Mbunge Juliana Masaburi Aibana Wizara ya Ardhi Kuhusu Kutumia Fedha za Kigeni Katika Malipo ya Upangishaji Nyumba

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

MBUNGE JULIANA MASABURI AIBANA WIZARA YA ARDHI KUHUSU KUTUMIA FEDHA ZA KIGENI KATIKA MALIPO YA UPANGISHAJI NYUMBA

Mhe. Juliana Didas Masaburi, Mbunge wa Viti Maalum, ambaye swali lake namba 15 kwa niaba limeulizwa na Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini, Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo lililoelekezwa Wizara ya Ardhi na kujibiwa na Waziri wa Ardhi, Mhe. Jerry Silaa

"Kwasasa hakuna sheria mahususi inayoelekeza aina ya fedha inayotakiwa kutumika katika kutoza pango kwa wapangishaji wa nyumba. Benki Kuu ya Tanzania imekuwa ikitoa miongozo ya fedha za kigeni nchini ambayo inakataza matumizi ya fedha za kigeni kwa wakazi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kulipia bidhaa na huduma nchini" - Mhe. Jerry Silaa, Waziri wa Ardhi

"Ili kuboresha utendaji wa soko la nyumba (Real Estate) nchini, Wizara ya Ardhi ipo katika mchakato wa kutunga Sheria ya milki ambayo itaweka utaratibu wa utozaji wa pango hususani kwa raia wa Tanzania" - Mhe. Jerry Silaa, Waziri wa Ardhi

"Ni lini Serikali kwa ujumla wake italeta Sheria kubwa na pana itakayosimamia sekta ya Makazi na upangishaji? Je, Serikali ina mpango gani wa kuanzisha kanzidata ya nyumba za kupangisha kwenye Majiji, Manispaa na Miji ndani ya nchi yetu?" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini

"Wizara ya Ardhi, ipo katika hatua za kuandaa Sheria itakayotoa muongozo wa jinsi ya kuenenda kwenye soko la nyumba (Real Estate). Sheria itaunda chombo ambacho kitasimamia Mawakala wote wa upangishaji na upangaji wa nyumba" - Mhe. Jerry Silaa, Waziri wa Ardhi

"Wizara ya Ardhi ipo katika mchakato na ipo katika hatua za mwisho ya kutengeneza mfumo mkubwa wa Menejimenti ya Ardhi nchini. Nyumba zilizomo kwenye maeneo yetu, matumizi ya nyumba, matumizi ya kiwanja. Tutazingatia kujua nyumba za wapangaji zipo ngapi" - Mhe. Jerry Silaa, Waziri wa Ardhi
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2024-02-11 at 14.11.21.mp4
    8.8 MB
Back
Top Bottom