Mbowe arejesha Shangingi la Kiongozi wa Upinzani Bungeni

ili ni bunge la wananchi au bunge la maslahi ya wabunge wa ccm.
point ni kuokoa matumizi ya fedha ya umma hayo mengine sisi hayatuhusu
tunaangalia mtu anafanya nini sio porojo.
kama ni sheria mbaya kulipana mamilioni kwa nini wanashindwa kuibadilisha si walihiweka wao?
 
"Wabunge wote wanaongozwa kwa masharti, Spika ana masharti yake, Kiongozi wa Upinzani Bungeni ana masharti yake na wabunge wengine nao wana masharti yao. Sasa mtu huwezi kukubali masharti fulani na kukataa mengine, huku ni kuvunja sheria."

Joel alisema moja ya masharti aliyopewa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ni kupokea gari la Serikali, dereva na kuwekewa mafuta kwenye gari hilo wakati wa shughuli za Bunge.

"Sasa pamoja na kupewa gari, Ofisi ya Bunge pia inawajibika kisheria kumpa kiongozi huyo nyumba mbili; Dar es Salaam na Dodoma na mlinzi wa kulinda usalama wake wa kila siku," alisema Joel.Aliendelea,"Sasa akisema gari sitaki, huu ni utashi wake, lakini kwa nini akatae gari tu wakati kuna huduma zingine anazopewa?"

CRAp cRApp
naombni cv yake huyu....bila shaka kawekwa kiundugu au ni gamba original
 
Kwani wengine wamelazimishwa kurudisha? Wangelikubali tu na watu wenye pesa kama Nyalandu, Lowassa, Rostam, Rita Mlaki pia wapewe changamoto yakurudisha hayo magari kwani na wao si wanauwezo? Mbona hawatuonei huruma. Naelewa wanaosema sio wabunge wote wataweza kurudisha lakini wengi (hasa wa CCM waliokaa zaidi ya temu moja) wanauwezo tayari. Badala yakumvunja moyo Mbowe wange-challenge wengine warudishe kwa manufaa ya taifa letu. yaani kweli tukipima katika mzani Mbowe kukosa popularity is important than ku-control spending ?? Priorities zetu ziko wapi?
 
OFISI ya Bunge imemtaka Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kususia pia huduma zingine anazopewa na Serikali kulingana na wadhifa wake, badala ya kukataa gari, dereva na mafuta pekee.Akizungumza na gazeti hili mjini hapa jana, Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel alisema huduma zote anazopewa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni zipo kisheria, hivyo hawezi kuchagua masharti anayotaka kuyafuata na mengine kuyakataa.

Huyu kaimu katibu wa bunge anashangaza kweli toka lini entitlements zikawa mashari, hizo ni stahili za hicho cheo na misingi ya mbowe kulikataa hilo shangingi ni ukubwa wa bei yake lakini still ataendelea kutumia gari.

"
Haya ni mambo ya kisiasa na sisi kama watendaji hatutaki kujiingiza kwenye siasa. Lakini niseme tu kwamba, lile gari hakupewa kufanyia shughuli za kisiasa ni la Serikali kwa ajili ya kazi zake kama Kiongozi wa Upinzani Bungeni," alisema Joel na kuongeza:

Huyu jamaa yeye ndiye analeta siasa, kuna tatizo gani kupokea gari na ikiwezekana kumjazisha fomu kwamba amefanya hivyo kwa hiyari yake mwenyewe and then kukaa kimya. Tatizo ninaloliona hapa ni pale huyu John Joel anapotaka kufikiri kwa niaba ya CCM.

"Wabunge wote wanaongozwa kwa masharti, Spika ana masharti yake, Kiongozi wa Upinzani Bungeni ana masharti yake na wabunge wengine nao wana masharti yao. Sasa mtu huwezi kukubali masharti fulani na kukataa mengine, huku ni kuvunja sheria."
Joel alisema moja ya masharti aliyopewa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ni kupokea gari la Serikali, dereva na kuwekewa mafuta kwenye gari hilo wakati wa shughuli za Bunge.

Huyu jamaa vipi hayo si masharti bali stahili, ina maana say Mbowe angeamua kimya kimya kupaki hilo gari na asilitumie angeshtakiwa?

"Sasa pamoja na kupewa gari, Ofisi ya Bunge pia inawajibika kisheria kumpa kiongozi huyo nyumba mbili; Dar es Salaam na Dodoma na mlinzi wa kulinda usalama wake wa kila siku," alisema Joel.Aliendelea,"Sasa akisema gari sitaki, huu ni utashi wake, lakini kwa nini akatae gari tu wakati kuna huduma zingine anazopewa?"

Wewe John Joel acha siasa haya mambo ya nyumba ya Dar na Dodoma yanaingiaje hapa? After all nyumba ni suala nyeti unless kama inalipiwa kama ile aliyokuwa akikaa spila Sitta. All in all gharama ya hizo nyumba (pango) kwa miaka mitano zinaweza zisifike hata hiyo gharama ya huo mgari wenu.

Bunge kuendelea kuwalipa posho
Kuhusu wabunge hao kutochukua posho, Joel alisema posho hizo hazitasitishwa kutolewa kwao hadi utaratibu utakapobadilishwa. "Haya mambo yapo kisheria jamani, nisipowalipa posho mimi nashtakiwa," alisema.

Joel alipuuza madai ya kambi hiyo kutaka kuwe na fomu mbili bungeni; kulipana posho bungeni na fomu ya mahudhurio ili wao wasaini fomu ya mahudhurio tu, wasipewe posho hizo, akisema "Fomu iliyopo ni ya mahudhurio, wanataka fomu gani sasa?.

Yaani nchi hii tuna watendaji wengine bure kabisa, sasa kuna ugumu gani kumpa sekretari kutengeneza hizo fomu? Tatizo ni lile lile kufikiria kwa niaba ya CCM.

… apongezwa kwa kurudisha shangingi

Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila aliunga mkono uamuzi huo na kusema hata katika nchi tajiri viongozi wenye nyadhifa za uwaziri wanatembelea magari ya kawaida.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (UDSM), Dk Benson Bana alisema, Mbowe ana hoja ambayo inapaswa kuungwa mkono na watu wengi wenye kuitakia mema nchi hii. Dk Bana alisema ingawa hoja hiyo inamjenga Mbowe kisiasa, lakini ukweli unabaki kuwa Serikali inatumia fedha

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro alisema kinachofanywa na Mbowe ni propaganda za kisiasa zenye lengo la kumpatia umaarufu.
“Mbowe ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, amepewa gari kwa ajili ya kazi hiyo, anarudisha gari kwa sababu yeye ni tajiri, angekuwa hana uwezo kama wabunge wengine angefanya hivyo?,” alihoji Mtatiro.

Mtatiro alisema Mbowe asijifanye kuwa anawahurumia Watanzania maskini wakati maisha anayoishi ni ya kifahari yasiyofanana na wananchi wa kawaida.

Huyu bwana mdogo yeye ndiye anatafuta huo the so called "umaarufu" Utajiri unaingiaje hapa? Kwani si kila mbunge ana gari hata kama sio kiongozi wa shughuli flani za bunge?

Source: Mwananchi
 
Sijapata kufikiria kwamba siku hizi waajiriwa na serikali ya CCM kiwango cha kufikiri kimeshuka kiasi cha kutotofautisha jitihada za kulijenga taifa letu na chuki binafsi dhidi ya mtu. Kurudisha gari kwa hiari yake na kuwa tayari kutumia mali yake katika shughuli za serikali badala ya kushukuru wanaleta kidada. Miaka 5 naona mbali mno nimeshachoka.
 
CRAp cRApp
naombni cv yake huyu....bila shaka kawekwa kiundugu au ni gamba original

Tanzania nadhani inaweza kuwa ni nchi pekee duniani ambayo inaonena ni KINYUME cha sheria kwa kiongozi kutoishi kwa anasa!
Yaani viongozi wanalizimishwa kupokea malipo wasiyotaka (posho) na kutembelea magari ya kifahari beyond the country's means!
 
Halafu eti yanaitwa masharti!!!
 
Bunge lina point; kwanini kati ya vitu vya kubana matumizi kachagua gari peke yake? Tukumbuke kuwa hoja ya kubana matumizi ilikuwemo kwenye ilani ya Chadema na ilihusisha vitu vingi tu. Lakini ni hki kilichosemwa:
(Chadema) Itapunguza mishahara na posho za viongozi wote wa juu wa kisiasa kuanzia Rais, hadi wakuu wa mikoa kwa asilimia 20. Mishahara na posho za wabunge zitapunguzwa kwa asilimia 15 huku mishara na posho ya watendaji wote na wakuu wa mashirika na taasisi za umma itapunguzwa kwa asilimia 15.

Tufikirie ahadi hii kwa sekunde chache..

Mbunge anapata karibu shilingi 6,915,000 kwa mwezi. Asilimia 15 ya kiasi hiki ni 1,037,250

Haijalishi kiashi kingekatwa wapi (kwa wakati huu) - ingeweza kuwa kwenye mafuta, fedha za posho n.k lakini at the end wabunge wangekatwa hicho kiasi kutoka mishahara yao kwa mwezi.

Kwa wabunge wapatao 350 tu tungeweza kukata 363,037,500 kama tu ingekubaliwa kukatwa asilimia 15 ya mishahara, posho na marupurupu yao mengine. Kwa muda wa mwaka mmoja tu tungeweza kuokoa shilingi 4,356,450,000 (karibu bilioni nne na nusu). Tukumbuke hii ni kwa wabunge tu. Kama gari moja la kifahari lingekuwa linagharibu shilingi milioni 60, fedha hizo peke yake zingetosha kununua magari 73 hivi.

Sasa najiuliza kwanini Chadema hawakugombania kupunguza mishahara na posho zao kwa asilimia 15? Tukumbuke kuwa ahadi yao inamhusu Rais, wakuu wote wa mikoa na viongozi wengine wote wa juu (I presume majaji, wakuu wa majeshi n.k wamo humo) ambao ingepunguzwa kwa asilimia 20 huku watendaji wengine wa umma wa juu mishahara na posho zao zingepunguzwa kwa asilimia 15 vile vile.

Kwanini hawakugombania kubana matumizi kwa kupunguza kwa asilimia mishahara na posho zao?

Hapa ndio utaona pointi ya Bunge, kama gari moja tu kulirudisha inaonekana ni kubana matumizi vipi kuhusu kupewa nyumba mbili, ulinzi n.k? Je gari hilo moja lina gharama kubwa kuliko gharama ya nyumba mbili n.k ambavyo yeye kama KUB anapewa? Kwanini kachagua kurudisha gari na si nyumba moja? Upande mwingine inaweza hata kuulizwa kwanini hakurudisha nyumba zote mbili; si tayari ana nyumba Dar, kwanini apewe nyumba nyingine?

Na hili linakuja pia hata kwenye posho ya vikao - kwanini wanakataa posho ya vikao lakini ya kujikimu, na madudu mengine yenye gharama kubwa wamekubali? Binafsi wangeweza hata kutaka asilimia 25 wapunguzwe kwa watu wabunge wote na hapo ndio tungeona serikali na hata CCM kwa kweli kabisa nadhani wangeweza kukumbatia wazo hilo.

Badala ya kufuta tu au kurudisha magari n.k wagombanie kubana matumizi kwa kupunguza matumizi - hii ndio njia ya kawaida sana katika serikali kufanya, sasa mkishakubaliana kuwa tupunguze matumizi kwa asilimia 20 bila kuwaathiri watu wa kima cha chini, huduma muhimu n.k na mmesema ni kwenye mambo x,y,z kinachofanyika ni makubaliano vyama (bi-partisan negotiation) ambapo mnaaamua ni vitu gani vinapunguzwa at the end everybody is jolly and dundee!

