Waziri: Mkopo wa Elimu ya Juu haijalishi Mwanafunzi kasoma Shule binafsi au umma (Bungeni)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 12, Kikao cha 1, leo Agosti 29, 2023.


WAZIRI: MKOPO WA ELIMU HAUZINGATII MWANAFUNZI KASOMA SHULE BINAFSI AU UMMA
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Omary Juma Kipanga amesema upangwaji wa mikopo ya elimu inaongozwa na Sheria za Bodi ya Mikopo Sura Namba 178 na kuwa inawahusu wenye sifa za kujiunga na Elimu ya Juu lakini hawana uwezo wa kumudu gharama za elimu.

Amesema hayo Bungeni wakati akijibu swali la Mbunge Sophia Hebron Mwakagenda aliyehoji sababu za kuwepo kwa ugumu kwa upatikanaji wa mikopo kwa Wanafunzi waliosoma shule binafsi.


MBUNGE: WATUMISHI NA WASTAAFU HAWAKITAKI KIKOKOTOO CHA MAFAO
Mbunge Kasalali Emmanuel Mageni akichangia mada kuhusu mafao ya mifuko ya hifadhi ya Kijamii na kuhoji Serikali itawasilisha lini hoja ya kufuta kikokotoo kilichopo kwa kuwa hakikubaliwi na watumishi na wastaafu.

Awali akielezea suala hilo Naibu Waziri,Ofisi ya Waziri Mkuu, Patrobas Katambi amesema mpango wa Serikali ni kuendelea kutoa elimu kwa Wananchi kuhusu Kanuni Mpya ya Mafao ya Kikokotoo iliyotangazwa kuanzia Julai 1, 2022, akitoa mfano sehemu ya maboresho ya mafao ya mkupuko yalikuwa 25% na baada ya mabadiliko yamekuwa 33%.


BUNGE LAPITISHA BUSWADA WA SHERIA MBALIMBALI WAPITISHWA
Bunge limepitisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.2) wa Mwaka 2023, uliowasilishwa mapema asubuhi leo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji, Dk Eliezer Feleshi .

Miongoni mwa sheria zilizowasilishwa kufanyiwa marekebisho ni Sheria ya Nguvu ya Atomu Sura ya 188, Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusu Umiliki wa Mali na Rasilimali Asilia, Sura ya 449.

Nyingine ni Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu masharti hasi katika mikataba Mali na Rasilimali Asilia na Sheria ya Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda, Sura ya 159.

Kuhusu marekebisho ya Sheria ya Nguvu ya Atomu Sura ya 188, Jaji Feleshi amesema kifungu cha 4 kinarekebishwa ili kuongeza mawanda ya udhibiti kwa kushusha viwango vya vyanzo mbalimbali vya mionzi inayosimamiwa na sheria hiyo.

“Lengo la marekebisho haya ni kudhibiti mmuliko wa mionzi unaotokana na Madini na Viasili vya Mionzi ya Asili (NORMs)” amesema Jaji Feleshi.
 
Kwenye suala la Mikopo ya Wanafunzi huyo Waziri kasema uongo hadharani. Mwanangu mwaka wa masomo wa 2022/2023 akiwa mwaka wa kwanza alikosa mkopo kwa kigezo cha kusoma private. Na ndivyo walivyomwambia pale Bodi ya Mikopo halafu leo anasema sio kigezo cha kukosa mkopo? PUMBAVU!!!
 
Back
Top Bottom