Mbowe na Slaa kutikisa Zanzibar kesho

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CDM) kesho kitazindua kwa kishindo kampeni za Uchaguzi mdogo wa Uwakilishi jimbo la Uzini ambapo chama hicho kimejizatiti kuchukua kiti hicho na kuandika historia mpya ya chama hicho huko Zanzibar.

Taarifa ya CDM imesema vinara wakuu wa chama hicho Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa watawaongoza maelfu ya wanachama wake wa Zanzibar hapo kesho katika uzinduzi unaotarajiwa kuwa wa kihistoria.

Taarifa zaidi kutoka Zanzibar zinasema tayari Dr Slaa amewasili tangu jana kupanga mikakati ya mwisho mwisho.Pia kuna taarifa kwamba kuna shamrashamra za hapa na pale za wafuasi wa CDM.

Habari zaidi:Tanzania Daima.


Kazi kweli kweli kwani Padre alikuwa na kikao kifupi na askofu mkuu wa jimbo katoliki nZnz kuweka mambo sawa ili waumini wote wakitoka tu kanisani waelekee uzini.

kazi kwenu.
 
ndilo tatizo wanafuasi wa mafisadi walio wengi like you hawawezi kusimamia wanachokisema

ni kweli kaka, wafuasi wa mafisadi wagumu sana kuelewa, nguvu ya umma hujidhihirisha palipo na utetesi wa haki kwa wote bila kujali Udini na Ukabila. Hongera CDMA.
 
Kwakuwa zanzibar ya leo haina chama cha upinzani hatimae watapata haki hiyo ya kuwa na mwakilishi anayetoa changamoto kwa kuichagua CHADEMA lakini ni lazima kujituma ktk kutoa elimu kwa wapiga kura maana akina mkama hawakawii kutangaza orodha hewa ya magaidi. Kila la kheri CHADEMA.
 
Mkuu,hata mimi nimeshangaa sana nilipoiona ile form iliyopostiwa na MAFILILI! yaani CDM ilishika nafasi ya pili baada ya ccm? siamini macho yangu.
sasa ni kupiga kambi ya uhakika wapiga kura hawafiki hata 9000 hawa ni rahisi kudhiti uizi wa kura onaonaje
Tuwahamasishe makamanda waende kutoa elimu stahiki
 
ila cdm wanamoyo japo wanajua hawatashinda ila wapo tu
mbona upo kama kipofu?? wanajuaje kama hawatashinda?? au wewe ndio miongoni mwa wezi wa kura?? kinachoamua ushindi ni kura so utapataje hizo kura bila kushiriki?? acha mawazo mgando
 
Ni ngumu Mpemba kuingia Kanisani...
aingie kanisani kufanya nini ? hapa tunazumzia siasa mambo ya kanisani yanatoka wapi safari hii moto mnao

ikumbuke kauli ya Mdee bungeni... mtataja kila sifa mbaya ... mtabadili majina ... hapo Chama kitaendelea kupata umaarufu Bara na Visiwani
 
sasa ni kupiga kambi ya uhakika wapiga kura hawafiki hata 9000 hawa ni rahisi kudhiti uizi wa kura onaonaje
Tuwahamasishe makamanda waende kutoa elimu stahiki

Hata NCCR 2003 walipiga kambi pemba. Kwa hiyo chadema haitakuwa ajabu.

Padre si ameshafika huko kuweka mambo sawa pale mji mkongwe!!

Kila la kheir ila muwe makini msije mkajuta.
 
Kazi kweli kweli kwani Padre alikuwa na kikao kifupi na askofu mkuu wa jimbo katoliki nZnz kuweka mambo sawa ili waumini wote wakitoka tu kanisani waelekee uzini.

kazi kwenu.

acha mawazo mgando ya udini wewe, utabadilika lini??
 
Kazi kweli kweli kwani Padre alikuwa na kikao kifupi na askofu mkuu wa jimbo katoliki nZnz kuweka mambo sawa ili waumini wote wakitoka tu kanisani waelekee uzini.

kazi kwenu.
walewale ila majina yatofautiana jenga hoja simamia maneno yenye tija ... ninyi tuwaelezeje muelewe ... Hata walimu wenu walipata shida sana kuwafundisha ndiyo maana hamukubali kubadilika kuachana na sumu ya UDINI nchini
 
Hata NCCR 2003 walipiga kambi pemba. Kwa hiyo chadema haitakuwa ajabu.
Padre si ameshafika huko kuweka mambo sawa pale mji mkongwe!!
Kila la kheir ila muwe makini msije mkajuta.
Usijali Chadema ya sasa ni tofauti na NCCR ya 2003
Kama Padre kesha ombea hapo safi sana maana uchaguzi utakuwa HAKI, AMANI na UTULIVU na pepo la uizi wa kura limesha kemewa kwa hiyo jimbo li mikononi mwa Chadema muda si mrefu ....AMENI
 
CDM kukata tamaa mwiko!!

2010 Parliamentary Election Results –
Region KUSINI UNGUJA
District KATI
Consituency UZINI

CandidatePolitical PartyNumber of VotesPercentage Votes
MUHAMMED SEIF KHATIBU CCM6,65181.96
ALI MBAROUK MSHIMBA CHADEMA6177.6
ABDI MOHD ADEYOUM CUF5246.46
LUSIANO BENEZENT MAREKANO SAU460.57
SPOILT VOTES2773.41
TOTALS8,115100


I hate huu uongo wa kupita kiasi. Jimbo hili linatokana na Mbunge wake Bw. Mussa Hamisi Silima (CCM) kufariki Agosti 23, 2011 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu kufuatia ajali mbaya ya barabarani iliyotokea eneo la Nzuguni karibu na Dodoma, iliyohusisha gari alilokuwa akisafiria mbunge huyo Agosti 21, 2011 akiwa na mkewe, Mwanaheri Twalib ambaye yeye alipoteza maisha papo hapo.

Sasa haya matokeo ya Mohamed Seif Khatibu yanatokea wapi?
 
Lakini nyie CDM si ndio mnapinga muungano sasa mnataka nini Zanzibar?

CDM ndo nini?unakuta hata viongozi wakubwa wa chadema wanatamka CDM! Jamani ni CHADEMA sio CDM.Mkumbo kitila na wenzio mmenipata?!
 
Back
Top Bottom