MBEYA mjini wana matatizo gani

Katika karne hii ya sayansi na teknologia mnawezaje kumchagua muimba bongo fleva asiye na elimu kuwakilisha mji kama wa Mbeya ........ Ni kweli hamuipendi ccm lakini si kumchagua Mr 2. Sasa amebakia kugombea wanawake na akina jaffer rhyme. KWELI TZ KUNA MAAJABU

Ama kweli ukistaajabun ya Musa utayaona ya Firauni,si hakika kwamba elimu ya mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini haitoshi kuwasilisha matatizo ya wakazi wa jiji hilo kwenye chombo cha maamuzi ya nchi(Bunge).Kama hoja ni elimu basi,WATANZANIA tuna matatizo nasema hivyo kwa sababu wakati fulani mkuu wa nchi mtu ambaye tuandhani ana elimu ya kutosha kuliongoza Taifa letu aliwahi kuulizwa swali ni kwanini Tanzania ni maskini,yeye alijibu hivi "hata mimi sijui kwa nini Tanzania ni maskini" Kwa mantiki hiyo basi,watanzania tuna matatizo tutategemeaje mtu asiyejua matatizo yetu yanasababishwa na nini ili atuongoze kutafuta ufumbuzi? ELIMU SI KIGEZO KIKUBWA KATIKA UONGOZI.
 
Katika karne hii ya sayansi na teknologia mnawezaje kumchagua muimba bongo fleva asiye na elimu kuwakilisha mji kama wa Mbeya ........ Ni kweli hamuipendi ccm lakini si kumchagua Mr 2. Sasa amebakia kugombea wanawake na akina jaffer rhyme. KWELI TZ KUNA MAAJABU

Nani kakwambia Sugu hana elimu degree sijui lakini vidato vipo vya kutosha, muulize Mulugo kati ya yeye na Sugu nani shule ilikuwa inapanda? Sugu mbona anapiga kazi tu, na wewe shule yako ikoje?
 
ulitaka tumchague babu yako?

Katika karne hii ya sayansi na teknologia mnawezaje kumchagua muimba bongo fleva asiye na elimu kuwakilisha mji kama wa Mbeya ........ Ni kweli hamuipendi ccm lakini si kumchagua Mr 2. Sasa amebakia kugombea wanawake na akina jaffer rhyme. KWELI TZ KUNA MAAJABU
 
wenye madigree wamesaidia nn tz kama kigeza ni elimu lipumba angekuwa rais.tuangalie kujituma,uadirifu, tukijari elimu pekee tutapoteza dira hasa zama hiz za degree fek
 
1738.jpg
Ha ha ha ha. Huyu ni profesa sugu siyo profesa mzee.
 
Hivi wasomi hawapo kinondoni? akawauliza kule Tanga kwa Profesa Majimarefu, walimtosa jama ana ACCA tangu miaka ya 70?

Kabla ya kuchangia lolote tunaomba utupe sifa ya kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Maana sisi wakazi wa Kinondoni kwenye wajanja wote Mbunge wetu Idd Azzan ni darasa la saba.
 
Kabla ya kuchangia lolote tunaomba utupe sifa ya kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Maana sisi wakazi wa Kinondoni kwenye wajanja wote Mbunge wetu Idd Azzan ni darasa la saba.
hawa jamaa hawajui katiba mbona Lukuvi ni Darasa la nane lakini kwenye uwaziri yupo poa, Huyu Jamaa afiche upumbavu wake
 
Mbona hujaanza kwanini watanzania walimchagua Jk wakati hajui kwanini wao ni masikini? ni haki rais kuomba kupiga picha na 50cents? rais kutumia hela zetu kwenda kumbembea Canada ndo kutusaidia watanzania?

Mwigula anajiita amebobea kwenye uchumi ni mtumishi pale BOT lakini anasema anaomba wachungaji waiombee tanzania ili uchumi utengemae je matatizo ya uchumi yanatatuliwa kwa maombi?

kuwa Great thinker wewe mburura
 
Bunge LETU linalaanika kwa kuwa kuna wabunge mle ambao ni waganga wa kienyeji pia.
 
Mbona hujaanza kwanini watanzania walimchagua Jk wakati hajui kwanini wao ni masikini? ni haki rais kuomba kupiga picha na 50cents? rais kutumia hela zetu kwenda kumbembea Canada ndo kutusaidia watanzania?

Mwigula anajiita amebobea kwenye uchumi ni mtumishi pale BOT lakini anasema anaomba wachungaji waiombee tanzania ili uchumi utengemae je matatizo ya uchumi yanatatuliwa kwa maombi?

kuwa Great thinker wewe mburura

mkuu naomba nikukate kauli kidogo, baba mwanaasha alienda kubembea Jamaica sio canada!
 
mkuu naomba nikukate kauli kidogo, baba mwanaasha alienda kubembea Jamaica sio canada!
Nashukuru mkuu ni kweli nilienda nje ya mstali kidogo

Canada alienda kupanda kigari kinachovutwa na farasi
tatizo baba mwana asha anamatukio mengi hadi tunachanganya
 
Hivi mbunge kama huyu anaweza kweli kuwakilisha wasomi , maprofesa na wafanyabiashara wa mji wa mbeya. Ataongea nini? Ana upeo gani? Ana elimu gani? Hajawahi kuwa hata monita wa darasa au mjumbe wa nyumba 10

Only the foolish dog barks at flying birds.
 
tulikuwa na profesa kigoma malima na alisafisha hazina nzima..goddamn it
 
Nenda Rungwa Mashariki kwa Prof.Mwandosya ukaone wananchi wakisafiri kwenye canter na Fuso kama nyasi za ng'ombe tangu 1961,aliyekwambia kuwa msomi ni kigezo cha kujua matatizo ya wananchi ni nani? Acha ushamba,kuna wasomi kibao nchini wameishia kusaini mikataba ya kudhulumu nchi au unadhani walioiba kwenye EPA,BOT,RICHMOND na hata mikataba hovyo kwenye madini wamehusika watu mnaowaita wasomi wa ccm.Watu wa Mbeya wanataka mtu anayewajali na kuwasikiliza wanachomwambia akawawakilishe. Nakushauri uache upuuzi wa kudharau maamuzi ya watu,demokrasia haibagui kiwango cha elimu,kipato,afya ya mtu,umri,jinsia wala dini.Na kwa sasa hakuna kipimo cha usomi Tanzania kwani hakuna tofauti ya msomi na asiyesoma ndiyo maana hata Mwigulu Nchemba alinunua jina la mtu alipofeli darasa la saba na kuendelea nalo hadi sasa mnamwita mchumi namba moja CCM.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom