Mbunge Makanika na Balozi wa China Nchini Tanzania kufungua huduma ya matibabu Jimbo la Kigoma Kaskazini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
942
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Mhe. Assa Makanika kwa kushirikiana na Balozi wa China 🇨🇳 Nchini Tanzania 🇹🇿 tarehe 16 Oktoba, 2023 Watafungua Huduma za Matibabu kwa wakazi wa Jimbo la Kigoma Kaskazini na Mkoa wa Kigoma.

Sherehe ya ufunguzi itafanyika tarehe 16/10/ 2023 katika Viwanja vya Mpira Amahoro Kata ya KALINZI kuanzia Majira ya Saa 4:30 AM (10:00) Asubuhi.

Aidha, mnamo tarehe 18/10/2023 Madaktari Bingwa watahamia Kituo cha Afya cha Simbo kwa ajili ya kusogeza huduma hizo kwa Kata jirani za Simbo, Kidahwe, Matendo, Mahembe na Nkungwe.

KARIBUNI WANANCHI WOTE KWA TUKIO HILI MUHIMU SANA KWETU.

Untitledtrew.jpg
 
Back
Top Bottom