Mbowe Aombe Radhi Kukubali Mwaliko wa Dhifa ya Obama; Inadhoofisha Harakati za Kuiondoa CCM

Nitaendelea kusema mpaka mwisho na wala sitabadili msimamo wangu kwamba:

Freeman Mbowe For Chadema Chairman 2013
Dr Wilbroad Slaa For Presidency 2015.

Hizi kauli zako mkuu huwa hazipendezi..!Wewe ndiye demokrasia mwenyewe?
 
Ukitaja VIONGOZI wanne wakubwa kabisa kwenye Bunge la Tanzania KUB Mbowe yumo. Wengine ni Spika na Naibu wake na Waziri Mkuu. Halafu akose dhifa kama hii!

Ni vizuri tukakumbuka pia kwamba CHADEMA wamesusa mengi mle Bungeni na Kitaifa. Yamewafikisha wapi?

WildCard naomba nsaidie KUB maana yake nini?
 
Last edited by a moderator:
Naikubali sana Chadema na uongozi wao kiujumla na sio siri ni chama nilichodhani kipo kwa ajili ya maslahi ya watanzania.serikali imesababisha mauaji ya wafuasi wako na bila mkuu wa nchi kufanya ulichotaka afanye ili ukweli uwe bayana leo hii kwa kuwa waliopoteza maisha hawakuwa ndugu zako umesahau umeenda kunywa wine na hiyo serikali.ingetokea nyumba yako imelipuliwa watoto wako wamekufa ungeenda kufurahi ikulu???mnacheza tu na akili za watanzania kumbe?Mbowe hufai na umenipa mashaka na chama chako.kwa hili kama mtanzania niliyewakubali sana mtupe maelezo kinyume cha hapo mnatafuta tu madaraka kama maccm

Bora wewe umeanza kuhisihisi ni ngumu sana kumpata mbadala wa ccm japo imechokwa.
 
wewe unaejitia mwanakijiji sijui ni wa kijiji gani cha upofu wa nadharia ya siasa. Maoni yako yana kiburi cha ujuwaji mkubwa kwa kuamsha hamasa za misleading attitude kwa hao wanaokufuata. Nimesema mwanzo watu wa jamii yako munalipeka taifa katika dimbwi la machafuko kwa kuongozwa na hamasa na kukosa hekima na ukomavu wa uwezo wa kufikiri. hizi hadithi za kuunganisha unganisha na kuzipa legitimacy inaonenya wazi umahiri wa siasa za kukomoana na majungu. Kuhudhuria kwa Mbowe kumepunguza nini harakati za CDM katika kuleta mabadiliko ya historia ya kweli? Hivi angeligoma kwenda ingelisaidia nini katika harakati za mabadiliko nchini? mchamba kiwngi huondoka na kinyesi mikononi ndio haya maoni yako na mengi tu yasio na mguu wala mkono. Wito kwa uongozi wa CDM, fanyeni mema kwa best interest of the nation, ukomavu wa kisiasa ni kujijenga na kuhakikisha hekima inatawala, siasa za kugomea, kununa, na kutunga tunga nadharia potofu kujstify UPUUZI haziwe kuwa ndio misingi ya msukumo wenu wa kukubalika na kukubaliwa na wananchi kama maturity ya uongozi. Maadui wakubwa waliopigana na kutoana damu wanakaa meza moja na kuwekeana heshima ya kukubali kutafautiana itakuwa nyinyi? Mwanakijiji rudi kijijini siasa huiwezi, hizi tamthilia zako ndizo ziliopeleka afrika ikatawa colonized bila ya kujijua.
Tulia kidogo, pata funda tatu za maji na kijiko cha asali. Jazba ni silaha dhaifu sana katika mapambano ya hoja.

Nilitegemea ungeshambulia hoja ili kudhihirisha 'upuuzi' kwa namna tofauti.
Nilitegemea uje na kauli za ku-justify kile unachodhani ni sahihi.
Na sikutegemea ushambulie watu badala ya hoja.
Tafadhali jikite katika hoja.

Umezungumzia the best interest of the nation, nadhani hoja yenyewe ni kwa the best interest of the nation.
Mbowe ni KUB hadi sasa ni kiongozi kwasababu ana kundi la wananchi wapatao asilimia zaidi ya 40 kwa kigezo cha kura.

Kwa msingi huo yeye ni 'person of national interest' na hivvo kila afanyalo lina reflect national interest kwasababu limefanywa na mtu ambaye ni 'national interest'
Foum Jnr, unaweza kutueleza nini kimetokea kukawa na communication breakdown kati ya Mbowe na Dr Salaa
-Unaweza kutueleza mwaliko wa Mbowe ulikuwa kama KUB,Businessman au friend of America consulate
-Unaweza kutueleza yeye akiwa kama KUB, ni protocol gani ilitumika kualikwa na state dept nje ya utaratibu wa nchi husika
-Unaweza kutueleza yeye kama KUB kwanini hakuwepo katika protocal na je hilo ni sahihi?
-Unaweza kutueleza kwanini waliacha kuhudhuria bajeti ambayo ni jambo la nationa interest na kuhudhuria dhifa ambayo ni national interest pia. Wapi mpaka wa national interest unaanzia na wapi unaishia.

Hebu tuanzie hapo maana yapo mengi yatokanayo.
 
Last edited by a moderator:
wewe ni mpuuzi.

