Laana au?

musicarlito

Senior Member
Dec 29, 2020
176
289
UJINGA WA MAJI NA NYAYO

Kitendawili! Tega! Ni bara gani ambapo watu wake wananunua maji ya upako eti wapate mali badala ya kufanya kazi? Afrika.

Kitendawili! Tega! Ni bara gani ambapo watu wake wanarudi nyumbani na mizigo ya udongo wakati watu wa mabara mengine wanachukua rasilimali zao? Afrika.

Kitendawili! Tega! Ni bara gani ambapo wanaume na wake zao na watoto wao wanakwenda kulia hadharani kusudi Mungu awasaidie badala ya kufanya kazi? Afrika.

Kitendawili! Tega! Ni bara gani ambapo watu wake wanajambiwa ushuzi ya kusudi wapate mali? Afrika.

Kitendawili! Tega! Ni bara gani ambapo wanawake wao wananyonywa matiti eti wapate wanaume wa kuwaoa badala ya kujichunga kwa uchapakazi na tabia njema? Afrika.

Kitendawili! Tega! Ni bara gani ambapo akina mama na akina dada wake wanaanguka chali hadharani eti kwa kupagawa na mapepo? Afrika.

Ongeza vitendawili vingine mwenyewe.

Sisi ni Wale Wale toka Zamani,
Twende kwenye mada yetu halisi.

Ni kwamba sisi ni wale wale. Sisi Waafrika ni wale wale. Chifu Mangungo wa Msovero alipewa na Wazungu shuka yeye akawapa ardhi. Kisiwa chote cha Kilwa kilinunuliwa kwa jora moja la nguo.

Mfalme wa Ashanti, Ghana, alipewa na Wazungu vikombe, sahani na sufuria, yeye akawapa mizigo ya dhahabu. Mfalme Lobengula wa Wandebele (Zimbabwe) aliwakodishia Wazungu ardhi yote ya Zambia na Zimbabwe kwa paundi 100 za Uingereza.

Machifu wengine walikuwa wanapewa na Wazungu vioo vya kujitazamia sura, na wao wakawapa ardhi.

Kabla ya hayo, wazee walikuwa wanakamatwa na kuuzwa na Wazungu na Waarabu kama ng’ombe mnadani. Walikuwa wanashindwa kuungana na kuwapiga waliokuwa wanawaswaga kuwapeleka kwenye masoko ya utumwa.

Ndivyo ndugu zetu walivyopelekwa barani Merikani au Asia kuuzwa kwenye minada ya kuuzia wanadamu. Biashara ya utumwa ilidumu takribani miaka 400 mpaka Wazungu walipoona haya na kuamua kuifuta wenyewe.

Ndipo wakabuni ukoloni mkongwe na kisha kutupatia uhuru ambao umefungulia milango ukoloni mamboleo unaoendelea sasa hivi.

Ushamba wa Vijana wa Zamani
Kutokana na kutumiwa na waliotuzidi ujanja, tukabaki hatuna mahali pa kujishikia. Tukalazimika wote kusubiri tu kuletewa vitu vya teknolojia na viwandani. Ndipo vijana wa zamani tukaanza msafara wa ulimbukeni.

Kifupi, sisi tulikuwa washamba wa vitu vingi vya wakati wetu. Wazee wetu walikuwa washamba wa shuka, sufuria, vikombe, sahani na vioo kama tulivyosema. Sisi tukawa washamba wa viatu na vitu vingine vipya.

Katika siku zetu mtu aliyepata viatu hasa vile “vya tumbukiza” alijulikana vijijini mwote na aliweza hata kupendwa na wasichana warembo wa kijijini kwake na hata wa vijiji jirani. Baada ya hapo ushamba wetu ukahamia kwenye umiliki wa radio.

Kijijini iliweza kuwapo radio moja tu. Mwenye radio akawa anaishonea mfuko na kuichukua kokote aendako. Akifika mahali alikuwa akitundika juu ya mti na Waafrika wenzake kukusanyika kusikiliza habari na muziki. Watu wakawa wanabaki bumbuwazi wakijiuliza hao wanaotangaza huko ndani walikuwa wanakula nini.

