaoshabikia haya mambo ya miujiza ya kina Lwakatare na wengine kama hawa, waje hapa na majina halisi na anwani (au angalao taja anakaa wapi au ilitokea wapi) ya watu waliopata miujiza hii.2.Kunena kwa lugha "feki" kama "ooooh rrroboshankaraktsika rraboshhhh". Lugha zilizonenwa katika biblia zilieleweka kwa waliosikia, kwani walizisikia katika lugha zao wenyewe tofautitofauti. Mbona hii "ooooh rrrobosshhhh" haieleweki ni kitu gani?
3. Kufufua "misukule" feki. Hii ni tofauti sana na Yesu ambaye alimfufua Lazaro "live" kutoka kaburini, mtu aliyejulikana kabisa.

Na mengine mengi ya ajabu. Sasa hii "miujiza" kweli ni ya Mungu au ndiyo ibilisi mwenyewe?

Naunga mkono kuwa huyo Mch Lwakatare na wenzie wa namna hiyo wachunguzwe, tutajua zaidi.

Nadhani Kithuku hautendi haki kwa Imani ya watu,

Wapo walioshuhusia miujiza na wangali wanashuhudia kila uchwao.Nafikiri suala hapa la msingi lazima lieleweke kuwa Yesu hajaacha kuponya, kuokoa.Bado Mungu anafanya kazi kama ilivyokuwa wakati wa agano la kale.Leo hayupo Mussa, Elia,Petro Wala Yesu haishi katika hali ya uanadamu lakini kazi zake zinatekelezwa na yye kupitia manabii, mitume na watumishi wengine.

Shida ni kwamba siyo kila mtu anaamini hayo na sababu yaweza kuwa moja au zaidi .Yawezekana mtu akawa haamini kwa kuwa hataki kuamini, yawezekana pia mtu asiamini kwa kuwa amewahi kukutana na watu wanaotumia dini kujipatia mradi wao wa kila siku.Hata kama wapo wanaotumia dini kujinufaisha na kuwahadaa wengine haitupi kibali cha kumwona kila aliitaye jina la Yesu kuwa ni mwongo.

Tuzipime roho na wala siyo kuzihukumu kwanza.Hili siyo jambo rahisi Kithuku, lahitaji uvumilivi na umakini wa kiroho.
 
Tujaribishe Taifa la kisayansi na tusibakie tu kwenye mambo yasiyoonekana...Hayo ni mambo ya kiimani.
Tunapokuja kwenye issue ambayo inawagusa wananchi walio wengi na kuimpact maisha yao na ufahamu na fikra zo..Basi ni muhimu kuitupia macho jamii yetu.
 
Hapa ieleweke misukule wanakuwa hawajafa kifo cha kawaida ila wanachukuliwa kimazingara kichawi!yaani wengine mnaona kabisa kuwa wamekufa ila inakuwa hawajafa bali wanachukuliwa!kwa taarifa yenu hata huko wanapokuwa kwa wachawi huwa kuna kipindi wanakufa kile kifo cha kawaida!

Sasa waliokuwa wamekufa na kuzikwa mwanzoni ni kina nani?
 
Back
Top Bottom