Mbunge Assa Makanika akutana na viongozi wa dini zote Jimbo la Kigoma Kaskazini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Mhe. Assa Makanika mnamo tarehe 10 Juni, 2023 alikutana na viongozi wa dini zote wa Jimbo la kigoma kaskazini ikiwa ni utaratibu wake kukutana na taasisi mbalimbali jimboni.

Lengo la kikao hicho ni Muendelezo wa kushukuru, kupokea ushauri na maoni kutoka kwa Viongozi hao wanaowatumikia watu muda wote na saa zote na kutatua shida zao za kiroho na kuwaunganisha katika Jamii na kumjua Mungu wao kwa siku zote za maisha yao hapa Dunia.

Mhe. Assa Makanika alizungumzia miradi ya Afya, Elimu na Maji ambayo imetekelezwa na inaendelea kutekelezwa katika Jimbo la Kigoma Kaskazini huku akiweka bayana utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Sekta ya Afya.

Mhe. Assa Makanika alisema ni miaka 3 tangu alivyolipokea Jimbo ambalo alikuta lina Vituo vya Afya viwili 2, Na Sasa kwenye uongozi wake amepata vituo vya afya 3 na Viwili muda si mrefu atafanikiwa kuvipata

Katika upande wa Elimu Mhe. Assa Makanika amesema amefanikiwa kusajili na kujenga Shule za Sekondari Mpya Nane (08); Bubango (Bitale); Kizenga (Bitale); Msimba (Mungonya); Nkungwe (Nkungwe); Kasima (Simbo); Kiziba (Mwam Mgongo); Kagunga (Kagunga); na Kigalye (Ziwani).

WhatsApp Image 2023-06-11 at 16.53.02.jpeg
WhatsApp Image 2023-06-11 at 16.53.02(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-06-11 at 16.53.03(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-06-11 at 16.53.03.jpeg
WhatsApp Image 2023-06-11 at 16.53.02(2).jpeg
 
Back
Top Bottom