Mbutananga: a sad story to tell kimahusiano

Nakadori

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
8,781
20,946
Waungwana salamu kwanza kama ilivyo desturi yetu.

Hii week kwangu ilikuwa hectic kidogo lakini pia nilipata nafasi ya kusafiri hadi kanda ya ziwa ndani ndani huko na kukutana na watu wapya hivyo kupata uzoefu mpya, wabheja sana wanawane.

Haya nirudi kwenye mada sasa. Mwanamama anamiliki vitu muhimu mambele huko (UK) na hapa Tanzania ana maduka yake kati kati hapo jijini na kweli ingekuwa bongo angeweza kulala atakapo na kula atakacho. Kwa kuongezea tu ni kwamba akawa hana mume wala mtoto.

Sasa mwanamama huyu anayekaribia kugonga miaka 50 amejikuta baada ya mahusiano yake na mzungu kuangukia pua miaka mingi iliyopita anatamani tena kuitwa mke wa mtu.

Katika pita pita za mitandaoni msukuma mmoja wa huko Swekeni mwanza akajaribu bahati yake wakawa wapenzi na bimama huyu kuonesha yeye ni lover mama bakajenga nyumba ya kisasa usukumani mwanza. Mahusiano japo yalikuwa ya muda mfupi lakini kijana bila kupepesa macho akajiongeza kwa kumuahidi bi dada ndoa kwa muda mfupi waliofahamiana.

Kwakuwa mwanamama huyu ndoa ilikuwa ndo tamanio lake na wanaume kadhaa walishamuahidi ndoa wakaingia mitini na hela ya pete akiwemo msanii maarufu wa bongo movie mlela, basi hakujiuliza mara mbili akaipokea hii ndoa kwa mikono miwili.

Bila hiyana taratibu za utambulisho hadi ndoa zikafwatwa mama akawa tayari amekuwa Mr and Mrs. Na ndoto sasa ikawa imetimia (hivyo akawa ana mali zake, ana mume bado mtoto).

Maisha ya ndoa yakaanza. Kiijana akawa ashapewa access ya mali za bi mama, kijana akaanza kung'aa, kijana akawa mtu katika watu. Baada ya muda na yeye akapaa UK kwenda kuuungana na mkewe halali kuendeleza maisha ya ndoa.

Maisha ya UK hayakuwa matamu sana kwakuwa kijana alifwata yake UK na sio ndoa, mara polisi, mara kuibiana mali kuhamishia kwake, mara vipigo kwa mke na kumbuka hapo kijana anamiliki p...umbu tu ila analishwa analala pazuri na entertainment anapata kutoka kwa mke.

Kijana hakuacha kufukuzia wanawake wa ndoto zake na mara kibao alikuwa bila aibu anawapost IG. Kwa maana nyingine fedha za mama wa UK zilitumika kugharamia mademu wa mwanaume a.k.a msukuma King Ngwesa.

Baada ya uvumilivu usio na Tija bi dada akayamwaga manyanga na kuamua kwamba "no matter how sweet or bitter it is ...it has to end here..." ndoa ikaisha kama ilivyoanza.
Maswala mengine yaliyobaki kama hayo ya kuibiana ni ya kisheria.

Sasa nachojiuliza ni kwamba yes unataka ndoa, ni lazima utafute Mario? Mbona wapo wazee watu wazima ambao angeweza kuoana nao na maisha yakawa matamu. Ilikuwa lazima awe na huyu opportunist?

Ameharibu cash flow yake kwa kuingiza mzigo kwenye maisha yake Ambao umemgharimu muda fedha na hisia. Kibiashara angekuwa mbali sana kama asingehangaika na huyu ngosha gold digger kutoka mwanza mallya...

Wanawake tuepukeni wanaume wa kulea a.k.a Mario. He can't provide back him off. Hakuna huruma. Msiendekeze genye, ohoo!

I see ngoja niishie hapa. Siko poa nimechoka sana. Bata la bariadi halikuwa poa.

Jamani wale wa matusi hala hala mje na mapya. Lile tusi lenu la kuniita mala....ya nshalizoea. Do the needful.

download (21).jpeg
download (20).jpeg

Hizi picha ni mbutananga na mumewe
 
Shida wanaume ambao hawana hela wanajua KUIGIZA kupenda. Yaani wakiona mwanamke ana hela wataonesha mahaba yote. Usipokuwa makini unazama mzima mzima.

Kwahiyo simshangai sana ila nimemuonea huruma.

Uzuri wa haya mambo, kupotea njia ni mara moja ukirudia kupotea tena basi wewe umeamua uteseke.
 
Principle ni moja tu
Huwezi ku provide nenda nyuma yangu shetani wewe...
Better be alone
 
Tena hao Marioo wanaomiliki mbupu tu wanapuliza balaa yaan kulala makaburini sio shida zao,

Kuna Marioo mwengine pro max aliyakanyaga kwa Mmama wa mjini tena wa Tandale, alizoea kuwadangia Mimama yenye hela na kupewa good life basi akajidumbukiza kwa mama huyo wa mjini akiamini angekula hela za Mama na Mtoto wake matokea yake anazeeshwa na cha maana hana,

Anamkumbuka yule jimama wa kule Mbweni alivyokua anampelekesha atakavyo sasa hivi anapelekeshwa yeye, kutoka hawezi kubaki anazidi kupoteza muda,
 
Nishamsoma huyo ankalii
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom