Feedback
JF-Expert Member
- Mar 14, 2011
- 7,988
- 4,507
Mh. Dr Slaa nina maswali mawili naomba ukipata muda unisaidie;
1.Watu wengi wametoa mawazo yao humu JF na nje ya JF kuhusu Jengo la Makao Makuu ya chama wakisema lililopo sasa pale Kinondoni halina hadhi kwa levo ya chama ilivyo sasa, chama kina majukumu mengi tofauti na mwaka 2000, kina idara nyingi kwa hiyo na watendaji na ofisi lazima ziongezeke, mbali ya watendaji wa ndani kinapata wageni mbalimbali wa ndani na nje ya nchi. Najua chama kina mambo mengi na kati ya hayo mengi kina priorities zake lakini suala la nyumba hata kwa ngazi ya kifamilia huwa linapewa uzito wake, je mmefikia wapi ktk hili.
2. Media ni nyenzo muhimu sana katika utendaji kazi wa siasa huwezi kueneza sera wala ujumbe bila kuwa na media. Je chama kina mikakati gani ya kuanzisha Chadema Television, Radio au Gazeti la chama kuliko kuendelea kutegemea vyombo ya watu binafsi au serikali ambavyo huchagua habari wanazozitaka. Nakumbuka ulishawahi kuligusia hili kipindi fulani kuwa tutegemee mabadiliko makubwa mwezi July naona july ndiyo hii, ni hatua gani mmeshafikia. Kwenye eneo hilo hilo chama kina mpango gani wa kupata mwanahabari(permanent) ambaye atakuwa yuko sambamba kila mnapofanya mikutano au maandamano na kusambaza matukio(live) zikiwemo picha kwenye mitandao na media zingine, kwa hili sina budi kumpongeza Mh. Regia lakini anahitaji mtu wa kumsaidia. Ni hayo tu asante nawatakia mafanikio mema.