Mbowe arejesha Shangingi la Kiongozi wa Upinzani Bungeni

Kwanza angerudisha fedha alizokopa NSSF zilizomfanya anunulie Vogue (namkumbuka brazamen). Huyu brazamen ni katika wana JF wa zamani na kuna siku aliweka nyuzi humu JF iliyoonesha kuwa jigari analotumia Mbowe ni la wizi huko Uingereza, akataja mpaka waliomuuzia. Sijui brazamen yuko wapi siku hizi? Atupe ma data ya uhakika.

Nashukuru Mungu kuwa JF haikuanza nikiwa kijana maana naingeshawishika kwenda kusomea fani ya udaktari wa upasuaji vichwa, kweli naapa!!
 
Acha kukurupuka wewe binaadamu, kama hauna cha kuchangia bora pumba zako ukaziweka kando, unakumbuka pinda alipoyoka ziara nchini india alisema nini kuhusu haya mashangingi na matumizi yasiyo na tija kwa taifa??
 
anatafuta uraisi 2015 kwa kila njia! Ameona zitto kamzidi kete kwa kukataa posho! Anata na yeye aonekane bora


hao ambao wanaiba hadi mchana kweupe ndiyo wankufaa???? Juzi hapa wamesafirisha wanyama hai, askari mwema kasanua issue hao kwako ndiyo safi???? Madini wamegawiana wewe uhoni, ebu tuambie ulitaka afanye nini??? Kuonyesha uzalendo wake?????????????
 
Dhamira na nia itawale katika kutenda aliyofanya kuliko kutafuta namna ya kuwa na waamini wengi katika itakadi na mlengo uku anawaza kutenda maajabu yasiyofikirika katika akili ya kawaida.Hongera sana kwa utashi huo.
 
safi sana, ameweza kuonyesha kwamba pinda alipotoka India alitakiwa kufanya ninni??? alipoona serikali ya wenzetu inavyotumia raslimali zao vizuri, Pinda alisema - serikali ya India viongozi wake wote wanatumia magari ya kawaida ambayo mengi hata hayana 4wd kama kiongozi anataka gari la gharama atumie lake, pia vazi la ofisi siyo suti kama sisi bali ni shati la batiki, ambapo hata wao walipofika ilibidi watafutiwe mashati hayo japo walifika usiku. MBOWE AMETUONYESHA NJIA, KAMA KWELI PINDA ALINUIYA KUFUTA MASHANGINGI AFUATE NJIA HIYO HAACHE POROJO ZA MAJUKWAANI
 
OFISI ya Bunge imemtaka Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kususia pia huduma zingine anazopewa na Serikali kulingana na wadhifa wake, badala ya kukataa gari, dereva na mafuta pekee.Akizungumza na gazeti hili mjini hapa jana, Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel alisema huduma zote anazopewa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni zipo kisheria, hivyo hawezi kuchagua masharti anayotaka kuyafuata na mengine kuyakataa.

"Haya ni mambo ya kisiasa na sisi kama watendaji hatutaki kujiingiza kwenye siasa. Lakini niseme tu kwamba, lile gari hakupewa kufanyia shughuli za kisiasa ni la Serikali kwa ajili ya kazi zake kama Kiongozi wa Upinzani Bungeni," alisema Joel na kuongeza:

"Wabunge wote wanaongozwa kwa masharti, Spika ana masharti yake, Kiongozi wa Upinzani Bungeni ana masharti yake na wabunge wengine nao wana masharti yao. Sasa mtu huwezi kukubali masharti fulani na kukataa mengine, huku ni kuvunja sheria."

Joel alisema moja ya masharti aliyopewa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ni kupokea gari la Serikali, dereva na kuwekewa mafuta kwenye gari hilo wakati wa shughuli za Bunge.

"Sasa pamoja na kupewa gari, Ofisi ya Bunge pia inawajibika kisheria kumpa kiongozi huyo nyumba mbili; Dar es Salaam na Dodoma na mlinzi wa kulinda usalama wake wa kila siku," alisema Joel.Aliendelea,"Sasa akisema gari sitaki, huu ni utashi wake, lakini kwa nini akatae gari tu wakati kuna huduma zingine anazopewa?"

Bunge kuendelea kuwalipa posho
Kuhusu wabunge hao kutochukua posho, Joel alisema posho hizo hazitasitishwa kutolewa kwao hadi utaratibu utakapobadilishwa. "Haya mambo yapo kisheria jamani, nisipowalipa posho mimi nashtakiwa," alisema.