Mbowe-lowasa-july3-2013.jpg
 
Pia sisi Tumesoma post yenu hapo juu,Je ni wapi au kaombea wapi hiyo Radhi na kupitia Media gani? Unajuwa hiyo si post nzuri hasa unapoandika Post za visa namna hii,kwa kuwa unamgwaya huyo Mbowe ila tunajuwa ni Kiongozi Bora,wa muda muafaka na kwa Taifa lililodidimia Kielimu,Kikazi na Kimaadili,licha ya chama Tawala kuamua kuuwa Upinzani kwa gharama kuuuuubwa isiyo na mfano kwa Taifa hili na mengine,huku ikipandisha Gharama za maisha kumkandamiza Mtu mwenye kipato duni,Masikini,post mambo ya maana si hili,Umetumwa tu
 
This was the right moment CDM kuonyesha kuwa mambo si kama wanavyodhani. Waliuliza makusudi wakijua hali iliyopo.

Kwa mantiki hiyo Mbowe alipelekewa sms! humiliation.

Hakuna msamaha na hili lazima awajibike. Mbowe atoke na kuomba radhi au apishe watu wengine.

Ampishe nani...na kwa faida ya nani...wahusika nini sisi wanachama na bado tunamuhitaji sana mwenyekiti wetu ....wewe nimegundua ni buku saba project
 
Hawa jamaa wanaongozwa kama misukule tu ndio maana hawajui hata kinachoendelea, Mbowe anapiga deals tu pale


Mkuu watu wanajadili hapa mambo ya afya naona wewe unakuja kima------ ma------, nashindwa kuelewa kama kweli wewe ulikuwamwenyekiti wa CDM naona uwezo wako wa kujadili kujua mambo ni mwembamba sana.
 
WanaJF!

Mawasiliano katika organaizesheni yoyote, kama ilivyo CHADEMA, ni jambo la muhimu sana. Kwani mawasiliano ndio yenye kuleta hali ya kuhabarishana na kufanya kila mmoja kwenye organaizesheni kujua nini kinaendelea kwa wakati huo ama kitakacho endelea kwa wakati ujao.

Kwa bahati mbaya kwa CHADEMA, mawasiliano sio jambo lililopewa uzito unao stahili. Kwani tumekuwa tukisikia matamko na misimamo tofauti tofauti kati ya viongozi na viongozi. Jambo hili ni hasara kubwa kwa CHADEMA.

Hivi karibuni katika ujio wa Obama, Dr Slaa kama katibu mkuu wa CHADEMA alitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa CHADEMA haitashiriki. Tena alilisema hili kwa msisitizo kuwa, wao kama chama kikuu cha upinzani hakijapata mualiko hivyo hawawezi (akimaanisha viongozi wa CHADEMA) kushiriki kwa namna yoyote ile.

Lakini kama tujuavyo, mhe Mbowe kama mwenyekiti wa CHADEMA na mbunge wa Hai, ambazo nafasi hizi zimemfanya awe kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni (KUB), yeye alijumuika ipasavyo kwenye dhifa iliyo andaliwa na serikali ya CCM.

Mbowe-lowasa-july3-2013.jpg Mbowe akiwa kwenye dhifa ya serikali Ikulu.

Aidha, mualiko wa mhe Mbowe umetolewa na Ikulu kupitia ofisi ya spika wa bunge, kwa heshima ya nafasi yake hiyo ya kuongoza kambi ya upinzani bungeni, mhe Mbowe kiprotokia anapaswa kushiriki kwenye dhifa ya serikali..

Kwa hali hiyo basi, Mbowe kama mwenyekiti wa CHADEMA alipaswa afanye mawasiliano na Dr Slaa kama katibu wake, ili amueleze juu ya mualiko alioupokea kutoka Ikulu kupitia kwa spika wa bunge, mama Anne Makinda.

Kama Mbowe angefanya mawasiliano na Dr Slaa kwa wakati, hii ingemsaidia sana Dr Slaa katika taarifa yake kwa vyombo vya habari juu ya ushiriki wa CHADEMA,na pia ingemuepusha Dr Slaa asiweze kuabika na kudhalilika kwa kutoa taarifa zinazo kinzana na uhalisia.

Freeman-Mbowe-Dk.-Slaa.jpg Mbowe akiwa ana fafanua jambo.

Kwani ingemuwezesha zaidi Dr Slaa kuweza kufafanua namna ambavyo CHADEMA itashiriki kwenye ujio wa Obama. Nayo si njia nyingine bali ni njia ya kumtumia Kiongozi wa Upinzani Bungeni (KUB) ambae ni mwenyekiti wa CHADEMA taifa.

Ilipaswa iwe hivi, Dr Slaa aliposema CHADEMA haitashiriki alikosea, alipaswa aseme CHADEMA itashiriki, lakini kwa kupitia bungeni kwa kumtumia kiongozi wa upinzani bungeni.

Lakini lawama hapaswi kupewa Dr Slaa, lawama zote aelekezewe mhe Mbowe, kwani yeye ndiye alikuwa na mwaliko kwa muda mrefu kutoka kwa spika, lakini alishindwa kumuharifu katibu mkuu wake. Hapa ndipo tunaona mapungufu ya Mbowe.

Kwa muktadha huu; ni dhahiri kuwa CHADEMA bado hakijajipanga, hivyo ni chama kichanga kuweza kuhimili changamoto za nchi. Na ni kweli wenda CCM imechokwa na wananchi, ila inabidi CCM iendelee tu kuongoza, kwani bado hakijapatikana chama mbadala wake hapa nchini.
 
Back
Top Bottom