Yaliyojiri Mahakamani kesi ya Mbowe na wenzake. Shahidi Justine Eliya Kaaya, amtaja Ole Sabaya. Kesi imeahirishwa hadi Oktoba 28, 2021

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,115
Kesi ya inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake itaendelea katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Rushwa, ambapo Ushahidi unaendelea kutolewa. Shahidi wa kwanza kwa upande wa Jamhuri ACP Kingai atamalizia Ushahidi wake.

========

Mawakili upande wa utetezi wapo katika chumba cha Mahakama

FCr0QCqWUAQRUyu

Watuhumiwa wote wamekwisha wasili katika ukumbi wa mahakama asubuhi hii

FCr679IXEAk9Gp8

Jaji ameingia

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Imetajwa

Wakili wa Serikali: Ikupendeze Mh Jaji Naitwa Robert Kidando nimeongozana na
1. Chriss ........
2. Abdallah Chavula
3. Jenitreza akitali
4. Ester Martin Ignas
5. Mwinuka Tulimanywa Majige

Kibatala: ikukupendeza Mheshimiwa Jaji naitwa Peter Kibatala nipo pamoja na

; 1. Alex Massaba
2. Seleman Matauka
3. Sisty Aloyce
4. Dickson Matata
5. Michael Mwangasa
6. Jonathan Mndeme
7. Hadija Aron
8. Evaresta Kisanga
9. Maria Mushi
10. Idd Msawanga
11. John Malya

JAJI: upande wa Jamhuri

Wakili wa Serikali: Shauri limekuja kwa ajili ya Re examination kwa Shahidi wa Kwanza, Yupo na tupo tayari kuendelea.

Jaji: Upande wa Utetezi..?

Kibatala: Na sisi tupo tayari Mheshimiwa Jaji

Jaji: Umesema kwa niaba ya Wenzio Siyo.?

Kibatala: Ndiyo

Jaji: Mshitakiwa namba 1,2,3, na 4 Wanainuka Kila Mmoja Ishara kwamba wapo Mhakamani

Jaji: Shahidi Jana ulihojiwa Maswali ya Dodoso na Upande wa Utetezi, Leo tukasema utakuja kwa ajili ya Re examination, Nakukumbusha bado upo chini ya kiapo.

Wakili wa Serikali: Jana Mtobesya alikuuliza wakati gani Jalada la Uchunguzi Lilifunguliwa na wakati gani Jalada la Kesi lilifunguliwa

Shahidi: Jalada la Uchunguzi tulikuwa tumefungia Baada ya Kukutana na Luteni Denis Urio katak Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai.

Wakili wa Serikali: Na Jalada la Kesi

Shahidi: Nilifungua baada ya Mimi Kupata Taarifa kuwa Vijana walipokuwa wanatafutwa na Luteni Urio kwa Amri ya Mbowe ndipo tulifungua Jalada.

Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali kuhusiana kama Ulikuwa na Taarifa ya kabla ya Kumchukua Maelezo Mshitakiwa wa Pili, Elezea ni taarifa gani.

Kibatala: OBJECTION swali lilikuwa kwamba Swala la Kumtafuta Moses Lijenje, Je Ulimuhoji Mshitakiwa wa Pili,"

Jaji: Wakili wa Serikali

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa sijauliza alichofanya Cross examination yeye, nipo kwa Mtobesya

JAJI: Uliza tena

Wakili wa Serikali: Uliulizwa kuhusu Kuwa na Taarifa za Moses Lijenje wakati unamuhoji Mshitakiwa wa Pili, Je ulijua Taarifa hizo kabla au Baada?

JAJI: Kibatala Umesikia Swali?

Kibatala: Nimesikia lakini kaniondoa Mimi, Sasa ni Eneo la Mtobesya

Shahidi: Nilipata Taarifa kuwa Freeman Mbowe alikuwa anatafuta Kundi la Waalifu

Kibatala: Wakili Mtobesya Hakufika huko, it's something New alisema alikuwa anatafuta Vijana

JAJI: Ndiyo namimi nimesikia hivyo Jana ulisema Alikuwa anatafuta Vijana siyo Kundi la Wahalifu

Shahidi: Ndiyo nilipata Taarifa kuwa Freeman Mbowe Alikuwa anatafuta Kundi la Vijana walioachishwa kazi Jeshini, Kwa dhumuni la Kudhuru Viongozi wa Serikali na Pia Mpango wa maandamano ya kushinikiza Viongozi ya siyo kuwa na Kikomo na Kwamba Lengo la Kufanya hivyo Nchi ........isitawalike na ionekane imefeli kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Wakili wa Serikali: Uliulizwa hapa Jana Kwamba wakati Mshitakiwa Wa pili Kama Ulikuwa Umempa Onyo, kuhusiana na Ukamataji, wewe Ukasema ulikuwa umeshampa Haki zake. Haki zake zipi?

Shahidi: Haki zake ni Pamoja na Kumfahamisha Kosa alilokuwa anashitakiwa nalo na Kwamba....... halazimishwi Kusema lolote ila Jambo analozungumza linaweza Kutumika kama Ushahidi Dhidi yake Mahakamani.

Wakili wa Serikali: Uliulizwa kwamba Matukio ya Kula Njama Yalifanyika kati ya 01 May 2020 na tarehe 05 August 2020 lakini katika Ushahidi wako ulisema Kula Njama huku kulifanyika tarehe 25 July 2020 hadi tarehe 01 August 2020 huko Aishi Hotel. Unasemeje Juu ya Ushahidi .......wako Kupinga na Hati ya Mashitaka?

