Mch. Mhe. Dr. Getrude Lwakatare achunguzwe!

Huyo mama ana historia ndefu ya utapeli. Kwanini mambo yote ya uchawi yanatokea kwake??Yule mtoto aliyekata kichwa alianzia kwake. Wako wato wanayoponya lakini hawajitangazi kama huyo mama.Anafanya mambo mengi mazuri laini pia na mabaya ameyafanya mengi.Kakusanya vitoto vya yatima vingi zaidi ya 700 lakini ameshindwa kuvilisha vimekondeana kama nini.Anahubiri kuhusu ndoa yeye yalimshinda miaka mingi iliyopita na isitoshe anaishi na mwanamke mwenzake!!!Hiyo misukule ameitengeneza mwenyewe anataka kuvutia watu waende kutoa sadaka akanunuwe dhahabu.
 
Jamani mweee!...
Uchawi upo na umeonekana toka enzi na enzi hivyo imani ya dini moja kati ya therapy ambazo zimewapa ponya watu wengi kiakili..
Binafsi huyu Mama hata kama ni zuga anachokifanya kinastahiri sifa kwa sababu hakuna kati yenu anayeweza kuwachukua watu hao na kuwapa hifadhi..
Kama binadamu hawa jamaa wanahitaji hifadhi na hakuna ushahidi wa kwamba wanakuwa abused isipokuwa kutendewa mema mbali na kuongozwa ktk imani ya dini...It's somekind of therapy kwao...
Iwe miujiza ya Mungu ama sababu ya kupata nafuu ni malezi mazuri ktk mazingira huru yote haya yanalenga kuwarudisha watu hawa katika uzima wa afya zaidi ya roho..
Kinachowaudhi wengi humu ni kufikiria tu kwamba lengo la Mama Lwakatare ni kueneza imani ya dini yake wakati sote humu tunaelewa wazi kwamba hawa jamaa ni vichaa kama sio wendawazimu... Sasa sijui hiyo dini ataweza vipi kuwafundisha wendawazimu wakaifuata...
My two cents kama wewe unaumwa sana kuona jinsi mama huyu anavyotumia nafsi yake basi volunteer kumchukua hata mmoja kati ya hao vijana..

Mkandara, kwanini unafikiri hawa watu wana magonjwa ya akili na hivyo wanahitaji msaada? Magonjwa ya akili yanahitaji tiba hospitalini au ushauri nasaha n.k lakini cha kwanza ni lazima wataalamu wa magonjwa ya akili wathibitishe kwanza kuwa ni wagonjwa wa akili au ugonjwa mwingine wowote ule.
 
mama yake au dada yake, au mtoto wa ndugu yake n.k? mbona umeshtuka hivyo?

Kuishi na mama yake, au ndugu yake ambaye ni mwanamke mwenzake siyo habari ya kuandika. Ni kama katika taaluma ya uandishi ya habari, mbwa akimuuma binadamu, siyo habari ya kuandika na kuuza gazeti, ila binadamu akimuuma mbwa ni habari ya kuandika na kuuza gazeti. Nadhani umenielewa!

Swali langu linarudi pale pale, na ninaomba nimnukuu mtu niliyemuuliza swali. Amesema..."anahubiri kuhusu ndoa wakati ndoa yake yeye imemshinda, anaishi na mwanamke mwenzake".

Kwa upana wa uelewa wako wa ulimwengu wa kisasa katika mahusiano ya jamii Mwanakijiji lazima utakuwa umeelewa maana ya nukuu hiyo hapo juu!!!
 
Kama nimekosea naomba nirekebishwe....Ila navyoelewa ni kuwa kabla ya kusema mtu alichukuliwa msukule ni lazima kuwe na ushahidi kuwa watu ama mtu huyo alikufa.

Kwa maana kwamba kuwe na udhibitisho wa aina flani kuwa ni kweli watu hao walikufa kwasababu maana halisi ya msukule ni kuwa mwili wako unaonekana kuwa umekufa na unazikwa kabisa mbele za kila mtu ila inasemekana kinachozikwa hapo ni gogo...Sasa kwanini hayo makaburi waliyosema walizikwa hayafukuliwi?

kwani hata serikali yenyewe si ina rekodi za watu waliokufa na ni nini kilichowasibu?

Sasa ni kwenda kwenye makaburi ambayo walizikwa awali na DNA ichukuliwe na ilinganishwe na hao waliokutwa huko msituni.

