Mbowe na Slaa kutikisa Zanzibar kesho

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CDM) kesho kitazindua kwa kishindo kampeni za Uchaguzi mdogo wa Uwakilishi jimbo la Uzini ambapo chama hicho kimejizatiti kuchukua kiti hicho na kuandika historia mpya ya chama hicho huko Zanzibar.

Taarifa ya CDM imesema vinara wakuu wa chama hicho Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa watawaongoza maelfu ya wanachama wake wa Zanzibar hapo kesho katika uzinduzi unaotarajiwa kuwa wa kihistoria.

Taarifa zaidi kutoka Zanzibar zinasema tayari Dr Slaa amewasili tangu jana kupanga mikakati ya mwisho mwisho.Pia kuna taarifa kwamba kuna shamrashamra za hapa na pale za wafuasi wa CDM.

Habari zaidi:Tanzania Daima.
 
Tunawatakia kila heri maana wemesema CDM haiwezi kulichua jimbo hillo sababu wanazitoa zimejijenga ktk udini
 
Hatujaja kujaribu nikufanya,Cadema na watu wake wanafanya,Serekali na Psa zao watakoma!!!!
 
Taarifa ya CDM imesema vinara wakuu wa chama hicho Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa watawaongoza maelfu ya wanachama wake wa Zanzibar hapo kesho
Hao wanachama wa CDM maelfu wametoka wapi zanzibar? Au mwandishi alikuwa naandika tu kujifurahisha?
 
go go go, piga kazi, mpaka wazee wa ghahawa wataelewa tu, kwamba CDM imedhamilia kuwakomboa mikononi mwa mafisadi
 
This story, is what the fools want to hear although it lacks substance
 
dj mbowe na padri slaa wamefuata posho tu ya laki 6 per day
usijali wala hilo lisikusumbue kwa sasa jali zaid namna jimbo litakavyo kuwa baada ya kuchukuliwa na CDM maana ukombozi wa kweli utafikia walio wengi Jali pili elimu ya uraia inayo tarajiwa kumwagwa huko hapa kifo chenu kiwadia RIP kingxvi etal
 
This story, is what the fools want to hear although it lacks substance !
 
Kwa kweli mkuu mafanikio yote ya chama hiki yanatokana na magwiji hawa wawili ambao ni fahari ya CDM.
Kumbe hiki ni chama cha watu wawili..nilikuwa silifahamu hili!
Wanataka kufanya kila kitu wao, hawataki kuwapa wengine nafasi! Kwa mtindo huu chama kitakua?
 
Back
Top Bottom