Shahidi: Naomba Kuona hiyo Hati ya Mashitaka

Jaji: Utetezi Mapingamizi Juu ya Hilo

MTOBESYA: Hapana apewe tu

Shahidi: Miye naona Hakuna utofauti bado, ipo kati ya (in between) bado

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Swali Kuhusiana Maelezo ya mshitakiwa wa Kwanza kwamba yaliandikwa Chang'ombe ukasema ndiyo Ni kweli Na Maelezo Mshitakiwa wa pili na watatu yalichukuliwa Central Dar es Salaam Eleza kwanini uliamuru Maelezo ya Mtuhumiwa wa Kwanza .......yachukuliwe Chang'ombe?

Shahidi: Kwanza Chang'ombe ni Dar es Salaam, Pili uwezi kufananisha na Moshi, Alafu pia na angalia Masaa Manne.

Utetezi: OBJECTION Mheshimiwa Jaji wamuelekeze Shahidi wao Vizuri hatutaki kila Saa Kusimama Simama.

Jaji: Jamhuri

Wakili wa Serikali: Shahidi Eleza sababu tu kwanini uliamuru Maelezo ya Mshitakiwa wa 01 yachukuliwe Chang'ombe?

Shahidi: Baada ya Mshitakiwa kudanganya kuhusu Makazi yake.

Utetezi: OBJECTION Mheshimiwa Jaji hayo ya Kudanganya ni Mapya Sheria ya Ushahidi ipo wazi haupaswi Kuongea Mambo Mapya

Jaji: Nafikiri shida ipo kwenye Neno Kudanganywa hata Mimi sikusikia Neno "Kudanganywa" ondoa hilo Neno uendelee

Wakili wa Serikali: Uliulizwa kwamba Mshitakiwa wa Pili uliomuonya kuhusu Kula Njama ya kutenda Matendo ya ugaidi, kwanini hukumuonya na Makosa mengine

Kibatala: OBJECTION hayo niliuliza Mimi sikumuuliza kwanini Hukumuonya kila Shitaka, Nilikuwa nauliza kwa kila Kosa........Kama Mnataka twende hivyo tutaomba kumuhoji tena.

Jaji: Unasemaje wakili wa Serikali

Wakili wa Serikali: Nitarudia swali Mheshimiwa

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Swali kuhusiana na Kuamini na Kutoamini hasa kwenye sababu ya Wakili.

Shahidi: Nilikuwa siamini kwamba Mkuu wa Wilaya anaweza Kushusha Bendera lakini pia ndiyo iwe sababu ya Kumdhuru Kiongozi wa Serikali. Lakini statement niliiamini sababu alitoa yeye.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Kupatiwa Kielelezo P1

Wakili wa Serikali: Shahidi chukua Karatasi hii Nitakuuliza maeneo ambayo ulihojiwa na Mawakili wa Utetezi

Wakili wa Serikali: Tafuta eneo ulikohojiwa kuhusiana Kumfikisha Mheshimiwa Mikocheni, ukipata nitakuuliza swali

Mahakama Bado Ipo Kimya Shahidi anatafuta

Wakili wa Serikali: Baada ya Kufika Dar es Salaam na Kumfikisha Mheshimiwa Mikocheni, hujaona

Jaji: Labda uchukue Kwanza wewe Usome halafu umuonyeshe.

Wakili wa Serikali: Kama hawatokuwa na pingamizi

Kibatala: Hatuna Mheshimiwa Jaji

Wakili wa Serikali: Soma hapa

Shahidi: Baada ya Kufika Dar es Salaam na Kumfikisha Mheshimiwa Mikocheni Mimi na Mohammed tulipewa Laki mbili mbili baada ya Kesho yake kuwa anakuja Lissu na hakumpokea.

Wakili wa Serikali: Uliulizwa kuwa huyo Mheshimiwa ni nani ukasema sasa ieleze Mahakama Huyo Mheshimiwa ni nani?

Mtobesya: OBJECTION Mheshimiwa Jaji Kifungu cha 61 Cha Sheria ya Ushahidi Inasema Nyaraka Isitafsiriwe Bali Nyaraka ijieleze yenyewe, hapo Shahidi anaulizwa tafsiri.

Wakili wa Serikali: Naona hiyo Objection haina Mashiko sababu tutakuwa hatuna Cha Kufanya.

JAJI: Nafikiri Mtobesya Hoja yako inahusu Thamani ya Nyaraka, Sasa Mahakama itaangalia hicho anachokisema Kipo kwenye Nyaraka.?

MTOBESYA: Sawa Mheshimiwa Jaji

Shahidi: Ni Mheshimiwa Mbowe, Kwa sababu Mheshimiwa aliyetajwa kwenye Statement hii ni Mheshimiwa Mbowe na Mbowe Mwenyewe anaishi Mikocheni

Wakili wa Serikali: Uliulizwa pia kuhusiana na Kupewa Laki mbili na Mohammed, huyu Mohamed med ni nani?

Shahidi: Ni Ling'wenya kwa sababu huko Juu tulikuwa tunazungumzia Mohamed Ling'wenya na statement hii alikuwa anatoa Mwenyewe.

Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali Kama kwenye Statement hiyo, kama alivyoelezea yeye kama Mshitakiwa Wa pili Kama alimfuatilia Sabaya katika Maeneo aliyokuwa akienda Arusha Uliulizwa swali wewe Ukasema Hapana, Sasa nitakupeleka kwenye Statement halafu utafafanua.

Kibatala: OBJECTION samahani Mheshimiwa Jaji labda kwa Maelekezo yako nitakubali Maelekezo ya Mahakama, anachoulizwa Shahidi Alisha Jibu kuwa Hakuwa Arusha anaulizwaje Jambo hilo hilo tena.

JAJI: Nafikiri Ngoja tusubiri swali lake.