Joel alipuuza madai ya kambi hiyo kutaka kuwe na fomu mbili bungeni; kulipana posho bungeni na fomu ya mahudhurio ili wao wasaini fomu ya mahudhurio tu, wasipewe posho hizo, akisema "Fomu iliyopo ni ya mahudhurio, wanataka fomu gani sasa?.

… apongezwa kwa kurudisha shangingi

Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila aliunga mkono uamuzi huo na kusema hata katika nchi tajiri viongozi wenye nyadhifa za uwaziri wanatembelea magari ya kawaida.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (UDSM), Dk Benson Bana alisema, Mbowe ana hoja ambayo inapaswa kuungwa mkono na watu wengi wenye kuitakia mema nchi hii. Dk Bana alisema ingawa hoja hiyo inamjenga Mbowe kisiasa, lakini ukweli unabaki kuwa Serikali inatumia fedha

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro alisema kinachofanywa na Mbowe ni propaganda za kisiasa zenye lengo la kumpatia umaarufu.
"Mbowe ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, amepewa gari kwa ajili ya kazi hiyo, anarudisha gari kwa sababu yeye ni tajiri, angekuwa hana uwezo kama wabunge wengine angefanya hivyo?," alihoji Mtatiro.

Mtatiro alisema Mbowe asijifanye kuwa anawahurumia Watanzania maskini wakati maisha anayoishi ni ya kifahari yasiyofanana na wananchi wa kawaida.

Source: Mwananchi
 
Namkumbuka Mtatiro tukiwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kati ya 2004 na 2007-8 (Kwa wale waliosoma miaka 4). Mtatiro alikua mstari wa mbele sana na jasiri wa kuongoza “migomo,” na ninachoweza kusema ni kwamba Mtatiro alikua “kiongozi wa migomo” na wala hakuwa “mwanaharakati”. Sina lengo la kupinga migomo iliyofanyika wakati ule, la hasha. Bali ni huyu ndugu Mtatiro ambaye alikua anatumia kivuli cha migomo na matatizo ya wanachuo kutafuta umaarufu binafsi.
Nasema hivyo kwasababu aliyokua akiyasema wakati huo na anayosema leo ni kama tofauti kabisa kama vile Maembe na Mayai. Nakumbuka siku moja mwaka 2005 mwezi September tukiwa tunaimba ‘SOLIDARITY FOREVER’ Ukumbi wa Nkrumah Hall Mtatiro alisema “Serikali imenunua ndege ya Rais, wakati ‘sisi wasomi’ tunakaa na njaa.” Leo Mtatiro anampinga Mbowe kwamba anatumia hoja ya posho kujenga umaarufu wa kisiasa kwakua yeye ana pesa. Nanukuu
“Mbowe ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, amepewa gari kwa ajili ya kazi hiyo, anarudisha gari kwa sababu yeye ni tajiri, angekuwa hana uwezo kama wabunge wengine angefanya hivyo?,” alihoji Mtatiro.
Mtatiro alisema Mbowe asijifanye kuwa anawahurumia Watanzania maskini wakati maisha anayoishi ni ya kifahari yasiyofanana na wananchi wa kawaida.” Mwananchi, 23/6/2011
.
Ukiangalia hii hoja ya Mtatiro imejaa chuki na wivu usio na msingi. Hoja ya posho za kupindukia si suala la kuleta siasa za uchama (Partisan Politics). Binafsi si mwanachama wa chama chochote, lakini Malcolm X alivyowahi kusema, “You're not to be so blind with patriotism that you can't face reality. Wrong is wrong, no matter who does it or says it.” Malcolm X 1965. Katika muktadha huu hata asiyekua mwanachama wa CHADEMA kama ana uzalendo lazima atalipinga suala la hizi posho na matumizi ya anasa ya serikali yetu. Kwa mantiki hiyo basi hata kama Mbowe ana dhamira ya kutafuta umaarufu kisiasa, lakini hoja yake ina mashiko. Kama amerudisha gari kwakua analo la kwake la anasa basi ni bora kwani inaonesha si mroho wa pesa za umma kwakua anazo za kwake tofauti na baadhi ya viongozi ambao wamelimbikiza mali na wanazidi kukwiba tu na kutumia rasilimali za umma kujinufaisha na kutapanya tu.
Swali je, yeye Mtatiro alivyokua anaongoza migomo UDMS ni kwasababu alikua ‘na umasikini wa kipato’, na kama angekua na uwezo wakati anasoma UDSM asingekua anagoma?

