Tushauriane: Mchepuko kamuweka selo Mke wa jamaa

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
40,497
99,296
Iko hivi,

Nna jamaa yangu mmoja wa karibu hasa kwenye maswala ya biashara,familia,viwanja vya starehe na huzuni Hadi kwenye mambo ya Michepuko huwa hatufichani.

Sasa jamaa yangu ana Mchepuko wake mmoja ila Ni single mother (keshazalishwa mtoto mmoja kabla) Yuko kwenye 36 hivi na Wana mwaka wa pili sasa kwenye mahusiano yao.

Katika heka heka za hapa na pale jamaa kajikuta kampa mimba Mchepuko wake yule. Kwa huruma ya jamaa na mazingira aliyokua akiishi mwanamke yule ikabd jamaa akamnunulie nyumba kigamboni na amhamishie kule Ili awe mbali kdg kwa ajili ya usiri.

Mimba ilivozidi kua kubwa Mchepuko na jamaa wakawa na maugomvi yasiyoisha kila mara, nakwenda nawasuluhisha maisha yanaendelea.

Ikafika kipind Mchepuko yule akawa analeta malalamiko sana kwangu kwamba jamaa ni kama kamtelekeza kusudi kule kigamboni, hatoi Tena matunzo kama zamani yaani Ni mpk wagombane Sana ndo jamaa anatoa hela.Nikamwambia nitaongea nae.

Ktk kuongea jamaa,
Akasema matunzo anatoa,Sema Hali Ni ngumu utoaji kweli mdg sio Kama zaman. Na mwanamke mwenyewe Ni Kama hataki kumuelewa. Nikamwambia zitakua ishu za mimba yake, nenda nae mdg mdg ataelewa.

Nakumbuka Mwez wa 6 MKE halali wa jamaa alinifata na kuniomba nimsaidie namna ya kutrac Simu ya mumewe, nikamuuliza kunani shemeji mpk umpeleleze mumeo.

Akasema kaskia mumewe ana mwanamke mwingine na kamjengea nyumba. Nikamtuliza na kumwambia Mimi kutrac simu ya jamaa siwez maana Ni iphone,ila nimtoe tu shaka kua anachokiwaza hakipo. Kwanza mumeo bahili Sana,kijiweni wote tunamjua.

Hela ya kuhonga mwanamke wa nje, amjengee na nyumba mumeo Hana, kua na amani kabisa shemeji.
Akanambia "Basi shemej usipuuze, wee ndo uko nae karibu sana nisaidie kumchunguza vizur mme Wangu, afu Kama Kuna chochote utanijuza" nikasema "sawa, ntamchunguza"

Bas Nikarudi kwa jamaa nikamwambia awe makini Sana kwenye nyendo zake,mkewe keshaanza mstukia.
Na Mimi rasmi ndo nmepewa rungu la kukuchunguza.

Tujitahidi nisije vunja uaminifu kwa shemej, wote tukaonekana vitombi maana shemej akiskia uko na Mimi Basi kwake Ni amani tele. Jamaa akasema "sawa"

Sasa ijumaa Niko kazini Mchepuko wa jamaa akanipigia kwamba kaenda clinic kakutwa na damu ndogo mwilini, kwaiyo kapewa kitanda apumzike na aongezewe damu. Ana siku ya pili pale. Ila Changamoto kila akimpigia jamaa amtumie Ela alipe bill aruhusiwe kutoka jamaa hapokei Simu na anaikata.

Nikamuuliza kwani sh ngapi unadaiwa? Akasema elfu 35, Basi nikamtumia 40 tigopesa Kisha nikampigia jamaa kujua imekuaje Mchepuko wake kalazwa na pale Hana ela.
Jamaa akanambia kwa kifupi
"Kaka, achana na uyo mwanamke, Ni mpumbavu Sana" nikamuuliza kivipi.
Jamaa akarudia tena,
"Nmesema achana na uyo mwanamke, Ni mpumbavu sana" Akakata simu

Basi nikajiongeza kua hawa washazinguana maana jamaa yangu Ni mwepesi Sana wa hasira,afu mwanamke mwnyw Hali ya mjamzito yule.
Basi ni tafrani tupu. nikawapotezea.

Jumamosi asbh Kanipigia akiniuliza Kama jana Yake niliongea na jamaa, nikamwambia niliongea nae ila Inaonekana Yuko safarini mtandao ukawa hauko vizr hivyo hatukuelewana. Nikiwa na nafas ntaongea nae Tena. Akasema sawa ila
mpk sahv hamna chochote ndani na jamaa hapokei sim yake. Nikamwambia kakope maduka ya jiran,jamaa akirud atalipa.

Akasema alikofikia hakopi Tena madeni.
Ikifika jioni jamaa hajatuma Ela ya matumizi, ataenda kufata matumizi Moja kwa moja dukani kwa mkewe (MKE wa jamaa anaduka la vyakula na nafaka) Hawez kulea kuiumbe chake kwa mateso namna ile.
Nikacheka Sana na kisha Nikamwambia "utakua utoto huo" nikamkatisha nikamwambia tutawasiliana baadae, akasema "sawa"

Sasa jumatatu mida ya jioni mwanamke yule Kanipigia kuulizia mrejesho, nikamwambia sijaongea na jamaa bado. Akanambia Jana yake alienda kuchukua posho ya kula kwenye duka la MKE wa jamaa. Nikamwambia "huwez kua serious".

Akasema serious kaenda pale dukan kamkuta kijana ila mwanamke hayupo na kaomba apimiwe mchele kilo 10,sembe kilo 5, ulezi kilo 1, karanga nusu, mahindi kilo 2 na soya nusu.
Alipoulizwa "PESA" akamjibu kijana kwamba amwambie mama mwenye duka kua MKE mdg ndie aliekuja kuchukua vitu hivyo na namba yake ya Simu akamuachia. Akifika ampigie.

Anasema kabla hata hajafika nyumbani, Simu yake ikaita MKE wa jamaa akamsihi arudi dukani kwa Nia njema ili amfahamu tu. Hana tatizo nae kabisa wayaongee.
Ndipo karudi Kisha akamsimulia A-Z ya mahusiano yao mpk pale alipo pata na mimba ya jamaa.

Pale pale MKE wa jamaa akampigia jamaa na kumuuliza khs Iyo ishu, ila anashangaa jamaa kamkana katakata kwamba Hana mwanamke nje yyt mwenye mimba yake nje na yeye hamjui.
Nikamjibu kuA
"Umekosea Sana, hata ningekua Mimi lazima ningekukana tu. Kama Ni kweli unayosema Basi jua meji Umeharibu Sana. Tena umetengeneza bomu kubwa mno. Sijapenda kabisa"

Akasema
"sikua na jinsi, yeye kajifanya mbabe nami acha nimkomeshe. Angenihudumia yasingefika huko"

"Mie Siwez kufa njaa nna kiumbe chake tumboni, angejua asingemwagia ndani"
Basi nikamkatisha mchepuko na kumpigia jamaa.

Jamaa akaniomba Kama naweza niende kwake MDA huo, kwny Simu hatuwez kuongea tukaelewana.
Basi nmefika kwa jamaa nakuta kikao kizito Cha wanafamilia, ba mkwe wa jamaa (bamdg wa mke wake) kaitwa na ndio mwenyekiti. MKE wa jamaa kafura Sana, jamaa kawa mpole.

Nilipopewa nafas ya kuzungumza,
Ikabd niwe upande wa jamaa,
Nikasema huyo mwanamke atakua shangingi TU wa mjini katumwa kuvuruga ndoa yao. Hakuna mwanamke mpumbavu atamwendea mke wa mtu kwa approach hiyo.
Mkigombana mkaachana iyo ndo itakua furaha Yao. Jamaa yangu namjua sana, Kama ingekua kweli basi ningeshajua zaman. Hana mwanamke mwngn zaidi ya mkewe.
Kwa Maneno Yale, kuna utulivu ukarejea pale. Bamkwe akawasihi wana ndoa watulie Ni majaribu TU hayo,kisha tusiohusika tukarud majumban mwetu.

Jana mchana Mchepuko wa jamaa akanipigia kulazwa hospitali, nikamuuliza
"vipi umelazwa Tena, damu imepungua tena? "

Akasema
"hapana, Ni mke wa rafki yako kanifata nyumban kwangu kanipiga sana na kaning'ata sikio limevuja nimelazwa wamenishona na nyuzi mbili. Na tumbo limeumia Sana na Hii mimba sidhan Kama iko salama"

Nikamuuliza "imekuaje kuaje kwani",
Akasema MKE wa jamaa asbh yake alimpigia kwa Nia njema akisema ana maongez nae, kwaiyo ndo nikamuelekeza Hadi kigamboni kwangu. Gafla akafika na shoga yake wakaanza nitukana wakisema Mimi Ni Malaya mdandia waume za watu nilipe pesa za vile vyakula dukan, nikasema silipi ndo wakanipiga mpk nmelazwa hospital.

Nikamwambia sio kichaa yule hawez kukuvamia TU bila sababu, Kuna namna mmejibizana. Ndo mkapigana.

Sijakaa sawa Simu ya jamaa inaingia,
Ananambia ananiomba nifike kituoni Kuna tatizo.Nikasema POA, ila Moyoni nishajua itakua ndo Ile kesi ya huyu mchepuko wake kupigwa. Chap nikaenda.

Nmefika kituoni maaskali wanafoka balaa, MKE wa jamaa na shoga yake wamewekwa ndani.
Tukafanya mchakato wa dhamana wakakataa kwamba aliepigwa na kung'atwa sikio Ni mjamzito, mpk wapate uhakika wa afya yake kwanza ndo wataruhusiwa. Ukizingatia kafatwa na kushambuliwa nyumbn kwake. Maana ake MKE wa jamaa na shoga yake walijipanga na walipania kumshambulia.
This is criminal case. Basi Ikawa ngumu kuwatoa.

MKE wa jamaa kalala kituoni jana,
Leo asbh tumeenda Tena kituoni kumuwekea dhamana mke wa jamaaa, maaskali wanakomaa kwamba mpk afya Ya mwanamke yule itengamae. Akifa kesi itawageukia.
Basi nikaona hapa Ni kucheza na yule Mchepuko maana ndie alieshika makali.

Nmejishusha sana
Nmemtafuta mchepuko wa jamaa kumsihi amalize ile kesi wakayaongee, amtoe MKE wa jamaa.
Mchepuko anajiliza TU anasema mpk vipimo vyote vikamilike anahisi kwa kipigo kile mimba yake imekaa vibaya.

Mpk MDA huu Niko kituoni na jamaa,
Vichwa vimewaza mpk vimechoka sijui tunafayaje kulimaliza hili.

Sijajua MKE wa jamaa akitoka ndani itakuaje, maana analia TU kwa hasira. kwa maongez ya shemej uko lokapu anasema katika ugomvi ule Mchepuko alimtambishia kua nyumba ile kanunuliwa na jamaa (Ni kweli jamaa alimnunulia).
Afu mke analalamika kua jamaa kagoma kuwajegea wazazi wake uko kijijini, kaenda kumjengea Mchepuko wake.
HILI NI BALAA JINGINE hili.

Nikarud kwa jamaa Nikamuuliza
"Inakuaje sasa mpk mmefika huku,
Hili naweza kukulaumu Wewe maana malalamiko ya Mchepuko yule tangu mwanzo Ni hutoi matunzo. Japo ana mimba ila Ungeishi nae kwa akili sidhan kaa mngefika uko"

Jamaa akanambia kisa Cha kuacha kutoa matunzo kwake Ni kitendo Cha kwenda Mara 3 pale kwake na kumkuta baba wa mtoto yule wa kwanza wa mwanamke yule nyumbani kwake. Na Mara mbili keshamkuta sebleni.

Akamuuliza mchepuko
jamaa yule kafata Nini pale hadi anakaa sebleni kwangu na tangu mwanzo ulishasema alikuzalisha akakutelekeza na mmeshaachana, mchepuko anajitetea kua jamaa walisha-achana ila Kaja kumuangalia tu mtoto wake.

Jamaa anasema akamkanya kua hataki Tena kumuona jamaa yule pale,
Kisha Mara ya 3 ndo alipokuja akamkuta jamaa seblen kakaa kwenye sofa na mwanae anakunywa Hadi juice na ndiz za kukaanga kwa posho aliyomwachia mwanamke yule.

Ndipo alipositisha kutoa huduma rasmi na kumwambia mwanamke yule kua huyu jamaa unaemng'ang'ania sana ndo huyo huyo akuhudumie rasmi.

Ikawa Ndo chanzo Cha chokochoko zote zilikoanzia.

Duh! Nikashangaa Sana
maana kwenye magomvi yao Mchepuko yule hakuwai kunambia vitu Kama vile.

Anyway,
Turudi kwa jamaa, Mchepuko wake, mke wake na ndoa Yao kiujumla. TUNALIWEKAJE HILI mambo yawe sawa.

HEBU Tushauriane hapa wakuu

Pia soma: Mrejesho: Mchepuko kamuweka selo mke wa jamaa
 
Kiufupi jamaa ana bahati mbaya, huyo mchepuko ni jambazi sugu na tayari kashaharibu ndoa. Mtu mwenye akili timamu huwezi kuwa umeshajengewa nyumba then ufanye mambo ya ajabu kama vile na bado hapo lazima jamaa pesa ndefu imutoke kuwatoa mke wake na huyo mwenzake na hizo pesa zitaliwa maaskari na huyo mjamzito.

Mwisho nimalize kwa kusema mshahara wa dhambi ni mauti, ninavyoona hapo lazima mauaji yanaweza tokea kama jamaa hataamu kuondoka kwanza kumpa space mke wake atulize hasira.
 
Kiufupi jamaa ana bahati mbaya, huyo mchepuko ni jambazi sugu na tayari kashaharibu ndoa. Mtu mwenye akili timamu huwezi kuwa umeshajengewa nyumba then ufanye mambo ya ajabu kama vile na bado hapo lazima jamaa pesa ndefu imutoke kuwatoa mke wake na huyo mwenzake na hizo pesa zitaliwa maaskari na huyo mjamzito. Mwisho nimalize kwa kusema mshahara wa dhambi ni mauti, ninavyoona hapo lazima mauaji yanaweza tokea kama jamaa hataamu kuondoka kwanza kumpa space mke wake atulize hasira.
Mpaka sasa
Ndoa ya jamaa ishaingia doa
Tena doa kubwa kwelikweli, nmemwambia arelax kwanza akili itulie
 
Nmemchukia mno Mwanamke mpumbavu Sana huyu
Kosa siyo la mwanamke, kosa ni la jamaa, kwa sababu alishindwa kujiongeza kuwa anafanya kosa kubwa sana kudate na mchepuko mwenye mtoto, let alone ambaye bado ana mawasiliano na Baba wa mtoto.

Na hapo kama unavyojua wanawake maamuzi yao yanatokana na hisia, basi demu kapuyanga na jamaa ndiyo kapuyanga mara mia zaidi, kumchagua mchepuko wa aina hiyo.

Mwambie kabisa wanaume tunatakiwa kutumia nguvu yetu ya kufanya maamuzi, ili kuweza kuamua maamuzi sahihi katika wakati sahihi, ili isije kutokea tukachelewa kufanya maamuzi sahihi tukawa tumeshaharibu kwa familia.

Mchepuko unatakiwa umchukulie kama mwanamke wa mpito tu kwa sababu tayari una chaguo lililo bora zaidi na la kudumu (mke)
 
Hahaaa ila inauma nyumba ujenge na matumizi unatoa unakuta jamaa limekaaa sebleni kwako kisa limezaa na mkeo mm huyo jamaaa nae angezaa awe mke wa pili.

Mm nimezalisha nje na dem kaolewa ila nina respect kubwa sana ya ndoa yao .Huyo jamaa amuombe msamaha mke wake tu hilo malaya aachane nalo
 
Du!! Hizo ndio hasara za kumwagia ndani.

Pamoja na hayo, jamaa ajishushe kwa mchepuko aende amuombe aondoe kesi mahakamani na amuahidi atamuhudumia na baada ya hapo mauombe radhi mkewe na mueleze kuwa yule mchepuko yeye alipota nae mara moja na akiwa tungi na baada ya hapo mchepuko akaanza kudai ana mimba yake. Ila jamaa hakumtilia maanani alijua kuwa ni tapeli wa mapenzi hivyo akawa amemfungia vioo.

Kutokana na kumfungia vioo ndio maana yule mchepuko akaanzisha figisu mpaka za kuja kujitambulisha kwa mkewe. Amwambie mkewe kwamba amekosa sana amekosa yeye na ndio ubinadamu.
 
Ukiona mwenzako ananyolewa zako tia maji.. DeepPond. Wewe na huyo mama J its just a matter of time. God is actually giving you a sign. Je ungependa uharibu familia yako hapo baadae??mama J atakuja achoke tu andika hii statement...utanikumbuka.

Ila dunia hii jamani. Ninachoweza kumshauri jamaa akamtongoze upya mchepuko. Amsaundishe ili mke atoke. Yani awe mpole. Baada ya hapo akishatoka asubiri mtoto azaliwe. Mimi kama mwanamke ningeumia sana unasikia flani kanunuliwa na nyumba. Inauma sana.

Amsikilize mkewe atakachoamua akitoka ndani. Hasira itapoa tu hata kama tayari jamaa kashatia doa nyumba yake. Ila akiamua kujirudi akaachana na mipango ya nje akawa baba mwema kwa familia yake basi atasamehewa.
 
1. Hapo kwa wife ake apenyeze rupia kwa maafande lazma apewe dhamana. Pia akiweza kumtoa lupango mke wake hata hasira zitapungua maana najua mpka sasa hv kashasota vya kutoSha. Wakirudi watayamaliza bila shida

2. Kwa mchepuko arudi kwa heshima debe (uongo ofkoz). Amlambe miguu kua wife amezingua n.k kwaio hataki tena kurud ameamua ayajenge na mchepuko walee mtoto wao n.k. lazma atalegeza kamba

3. Akishatoka hossy, aende akaombee mkopo hyo nyumba apige dili na madalali iuzwe, mchepuko atarudi ground zero na kytulia. Akileta kelele ataenda ustawi huko hakuna jam sana

4. Amkane mchepuko kwa kigezo cha kutokua na uhakika na hyo mimba kwakua mzaz mwenzie inaonekana wanatiana so yaezekana mtoto si wake
 
Nmemchukia mno
Mwanamke mpumbavu Sana huyu
Ni kweli huyo mchepuko ni mpumbavu lakin jamaa yako naye kazingua,, kuna hatua ikifikia basi kuuficha ukweli huleta balaa Sana, ilipofikia hatua ya mchepuko kwenda Kwa mke wa jamaa na kuchukua chakula kisha kuongea na mke wa jamaa basi kwenye kikao jamaa ilitakiwa akubali tu kuwa kazaa nae then yangezungumzika tu.

NB: KUKUBALI KOSA NI ISHARA YA UKOMAVU KIAKILI
 
Back
Top Bottom