Inawezekana pia hao ndugu wengine waliwapoteza hao ndugu zao na kuamuwa kuwa inawezekana wamekufa na wakaamuwa kuripoti hivyo na kuvunja matanga kumbe kwasababu ya matatizo ya akili ndugu zao hao wako porini....Hilo linawezekana na zamani ilikuwa popular watu kufanya matanga mara baada ya ndugu kutoonekana kwa muda mrefu...Na kwa jinsi ambavyo jamii zetu at least baadhi zinavyoishi kwenye ujima...This is quite possile...Ya Maalbino si tunaona?

Utajiri tunao badala ya sayansi tumebakia kwenye imani potofu tuuu!

Miujiza ipo...Ila kwenye this particular one tunaweza kufanya uchunguzi wa kisayansi ili kuwawezesha wananchi kupata habari za pande zote kwa manufaa yao na uelewa wao na kwa manufaa ya jamii nzima kwenye karne hii mpya ya sayansi na teke lililokwisha tutandika kiaina...

NB:Kwenye suala la mwanamke...Hapo bado sijaweza kujuwa lipi ni lipi kwani FMES naye amesema kuna habari za kiongozi wa ccm....
 
Aliwahi kutokea mtu moja huko Kenya akaanzisha kanisa lake na kujitangaza kuwa ni Yesu amerudi kwa mara ya pili duniani kama mtu mweusi. Huyu mtu alikuwa na mvuto mkubwa na aliweza kuteka mioyo ya waumini wake kiasi cha kuwa hakuna aliyethubutu kutilia shaka yote aliyohubiri. Miongoni mwa waumini wake walikuwepo watu wa aina zote - wake kwa waume, wasomi waliobobea, vigogo waliokuwa na madaraka makubwa kama mawaziri nk.

Alipoanza kuumwa ilielezwa kuwa shetani alikuwa kazini na kama ilivyotabiriwa huyo shetani angeshindwa. Pamoja na kuwa hali yake lizidi kudhoofika, waumini walimzunguka wakimtukuza Mungu na kutotaka kabisa kumpeleka hospitali. Waliamini kuwa lazima apitie kifo na kukishinda kwa kufufuka siku ya tatu kama njia ya kuwaokoa watu weusi.

Siku alipokata roho waumini wote walikusanyika na kufunga wakisali na kumtukuza Muumba - hakuna aliyetaka kuondoka asije akakosa kushuhudia ufufuko. Siku ya tatu pamoja na njaa na uchovu wa kukesha bila kulala, bado walisubiri kwa hamu licha ya harufu kali iliyoanza kutanda kila kona. Maprofesa, madaktari, wanasheria nk walikuwa na imani kuwa bado tu mwokozi wao angefufuka.

Ilibidi serikali ya Kenya iingilie kati hali ilipoanza kuwa mbaya na harufu kutanda kijiji kizima na tishio la kulipuka kwa magonjwa ya kuambukiza. Marehemu alizikwa chini ya usimamizi wa GSU na huo ndio ulikuwa mwisha wa kanisa hilo.

My take: Imani potofu jeuri - haichagui na isipothibitiwa mapema yaweza leta maafa.
 
.........lazima miujiza ichunguzwe ...tena ikidhibitika ni kweli hamuoni kuwa itampa heshimna zaidi muhubiri husika????...kuna ugumu gani wa kupokea shuhuda za waliohudhuria msiba wa msukule husika,waliomuuguza na kumtunza na kumtibu, majirani, marafiki, kuoneshwa kaburi[siku hizi kuna hadi picha za msiba], kuoneshwa cheti cha kifo,watoto,wake zao au waume.............

Nadhani wote hao hawaweezin kudanganya........wakristo tunaamini kwenye uponyaji...na ponyaji lazima ziwe na shuhuda zisizokuwa na mashaka..ili huudhihirishia ulimwengu na wasioamini.....

....watu wa Mungu ni wengi wanapita humu..kuliko kumlaumu tu mama ..bora mchakato wa kuchunguza miujiza yake ufanyike wazi...naye aaufurahie...

siku hizi makanisa ya miujiza yameshamiri mengi..eti watu wanataka kuona miujiza ..basi ,ndio waamini...watu wanakosa imani hadi uoneshe miujiza...tunapotea!!..nashauri haya makanisa yaunde chombo huru cha kudhibitisha miujiza inayotendeka ,ili taifa la Mungu lisijekuwaamini ...wanaoponya kwa jina lake ..kumbe na mawakala wa lusifah!!!!
 
Nahisi hapa tunataka kuchanganya dini na sayansi,imani na facts.Hivi kwa Wakristo tunaposoma kwamba Yesu aliponya wagonjwa,do we need any proof?Au resurrection yake,tuna ushahidi wowote?As I Christian myself,I dont even have time to question that kwa vile kufanya hivyo,kwa mujibu wa imani yangu,ni sawa na kutenda dhambi.Naelewa kwa mtizamo usio wa kidini hiyo ni sawa na blind followship,lakini hiyo ndio dini.

Iwe Lwakatware,Kakobe au yeyote yule anayetangaza miujiza kama ya Yesu,kuamini au kutoamini inategemea mtizamo wako kuhusu masuala ya imani.Je kwa wanaoamini miujiza ya Yesu haiwezekani kwa mtumishi wake kuwaibua misukule?Jibu ni NDIO INAWEZEKANA.I am in no way whatsoever suggesting kuwa kila mtu amiini kwani nafahamu kila mtu ana uhuru wa kuamini au kutoamini kutegemea na mtazamo wake.

Kama hayo ya Lwakatware kutoa misukule ni incomprehensible vipi kuhusu alofanya Mwakasege in his recent US tour?
 
As a nation, kwa kweli hatupaswi kuwa na this kind of debate nationally.

FMES,

Heshima yako natanguliza.

Swali: If the woman in question is a member of the National Assemmbly,
then why shouldn't this be a 'national' debate?

....To Whom Much Is Given, Much Is Required.
 
Linapokuja swala la fedha, sadaka, na kujitengenezea empire ya biashara tusichukulie jambo lolote kwa urahisi. Tumeyaona hapa US ya kina Jimmy Swaggart, na kina Poppoff; Tumeyaona ya kina Deya kama nilivyotolea mfano. Itakuwa ni makosa makubwa kwa akili zetu tukisema ati kwa vile mtu anasema "anatenda miujiza" basi tukubali tu na tusihoji.

Tutakuwa tunafanya makosa makubwa kabisa tukikubali madai ya kidini kwa vile ni ya kidini bila kuangalia athari zake.

a. Kama kuna kikundi cha watu (bila Rev. Lwakatare kujua) wameamua kuigiza, kujificha vichakani na wengine kwenda kudai kuwa wameona misukule wakiwa na lengo la kujipatia maisha ya bure nani atajua?

b. Kama mama Lwakatare mwenyewe katika haja ya kuongeza waumini, sadaka na ujiko kwa shughuli zake za biashara ameamua kufanya hoax hii akijua kwamba Watanzania wataamini bila kuhoji, na kwa kweli watu wanaanza kuamini kutoa sadaka zaidi na kupeleka watoto wao kwenye shule za mama huyo kwa sababu hiyo, je haionekani hii ni kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu?

c. Kama watu hawa kweli walikuwa ni misukule na sasa wanaishi; sayansi itafaidika katika kufahamu kilichozikwa ni nini basi na kwa vile aliyechukua misukule amejitangaza wazi basi atakuwa msaada wa kuonesha jinsi/madawa aliyotumia kufanya hivyo. Yawezekana yakawa na application nyingine kubwa sana kama vile kwenye mambo ya upasuaji n.k Je tusichunguze mambo haya ili kujiridhisha?

d. Kama watu hawa siyo waliokufa (yaani miili bado iko kaburini) hawa misule ni kina nani? Yawezekana ni watu waliokuwa wanahsikiliwa kinyume cha sheria na kutumikishwa kama watumwa?
 
yale yale ya akina Kimbwotere........DR Mchungaji Mbunge Mrs Lwakatare

.......nina ombi moja tupitie biblia kikamilifu ili twende kwenye mstari ulionyooka bila hivyo siku 7-8 zijazo itakuwa hatari hapa......
 

..........kanisa katoliki kinaamini kuwa miujiza yote ni lazima ichunguzwe kabla ya kutangazwa kikanisa......!!!..kwa utaratibu huo kwenye kanisa katoliki mtumishi au muumini yeyote akifanya miujiza hatakiwi kuanza kujitangaza hadi ...uchunguzi na maombi ufanyike kubaini kama uponyaji au miujiza umetokaana na jina la bwana yesu au tofauti!!!..na ikiweza kudhibitika kuwa mtu ana nguvu hizo basi huwekwa kwenye kundi la watakatifu....

makanisa mengi yanaibuka siku hizi ie mtume na nabii mwingira,askofu mkuu kakobe na wengine.......wanafanya kazi nzuri ..lakini kinachonitia hofu ni kuwa wengi kati ya hawa..hawapendi MASWALI KWENYE MIUJIZA WANAYOTENDA ...WALA HAWATAKI UCHUNGUZI....!!!

LAKINI BADO NAAMINI umuhimui wa nadharia ya kanisa katoliki na makanisa mengine ya asili kama orthodox ,lutheran etc .....kwenye "kusikiliza kwa makini sauti"...kwani hata shetani anaweza kuiga sauti ya Mungu!!


Katika hiyo miujiza ambayo wakatoliki huwa wanachunguza na kutangaza ni ipi? sijawahi kusikia miujiza katoliki , kama una mifano toa mkuu!??

Waberoya
 
Ya kaisari mpeni kaisari na ya MUNGU muachieni MUNGU!miujiza haijaanza leo toka kabla ya YESU ilikuwepo na Enzi za YESU ikawepo na itaendelea kuwepo!MKJJ hulazimishwi kuamini!Kwanza YESU mwenyewe alisema watu watafanya miujiza kuliko hata aliyofanya yeye!hapa ni IMANI tu!hakuna jipya alilofanya mtumishi wa MUNGU kwanza yeye hajafufua!ila hao misukule hawakufa kifo cha kawaida!kama YESU aliweza kumfufua Lazaro tena aliyekufa kiukweli!leo watumishi wake washindwe kuibua misukule!Kwa MUNGU yote yewezekana!
 
Kama tunadhibiti vyama vya siasa na NGOs, kwanini tusidhibiti shughuli za kikanisa? Je, leo hayo makanisa wakisema wanajikusanya na kuandamana hadi IKULU kudaiwa pesa ya EPA watanyamaza?
 
Linapokuja swala la fedha, sadaka, na kujitengenezea empire ya biashara tusichukulie jambo lolote kwa urahisi. Tumeyaona hapa US ya kina Jimmy Swaggart, na kina Poppoff; Tumeyaona ya kina Deya kama nilivyotolea mfano. Itakuwa ni makosa makubwa kwa akili zetu tukisema ati kwa vile mtu anasema "anatenda miujiza" basi tukubali tu na tusihoji.

Tutakuwa tunafanya makosa makubwa kabisa tukikubali madai ya kidini kwa vile ni ya kidini bila kuangalia athari zake.

a. Kama kuna kikundi cha watu (bila Rev. Lwakatare kujua) wameamua kuigiza, kujificha vichakani na wengine kwenda kudai kuwa wameona misukule wakiwa na lengo la kujipatia maisha ya bure nani atajua?

b. Kama mama Lwakatare mwenyewe katika haja ya kuongeza waumini, sadaka na ujiko kwa shughuli zake za biashara ameamua kufanya hoax hii akijua kwamba Watanzania wataamini bila kuhoji, na kwa kweli watu wanaanza kuamini kutoa sadaka zaidi na kupeleka watoto wao kwenye shule za mama huyo kwa sababu hiyo, je haionekani hii ni kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu?

c. Kama watu hawa kweli walikuwa ni misukule na sasa wanaishi; sayansi itafaidika katika kufahamu kilichozikwa ni nini basi na kwa vile aliyechukua misukule amejitangaza wazi basi atakuwa msaada wa kuonesha jinsi/madawa aliyotumia kufanya hivyo. Yawezekana yakawa na application nyingine kubwa sana kama vile kwenye mambo ya upasuaji n.k Je tusichunguze mambo haya ili kujiridhisha?

d. Kama watu hawa siyo waliokufa (yaani miili bado iko kaburini) hawa misule ni kina nani? Yawezekana ni watu waliokuwa wanahsikiliwa kinyume cha sheria na kutumikishwa kama watumwa?

Mbona kuna misukule wengine wameshachukuliwa na ndugu zao?
 
Hivi hizo habari za misukule zinaenezwa na Lwakatarwe mwenyewe au media?Okay,tunafahamu udhaifu wa journalists wetu ambao wengi hujua kuandika tu wanachosikia au kuona pasipo kwenda mbali zaidi kutafuta background au aftermath.Lakini kwanini tusifanye kwamba hadithi za misukule ni kweli hadi hapo zitakapokuwa proven wrong?

Pengine pazuri pa kuanzia,for you doubters,ni je hakuna miujiza inayotokea katika Kanisa la huyo mama,apart from hiyo ishu ya misukule?
 
Back
Top Bottom