KATIBU Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Japhet Maganga, na wenzake 10 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kufanya fujo kwenye mkutano wa Baraza Kuu la chama hicho wakati wakipitisha bajeti ya mwaka.
Tukio hilo lilitokea baada ya baraza hilo kuazimia kumsimamisha kazi Maganga kutokana na kupoteza sifa baada ya kufukuzwa kazi na mwajiri wake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno, amethibitisha kukumatwa kwa kiongozi huyo pamoja na wenzake wakati wa mkutano huo.
“Tulipata taarifa kuwa kuna watu wanafanya fujo tukaenda kudhibiti kabla hayajatokea madhara. Kwenye mkutano huo sisi hatufahamu ilikuwaje zikatokea fujo. Ukitaka kufahamu zaidi waulizwe CWT wenyewe,” amesema Kamanda Otieno.
Source - Nipashe