Mbowe awashangaa watanzania... Uwanja wa Ndege Kilimanjaro unakodishwa kwa Dola 1,000 kwa MWAKA!

Alihoji kama Naibu Waziri atakubali kufuta jibu lake juu ya mwekezaji huyo wa KIA kwa sababu hakusema ukweli.

Hata hivyo, Spika Anne Makinda alisema ni vizuri Mbowe apeleke maelezo yake kwa maandishi ili kuwa na ushahidi na Serikali ipeleke maelezo yake yalinganishwe na kuona jibu sahihi ni lipi.

Hapa kuna shida, tena shida kubwa sana. Kazi ya Spika ni kuendesha/kusimamia mijadala ya wabunge na sio kutoa hukumu. Kama waziri (serikali) inatoa majibu yenye utata na waziri akitakiwa kufuta au kurekebisha matamashi yake basi anatakiwa afanye hivyo papo hapo au kama hana data basi anatakiwa aseme ni lini ataleta mbele ya bunge. Huu ndio utamuduni unaotumiwa na mabunge ya madola ambapo Tanzania inafuata mfumo huo. Sio kazi ya Spika kusemelea serikali wala kugeuza bunge kuwa mahakama.

Mbowe ameeleza hela za kukarabati KIA zilitolewa na World Bank sio hao wawekezaji kama Waziri alivyowakilisha. Sasa Spika anataka Mbowe aandike maelezo gani tena mengine? Mpotashaji yupo kwa nini asijibu? Kwa nini Spika anataka kufanya maamuzi kichini chini?

Ni vizuri wabunge kupitia kamati ya uongozi na kanuni kurekebisha hili haraka vingenevyo bunge kama mhimili utashindwa kuhoji na kupata majibu toka kwa serikali. Kila kitua watatakiwa waandike kwa Spika na yeye (Spika) atatolea uamuzi kama ambavyo anaona inafaa! Huyu Spika hafai hata kidogo. She is a total disaster.
 
Huyu mama anaendesha bunge kwa matakwa ya waliomuweka mapacha watatu na mkwerez
Yani ameharibu heshima ya bunge kupita kiwango! Sijui kama tutafika 2015!!
 
Kwa kweli spika wenu ni mtihani mkubwa sana.

Kila kitu leteni kimaandishi na hakuna majibu sahihi kwa wananchi ambao ndio waliowachagua kuwawakilisha pale.


Vipi sakata la Mh Lema na Waziri Mkuu, Vipi suala la Mh Tundu Lissu na waziri wa maliasili , Je kuna majibu yoyote kutoka kwa spika. nani muongo Lema au waziri mkuu, Tindu lisu au waziri nishati? na nini adhabu zao.

naomba majibu kwa spika
 
tatizo kubwa huyu mama kawekwa kuficha makosa au maslahi ya watu so lazima afanye kazi kwa matakwa ya waliomuweka thats CCM bwana yaani chama kinaboha sana hiki!walimtupa sita kwa kua alikua mtendaji mzuri wa bunge wakampa huyu mama yaani hapa mpaka muda wake wa uongozi uishe wabongo tutakua tumekonda sana
 
Kuna tetesi za kuaminika kuwa mmiliki wa Kilimanjara Internationa Airport ni mama Mkapa anayetumia mwavuli wa mwekezaji mkaburu wa sauz.Source mfanyakazi wa KADCO.Hivi hii nchi inaelekea wapi?hajatosheka na fursa saw kwa wote?
 
Kuna tetesi za kuaminika kuwa mmiliki wa Kilimanjara Internationa Airport ni mama Mkapa anayetumia mwavuli wa mwekezaji mkaburu wa sauz.Source mfanyakazi wa KADCO.Hivi hii nchi inaelekea wapi?hajatosheka na fursa saw kwa wote?
Hapa kwa kweli sijui tufanye nini ili kuondoa kizazi hiki kinachotafuna taifa letu..
 
Kuna tetesi za kuaminika kuwa mmiliki wa Kilimanjara Internationa Airport ni mama Mkapa anayetumia mwavuli wa mwekezaji mkaburu wa sauz.Source mfanyakazi wa KADCO.Hivi hii nchi inaelekea wapi?hajatosheka na fursa saw kwa wote?

The Game hebu kaa na hiyo source yako vizuri afu urudi tena mkuu naona kama bado haijakaa vyema hii.
 
hapo KADICO mbona pia nasikia mkuu wa usalama ni darasa la 7, pia ni wizadi waukweli. Na sasahivi amesafiri kwenda kuloga ili ile kesi ya kusafirisha wanyama nje ya Nchi kinyume cha sheria iishe kimya kimya.
 
Kumbe nipo nyuma sana! hata nilikuwa sijui kama Kilimanjaro Internation Aiport (KIA) ni mali ya mtu Binafsi au hii taarifa mimi ndio siielewi vyema!?
 
Kumbe nipo nyuma sana! hata nilikuwa sijui kama Kilimanjaro Internation Aiport (KIA) ni mali ya mtu Binafsi au hii taarifa mimi ndio siielewi vyema!?

mkuu naridhia kabisa kwamba hii habari ni ya uongo kwani mtoa mada ameshindwa kutofautisha kati ya KIA na KADCO
 
Uweli( KIA )ni kifupi cha Kilimanjaro International Airport na (KADCO)ni kifupi cha Kilimanjaro Airport Development Company ambalo ndilo kampuni lilowekekeza na lenye mamlaka na uwanja.Hii habari ni ya ukweli kwani mimi nimefanya kazi pale mwaka jana wote na niliambiwa mkaburu ni kama pazia tu pale.
 
Nadhani huyu mama kuwa mmiliki sio issue tatizo ni
1. Uwanja huo unatakikana kuwa ni wa serikali
2. umebinafsishwa au KIDCO wameingia katika ubia na serikali?
3. Huo ubia au ubanifsishwaji ulifanyika competitively au vipi?
4. Are the interests of the government been fully considered or were fully damped,
Katika hili ndio sasa na mmiliki wake anapokuwa issue.
5. Kuna hili limeibuka juzi la kusafirisha wanyama, hili nalo liko complicated kweli kweli.

Kwa hiyo mnaomkingia kifua mother, punguzeni speed, issue iko sensitive
 
nina shaka na chanzo chako cha habari...asije kuwa ni mfagiaji

nimewahi kufanya kazi ya kumwagilia maua sehemu flani lakini lengo lilikuwa lingine kabisa.........not everything you see is as it is meen!!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom