BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,120
#UWAJIBIKAJI: Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Paul Makonda amesema katika ziara zake alizofanya katika Mikoa 23 nchini, amebaini matatizo na kero kubwa zinazowakabili Wananchi ikiwemo Watu kudhulumiwa Ardhi na tatizo la Hati Batili.
Amesema Ipo dhulma kubwa kwenye Sekta ya Ardhi, huko imekithiri. Kilio cha Watu kunyang'anywa maeneo yao na Watu wenye nguvu ya Fedha, kupewa Nyaraka au Hati Feki kimetawala. Tulitoa maelekezo kwa Wizara na tunatiwa Moyo na hatua zinazochukuliwa na Waziri wetu wa Ardhi, Jerry Silaa".
Ameongeza kuwa Chama kilimuelekeza Waziri Silaa kuendelea na kazi ya kutatua migogoro ya Ardhi pamoja na kuhakikisha Watu waliodhulumiwa Ardhi wanarejeshewa mali zao pamoja na kuchukua hatua kwa Waliohusika na dhulma hizo wakiwemo Watumisi wa Sekta ya Afya.
==========