Wakili wa Serikali: Kwa Utaratibu wa Mahakama Kibatala anapaswa aongee kwa Ushahidi Kama Kuna kitu kweli Umekiona Kitolee Ushahidi, Siyo kuja na Neno Una suspect, Nani kafanya na Kitu gani Kimefanywa

Jaji: Kibatala ulikusudia Nimuonye, na Tunachukulia una Taarifa za ......kiintelijensia kwamba tumuonye shahidi kwa Intelijensia yako. Kibatala: Mimi nimesema Mahakama imuangalie.

Jaji: Basi kwa sababu Mimi sijaona naomba Upande wa jamhuri waendelee Kuuliza Maswali

Shahidi: Katika Kufuatilia Nyendo za Sabaya tulienda Club Kokoriko lakini hatukumpata Mheshimiwa Sabaya Siku hiyo.

Wakili wa Serikali: Eleza sasa Kwenye Statement hii Kama Mshitakiwa alifika Club Kokoriko.

Shahidi: Alifika

Wakili wa Serikali: Uliulizwa pia swali kuhusiana kama Kuna sehemu yoyote kama Mshitakiwa Wa Pili amechukuliwa finger print katika Statement hii, NI kwanini katika Statement hii hakuna Maelezo ya Kuchukuliwa finger Print

Shahidi: Mimi kama Mchunguzi nilishaona Hakuna haja.....Ya kuchukua Finger prints

Shahidi: Hitaji la Kuchukua Finger Prints lilikuwa baada ya Kumpekua Mshitakiwa Namba Moja na baada kukuta Kijitabu ikabidi sasa Kuchukua Finger Prints. Wakati nachukua Maelekezo Mshitakiwa wa pili ilikuwa tarehe 07 August 2020 kabla ya Kupata Kijitabu hicho.

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Kama Ulichukua Sampuli za Finger Prints za Pistol inavyodaiwa kukutwa na Mshitakiwa wa Pili. Sasa wewe Kama Mchunguzi ni kwanini hukuchukua Finger Prints na Sampuli za DNA.

Shahidi: Mimi sikuona haja ya kuchukua Finger Prints kwa sababu.......Mshitakiwa tulikuwa naye, Tunafanya Finger prints kama Mshitakiwa amevunja na hayupo Sisi Hatukuwa na hitaji hilo kama alivyo uliza wakili.

Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali kuwa Kwa kipindi Chote baada ya Kupata nia ya Uhalifu, kama ulimtaarifu Kiongozi aliyelengwa Ole Sabaya, kama ulimpatia taarifa. Ukasema hukumpati na wala Kamati ya Ulinzi ya mkoa wa Kilimanjaro, ni kwanini sasa.

Shahidi: Tulikuwa kuwa na....Uhakika wa Taarifa zetu, hatukuona sababu za kuwaambia Watu wengine kwa kuwa tunge Create Pressure.

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Wakati Mtuhumiwa wa kwanza anakamatwa palikuwa na Askari Jeshi na Ukasema Hakukuwa na Askari Jeshi

Shahidi: Hapakuwa na Askari Jeshi kwa sababu Mimi Ndiyo nilikuwa Arresting Officer na Nikisaidiwa na Inspector Mahita pamoja na ASP Mahita

Wakili wa Serikali: Uliulizwa kuhusiana na Maandamano Ukasema ni Sheria Inaruhusu lakini kwa Kufuata taratibu eleza Unamaana gani?

Shahidi: Ni kweli Sheria Inaruhusu Maandamano lakini kuna Sheria zingine pia zinaweka taratibu kuwa kabla ya Kufanya Maandamano awe amepata kibali

Wakili wa Serikali: Kibali gani

Shahidi: Cha Polisi

Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali Kuhusiana na Mtu wa Pili katika Maelezo yake kuwa Mtu Mmoja anaitwa Kakobe, Ukasema ukabaini Kuwa Mtu huyo anayeitwa Kakobe ndiyo Moses Lijenje, eleza ni wakati gani ulibaini

Shahidi: Wakati tunawakamata Watuhumiwa walikuwa wawili......lakini tulikuwa tuna Taarifa wapo watatu, Tukiwauliza Yupo wapi Mwenzetu Wakasema anaitwa Kakobe ambaye ndiyo Lijenje.

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Swali kuhusiana na Sheria ya Ushahidi Wakati wa Onyo Kuwa section one na Two hukuweka, Ukasema hiyo ni Curable, Ulikuwa unamaanisha nini.

Shahidi: Haiwezi Kuathiri Maelezo ya Kuonywa

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji tunaomba Tukomee hapa.

Jaji: anaandika Kidogo

JAJI: Upande wa Utetezi

Kibatala: Mheshimiwa Tumekubaliana kuwa hatuna Pingamizi lolote

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji tuna Shahidi Mwingine lakini Kabla ya Kuendelea naye tunaomba ahirisho fupi, Ikiwezekana tuweze Ku resume Saa 5:30.

Jaji: Maombi yanakubaliwa, tutarudi Mahakamani saa Tano na Nusu.

Jaji: Kama tumekukwaza Kwa niaba ya Mahakama naomba Radhi, Naomba Radhi kwa niaba ya Utetezi na Ninakushukuru Kwa Ushahidi wako.

Jaji anatoka Mahakamani

---------

JAJI anaingia

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021



Wakili wa Serikali Kidando
: Wapo tayari Kuendelea na Mashahidi

Jaji: Upande wa Utetezi Mpo tayari

Kibatala: Tupo tayari kwa ruhusa yako Mheshimiwa

Jaji: Shahidi wa Pili

Wakili wa Serikali: Shahidi amefuatwa

Mahakama ipo kimya ina subiri shahidi aingie

Shahidi amefika

JAJI: Majina shahidi: JUSTINE ELIYA

Jaji: Umri wako

Shahidi: Umri 31, Kabila Mmeru, Dini Mkrito, Shughuli Mkulima

Shahidi: Naapa Mbele ya Mahakama hii kuwa Ushahidi nitakao toa utakuwa ni kweli, kweli tupu Eenheeeee Mwenye Mungu nisaidie

Wakili wa Serikali: Ataongozwa na Wakili wa Serikali Abdallah Chavula

Jaji: Karibu

Wakili wa Serikali: Nitakuwa nakuhoji Maswali utakuwa unajibu kwa Kuelekea kwa Mheshimiwa Jaji

Wakili wa Serikali: Majina yako yapi:

Shahidi: Justine Eliya Kaaya

Wakili wa Serikali: Bw Kaaya Kwa sasa Shughuli zako ni Zipi?

Shahidi: Kilimo na Biashara

Wakili wa Serikali: Kilimo cha aina gani

Shahidi: Cha Mboga Mboga na Nafaka

Wakili wa Serikali: Unamaanisha nini

Shahidi: Mboga Mboga Nyanya, Vitunguu na Karoti na Nafaka, namaanisha Mahindi na Maharage

Wakili wa Serikali: Shughuli hizi unazifanyia wapi

Shahidi: Arumeru Mkoani Arusha

Wakili wa Serikali: Wateja wako hasa ni wanunuzi wa hayo mazao ni akina nani?

Shahidi: Ni watu tofauti Watanzania na Wageni wanaokuja Mkoa wa Arusha

Wakili wa Serikali: Unazifanyia wapi

Shahidi: Mkoani Arusha, wilaya ya Arumeru, Longido na Wilaya ya Arusha Mjini.

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Mwaka 2017 wewe Maskani yako yaliku a ni wapi?

Shahidi: Nilikuwa naishi Longido

Wakili wa Serikali: Wilaya ya Longido ipo Mkoa gani

Shahidi: Arusha

Wakili wa Serikali: Hapo Wilaya ya Longido ulikuwa unajishughulisha na Shughuli zipi?

Shahidi: Kupiga Picha na Kilimo katika Wilaya ya Arumeru

Wakili wa Serikali: Mwaka 2017 ulikuwa unajishughulisha na Kilimo cha aina gani

Shahidi: Nilikuwa nalima Karoti

Wakili wa Serikali: Wateja wako walikuwa ni akina nani?

Shahidi: Waliotoka Sokoni na baadhi ya watu pale Arusha

Wakili wa Serikali: Tueleze sasa hii Shughuli ya Kupiga Picha nayo, Ni Shughuli gani?

Shahidi: Picha za Mnato kwa kutumia Camera na Simu

Wakili wa Serikali: Ulikuwa ukiwapiga akina nani

Shahidi: Viongozi wa Serikali na Viongozi wa Kisiasa

Wakili wa Serikali: Unaweza ukatuambia ni akina nani hasa

Shahidi: Dr. Steven Kemomo Kiruswa Mbunge wa Longido

Wakili wa Serikali: Mwingine

Shahidi: Mrisho Gambo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Gabriel Daqaro aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Na wengine wengi

Wakili wa Serikali: Hao umewataja wa Ki-serikali, Je wa kisiasa

Shahidi: Lengai Ole Sabaya

Wakili wa Serikali: Huyu Lengai Ole Sabaya ulikutana naye wapi mara ya kwanza?

Shahidi: Mwaka 2017 Uchaguzi Mdogo wa Marudio Jimbo la Longido, Akanitaka nikamsaidie Kupiga Picha katika Shughuli zake zingine Mbalimbali

Wakili wa Serikali: Nini Kilijiri wakati huo baina yako wewe na yeye?

Shahidi: Alikuwa Diwani wa Kata ya Kisambasha, Wilaya ya Arumeru alivutiwa na Upigaji wangu wa picha

Wakili wa Serikali: Alikutaka ukamsaidie Wapi?

Shahidi: Katika kata yake ya kisambasha, Wilayani Arumeru

Wakili wa Serikali: Ulipokea Vipi Ombi hilo

Shahidi: Nilimkubalia kwa kuwa ilikuwa ni fursa kwangu

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama baada kukubali lile Ombi Utaratibu wa Ufanyaji kazi wenu ulikuwaje

Shahidi: Longido ni Mbali, hivyo ilinipasa kuhama Longido na Kuhamia Arusha, Nyumbani Kwa Lengai Ole Sabaya, Sehemu Inaitwa Kibanda Maziwa SAKINA

Wakili wa Serikali: Ulifanya kazi na Ole Sabaya na kuishi kwenye Nyumba yake kwa muda gani?

Shahidi: Mwaka 2017 Mpaka Mwaka 2018 July Alipoteuliwa Kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai

Wakili wa Serikali: Wewe ulienda kuishi wapi baada ya Kuteuliwa?

Shahidi: Nilienda Kuishi naye Hai Mkoani Kilimanjaro katika Makazi ya Mkuu wa Wilaya

Wakili wa Serikali: Kwenye hiyo Nyumba ya Ole Sabaya ulikuwa ukiishi na nani?

Shahidi: Yeye Mwenyewe Sabaya na Mke wake Jesca

Wakili wa Serikali: Ulipokuwa ukiishi naye wewe hasa ulikuwa Ukifanya Shughuli zipi

Shahidi: Kufanya Shughuli zake ndogo Ndogo ikiwemo Kumpelekea Nguo zake Dry Cleaner, Ikiwemo Kumpelekea Chai na Chakula Ofisini Kila Siku.

