Serikali Kukamilisha Barabara kwa Kiwango cha Lami Mpanda, Uvinza na Inyonga katika Mwaka wa Fedha 2023-2024

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

SERIKALI KUKAMILISHA BARABARA KWA KIWANGO CHA LAMI MPANDA, UVINZA NA INYONGA KATIKA MWAKA WA FEDHA 2023-2024

Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Atupele Mwakibete amejibu maswali Bungeni jijini Dodoma aliyoulizwa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi, Mhe. Martha Festo Mariki juu ya ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami katika Mkoa wa Katavi

Je, Serikali ina mkakati gani wa kujenga barabara ya kibaoni - Majimoto hadi Inyonga kwa kiwango cha lami? - Mhe. Martha Festo Mariki, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROAD) imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi wa Barabara ya Kibaoni-Majimoto-Inyonga yenye kilomita 162 hadi sasa jumla ya kilomita 9.3 zimejengwa kwa kiwango cha lami sehemu ya Inyonga yenye kilomita 4.2 na Majimoto kilomita 2.6 na Usevya kilomita 2.5 ambapo ni Halmashauri Kuu ya Mpimbwe. Serikali inaendelea kutafuta fedha kuendelea na sehemu ya ujenzi iliyobaki" - Mhe. Atupele Mwakibete, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi

"Wananchi wa Mkoa wa Katavi wamekuwa wakizunguka umbali mrefu kupitia eneo la Mpanda hadi Inyonga kutokana na Barabara kipindi cha masika haipitiki kabisa. Je, Serikali haioni umuhimu wa haraka kufanya ujenzi wa Barabara? - Mhe. Martha Festo Mariki, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Serikali inafanya ujenzi wa Barabara ya kutoka Mpanda, Uvinza mpaka Katavi. Je, ni lini Serikali itakamilisha Kilomita zilizobaki mpaka Uvinza ili tuweze kuunganishwa na wananchi wa Mkoa wa Kigoma kwa ujenzi wa kiwango cha lami" - Mhe. Martha Festo Mariki, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Barabara ya Mpanda hadi Inyonga ni ya kilomita 60 ambayo inahitaji kujengwa kwa kiwango cha lami. Serikali iliona umuhimu kwanza kujenga Daraja la Kavuu ambalo lilikuwa la Chuma na sasa linakwenda kuwekewa Zege na kazi inaendelea. Katika mwaka huu wa fedha tutakamilisha kilomita zilizobaki" - Mhe. Atupele Mwakibete, Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi

"Barabara ya Mpanda na Uvinza ina Mkandarasi anaitwa CHIKO na tayari tumeanza ujenzi wa kiwango cha lami kilomita 25 na tunategemea mkataba huu utaisha baada ya mwaka mmoja na miezi sita" - Mhe. Atupele Mwakibete, Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-05-16 at 17.49.58(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-16 at 17.49.58(1).jpeg
    50 KB · Views: 7
  • WhatsApp Image 2023-05-16 at 17.50.20.jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-16 at 17.50.20.jpeg
    139 KB · Views: 7
Back
Top Bottom