Ukipunguza kitu ambacho hukiitaji in the first place (you can leave without) unaweza vipi kusema kuwa umelipa gharama kidogo ya machungu? Wengi wetu tunapobana matumizi tunajikuta tunatoka nyumba kubwa tunaenda nyumba ndogo (pun not intended)..

Lakini pointi ya pili ya Bunge (ambayo nayo ni valid) ni kuwa kuna vitu ambavyo vimewekwa kisheria na kama vimewekwa kisheria haviondoki tu kwa mtu kuvikataa. Tatizo lililopo kwenye hoja ya Bunge hata hivyo ni kuwa baadhi ya vitu vilivyopo kisheria havilazimishi mtu kuvipokea - yaani sheria haisemi "ni lazima KUB akubali kukaa kwenye nyumba anayopewa, ni lazima achukue mafuta n.k"; na hili linaendana na tatizo jingine kuwa sheria haifanyi kuwa option kwa mtu kukubali perks fulani na kama akikataa perks hizo ziende wapi. Kwa mfano, Serikali itaendelea kutenga posho kwa wabunge wa Chadema - kwani sheria inasema walipwe - sasa wabunge wamekataa hizo fedha zinaenda wapi?

Hivyo, tatizo jingine la Mbowe na hata Zitto kwenye hili ni wao kama wabunge kushindwa kuletwa mswada binafsi wa mabadiliko ya sheria zinazosimamia hizi posho. Kama wabunge hawako tu ili kupinga serikali au kuikosoa jukumu lao la kwanza ni kutunga sheria. Kama baadhi ya posho zipo kisheria then ni jukumu lao kuziondoa kisheria siyo kuzipinga kwa kutumia msimamo wa kimaadili tu. Hivyo, Mbowe alitakiwa kuleta mapendekezo ya sheria ambayo yatamuondolea kiongozi wa upinzani tuzo hizo za magari n.k Sasa sheria ikishindwa kupitishwa au kutoungwa mkono then on moral ground anaweza kukataa perks fulani.

Na hii ina maana kwenye hizo sheria wangeweeza kuweka the "optional clause" or "conscious clause" ili kwamba kama mtu hataki vitu fulani asilazimishwe kufanyiwa based on religious or moral ground.

Ninachoona ni kushindwa kufikiri strategically na methodically kwa baadhi ya viongozi wetu hawa ili kuweza kufikia a desired outcome na badala yake wanafikiria mno kisiasa (political thinking).
 
- Kuhusu MBowe kukataa gari ni haki yake, lakini sio haki ya sheria kumlazimisha Mbowe asichotaka au anachotaka, isipokuwa Mlinzi tu usalama wake kama Kiongozi wa Upinzani hili halina mjadala ni lazima awe na mlinzi wa kutoka Taifa, otherwise serikali sometimes iwe inakubali yaishe kuliko kujivua nguo na hoja hewa kama hizi siasa kuna wakati inafika kwenye dead end kama kwenye hii ishu ya Mbowe na gari!

- HOWEVER: Ushauri wangu kwa Chadema ni kwamba unganisheni nguvu jamani, sasa hizi hoja mara ni hoja ya Zitto, mara hoja ya Slaa, na sasa ya Mbowe, ifike mahali ziwe ni hoja za chama Chadema Collectivelly badala ya indivividual ni ushauri wa bure tu, Chama kiwe mbele kuliko majina majina wananchi wa Tanzania tumechoshwa na siasa za majina ambazo ndio zimelifikisha taifa hapa tulipo, yaani pabaya sana!

- Much Respect!

Willie @ NYC, USA.
 
aise Mtatiro ana hoja hapa
na we tulia. Kama utajiri si wake? Kwa hiyo kama angekuwa masikini ndio achukue shangingi? Na toto la mafisadi aka pinda si aliwahi kukataa shangingi? Mbona huyo kiherehere wa bunge hatukumsikia akimponda? Angalieni mnajidhalilisha hivihivi.
 
"Politics comes from the Greek word poly, meaning many, and ticks meaning blood sucking parasites". Watch out
 
Kwani kupewa gari na masufu mengine ni masharti au privileges? Hawa wataalamu wetu wa serikali nao bwana!!
 
OFISI ya Bunge imemtaka Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kususia pia huduma zingine anazopewa na Serikali kulingana na wadhifa wake, badala ya kukataa gari, dereva na mafuta pekee.Akizungumza na gazeti hili mjini hapa jana, Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel alisema huduma zote anazopewa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni zipo kisheria, hivyo hawezi kuchagua masharti anayotaka kuyafuata na mengine kuyakataa."Haya ni mambo ya kisiasa na sisi kama watendaji hatutaki kujiingiza kwenye siasa. Lakini niseme tu kwamba, lile gari hakupewa kufanyia shughuli za kisiasa ni la Serikali kwa ajili ya kazi zake kama Kiongozi wa Upinzani Bungeni," alisema Joel na kuongeza:"Wabunge wote wanaongozwa kwa masharti, Spika ana masharti yake, Kiongozi wa Upinzani Bungeni ana masharti yake na wabunge wengine nao wana masharti yao. Sasa mtu huwezi kukubali masharti fulani na kukataa mengine, huku ni kuvunja sheria."Joel alisema moja ya masharti aliyopewa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ni kupokea gari la Serikali, dereva na kuwekewa mafuta kwenye gari hilo wakati wa shughuli za Bunge."Sasa pamoja na kupewa gari, Ofisi ya Bunge pia inawajibika kisheria kumpa kiongozi huyo nyumba mbili; Dar es Salaam na Dodoma na mlinzi wa kulinda usalama wake wa kila siku," alisema Joel.Aliendelea,"Sasa akisema gari sitaki, huu ni utashi wake, lakini kwa nini akatae gari tu wakati kuna huduma zingine anazopewa?"Bunge kuendelea kuwalipa poshoKuhusu wabunge hao kutochukua posho, Joel alisema posho hizo hazitasitishwa kutolewa kwao hadi utaratibu utakapobadilishwa. "Haya mambo yapo kisheria jamani, nisipowalipa posho mimi nashtakiwa," alisema.Joel alipuuza madai ya kambi hiyo kutaka kuwe na fomu mbili bungeni; kulipana posho bungeni na fomu ya mahudhurio ili wao wasaini fomu ya mahudhurio tu, wasipewe posho hizo, akisema "Fomu iliyopo ni ya mahudhurio, wanataka fomu gani sasa?.… apongezwa kwa kurudisha shangingiMwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila aliunga mkono uamuzi huo na kusema hata katika nchi tajiri viongozi wenye nyadhifa za uwaziri wanatembelea magari ya kawaida.Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (UDSM), Dk Benson Bana alisema, Mbowe ana hoja ambayo inapaswa kuungwa mkono na watu wengi wenye kuitakia mema nchi hii. Dk Bana alisema ingawa hoja hiyo inamjenga Mbowe kisiasa, lakini ukweli unabaki kuwa Serikali inatumia fedha Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro alisema kinachofanywa na Mbowe ni propaganda za kisiasa zenye lengo la kumpatia umaarufu."Mbowe ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, amepewa gari kwa ajili ya kazi hiyo, anarudisha gari kwa sababu yeye ni tajiri, angekuwa hana uwezo kama wabunge wengine angefanya hivyo?," alihoji Mtatiro.Mtatiro alisema Mbowe asijifanye kuwa anawahurumia Watanzania maskini wakati maisha anayoishi ni ya kifahari yasiyofanana na wananchi wa kawaida.Source: Mwananchi
Aisee,hivi tangu lini mchungaji akamlazimisha ng'ombe wake kunywa maji?Kazi yake ni kumfikisha mtoni,basi inatosha!Huyu watumishi wa bunge,wanamlazimisha Mbowe achukue gari! Km ni sheria si wampeleke mahakamani kwa kukataa gari?au nao wanatafuta umaarufu kupitia hapo? mbona hata pinda alikataa shangingi mpwa lakini hakulazimiswa?
 
