Mbowe Aombe Radhi Kukubali Mwaliko wa Dhifa ya Obama; Inadhoofisha Harakati za Kuiondoa CCM

Kalaghabaho.



This was an own goal, you cannot explain that any way you cut it, unless as a blunder.



Hapa Waswahili ndipo walipopatungia methali ya "Kipendacho roho, hula nyama mbichi".



This is called "wishy washy fence sitting".



This is called "gradual justification". Unaanza ku justify mambo polepole ili kesho keshokutwa ukijikuta huna jinsi uweze kesema "nilishasema sio kitu cha ajabu".

Labda sio kitu cha ajabu.

Kitu cha ajabu ni jinsi CHADEMA kinavyozidi kuendelea kujinadi kama "Chama Cha Demokrasia na Maendeleo" kwa kuongozwa na watu kama hawa ambao basic organization tu inawashinda.

Asante kwa "misemo"...
 
Mwalimu, kwa taarifa zilizopo na zenye utata lakini kutoka katika vyanzo vya CDM ni kuwa Mbowe alipewa mwaliko saa 5 asubuhi kwa shinikizo la Marekani.
Kwamba hata alipofika viwanja vya Ikulu alitumiwa ujumbe aingie ndani haraka jambo lililowakera mawaziri wa JK

Now this is interesting....

Kwa nini walishinikiza ahudhurie kwenye dhifa ile wakati muandaaji wa karamu mwenyewe hakutoa mwaliko?? Dhumuni la kutaka ahudhurie ilikuwa kufanya mazungumzo naye au ilikuwa ni ishu ya PR tu? Kama ni mazungumzo wamezungumza nini?

Ingekuwa mimi ningechimba kupata maswali ya majibu haya kabla sijatoa hukumu...
 
Lakini leo wako tayari ku-compromise kwa kuacha kuomboleza vifo vya makamanda wenzao na kwenda kunywa togwa na wale wale wanaowatuhumu kuhusika na mauaji ya makamanda wenzao.

Makamanda wengine wako lupango kwa tuhuma ambazo Chadema inadai ni za kutunga.

Makamanda wengine wameshtakiwa na makosa ya ugaidi (a serious crime) ambayo yanadaiwa ni ya kutengeneza.

These are the priority issues which Chadema should deal with na siyo tafrija kwa kiini cha utaifa.

Kamanda mkuu anayevaa kombati na kwenda kujumuika kwenye tafrija na adui yake mkubwa lazima atakuwa anawa-betray wapiganaji wenzake. Atakuwa anapunguza morali na commitment ya wapiganaji wenzake wanaoamini kuwa hakuna kulala mpaka kieleweke aka hakuna compromise mpaka kieleweke.
Thank you sir!
 
Mwalimu;6779546]Now this is interesting....

Kwa nini walishinikiza ahudhurie kwenye dhifa ile wakati muandaaji wa karamu mwenyewe hakutoa mwaliko?? Dhumuni la kutaka ahudhurie ilikuwa kufanya mazungumzo naye au ilikuwa ni ishu ya PR tu? Kama ni mazungumzo wamezungumza nini? Ingekuwa mimi ningechimba kupata maswali ya majibu haya kabla sijatoa hukumu...
Mwalimu, mwaliko wasaa 5 na kutumiwa ujumbe aingie siyo maneno yangu, ni kauli za viongozi wa CDM na kunukuliwa na gazeti.
Kwamba kuna uhakika wa maneno hayo linabaki swali la kujiuliza kwasababu tangu kashfa ya Togwa ilipoibuka kuna mkanganyiko the least to say.

Lakini pia lazima tujiulize, kiongozi wa upinzani bungeni, Mbunge na Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani hivi kweli anaweza kutumiwa ujumbe wa 'dharura kwenda kwenye togwa' na yeye akaitikia.
Mimi ukiniletea kadi ya send off less than 24 sihudhurii. Sasa huyu KUB mwenye majukumu ya kitaifa na kimataifa leo amepata dharura ya Togwa, serious, real! Hebu msome EMT nilliyemnukuu hapo juu halafu ujiridhishe na busara za KUB
 
USIKATAE WITO, KATAA NENO!
Wito uliitikiwa vizuri na Mhe. Mbowe, suala la kujiuliza ni je kilichoongelewa kule ni kwa faida ya watanzania wote wapenda demokrasia na maendeleo au ni mikakati ya ukandamizaji wa serikali ya magamba? Naamini Ugeni haukuwa kwa ajili ya mafisadi, ulikuwa kwa ajili ya watanzania wote, sasa sisi wapinga ufisadi, kama Mh. Mbowe asingeenda tungekuwa tumewakilishwa na nani.
Bro Mbowe uko sahihi kabisa.
 
On the one hand, kwa chama tawala (sio tu Tanzania bali katika taifa lolote lile), kitendo cha kutomwalika kiongozi wa upinzani kwenye 'state banquet' ni "political immaturity";

On the other hand, kwa kiongozi wa upinzani katika nchi inayoendelea kupambana na uhaba wa ideal liberal democracy (e.g Tanzania), kukataa mwaliko wa a state banquet is "political maturity";

Swali linalofuata ni je, among the two, nani ni matured na nani immature? Na katika hili, who has gained a political mileage - is it the matured or the immature?

Mpaka hapa nadhani ni rahisi kuona kwamba hoja za mzee mwanakijiji, nguruvi3 pamoja na wale wanaowaunga mkono kuhusiana na suala zima la ujio wa rais of the free world (Obama), zina mashiko depending unachagua kuwa upande upi wa hoja kwani hoja zipo very objective especially in the context of the double edged sword narrative yangu hapo juu, tatizo, wale wenye counter arguments wanaegemea zaidi kwenye hoja subjective;

That said and done, niseme mambo matatu ya mwisho kama ifuatavyo:

Kwanza, ni muhimu kwa pande zote mbili za hoja zikatambua kwamba a state banquet is a public event, a state banquet is not a private event na ndio maana tumeona mambo kadhaa yanayo husisha fedha za walipa kodi yakitolewa maelezo katika dhifa ile; Kwa maana hii, expression of public sentiments hata on a one on one basis (mfano mbowe kutumia fursa hiyo kuzungumza na Obama au wasaidizi wake in private) ni sawa;Swali linalofuatia ni je - Mbowe alitumia fursa hiyo?

Pili, hoja kwamba Mbowe alialikwa kama KUB na sio kiongozi wa chadema inawezekana ina mashiko lakini inapwaya kwa sababu moja kuu ambayo ni kwamba - tumeshuhudia jinsi gani ndani ya bunge chadema imepigania kufa na kupona kudai haki yake ya kuwa ndio chama kikuu cha upinzania bungeni, hence kuwa synonymous na KUB kwa hoja zenye mashiko na zisizo legelegeo; Sasa viongozi wa chadema kutenga Chadema na KUB kwa madhumuni ya kisiasa, hasa kukingia kifua maamuzi ya kukubali mwaliko wa ikulu, ni tatizo;

Tatu na mwisho, last minute invitation of the opposition leader or KUB for thay matter katika muktadha wa itifaki za nchi ni one of the worse protocol blunders than can happen in any country na ilitakiwa uongozi wa chadema ulikemee hilo pale pale na kutaka mkuu wa itifaki apewe onyo kali, lakini kama anavyojadili nguruvi3, chadema imeshindwa kutenganisha dhana na uongozi na dhana ya kiongozi/viongozi;Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Mkuu Mchambuzi, kitendo cha serikali kutoalika wapinzani siyo political immaturity ni dharau kwa kujua udhaifu wa wapinzani.

Serikali inajua kuwa wapinzani 'wata compromise' nayo kwasababu historia inaonyesha wao kuwa wadhaifu katika eneo hilo.

Kitendo cha CDM kuhudhuria Togwa katika hostile political atmosphere tuliyo nayo ni political blunder and immaturity.

Kitendo cha CDM kuhudhuria dhifa badala ya kutumia dhifa hiyo kueleza hisia zao ni political immaturity ya kiwango bora sana. Hiyo ilikuwa golden chance ya kuwaheshimu waliofariki, kutetea walioko magereza na kuuambia ulimwengu kuhusu hali mbaya ya kisiasa iliyopo nchini ikiwa ni pamoja na uonevu, ukandamizaji na udhalilishwaji.
Dunia ingesikia kuna watu wamegomea dhifa ya 'anointed One' ingekuwa news.

George Bush alipokwenda Iraq dunia haikuangalia walikufa askari na wananchi wangapi, dunia ilijadili Bush kukoswa na kiatu na kuanzia hapo kila mmoja alijuiliza hivi imefikia mahali rais wa Marekani anakwepa buti! kuna nini?

Mbowe alikuwa na opportunity ya kukacha na kuwa news, hakuitumia.

Kuhusu CDM kutenganisha kati ya KUB na CDM, hili linafanyika makusudi ili kuondoa aibu ya viongozi kutowasiliana.

Kwamba Dr Slaa ni CDM na Mbowe ni KUB. How possible could that be.
Hoja hapa ni kuwa CDM walialikwa, kukawa hakuna mawasiliano kwasababu mtendaji hana taarifa na mwenyekiti akatumiwa ujumbe haraka na bila kutafakari majukumu aliyo nayo na heshima yake katika ujumbe wa chini ya masaa 10 yeye aliona bora atimkie Ikulu.

Hakuna kupwaya ni jitihada za kuupumbaza umma kuwa Katibu mkuu wa CDM na KUB wanafanya kazi tofauti hata kama KUB ni mwenyekiti

Kuhusu kutumia nafasi ya dhifa, nakuhakikishia kuwa dhifa za kitaifa ni sehemu za kujenga PR. Watu kufahamiana na kuweka mawasiliano. Mbaya sana kwa ziara ya Obama kama ulivyoona hata mawaziri wakuu wastaafu kama akina Salim Ahmed walikuwa na nafasi ndogo sana ya kuongea naye.

Sidhani kama Mbowe alikuwa na fursa hiyo kwa namna yoyote ingawa tunaaminishwa hivyo.
Pale ilikuwa PR na togwa, kushikana mikono, hi,hallo, longtime, please etc

Hoja hapa ni kuwa Mbowe aliweka interest zake mbele kwa gharama ya chama.
1. Kusahau majukumu ya chama katika nyakati nzito kama hizi(vifo, ukandamizaji, uonevu na udhalilishwaji)

2. Kutokuwa na mawasiliano na viongozi wenzake kulikozua mtafaruku na hadi sasa hakuna maelezo ya maana

3.Kukidhalililisha chama kwa kukubali mwaliko ambao hata send off mtu asingekwenda (less than 10 hrs)

4. Kudumaza jitihada za ukombozi na kupeleka mixed signal kwa wapambanaji

5. Kuonyesha udhaifu wa ku-compromise wakati anatakiwa aongoze mapambano

6. Kushindwa kutumia fursa iliyojitokeza kuelezea hisia za umma.

Je, huo ndio mwisho wa dunia? Hapana. Je, kuna anachoweza kufanya? ndio ! ajitokeze aombe radhi, au atetee uamuzi wake. Kama akishindwa basi ajiulize kama bado ana public trust ya kuongoza mapambano
 
Nguruvi3 inatosha baba.Hayo mawe unayotupia humu lazima dhaifu Mbowe akili imkae sawa.Wasilete masikhara kabisa kwenye mambo ya ukombozi kama kazi imewachosha waachie ngazi.Sasa kama kweli yeye ni mkomavu aombe radhi kinyume chake ni dikteta na ile dhana ya nguvu ya umma itakuwa ni usengeri mtupu.
 
umesahau kutumia neno "baadhi ya" kama nilivyofanya mimi, kwani hivyo ndivyo hoja yangu na pia hoja yako itaeleweka kwa urahisi;tabia ya kunukuu maneno ya mtoa hoja kwa mtindo unaotaka wewe badala ya kutumia kitufe cha quote hapo chini aidha kwa bahati mbaya au kwa makusudi, ni ku entertain upotoshaji wa hoja husika;


Asante kwa maelekezo na masahahisho.
ila kitendo cha kutumia neno BAADHI YA ni yaleyale tu tulio zoea ya siku zote kufichaficha ukweli na kutafuta chembechembe za uongo na kuzifanya ziwe kweli na kujenga hoja MUFILISI isiyo na mashiko.

Mimi nacheweza kukuambia hakuna cha Baadhi wote wanaoenda nisawa na wanania moja, na ndio maana unawakuta wakitulia na kufuatilia hizo hoja na sio kwenda kupiga kelel au kufanya fujo kwney hiyo miihani.,

hao unaosema wewe wanaoenda huko PICNIC na OUT utawakuta kule kwa DIAMOND aka WASAFII naamini unaielewa.

Kama utabisha na hili nakuomba uje na DATA kuthibitisha hayo na utuambie mfano mkutano gani na ulifanyika wapi na walioneda PICNIC ni wangapi.
Maana siwezi kuelewa mtu anayeenda PICNIC ya kusikiliza risala/hotuba za ukombozi zinazongumzia mateso ya waTanzania( unajua nashindwa kukuelewa yani kwa uchungu ambao watu huwa wanaupata wakati wa Hotuba ambazo nyingi huzungumzia jinsi wanavyoibiwa rasilimali zao na wewe kusema ni PICNIC ? hii ni kejeli kubwa sana.)
 
Asante kwa maelekezo na masahahisho.
ila kitendo cha kutumia neno BAADHI YA ni yaleyale tu tulio zoea ya siku zote kufichaficha ukweli na kutafuta chembechembe za uongo na kuzifanya ziwe kweli na kujenga hoja MUFILISI isiyo na mashiko.

Mimi nacheweza kukuambia hakuna cha Baadhi wote wanaoenda nisawa na wanania moja, na ndio maana unawakuta wakitulia na kufuatilia hizo hoja na sio kwenda kupiga kelel au kufanya fujo kwney hiyo miihani.,

hao unaosema wewe wanaoenda huko PICNIC na OUT utawakuta kule kwa DIAMOND aka WASAFII naamini unaielewa.

Kama utabisha na hili nakuomba uje na DATA kuthibitisha hayo na utuambie mfano mkutano gani na ulifanyika wapi na walioneda PICNIC ni wangapi.
Maana siwezi kuelewa mtu anayeenda PICNIC ya kusikiliza risala/hotuba za ukombozi zinazongumzia mateso ya waTanzania( unajua nashindwa kukuelewa yani kwa uchungu ambao watu huwa wanaupata wakati wa Hotuba ambazo nyingi huzungumzia jinsi wanavyoibiwa rasilimali zao na wewe kusema ni PICNIC ? hii ni kejeli kubwa sana.)

Suala la "baadhi" ya wananchi kwenda kusikiliza mikutano ya kisiasa kama "outing" ni suala lililo wazi na sijui kwanini unajaribu kulikataa, na it applies kwa shughuli za vyama vyote vikuu viwili, chadema na ccm; nini cha ajabu katika mazingira ya siasa zetu uchwara kwa "baadhi" ya wananchi kuwa na mtazamo huo? I also have had personal experience kwani sio mara moja, sio mara mbili nimekuwa mikoani na wenyeji wangu tena wakulima wa hali ya chini kabisa kuniuliza kwa mfano huko kusini mtu mmoja:

"unafanya nini mida hii? kama hauna shughuli kwanini tusiende kusikiliza vituko vya upinzani wakati tunangojea mwenyekiti wa kijiji arudi kutukamilishia shida yetu?"

Na tukiwa njiani mwenyekiti alitupigia simu, tukahairisha safari kwenda mkutanoni na pamoja na kwamba shughuli na mwenyekiti iliisha ndani ya nusu saa, mwenyeji wangu hakushauri tena juu ya mkutano wa hadhara na badala yake akanipeleka kwake tukapumzike kidogo chini ya mti tukipiga soga;Na mhadhara huu ulikuwa ni operation sangara; Kimsingi wapo wananchi ambao wanaenda kwa matumaini lakini pia usipinge kishabiki tu kwamba pia wapo baadhi ya wanavijiji wanaojenga hoja kwamba kwa upande mmoja ccm ina siasa za porojo na tukiwapa kura hawarudi kutekeleza ahadi zao zaidi ya kuja na kujitetea kwa wananchi dhidi ya hoja za chadema na kwa upande mwingine chadema nao siasa zao kila siku ni za kukosoa na kuchongea ccm kwa wananchi huku wakishindwa kufafanua vyema nini watafanya kama mbadala wa ccm na kwa mikakati ipi;

Wake up and smell the coffee!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hoja yangu bado ina simama; tena imepata nguvu zaidi baada ya kauli ya kukataa mwaliko wa TCD. Mbowe anapaswa kuomba radhi au kuelezea kwanini alikubali mwaliko - wa muda mfupi - wa kwenda dhifa ya Obama, Ikulu na hawakutumia nafasi zilizokuwepo kumulika utendaji kazi wa vyombo vya dola wakati macho ya kimataifa yapo Tanzania.
 
Hoja yangu bado ina simama; tena imepata nguvu zaidi baada ya kauli ya kukataa mwaliko wa TCD. Mbowe anapaswa kuomba radhi au kuelezea kwanini alikubali mwaliko - wa muda mfupi - wa kwenda dhifa ya Obama, Ikulu na hawakutumia nafasi zilizokuwepo kumulika utendaji kazi wa vyombo vya dola wakati macho ya kimataifa yapo Tanzania.

Mzee hivi kimya hivi haimaanisha Mwenyekiti kakuelewa,na hata absence yao TCD sio zao la post yako.basi inatosha mkuu
 
Duh.. mada nyingine hata nikizipitia zinasikitisha kwa kweli... yaani watu walivyobadilika..
 
Back
Top Bottom