Baada ya hapo tukawa washamba wa saa. Kijana aliyebahatika kupata saa aliweza kuoa mabinti warembo kadhaa kwa sababu alijipambanua kama “mtu mwenye nazo” akilinganishwa na vijana wenzake. Alipopiga picha akawa anautundika mkono kusudi saa yake ionekane.

Baada ya hapo ushamba wetu ukahamia kwenye simu za mezani, radio call na kamera za kunyonga. Sambamba na vitu hivi ulimbukeni wetu ukahamia kwenye vyombo vya usafiri.

Kwanza mwenye baskeli alionekana tajiri, baadaye mwenye pikipiki (Honda, Suzuki n.k.) na kishapo ikawa zamu ya wenye magari kutamba vijijini au mijini.

Siku hizi vitu hivi havitutii sana ulimbukeni hasa kwa sababu Mchina katutengenezea Waafrika viatu, radio, saa na vitu vingine vya bei nafuu. ASANTE SANA MCHINA! Mchina umetuokoa sana Waafrika. Bila wewe sisi tulikuwa basi hivyo! Mungu akubariki na akuzidishie Mchina!

Punde ikaja mitumba ya nguo pamoja na vyombo vya usafiri, tukapata ahueni katika ushamba vya vyombo vya usafiri. Siku hizi tuna Toyota, Scania, Tata na Yutong tele. Tukiwa na pesa au tukikopa pesa tunaweza kununua ndege nzuri kama Boeng na Bombadier pamoja na kujenga reli za kisasa.

Asante Wazungu, Wajapani, Wahindi na Wachina! Kweli Baniani mbaya lakini kiatu chake dawa! Tungelibaki na hadithi zetu za kuruka na nyungo, fisi au pembe tungekuwa bado tunakula patupu.

Ushamba wa vijana wa leo lakini Waafrika ushamba haujatuisha. Ushamba unaoendelea kwa vijana wa sasa ni simu. Kila toleo la simu linawatoa ushamba. Siku hizi vijana wanababaika na simu za mkono hasa zile za kupapaswa na vidole pamoja na mitandao yake.

Vijana wetu ushamba umewajaa kiasi kwamba wengine hawalali hususan kwa sababu ya kuchungulia picha chafu. Mitandao kama WhatsApp, Facebook, Twitter na Instagram inawatoa ushamba kwa sababu ya kujipiga picha hasa akinadada wanaojipiga picha wakiwa wamebinua viuno kama manyigu.

Ha! Zamu yao ya ushamba! Ukitilia maanani ukweli kwamba simu zote zimepitwa na wakati si miaka mingi ijayo watajifuma walivyokuwa washamba pale tutakapokuwa tunatumia vyombo vingine vya mawasiliano nje ya simu hizi.

Hatujui baada ya simu kitakuja kitu gani kutotoa ushamba, Waisraeli wanajua sisi hatujui. Waisraeli wanajua kwa sababu wao ndio mhimili wa tafiti na teknolojia, sisi Waafrika ni “magolikipa” wa teknolojia tu.
Vijana Waafrika kumbe nao ni washamba wa leo. Wanavyojidai navyo sasa wala si vyao maana havijatoka kwao wala kwa sisi wazee wao.

Wazee wao tulikuwa washamba katika wakati wetu lakini leo ni zamu ya watoto wetu. Ndiyo hivyo tena maana sisi ni wale wale. Tuko kama familia ya kuku, wote kulishwa: baba (jogoo), mama, pamoja na watoto wao, ndio vifaranga kulishwa tu.

Kwa jinsi tusivyokuwa na vyetu katika sayansi na teknolojia, nimeamini wanavyosema watu: DUNIA YA MUNGU, VITU VYA MZUNGU, NGOMA YA MWAFRIKA.

Popote tulipo watu weusi, kazi yetu ngoma tu: singeli, “hip pop”, “bongo fleva”, “samba” na kadhalika. Hayo ya juu sisi hatuyawezi. Mambo ya sayansi na teknolojia si yetu, hata wasomi wetu wa Kemia, Fizikia, Hesabu, Madawa wamekariri formula na kanuni tu. Si lolote!

Ujinga wa Maji
Sisi ni mafundi wa kufanyana vibaya wenyewe pia. Kifupi, hatuwezi kutatua matatizo yoyote makubwa kiutuuzima. Majibu yetu kwa matatizo yetu ni ya kitoto ndiyo maana tunasemwa tuna Hisa ndogo ya Akili (IQ).

Ajabu ya kukirihisha ni kwamba, Waafrika tunapofanywa soko na “magolikipa” wa teknolojia za wenzetu huwa tunafanyiana vibaya wenyewe pia. Sisi ni wale wale. Ndiyo maana kila kizazi kinadanganyika. Narudia. Wakati Waafrika tunapofanyiwa kitu cha kutuzidi akili na watu wanaotuona malighafi yao, sisi wenyewe wakati huo huo huwa tunazidi kuambizana na kufanyizana mambo ya kijinga.

Nakupa mifano. Tulipokuwa tunatawaliwa, Kinjikitile akatuambia tutamweza Mzungu tukipigana naye. Alituambia Mzungu akija na risasi na sisi tukisema tu, “MAJI, MAJI, MAJI!”, risasi za Mzungu zitageuka maji matupu. Tukamwamini Kinjikitile, tukafa. Je, tulikoma hapo? Hapana hatukukoma. Ujinga wa maji huo! Maji yayeyushe chuma kweli!

Mimi sijui, Waafrika na maji kuna nini! Hakika, sijui kwa nini tunayaamini sana maji ya dawa. Tazama, baada ya miaka kadhaa alikuja Babu wa Loliondo akatuambia tukinywa maji yake katika vikombe vyake magonjwa yoyote ya kutisha yatatutoka. Tukamwamini. Tukanywa vikombe vya Babu, tukafa. Huo ulikuwa ujinga wa maji vile vile!

Lakini eti hadi hapo tukawa hatujajifunza lolote. Ndipo pasipo haya, siku hizi tumejiwa tena na ujinga wa maji. Tunakusanywa kwa maelfu, kwenye viwanja vya Furahisha (Mwanza), Jangwani (Dar es Salaamu), sijui wapi huko Mbeya na Tabora, na Dodoma na Bukoba na kuambiwa eti tukinunua maji ya upako, mambo yetu yatanyooka, yaani tutapata utajiri na maradhi yatatuondoka.

Haya tunanunua kwenye vyupa. Tunakwenda nayo nyumbani ambako hakibadiliki chochote kile. Kinachoniuma ni kwamba hata Wasukuma, Wakerewe, Wakara, Waikizu, Wakurya, Wazanaki, Wajita, Wahaya na kadhalika wenye mto Simiyu na Ziwa Victoria upenuni, wananunulishwa maji ya upako kwenye vyupa vidogo.

Ha, maji ya ziwa zima hayajawaletea maendeleo, yatakuwa maji wanayouziwa kwenye chupa? Ujinga wa maji huo! Wangoni, Wamatengo, Wanyakyusa, Wananyasa na Wakisi wanauziwa maji ya upako kwenye vyupa wakati wana maji ya mto Ruvuma, mto Ruhuhu na Ziwa Nyasa upenuni.

Ujinga wa maji huo! Waha, Wanyambo, Wanyarwanda na kadhalika wenye mto Malagarasi, mto Kagera na Ziwa Tanganyika upenuni wanauziwa nao maji ya upako! Wanyiha na Wasafwa wenye Ziwa Rukwa na mto Songwe nao eti wanauziwa maji ya upako kwenye vyupa wakati wana maji tele upenuni.

Ujinga wa Kukomboa Ardhi, ujinga bin ujinga. Tunaaminishana kwamba ardhi yetu ina mikosi, eti tuikomboe. Ha, ardhi nzuri kama hii ina mikosi gani? Ndani yake mna dhahabu, almasi, tanzanite, shaba, uranium, madini wanayotafuta Wazungu, Wachina, Wahindi na Wamerikani. Sisi tunaikomboa kwa kosa lipi? Mwishoni mwa “kujingishana” huko, tunakwenda kwenye makongamano na kurudi nyumbani na udongo.

Ha, Mzungu anarudi kwao na dhahabu na madini mengine, Waafrika tunarudi nyumbani na mizigo ya udongo! Ha, ujinga kweli! Pamoja na ujinga wa maji, tunanunulishwa vitu chungu mzima vya kijinga. Mfano, tunanunulishwa vyupi vya upako. Ha, mtu uvae chupi ndiyo upate gari au nyumba? Tunanulishwa keki za upako.

Ha, mtu ule keki iingie tumboni, ndiyo upate gari, nyumba au mali? Mengine nayaonea haya kuyasema. Ashakum si matusi! Wapo wanaoaminishwa eti wakijambiwa ushuzi wa upako watapata mali. Ha, ujambiwe na mchungaji hewa yake ya tumboni, ndiyo upate mali huko uendako? Ujinga wa mwisho kweli kweli!

Naendelea kidogo. Wapo wanaoaminishwa wakinyonywa matiti na mchungaji watatokwa na mikosi na wao kupata kuolewa au kuzaa watoto na kadhalika.

Ha, matiti anyonye mchungaji, bwana unampataje? Haya yalikuwa ya kanisa moja huko Kenya. Wengine waliambiwa watapata mabwana kwa upepo wa kisulisuli. Ha, bwana anaweza kuletwa na upepo, kwani yeye karatasi au unyoya?

Wengine waliambia wafungue mikoba yao, wafanye ishara kama ya kuingiza pesa mikobani mwao watapata utajiri. Watu wazima walifanya ishara hiyo, lakini mpaka leo wamebaki fukara. Lakini hawakufundishika lolote hapo.

Wapo vipofu, viwete, bubu na wagonjwa kibao walioitiwa maombi na mikesha, wakarudi patupu. Hata hivyo, hawakujifunza lolote. Eti yakiitishwa makongamano mengine watajipeleka tena! Mungu tuhurumie Waafrika!

Siku hizi, huku kwetu wengine wanaambiwa wapeleke nywele na kucha zao kanisani zikafanyiwe mambo, mambo yao yafanikiwe. Ha, huu si ujinga wa imani za kishirikina? Hayo si sawa na kujikinga na hirizi zenye kucha za kuku au za fisi ndani yake? Hayo si sawa na mtu kuamini nguvu ya hirizi yenye jino la nguruwe au jino la simba ndani yake? Meno ya marehemu nguruwe au marehemu simba yanatulindaje wanadamu?

Hayo si sawa na kuamini nguvu za mikia ya kenge na mayai ya bundi? Yana faida gani hayo? Watu tulioumbwa kwa sura na mfano wa Mungu kusudi tukatawale ndege, samaki, wanyama na vyote vitambaavyo, tunageuzaje mambo kwa kuvichukua vitu vile vile tulivyoambiwa tuvitawale vitutawale watawala? Soma Mwa 1:26-28 usikitike pamoja nami ikiwa utaelewa mambo yalivyokaa ovyo.

Mifano ni mingi mno, nakuomba uendelee mwenyewe na mifano ya vitu vya kijinga unavyofanyiana Waafrika weusi, mimi nimechoka; halafu si mtumwa wako!

Ujinga wa Kukomboa Nyayo,
Maajabu watu wanafanyiwa ibada ya kukomboa nyayo zao eti watembee kwa baraka duniani. Ujinga mtupu! Badala ya kukomboa akili, tunakomboa nyayo? Nyayo si kwato za mwadamu tu? Nyayo zina nini? Hivi sisi watu kweli? Ndugu zanguni, tukomboe akili, maana kwa hiyo tutatazama vizuri mambo.

Tutafahamu tuna majaliwa ya akili na utashi; tutafahamu tuna ardhi nzuri; tutafahamu tuna rasilimali nyingi na kadhalika. Kwa akili hiyo tunaweza kujua tunapoibiwa na tunapodanganywa na kufanywa “wajinga ndio waliwao.”

Kwa akili iliyokombolewa tunaweza kuzaa ubunifu wa kutumia mali tulizo nazo kwa mustakabali wetu na wa watoto wetu.

Tusikubali kufanyiwa ibada ya kukomboa nyayo (kwato). Mtu mwenye akili nzuri hata kama hana miguu na mikono atajikwamua na magumu ya dunia hii. Akisali atasali vyema pasipo kupigapiga kelele na kupayukapayuka.

Magumu yanayomshinda kabisa atamkabidhi Mungu kwa utulivu mkubwa hata kama iwe ni ugonjwa mbaya, au mahusiano ya kijamii magumu, hata iwe ujane, hata iwe ni magumu ya kiuchumi. Mwenye akili hutulia na kufikiri. Kinyume chake mtu anayetumia nyayo tu kutembea huwa “changudoa wa imani” akihama kutoka kanisa moja kwenda lingine na akikimbia kimbia huko na huko akitafuta miujiza isiyokuwapo.

Sala za Kijinga
Mwishowe, wengine wanaaminishwa wakikesha na kulia na kufunga kavu watapata mali. Ha, tukeshe pasipo kuitendea kazi ardhi na rasilimali kwa akili uliyopewa, mali itakujaje? Mungu hataki hivyo. Katuambia tufanye kazi siku sita kati ya saba za juma (Kut 20:8-9). Tena katuambia kwa kupitia kinywa cha Mtume Paulo kwamba asiyefanya kazi asile (2Thes 3:10).

Ni aibu. Anachotaka Mungu ni kwamba tufanye kazi na ndipo tunapokwenda kwake kusali tumwambie tunafanya hiki na hiki kisha yeye aweke mkono wake hapo kusudi mambo yaende kwa wepesi (Zab 90:17). Si suala la kwenda kumlilia kama watoto wadogo.

Wengine huwakusanya watu kwenye kongamano na kuwaambia wenzao wao wakikemea umaskini na maradhi kwa sauti kubwa, “UMASKINI ACHILIA! UMASKINI ACHILIA! UMASKINI ACHILIA!” au “UMASKINI ONDOKA! UMASKINI ONDOKA! UMASKINI ONDOKA!” umaskini utakwisha kabisa. Ha, hii si akili ile ile ya Kinjikitile? Umaskini unaondokaje kwa kuukemea tu?

Kinachonikera mimi ni kwamba mambo mengine ya kijinga yanatendwa kwa jina la Ukristo. Yanatendwa na walei wetu, au mapadre wetu na pengine maaskofu wetu. Ha, hii ni aibu sasa! Huku ni kuudhalilisha Ukristo vibaya kabisa. Naamini Yesu atatukataa mwishoni mwa maisha haya na kutuonesha “cha mtema kuni kilichomtoa kanga manyoya” kwa kututupa jehanamu.

Tunayatafuta, Tutayapata!
Mwanakulitafuta, mwanakulipata! Ninayosema si mzaha, Yesu ameahidi na alichoahidi Yesu lazima kitimie. Tusomeni Maandiko, “Wengi wataniambia siku ile ya hukumu. ‘Bwaana, Bwana! Kwa jina lako tulitangaza ujumbe wako, na kwa jina lako tuliwatoa pepo na kufanya miujiza mingi.’ Hapo nitawaambia, sikuwajua ninyi kamwe, ondokeni mbele yangu, enyi watenda maovu’” (Mt 7:22-23).

Mzee wenu Pd. Titus Amigu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bila kujali andiko limeandikwa na nani, naomba nikiri wazi ya kwamba yote yaliyoandikwa humu ni ukweli mtupu. Laiti kila Mwafrika angelisoma hili bandiko kwa akili huru!!
Ahsante sana Pd. Titus Amigu.
 
Back
Top Bottom