huyu mwalimu ni njaa kinoma....af hajijui kama kawekwa pale cuf ili kukifanya chama kionekane hakina mlengo wa kiislam......akiwapa mgongo wanamcheka kinoma......chuo tulimzingua sana huyu bw mdogo...
 
Hamna ubunifu babuwee, vitendo vya kukataa gari kavianza Pinda. HeEeeeee! Ishakuwa sera kwenu?
hata kama kaanza huyo jamaa, mbona hatukumsikia kiherehere yoyote akisema pinda kavunja sheria? Na akatae na stahiki zingine basi
 
OFISI ya Bunge imemtaka Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kususia pia huduma zingine anazopewa na Serikali kulingana na wadhifa wake, badala ya kukataa gari, dereva na mafuta pekee.Akizungumza na gazeti hili mjini hapa jana, Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel alisema huduma zote anazopewa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni zipo kisheria, hivyo hawezi kuchagua masharti anayotaka kuyafuata na mengine kuyakataa.

"Haya ni mambo ya kisiasa na sisi kama watendaji hatutaki kujiingiza kwenye siasa. Lakini niseme tu kwamba, lile gari hakupewa kufanyia shughuli za kisiasa ni la Serikali kwa ajili ya kazi zake kama Kiongozi wa Upinzani Bungeni," alisema Joel na kuongeza:

"Wabunge wote wanaongozwa kwa masharti, Spika ana masharti yake, Kiongozi wa Upinzani Bungeni ana masharti yake na wabunge wengine nao wana masharti yao. Sasa mtu huwezi kukubali masharti fulani na kukataa mengine, huku ni kuvunja sheria."

Joel alisema moja ya masharti aliyopewa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ni kupokea gari la Serikali, dereva na kuwekewa mafuta kwenye gari hilo wakati wa shughuli za Bunge.

"Sasa pamoja na kupewa gari, Ofisi ya Bunge pia inawajibika kisheria kumpa kiongozi huyo nyumba mbili; Dar es Salaam na Dodoma na mlinzi wa kulinda usalama wake wa kila siku," alisema Joel.Aliendelea,"Sasa akisema gari sitaki, huu ni utashi wake, lakini kwa nini akatae gari tu wakati kuna huduma zingine anazopewa?"

Bunge kuendelea kuwalipa posho
Kuhusu wabunge hao kutochukua posho, Joel alisema posho hizo hazitasitishwa kutolewa kwao hadi utaratibu utakapobadilishwa. "Haya mambo yapo kisheria jamani, nisipowalipa posho mimi nashtakiwa," alisema.

Joel alipuuza madai ya kambi hiyo kutaka kuwe na fomu mbili bungeni; kulipana posho bungeni na fomu ya mahudhurio ili wao wasaini fomu ya mahudhurio tu, wasipewe posho hizo, akisema "Fomu iliyopo ni ya mahudhurio, wanataka fomu gani sasa?.

… apongezwa kwa kurudisha shangingi

Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila aliunga mkono uamuzi huo na kusema hata katika nchi tajiri viongozi wenye nyadhifa za uwaziri wanatembelea magari ya kawaida.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (UDSM), Dk Benson Bana alisema, Mbowe ana hoja ambayo inapaswa kuungwa mkono na watu wengi wenye kuitakia mema nchi hii. Dk Bana alisema ingawa hoja hiyo inamjenga Mbowe kisiasa, lakini ukweli unabaki kuwa Serikali inatumia fedha

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro alisema kinachofanywa na Mbowe ni propaganda za kisiasa zenye lengo la kumpatia umaarufu.
“Mbowe ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, amepewa gari kwa ajili ya kazi hiyo, anarudisha gari kwa sababu yeye ni tajiri, angekuwa hana uwezo kama wabunge wengine angefanya hivyo?,” alihoji Mtatiro.

Mtatiro alisema Mbowe asijifanye kuwa anawahurumia Watanzania maskini wakati maisha anayoishi ni ya kifahari yasiyofanana na wananchi wa kawaida.

Source: Mwananchi

Kwa hiyo wananchi ambao hawajui leo watapata mkate wa kulisha watoto, lakini bado wanakamuliwa na hao viongozi wetu. Nyumba mbili magari ya kifahari, posho za kila vikao kwa pesa za walala hoi na madeni ambayo tunawaachia watoto wetu. Je kweli kuna kiongozi yeyote
ambaye anaweza kusimama na kusema ni mzalendo?

Hii nchi sasa imekuwa ya kisanii, hayamkini ndo kwa maana Rais wetu yuko safari kila siku bado anadhania ni waziri wa mambo ya nje hii ni aibu kubwa kwake na hata kwa washauri wake wote katika idara zote zinazo mshauri.

Ushauri wangu kwa hawa wakuu wetu, ni kwamba wasome nyakati hatukumtegemea rais kama Mbaraka atafikishwa mahala alipofikia.Rekodi zao zinawekwa upepo ukigeuka watajutia haya wanayofanya kwa sasa. Viongozi wamelewa madaraka hawakumbuki wapo leo na kesho hawapo. wanahatarisha familia zao huko tunakoelekea kuna familia zitakimbilia uhamishoni. Jifunzeni kwa kina Mobutu, washauri wengine mko humu kwenye hili jamvi someni maoni ya watanzania mshaurini vizuri kiongozi wetu msikalie kujaza taarifa za watoa maoni humu kwenye majarada yenu hilo halitasaidia hali ya hewa ikichafuka (heri kuzuiz kuliko kuponya, ukiponya kidonda kovu litabakia itakuwa ni alalma ya kumbukumbu).

Kushindwa kwa rais ni kushindwa kwenu nyote. Umma utawalaumu collectively. Mbona hata aibu kidogo haipo je kweli kuna serikali au mko likizo ili kijulikane kitu kimoja.
 
Mimi naona ungeandikwa muswaada (bipartisan) kuhusu hizi posho,uwe crafted na watu waliobobea kwenye mambo ya sheria na uchumi halafu ukawa lobbied kwa wabunge ambao wako influencial kama mbowe,mnyika,zitto,mdee,january,jussa,hamad and the like.
Kuna watu kama kina chiume n.k ambao wana lobbying companies,au watu wengine ambao wapo kwenye NGOs mbalimbali.Wabunge mara nyingi husukumwa na lobbyists,badala ya kulobby kwa ajili ya Barrick(even though they pay good for it),tunaweza tukaandika muswaada wa kufuta posho za viongozi wa serikali na ku-lobby huo muswaada.
For the time being,ningeshauri wabunge ambao wako tayari kujitolea posho zao kwenye majimbo au NGOs zao (especially wale wa viti maalum/kuteuliwa) wafanye hivyo kwa ku-instruct bank zao (kama wana direct deposit) ku-redirect some percentage to their cause.Kwani bila hivyo tutakuwa tunawaingilia na ku-complicate kazi za wahasibu wa bunge kwani wao wana directives ambazo wanahitaji ku fulfill.
Nkumbuka hadi leo,marehemu Sokoine kwenye hotuba yake ya bunge ya 1982 or 83 alijitolea sehemu ya mshahara wake na kuwashauri wabunge wengine wafanye hivyo,na alikuwa analipwa less than 4,000shs as a salary.
Kama kuna mtu atawachezea hiyo tape ambayo nadhani either RTD au Xinhua watakuwa nayo kwenye archives zao,ingewaaibisha sana hawa wahuni.Mimi ni CCM damu,ila hapa asilimia mia moja nipo na CDM.
 