Kwa kauli zake Mtatiro anaonesha ni mtu wa aina gani, na ni bora hata hakuthubutu kujiunga na vyama makini kwani kwa alivyokua ‘domo la upawa’ hata asingefaa kabisa. Ni mtu anayependa sifa na umaarufu binafsi.
NAJUA KUNA THREAD HAPA JAMVINI ILIMJADILI MTATIRO KWA UNDANI, NA KWA KIASI HOJA NYINGI ZILIMPAMBANUA KAMA MPAMBANAJI NA MWANAHAKATI WA KWELI, LAKINI BINAFSI NAMUONA KAMA ‘OPORTUNIST’ OR ELSE HE IS A ‘SELL OUT’.
Wakatabahu, Mzalendo
Naomba kuwasilisha
 
Hapo ndipo serikali inapojiidhirisha wazi kuwa haina nia ya kubana matumizi, ungetegemea serikali imwandikie
mbowe barua ya kumshukuru kwa kuonyesha kwa vitendo nia ya kuipunguzia gharama serikali na siyo kumkasirikia
kwa kuipinguzia gharama serikali yenyewe ni kichekesho na mzaa wa kupindukia. Naibu katibu wa bunge na mwenyewe
anatumiwa na wanasiasa kumjibu mbowe badala ya wahusika wenyewe wanaopashwa kujibu kwani yeye ni mtendaji
tu serikali na hatakiwi kujihusisha na siasa. Nauliza nia yao ya kubana hayo matumizi hiko wapi kama haikuwa ni kuwalaghai watanzania ???
 
Uyu Mtatiro ndio Nani?amejuaje utajili wa Mbowe?...na swala n utajili wa Mbowe au dhamila na nia ya kuonyesha mfano wa kupungza "unnecessary gvt Expenditure"...afu hi hoja amekopi kwa Vilaza wa Cloudz Power brkfast!!na Viongoz maskn ndo hatutaki..wanatsumbua sana Kina Pinda..bora waliozjua hela toka utoton kulko watoto wa wakulima
 
Wakajifunze kwenye serikali ya Kagame labda wanaweza pata hint what to do!!
 
Rais Kikwete amesikika huko Malaysia akilalamika kuwa ukosefu/upungufu wa fedha ni sababu mojawapo kubwa ya kuwa na maendeleo duni. Sijui kama office ya Bunge, Rais, Cabinet and CCM walishasikia maneno 'Austarity measure'?
 
Huyu katibu hajui maadali na itifaki ya kazi yake. Kwa kuwa hajapata barua alitakiwa aseme " no comment" mpaka pale atakapo pata barua rasmi. Je barua ikionyesha yote hayo yametekelezwa atakanusha kauli yake au la?. Hawa magamba kazi zao kuropoka tu.
 
Ndo leo unajua uyu Mwalimu Mtatiro ni komamanga?..ana hasira za kufunikwa na Mnyika Ubungo...mana Ubngo alizamishwa ilikuwa ni Dada Hawa na Kamanda Mnyka...Mtatiro kimyaaaaa....he was my student...i dare to say he has to look on the new jogging political path to finish the race!
 
Ndo leo unajua uyu Mwalimu Mtatiro ni komamanga?..ana hasira za kufunikwa na Mnyika Ubungo...mana Ubngo alizamishwa ilikuwa ni Dada Hawa na Kamanda Mnyka...Mtatiro kimyaaaaa....he was my student...i dare to say he has to look on the new jogging political path to finish the race!

Mkuu nashukuru kwa kuongeza msisitizo, binafsi nilimjua kwamba ni mtu anayependa 'misifa' lakini huu unafiki wake na kukosa uzalendo kwa kweli nakiri sikuwahi kutarajia kwamba anaweza kuwa mtu wa magamba kiasi hiki.
 
Wakati ndo anaanza kuingia katika siasa nilijua tumepata mpiganaji. Kumbe sivyo. Hata hivyo ana fursa bado ya kufanya uamuzi wa kuwa mpiganaji vinginevyo tutamuweka katika daftari la historia (kama Tambwe et al)
 
Back
Top Bottom