Mbowe atakiwa kuachana na siasa kabla ya 2015

unajua kuna watu humu jamvini sijui wanafikiria na makalio? hilo la CHADEMA KUchukua nchi mbona lipo waaaazi.mimi mwenyewe mwanaccm nimekitafakari chama kwa undani naona kimekata netework.Ona mikutano ya nape kama ya kijiji.watu mia hamsini wakizidi saaana 300 huoni wananchi weshachoka au kwa sababu ya ushabiki?ni vema tuishauri chadema kujijenga kupata wasomi wengi kabla ya 2015 ili tupate serewkali mpya na SI VINGINEVYO.CHAMA CHETU KIMEZEEKA,DONT YOU SEE?
 
CDM kwanza muanze kwa kuiendesha kidemokrasia, ikiwa hata viti vya ubunge vya upendeleo mnapeana kikanda, utawala ndani ya ofisi za cdm kiuchumba, halafu unataka wenye macho tuhamie huko?

Muulize TUNTEMEKE.

Tumeshamaliza kusini sasa tunaenda kati hapo kwa yule mla rushwa wa bahi tukamalize kazi
 
CDM kwanza muanze kwa kuiendesha kidemokrasia, ikiwa hata viti vya ubunge vya upendeleo mnapeana kikanda, utawala ndani ya ofisi za cdm kiuchumba, halafu unataka wenye macho tuhamie huko?

Muulize TUNTEMEKE.

Mkuu usiamini propaganda chafu hamia basi kubwa .
 
Katibu wa CCM katika Manispaa ya Moshi amesema Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa FREEMAN MBOWE amefilisika kisiasa na kumtaka aachane na siasa kabla ya 2015 ili akaendelee na biashara zake. Katibu huyo amesema hayo siku chache baada ya MBOWE kusema akiwa mikoa ya kusini kuwa CCM ikinusurika 2015 ataachana na siasa. Katibu huyo wa CCM alisisitiza kuwa hiyo ni ndoto ambayo MBOWE alikuwa akiiota mchana kweupe kwa vile tayari wananchi wameshajua janja ya CHADEMA na kamwe hawawezi kuwapa ridhaa ya kuongoza nchi. Aidha Katibu huyo amewashambulia viongozi wa CHADEMA jinsi wanavyowalaghai wananchi kwa hoja ya mfumuko wa bei, tatizo ambalo ni la nchi zote za Afrika. Amewataka wawaeleze wananchi namna ya kuondokana na umaskini badala ya maneno ya ulaghai.Source: Mwananchi.
Huyu jamaa kichefuchefu kweli,kama ni la nchi zote za afrika,aseme uwongo aonekane mkweli???
 
Katibu wa CCM katika Manispaa ya Moshi amesema Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa FREEMAN MBOWE amefilisika kisiasa na kumtaka aachane na siasa kabla ya 2015 ili akaendelee na biashara zake.

Katibu huyo amesema hayo siku chache baada ya MBOWE kusema akiwa mikoa ya kusini kuwa CCM ikinusurika 2015 ataachana na siasa.

Katibu huyo wa CCM alisisitiza kuwa hiyo ni ndoto ambayo MBOWE alikuwa akiiota mchana kweupe kwa vile tayari wananchi wameshajua janja ya CHADEMA na kamwe hawawezi kuwapa ridhaa ya kuongoza nchi.

Aidha Katibu huyo amewashambulia viongozi wa CHADEMA jinsi wanavyowalaghai wananchi kwa hoja ya mfumuko wa bei, tatizo ambalo ni la nchi zote za Afrika.

Amewataka wawaeleze wananchi namna ya kuondokana na umaskini badala ya maneno ya ulaghai.


Source: Mwananchi.

kwa kweli ccm watu wake wana akili fupi sana,hii kauli nimeisikia na magufuli nae akiiongea,hivi wewe na jirani zako mkiwa na tatizo la njaa ndo hujishughulishi kulitatua eti kwa kuwa na kwa jirani zako kuna njaa.Nakasirika sana naona kama 2015 haiji haraka.............piga chini magamba wooooooooooooote.............
 
mh mbowe aligombea urais wa tanzania mara mbili mfululizo lakini hakufanikiwa,kwa sasa amejitahidi kukijenga chama chake na kufikia hapo kilipo.ni vyema sasa apumzike awaachie vijana nao wakipeleke mbele chama.aachie uenyekiti awape majembe mapya,kama kina lema,wenje,mnyika na zitto
 
Ni upuuzi kusema mfumuko wa bei ni tatizo la Africa yote! kwa hiyo kwa kuwa ni tatizo la africa yote sio tatizo? tulikubali, tulilee na kuliendeleza!! that is nonsense!
 
:angry: i am not yet convinced by Chadema , what they do is only crying foul without showing the solution for it..still very naiive politicians .. i mean i havent even heard any thing convincing from chadema how they will run this country apart from making noises, they are not matured into politics..it is just a wave and this too shall pass..long live CCM...
 
M/kiti wilaya, M/kiti taifa, wapi na wapi! katafute umaarufu kwingine siyo kwa Kamanda Mbowe!
 
Huyo Katibu wa CCM ni hayawani au nini?, kwani wapi pameandikwa kukiwa na tatizo nchi za afrika lazima tatizo hilo liwe na Tanzania?? mbona kama kunamaendeleo nchi za afrika Tanzania haimo??

Mfumko wa bei si wa CDM, wala wananchi hawahitaji kuambiwa wanaufahamu wanakutana nao kila siku, soda ilikuwa 200/-TZS mwaka 2005, leo ni 600/-TZS unataka tuambiwe na nani wakati hata watoto wadogo wanajua.
 
:angry: i am not yet convinced by Chadema , what they do is only crying foul without showing the solution for it..still very naiive politicians .. i mean i havent even heard any thing convincing from chadema how they will run this country apart from making noises, they are not matured into politics..it is just a wave and this too shall pass..long live CCM...

utaendelea kuwa mtumwa wa ccm/lugha mpaka cku ya kufa kwako!
 
Back
Top Bottom