Katibu wa Bunge kaongea baloney, mara anasema angetegemea Mbowe akatae mafao yote mara anadai yapo kwa mujibu wa sheria, ina maana angekataa mafao yote angekubaliwa? Ridiculous.
 
Pinda alitangaza kukataa gari la kifahari wapuuzi walimpongeza, ingawa magari hayo hayo aliyotangaza kayakataa bado anayatumia, Je Pinda hakuwa anataka cheap popularity?

Kikubwa nionavyo ni wapinzani kama kweli wako serious wapeleka mswada wa kambi ya upinzani wa kuondoa baadhi ya posho, kuweka viwango vipya vya posho, mishahara yao na viongozi wengine ikatwe kodi, nk.
Bila kupeleka mswada wa kisheria kwa vile mambo karibu yote yako kisheria basi binafsi wanachosema na kufanya ni yale yale kama ya Pinda ya kutafuta kupata 'cheap popularity' , hivyo ni unafiki tu wa kisiasa hamna lolote
 
Mimi naona ungeandikwa muswaada (bipartisan) kuhusu hizi posho,uwe crafted na watu waliobobea kwenye mambo ya sheria na uchumi halafu ukawa lobbied kwa wabunge ambao wako influencial kama mbowe,mnyika,zitto,mdee,january,jussa,hamad and the like.
Kuna watu kama kina chiume n.k ambao wana lobbying companies,au watu wengine ambao wapo kwenye NGOs mbalimbali.Wabunge mara nyingi husukumwa na lobbyists,badala ya kulobby kwa ajili ya Barrick(even though they pay good for it),tunaweza tukaandika muswaada wa kufuta posho za viongozi wa serikali na ku-lobby huo muswaada.
For the time being,ningeshauri wabunge ambao wako tayari kujitolea posho zao kwenye majimbo au NGOs zao (especially wale wa viti maalum/kuteuliwa) wafanye hivyo kwa ku-instruct bank zao (kama wana direct deposit) ku-redirect some percentage to their cause.Kwani bila hivyo tutakuwa tunawaingilia na ku-complicate kazi za wahasibu wa bunge kwani wao wana directives ambazo wanahitaji ku fulfill.
Nkumbuka hadi leo,marehemu Sokoine kwenye hotuba yake ya bunge ya 1982 or 83 alijitolea sehemu ya mshahara wake na kuwashauri wabunge wengine wafanye hivyo,na alikuwa analipwa less than 4,000shs as a salary.
Kama kuna mtu atawachezea hiyo tape ambayo nadhani either RTD au Xinhua watakuwa nayo kwenye archives zao,ingewaaibisha sana hawa wahuni.Mimi ni CCM damu,ila hapa asilimia mia moja nipo na CDM.

Kobello acha hivyo.. binafsi kukataa hizo posho hivi hivi ni kutokuwa wabunivu.

Chadema ina wabunge 47? x 80,000 =3,760,000 kwa siku

Kwa muda wa miezi hii mitatu ya bunge la bajeti (siku karibu tisini) = 338,400,000

Naomba mniambie Chadema haikuwa na fikra za kuona jinsi gani fedha hizo badala ya kuwanufaisha wao binafsi zingeweza kusaidia chama - say Kujenga Makao Makuu Mapya? c'mmon.. au kama hawataki kunufaisha chama wangeziweka kwenye akaunti ambayo ingekuwa ni "Foundation ya Chadema" kusaidia katika mambo mbalimbali ya kijamii?

I'm sorry guys.. not strategic thinking. Kubana matumizi siyo sawasawa na kutotumia kwa hekima. Mtu anaweza kubana matumizi na kile alichobakia nacho bado kikawa kinatumika bila hekima.
 
Back
Top Bottom