Mbunge wa Mufindi Kusini (CCM) apata ajali

mgeni wenu

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
3,664
1,730
Wanajmvi Habari kutoka Iringa zinasema kuwa Mbunge wa Mufindi Kusini(CCM) Mh Menrad Lutengano Kigola amepata Ajali mbaya ya Gari jioni ya leo akitokea Jimboni Kuelekea Dar katika vikao vya Kamati za Bunge,Habari kutoka Hospitali ya Mkoa wa Iringa zinasema ni kweli kapata Ajali na Atahamishwa Muhimbili kwa Uchunguzi na Matibabu zaidi..
Mungu amponye Haraka.
Ni mimi Mgosi Mgeni wenu wa JF
 
asante kwa taarifa. ni mbunge wa kuchaguliwa au kuteuliwa na rais.
 
Mola amponye haraka ili awahi mapambano Juni 2012

mapambano ya kutetea ujinga wa jk na wenzake? Seriously kwa hali anayotupatia na atakayotuachia mi huwa naomba huyu jamaa afe tufanye uchaguzi mwingine wa rais. Rais ajaye atapata shida sana kwenye kuongoza hii nchi! Mpaka ukawageuze watu warudi kwenye kukusanya kodi na kufanya biashara halali japo kwa two third itakuwa ni ngumu sana. Imefika hatua serikali inaongozwa kwa kodi za wafanyakazi walio wachache,ni aibu kubwa sana.
 
Namtakia afya njema na uponaji wa haraka.
Awe alisaini petition ama hakusaini, si hoja ya msingi kwa muktadha huu.
 
Back
Top Bottom