Alihoji kama Naibu Waziri atakubali kufuta jibu lake juu ya mwekezaji huyo wa KIA kwa sababu hakusema ukweli.
Hata hivyo, Spika Anne Makinda alisema ni vizuri Mbowe apeleke maelezo yake kwa maandishi ili kuwa na ushahidi na Serikali ipeleke maelezo yake yalinganishwe na kuona jibu sahihi ni lipi.
Hapa kuna shida, tena shida kubwa sana. Kazi ya Spika ni kuendesha/kusimamia mijadala ya wabunge na sio kutoa hukumu. Kama waziri (serikali) inatoa majibu yenye utata na waziri akitakiwa kufuta au kurekebisha matamashi yake basi anatakiwa afanye hivyo papo hapo au kama hana data basi anatakiwa aseme ni lini ataleta mbele ya bunge. Huu ndio utamuduni unaotumiwa na mabunge ya madola ambapo Tanzania inafuata mfumo huo. Sio kazi ya Spika kusemelea serikali wala kugeuza bunge kuwa mahakama.
Mbowe ameeleza hela za kukarabati KIA zilitolewa na World Bank sio hao wawekezaji kama Waziri alivyowakilisha. Sasa Spika anataka Mbowe aandike maelezo gani tena mengine? Mpotashaji yupo kwa nini asijibu? Kwa nini Spika anataka kufanya maamuzi kichini chini?
Ni vizuri wabunge kupitia kamati ya uongozi na kanuni kurekebisha hili haraka vingenevyo bunge kama mhimili utashindwa kuhoji na kupata majibu toka kwa serikali. Kila kitua watatakiwa waandike kwa Spika na yeye (Spika) atatolea uamuzi kama ambavyo anaona inafaa! Huyu Spika hafai hata kidogo. She is a total disaster.