Mbinu za kumuaminisha shemeji yenu kuwa sina mchepuko kabisa

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,232
103,862
Unajua kama kuna wajinga (sio tusi bali ni kutokuwa na ufahamu) wanaamini waume zao hawana kabisa mchepuko? Wapo, ndio hawa mnaowasikia kanywa sumu baada ya kujua ukweli.

Nakwambia hivi wewe mdada, hakuna kitu kama hicho, Labda mume wako awe na matatizo ya kiafya. Hata kama hana hela atakula hata kwa mkopo au kwa kuonewa huruma.

Wewe si umesikia mapadri kuna watu wamewazalisha? Au wachungaji wakipiga wana kwaya? Sasa kwa nini ufikiri una mume wa kwako peke yako? Tofauti yao na hawa wanaojulikana viwembe ni nidhamu ya kuchepuka tu. Wengi wao hupigia show za mbali anaenda kulia mzigo mkoa mwingine.

Mimi ni mmoja wapo. Shemeji yenu akiwa na wenzie waliotendwa hupenda kunitolea mfano kama mpenzi bora kabisa kuwahi kutokea. Pengine yeye ndio mmoja ya wadada humu hukomaa ana bwana hachepuki. Watch out utakuja kufa wewe.

Kuna mbinu kadhaa hutumika;
1. Kuwa muwazi kwa mchepuko kwamba umeoa. Hata kama hujaoa mdanganye umeoa ili akuheshimu na awe na mipaka kwenye mawasiliano. Hata nikiwa nao nakuwa huru kupokea simu za shemeji yenu na kumpanga.

2. Kuwa na Mchepuko wenye roho ngumu na ulio busy na mishe zake. Usichukue mchepuko laini laini wa kutaka kila saa ukutafute. Tafuta wenye roho ngumu na unaojua sex is for fun na mahusiano yenu hayana future yeyote.

3. Kutoupenda mchepuko kupitiliza
Ukiwa na moto naye itakufanya upate muda wa kuwasiliana kujua maendeleo yake. Hapa ndio utakapodakwa kwenye simu.

4. Kuwa huru na matumizi ya simu. Mimi sifichi simu. Ingawa yeye hapendi kusachi simu ila simu yangu ipo huru muda wowote anaweza kuchukua na kuunga WiFi nk.

5. Kusafiri naye
Huwa nikisafiri kikazi anapenda kujua nimefikia wapi, ili akija anikute sijahama lodge. Kwa hiyo siku nikiwa na mzigo nahama gest kwa muda halafu nikimaliza narudi kwa siku zote.

My Take
Sina nia ya kujisifia ila ni kuwajengea uwezo hawa dada zetu kwamba hakuna bwana wa peke yako. Bali kuna mbinu hutumika kukuaminisha hivyo. Ijenge saikolojia yako kwamba lolote linaweza kutokea uwe tayari kukaza roho.

5. Mkakati mizito wakati wa kuchepuka
Nikitaka kuchepuka huwa ninamuandaa. Kwanza ananipishwa stori kwenye simu kama nusu saa hivi. Anapewa ahadi za vizawadi na kila ujinga wa mapenzi. Inakuwa kama tumetongozana jana. Nikimuacha hapo anabaki kuchekacheka tu, kumbe mwenzie nina show nataka kupiga.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom