Mbunge wa Mufindi Kusini (CCM) apata ajali

Siyo waunge wa maeneo hayo tu. Ila wabunge wanapofika maeneo hayo ndo wanapata ajali. Mfano Salome Mbatia

Stupid contribution inayoonyesha watu wenye kawaida ya kutumia makalio kufikiri.
Badala ya kuanalyse nature ya bara bara na design yake watu wanafikiria barabara kisiasa.
Lakini sishangai kwani thinking capacity ya aina hii ndo ilipofikia ukomo.
 
Mungu amponye haraka ili arudi kwenye mapambano ya kulisaidia jimbo lake.
 
Alalala laaa almanusura jimbo lingine kubaki wazi tena nini sasa anafanya huyu dereva wa lori hapa!?
 
habari za kusikitisha ukizangatia jinsi alivyo pambana kuwatoa wale jamaa walioshikiria lile jimbo hafu hata hajafaidi duuuu.ama kweli hii kali.let him recover soon
 
Ni kweli Mhe. Menrad Kigola Mbunge wa Mufindi Kusini alipata ajali tarehe 18/5/2012 akiwa safarini kuelekea Mafinga. Alikuwa akitoka katika kikao cha Ushauri cha Mkoa (RCC) jana majira ya saa 12 Jioni katika barabara kuu iendayo Mbeya katika eneo la Ihemi. Ndani ya Gari walikuwa watatu yeye, Msaidizi wake Bw. Mwapinga na Mtangazaji wa Ebony FM ya Iringa Bw. Gerson Maregesi. Wote walipata majeraha madogo madogo na walifika kwenye hospitali ya Mkoa wa Iringa kwa uchunguzi na matibabu. Wamechunguzwa na kutibiwa na leo tarehe 19/05/2012 majira ya saa 3:00 asubuhi wameruhusiwa kurejea nyumbani. Hali zao ni nzuri.
 
kwa nini wabunge wa maeneo haya wanapata sana ajali?

Toa takwimu mkuu,,nijuavyo iliwahi mtokea Mwagamalindo Mpilika(rip) wakati huo lilikuwa jimbo tu moja la mufindi kabla kugawanywa otherwise sidhani tunaweza kusema "......wa maeneo haya wanapata sana ajali"
 
...naomba huyu jamaa afe tufanye uchaguzi mwingine...

Kama hakusaini waraka wa Zitto basi na iwe R.I.P ili M4C ikachukue jimbo hilo
Kusema kweli nimesikitishwa sana na kauli zenu, kwa upande mwengine ninawasikitikia wenye mawazo kama haya. Cha kuangalia hapa ni kuwa barabara zetu ni mbovu na madereva wanakuwa wazembe sana. Hata kama huyu jamaa akifa (Namuombea kwa moyo mmoja apone haraka) na M4C kuchukua jimbo hilo na mengine kama mnavyoomba, bado watu wataendelea kupata ajali wakafa au kupata ulemavu kwa sababu barabara ni mbovu na madereva ni wazembe.
 
Back
Top Bottom