Ufipa-Kinondoni
JF-Expert Member
- Jan 3, 2012
- 4,582
- 2,783
Mbunge wa Kilwa Kusini Mh. Suleiman Ally Bungara maarufu kwa jina la ***** leo asubuhi amekematwa na polisi katika kituo cha polisi Wilaya ya Kilwa na kufikishwa Mahakamani kwa kosa la kufanya vurugu katika kituo hicho jana usiku. Tukio hilo nimetokana kwenda kumtoa shehe maarufu wa hapo Wilayani aliyekamatwa na polisi kwa kosa la Kukataa kuhesabiwa sensa. Alipofika alifanya fujo ambazo zilipelekea kukunjwa vibaya na OCD wa kituo hicho na kuwekwa chini ya ulinzi kwa muda. Hata hivyo, aliachiwa baada ya kufanya mawasiliano na RPC wa Mkoa wa Lindi.
Leo asubuhi, mbunge huyu alikwenda tena kituoni hapo na ndipo alipokamatwa muda wa saa 2 nakupelekwa mahakamani pamoja na shehe.
Kwa taarifa zaidi inaonyesha mh. mbunge ameachiwa leo saa 1 usiku huu kwa dhamana.