Marais wakataa ndoa duniani

Mto Songwe

JF-Expert Member
Jul 17, 2023
6,006
12,267
Haya wakataa ndoa mmefikiwa🤡

Kumbe kampeni yenu ni kubwa ina watu wazito duniani.

1. Vladimir Putin
Huyu bwana nafikiri watu wengi wanamfahamu hapa duniani.

Kwa wasio mfahamu huyu ni Rais wa taifa la Russia huyu bwana yeye kama Rais wa wakataa ndoa duniani toka 2013 amekuwa akiishi maisha ya ubachela mpaka sasa 2024.

Huyu ni role model wa watu wengi duniani upande wake wa pili wa sarafu ni Rais wa wakataa ndoa duniani.

2. James Buchanan
Huyu mwamba alikuwa Rais wa 15 wa Marekani huyu alikuwa bachela mbombevu au Rais mkongwe wa wakataa ndoa duniani.

Katika kipindi chote cha muda wake wa madarakani huyu mwamba hakuwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke yoyote yule.

3. Park Guen-hye

Haya bwana namba tatu tunaruka na huyu former president wa South Korea huyu alikuwa mtoto wa General park yule mwamba aliye ibadilisha SK na kupata maendeleo.

Tuachane na hayo, watu wengi wanadhani harakati za hawa kataa ndoa ni za wanaume pekee hapana hata wanawake malegend huko duniani waliko endelea wapo na huyu ni mmoja wao.

Huyu mwanamama aliwahi sema ameolewa na south korea na South Korea ndio familia yake.

4. Pope Francis
Twende namba nne hapa tunamkuta kiongozi wa kanisa katoliki duniani na kiongozi wa taifa la Vatican.

Huyu mwamba naye ni mfuasi wa kataa ndoa kwa kutumia sheria za kidini.

Hawa wazee wa kataa ndoa wapo katika taasisi mbalimbali duniani kama utandu wa buibui.

Hapa wazee wa kataa ndoa katika dini wana mfuasi wao.

5. Tsai ing wen
Haya sasa huyu mwanamama legend mwingine toka pande za Taiwan.

Huyu ni Rais wa Taiwan naye ni kataa ndoa kwa upande wa wanawake mwanamama huyu hajawahi kuwa na mume wala familia.

Huyu ni bachela wa kike mzoefu haswa.


Uzi mwengine utataja watu maarufu ambao ni wanaharakati wa kataa ndoa hapa ni wana muziki, wana sayansi, wafanya biashara, wanamichezo na wengine wengi.

Kama kuna kiongozi mwengine nimemsahau wa hawa wazee wa kataa ndoa unaweza mtaja.
 
KATAA katakata.

Nje ya mada/ wanasayansi wengi Wali iishi hii kampuni vilivyo maana kuoa au kuwa na mwanamke kiujumla kulidumaza jinsi ya kufikiri gunduzi mbalimbali
 
Kiongozi wao mkuu ni Narendra Modi, Waziri Mkuu na mkuu wa nchi ya India. Huyo bwana alipewa mke akakimbia nyumbani, na mkewe naye akakataa kuolewa hadi uzee.
 
Kiongozi wao mkuu ni Narendra Modi, Waziri Mkuu na mkuu wa nchi ya India. Huyo bwana alipewa mke akakimbia nyumbani, na mkewe naye akakataa kuolewa hadi uzee.
Daaah! Nilimsahau mwamba Modi😎 halafu wahindi inaonekana wanapenda sana ubachela
 
Back
Top Bottom