Wakili wa Serikali: Katika hiyo Nyumba ya Mkuu wa Wilaya Hai, Lengai Ole Sabaya Ulikuwa ukiishi na nani?

Shahidi: Nilikuwa nikiishi naye, yeye Mwenyewe na Mke wake.

Wakili wa Serikali: Umeishi Pale kwa Muda gani?

Shahidi: Kutoka July 2018 Mpaka Mwezi wa 10, 2018

Wakili wa Serikali: Nini kilitokea?

Shahidi: Niliamua Kurudi Longido Kuendelea na Shughuli zangu Nyingine sababu nikiacha Mchumba na Kutaka Kusimamia Shughuli zangu zingine za Kilimo.

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama sasa Mwaka 2018 uliporudi Longido unaweza Kukumbuka watu gani katika Medani za Kisiasa Ulianza Kufanya nao Mawasiliano

Utetezi: OBJECTION, Quite Leading kwa Kutaka Kuuliza ni watu gani wa Kisiasa Ulifanya Mawasiliano nao.

Wakili wa Serikali: Shahidi hebu tuambie Ulifanya Mawasiliano na Watu Gani?

Shahidi: Siku Moja nikiwa nyumbani nilipigiwa simu kwenye simu yangu Airtel 0693006700 kutoka kwenye namba ya Airtel 0784779944 na Mtu aliyejitambulisha Kuwa ni Freeman Mbowe

Wakili wa Serikali: Akakwambia kitu gani?

Shahidi: Nilishtuka sana akaniuliza Ujambo?. Nikamwambia sijambo akasema anashida ya Kuniona

Wakili wa Serikali: Ukafanyeje?

Shahidi: Nikamuuliza Upo wapi, Akajibu yupo Arusha

Wakili wa Serikali: Ukajibu Kitu gani,

Shahidi: Nikamwambia Nipo Longido kwa sasa Siwezi Kuja kwa sababu ya Changamoto ya Usafiri

Wakili wa Serikali: Nini Kikatokea?

Shahidi: Akaniambia Chukua Gari Noah Gharama Nitakuja Kulipa Ukifika Arusha. Kwa sababu ya Ile hofu nikamwambia siwezi Kuja

Wakili wa Serikali: Hofu ya Nini?

Shahidi: Kwanza Nikiongozi Mkubwa lakini Pia sina Ukaribu na Yeye

Wakili wa Serikali: Baada ya Kumueleza hayo nini Kilitokea

Shahidi: Aliniambia Subiri nakupigia, akakata simu.

Shahidi: Baada ya Muda akaniambia nipo Njiani nakufuata Longido.

Wakili wa Serikali: Muitikio wako ulikuwaje?

Shahidi: Kwa kuwa alisema yupo Njiani nakuja nikasema wacha nisubiri nisingeweza Kumzuia

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama nini kilitokea

Shahidi: Baada ya Dakika 40 alinipigia Simu kuwa Njoo hapa Uwanja wa Mpira

Wakili wa Serikali: Uwanja wa Mpira wa wapi?

Shahidi: Ndani ya mji Mdogo wa Longido

Wakili wa Serikali: Baada ya Kumueleza hayo Ulichukua hatua zipi?

Shahidi: Nilichukua Bodaboda na Kwenda

Wakili wa Serikali: Tuambie yaliyojiri

Shahidi: Akunichukua Bodaboda Nikaenda mpaka Uwanjani, na Kukuta Gari inaunguruma

Wakili wa Serikali: Ilikuwa ni Majira ya Muda gani

Shahidi: Saa 3 Usiku

Wakili wa Serikali: Baada ya kukuta gari,

Shahidi: Akaniambia Sogea hapa kwenye Gari Kwa namba ile ile ya 0784779944, Akaniambia ingia Kwenye gari Chief acha Kuogopa

Wakili wa Serikali: Kwenye Gari kulikuwa Kuna watu wangapi?

Shahidi: Nilimkuta yeye na Dereva na Nyuma ya upande wa Dereva palikuwa na Mwanamke

Wakili wa Serikali: Alikwambia Dhumuni lake lilikuwa na Ujumbe gani?

Shahidi: Akaniambia kuwa Lengai anamsumbua Sana

Wakili wa Serikali: Lengai ni nani..?

Shahidi: Mkuu wa Wilaya ya Hai

Wakili wa Serikali: Endelea

Shahidi: Akataka nimpatie Taarifa na Shughuli anazofanya pamoja na Watu anaofanya nao kazi pale Hai

Shahidi: Nikamwambia haitowezekana, kwa sababu mimi Sipo tena kwa Sabaya

Wakili wa Serikali: Ulipomueleza haya, yeye alifanya nini?

Shahidi: Akaniambia yeye Kiongozi Mkuu wa Chama Cha Upinzani Kwenye Nchi hii, Hivyo atafanya Vyovyote vile anavyoweza ili nirudi kwa Sabaya Kuendelea na Kazi

Wakili wa Serikali: Muitikio wako Ulikuwa ni Upi?

Shahidi: Nikamwambia haitowezekana kwa sababu nimechagua Kufanya Shughuli zangu Binafsi

Wakili wa Serikali: Nini Kilitokea?

Shahidi: Akaniambia samahani kwa Usumbufu wa Kunisumbua na akanipa TSh Laki 3

Wakili wa Serikali: Nini kikaendelea?

Shahidi: Akaniambia ni za Usumbufu, Tutawasiliana

Wakili wa Serikali: Nini kiliendelea

Shahidi: Tuliagana na aliondoka

Wakili wa Serikali: Baada ya Yeye Kuondoka wewe Ulielekea wapi

Shahidi: Baada ya kushuka kwenye Gari nilimpigia Ole Sabaya simu lakini hakupokea simu

Wakili wa Serikali: Wewe Ulienda wapi sasa

Shahidi: Nilibakia pale pale kwenye Uwanja na Kumpigia Dr Steven Kiruswa na Kumueleza kilichotokea?

Wakili wa Serikali: Wewe sasa Ulienda wapi?

Shahidi: nilirudi Nyumbani Kwangu

Wakili wa Serikali: Ulirudi Vipi Nyumbani kwako

Shahidi: Niliita Bodaboda nikarudi Nyumbani Kwangu

Wakili wa Serikali: Ni wakati gani tena Ulikuja kuwasiliana na Mtu uliye mtaja kuwa ni Freeman Mbowe pale uwanjani?

Shahidi: Mwaka 2020 Mwanzoni alinipigia Simu kupitia Whatsap

Wakili wa Serikali: Kwa namba ipi?

Shahidi: Kwa namba ile ile ya 0784779944

Wakili wa Serikali: Alikuwa na ujumbe gani

Shahidi: Akasema tumepotezana sana Chief

Wakili wa Serikali: Alikupa ujumbe gani?

Shahidi: Akasema anataka tuonane

Wakili wa Serikali: Wapi?

Shahidi: Moshi, wakati huo nilikuwa Arusha

Wakili wa Serikali: We Ukasemaje?

Shahidi: Ngoja nimalizie Kumwagilizia Shambani huku nikishamaliza nitakuja

Wakili wa Serikali: Nini kilitokea Kutokana na ahadi yenu?

Shahidi: Baada ya Kumalizia Shughuli zangu nilipanda Costa na Kumpigia Simu Kwamba naenda

Wakili wa Serikali: Ulipanda Costa Kuelekea wapi?

Shahidi: Moshi Kilimanjaro

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama ukifika hadi wapi?

Shahidi: Baada ya Kumpa Taarifa kuwa Nipo kwenye gari akasema nishuke Machame road.

Wakili wa Serikali: Kwa namba ipi?

Shahidi: ile ile ya 0784779944

Wakili wa Serikali: Ulipomueleza akakupa Maelekezo yepi?

Shahidi: Akaniambia nishuke Machame Road

Wakili wa Serikali: Ipo wapi?

Shahidi: Ipo Wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro

Wakili wa Serikali: Tueleze sasa baada ya Kupewa Maelekezo hayo nini kilitokea?

Shahidi: Nilishuka kwenye Gari nikapiga tena simu

Wakili wa Serikali: Simu ipi?

Shahidi: Namba yake ile ile ya 0784779944

Wakili wa Serikali: Ulipompigia simu nini kilitokea?

Shahidi: Akaniambia ni subiri hapo nakuja

Wakili wa Serikali: Nini kilijiri?

Shahidi: Baada ya Muda akinipigia simu kuniambia, Umefika, umekaa Upande upi, Akaniambia Vuka kaa Upande wa Kulia.

Wakili wa Serikali: We Ulikutana na nini?

Shahidi: Palikuwa na Barabara ya kwenda Machame na Nyingine kwenda Arusha na Nyingine Moshi

Wakili wa Serikali: Nini kikatokea?

Shahidi: Ilikuja Gari aina ya Land cruiser V8 Yenye Mlingoti na Bendera ya Bunge ikiwa na Plate Namba zilizoandikwa KUB

Wakili wa Serikali: Nini kilitokea?

Shahidi: Ilisimama Upande wangu, ikashusha Kioo Upande wa Abiria, nikamuona Mwenyekiti akaniambia Panda

Wakili wa Serikali: Baada ya Kuambiwa Upande nini kili tokea?

Shahidi: Alishuka Mtu kutoka Siti ya Nyuma akaniambia pita nikaingia kwenye Gari

Wakili wa Serikali: Enheeeee

Shahidi: Ile gari ilienda Muelekeo wa Kwenda Machame, Baadae tukaingia sehemu ambayo nilikuja Kugundua Hotel ya Aishi

Wakili wa Serikali: Palikuwa na watu gani kwenye Gari?

Shahidi: Palikuwa na Dereva na huyo Mlinzi wake aliyenipisha nikaingia kwenye Gari

Wakili wa Serikali: Mahusiano yenu ya Dereva na huyo Mlinzi kabla ya Siku hiyo yalikuwaje?

Shahidi: Tulikuwa hatufahamiani

Wakili wa Serikali: Ulijuaje aliyekupisha kuwa ni Mlinzi wake

Shahidi: Baada ya Yeye Kunitambulisha kuwa ni Mlinzi lakini pia ni Diwani wa Kata ya kiboriloni

Wakili wa Serikali: Baada ya Dakika 08 Mlifika wapi Vile?

Shahidi: Hotel ya Aishi Machame Wakili wa Serikali: Wewe ulitambuaje

Shahidi: Sababu ya Kibao Kilichoandikwa Aishi Hotel

Wakili wa Serikali: Tueleze sasa yaliyotokea

Shahidi: Baadae tulishuka kwenye Gari Mimi, yeye na Yule Mlinzi wake

Wakili wa serikali: Mlivyoshuka nini Kiliendelea?

Shahidi: Tulielekea Upande wa Mgahawa

Wakili wa Serikali: Umekuwa ukielezea Yeye na Mlinzi wake. Mlinzi wake na Yeye nani?

Shahidi: Freeman Mbowe

Wakili wa Serikali: Baada ya kushuka kwenye Mgahawa

Shahidi: Akasema tuongee kidogo sababu anamikutano kwenye jimbo lake akaniambia niagize Chakula

Wakili wa Serikali: Muda huo ilikuwa saa ngapi?

Shahidi: Saa Saba Mchana

Wakili wa Serikali: Wakati anakutaka Mkutane Moshi ilikuwa ni Saa Ngapi?

Shahidi: Saa Mbili Asubuhi

Wakili wa Serikali: Wewe Safari yako Kuelekea Moshi ulianza Saa ngapi?

Shahidi: Saa Tano kasoro

Wakili wa Serikali: Ulianzia wapi hiyo saa Tano kasoro

Shahidi: Sehemu inaitwa Kilala Wilaya ya Arumeru

Wakili wa Serikali: Alikwambia nini sasa?

Shahidi: Akauliza Mnampango gani Juu ya Mkutano inayoendelea Jimboni

Wakili wa Serikali: Jambo gani lingine alikwambia

Shahidi: Akaomba nimtajie wale wasaidizi wa Sabaya alipokuwa anatembea nao

Wakili wa Serikali: Wewe ulimwambia nini

Shahidi: Nilimwambia sina Taarifa yoyote ya kumwambia kwa wakati ule

Wakili wa Serikali: Nataka kuhusu hayo Majina

Shahidi: Nikimtajia Majina na Yule Diwani akawa anaandika kwenye Kikaratasi

1.Japhet Rwendela
2.Vedastus sibula
3.Mtoto wa Mkulima
4.Sylvester Nyegu
5.Binti wa kichaga
6.Mwalimu Doreen
7.Watson Malimumgu

JAJI: Mtoto wa Mkulima na Binti wa Kichaga ni Majina?

Shahidi: Ndiyo Majina nilivyokuwa nayafahamu wanayatumia kwenye Mitandao

Wakili wa Serikali: Kipi Kingine alikueleza

Shahidi: Nilitoa hizo namba kwenye simu niliwatajia Wakaziandika

Wakili wa Serikali: Lipi lingine alikueleza

Shahidi: Akasema atashughulika nao tutawasiliana na Wewe na Mimi baadae

Wakili wa Serikali: Nini kilitokea Baina yako wewe na yeye?

Shahidi: Akaniaga kasema atanitumia Chochote jioni

Wakili wa Serikali: Ulisema Chochote umaanisha nini?

Shahidi: Gharama zangu za Nauli

Wakili wa Serikali: Ilikuwaje baada ya hiyo ahadi

Shahidi: Hakutimiza hiyo ahadi na pia hakunitafuta baada ya pale

Wakili wa Serikali: Baada ya Makutano yenu pale Aishi Hotel wewe ukielekea wapi?

Shahidi: Nilirudi Arusha

Wakili wa Serikali: Ni wakati gani Mwingine uliwasiliana na Mbowe?

Shahidi: Mwezi 07 Mwaka 2020

Wakili wa Serikali: Tarehe ngapi?

Shahidi: Sikumbuki tarehe

Wakili wa Serikali: alikutafuta kwa namna gani

Shahidi: Alinipigia kwa Njia ya Mtandao wa Whatsap

Wakili wa Serikali: Kwa namba ipi

Shahidi: 0784779944

Wakili wa Serikali: ujumbe wake ulikuwa nini

Shahidi: Nipo Dar es Salaam nakuja Moshi, Naomba tuonane Nina Jambo la Kuzungumza na wewe

Wakili wa Serikali: Wakati huo wewe ulikuwa wapi

Shahidi: Shambani Kwangu Maji ya Chai

Wakili wa Serikali: Majira ya Saa ngapi

Shahidi: Mchana wa Saa Nane

Wakili wa Serikali: Ulichukua hatua zipi baada ya Ujumbe huo

Shahidi: Nikafanya Shughuli zangu, nikaanza Safari ya kwenda Moshi

Wakili wa Serikali: na ulienda Moshi kwa aina gani ya Usafiri

Shahidi: nikipanda Basi la Kilimanjaro Kutokea singida

Wakili wa Serikali: ahadi ilikuwa Mkutane Majira gani

Shahidi: alisema Saa 1 atakuwa amefika Moshi

Wakili wa Serikali: baada ya Kupanda Basi la Kilimanjaro ulifikia wapi

Shahidi: Moshi stendi

Wakili wa Serikali: wakati unashuka ilikuwa Majira gani

Shahidi: Saa 1 Usiku

Wakili wa Serikali: ikawaje

Shahidi: nilimpigia Simu Freeman Mbowe kuwa nimefika

Wakili wa Serikali: Kwa namba gani

Shahidi: 0784779944

Wakili wa Serikali: akasemaje

Shahidi: nichukie Pikipiki nimfuate Keys Hotel

Wakili wa Serikali: Baada ya Maelekezo hayo nini kilitokea

Shahidi: Niliita Bodaboda Nikaenda Hadi Keys Hotel na baada ya Kufika Keys Hotel nikampigia Freeman Mbowe kwamba Nimefika

Wakili wa Serikali: Kwa namba ipi

Shahidi: 0784 779944, Nikamwambia nimefika, Akasema namtuma Msaidizi wangu anifuate

Wakili wa Serikali: Baada ya hapo nini kilitokea

Shahidi: alikuja Dereva wake ambaye namtambua kwa Jina Moja la Willy

Wakili wa Serikali: Nini hasa kilikufanya Umtambue

Shahidi: Siku nakutana naye kwa Mara ya Kwanza Machame ndiye aliyekuwa anamuendesha na Alinitambulisha

Wakili wa Serikali: Kule Nyuma ya Hotel Ulipoenda, Nyuma ya swimming ukikutana na Jambo gani

Shahidi: waliniambia Mheshimiwa Yupo Kwenye Kikao, Tukae hapa tukiwa tunasubiria amalizie Kikao

Wakili wa Serikali: ukiacha wewe na Dereva nani Mwingine Mlikaa naye

Shahidi: tulikaa na Mlinzi wake alikuwa baunsa baunsa Kidogo

Wakili wa Serikali: Ulifahamu Vipi huyo Baunsa baunsa ni Mlinzi wake

Shahidi: Willy aliniambia, huyo ni Mlinzi wa Mheshimiwa usiwe na wasi wasi

Wakili wa Serikali: nini kiliendelea hapo Mlipokuwa mmekaa

Shahidi: tulikula baada ya kula Mlinzi wake akaenda Kule alipokuwa Mwenyekiti Freeman Mbowe, na baada ya muda alirudi na Kusema tunaondoka

Wakili wa Serikali: Wewe SHAHIDI ulijuaje Kuwa Kule alipo Mwenyekiti ndipo alikuwa Mwenyekiti

Shahidi: Ilikuwa ni sehemu ya wazi tulikuwa tumetengenishwa na Swimming Pool

Wakili wa Serikali: tueleze wakati hayo yanatokea ilikuwa ni Majira ya saa ngapi

Shahidi: Saa tatu kasoro Usiku

Wakili wa Serikali: aliporudi na kuwaambia sasa mnaomdoka, nini kilitokea

Shahidi: Tulinyanyuka wote na kuelekea Kule alipo Freeman Mbowe

Wakili wa Serikali: tueleze wakati hayo yanatokea ilikuwa ni Majira ya saa ngapi

Shahidi: Saa tatu kasoro Usiku

Wakili wa Serikali: aliporudi na kuwaambia sasa mnaomdoka, nini kilitokea

Shahidi: Tulinyanyuka wote na kuelekea Kule alipo Freeman Mbowe

Wakili wa Serikali: Mlipoelekea huko alipokwepo Mwenyekiti nini Kilitokea

Shahidi: akatuambia pole sana kwa kutuweka, Baada ya muda Mlinzi wake akatufungulia Mlango wa Gari, Naye Mwenyekiti akaingia kwenye gari na nyuma ya Dereva akaingia aliyekuwa mlinzi wa Chadema Joyce Mukya

Mimi NikaKaa Katikati na Nyuma akakata Mlinzi wake

Wakili wa Serikali: Mlielekea wapi

Shahidi: tukitoka keys Hotel tukaelekea Mwelekeo wa Arusha

Wakili wa Serikali: iliwafikisha wapi

Shahidi: Aishi Hotel

Wakili wa Serikali: We Ulijuaje Kuwa Mmefika Aishi Hotel

Shahidi: nilishafika pale, haikuwa mara ya kwanza

Wakili wa Serikali: nini Kilitokea

Shahidi: aliwaambia watangulie ndani sisi tuna Kikao kifupi

Wakili wa Serikali: Kikao Kifupi mlifanya nani na nani

Shahidi: Freeman Mbowe, Mlinzi wake. Dereva alipotaka Kujumuika akamwambia hiki Kikao ni Cha watu watatu

Wakili wa Serikali: Hebu tuambie sasa, Mahusiano yako na Huyu Mtu unayesema ni Mlinzi, kabla yakikuwaje

Shahidi: nilikuwa sifahamiani naye

Wakili wa Serikali: Kwenye hicho Kikao mliongea Maswala gani

Shahidi: alinitambulisha kwanza kuwa Huyu ni Mlinzi wake anaitwa Khalfani Bwire na Msiri wake na hivyo niwe huru Kuzungumza naye

Wakili wa Serikali: yeye Mlinzi alikuwa wapi

Shahidi: tulikuwa tumekaa naye Upande wa kushoto

Wakili wa Serikali: Kikao chenu Mlizungumza Mambo yepi

Shahidi: alikuwa ananiambia nitaje tena Majina ya wale Vijana na Namba zao za simu na kazi wanazozifanya kwa Sabaya

Wakili wa Serikali: Wewe baada ya kukutaka Ufanye hivyo Ulichukua hatua gani

Shahidi: Kabla ya kuanza kuwataja nikamtaka Mlinzi wake akachukue kalamu na Karatasi ilituweze kuandika

Wakili wa Serikali: Baada ya hayo Maelekezo ikawaje

Shahidi: alirudi na kalamu na Karatasi Nikaanza Kuziandika

Wakili wa Serikali: Wewe Majina na namba za Simu za hao watu wewe ulizitoa wapi

Shahidi: nilikuwa nawafahamu tangu nafanya kazi kwa Sabaya

Wakili wa Serikali: hizo namba za Simu ulizitoa wapi wewe

Shahidi: nilizitoa kwenye simu

Wakili wa Serikali: Majina ya akina nani shahidi:
1. Japhet Rwendela
2. Vedastus sibula
3. Mtoto wa Mkulima
4. Sylvester Nyegu
5. Binti wa kichaga
6. Mwalimu Doreen
7. Watson Malimumgu
8. Enock kirigiti

Baada ya pale aliniambia nimtajie sehemu anazopenda kutembelea Mheshimiwa Sabaya

Wakili wa Serikali: Ulimtajia Sehemu gani

Shahidi:
1. Cocoriko Annex iliyopo Arusha
2. Cocoriko ya kijenge
3. The Don, Ipo karibu na Tanzania Breweries
4. Milestone Park iliyopo Sakina

Na hotel anazolala Sabaya
1. SG resort Iliyopo Sakina Arusha
2. Golden Crest Hotel ipo Arusha

Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama baada ya kuwa wewe Umetoa Taarifa hizi ulifanya nini

Shahidi: Nilimuuliza mwenyekiti haya Majina na hizi sehemu unataka za Nini?

Akaniambia hilo niachie Mimi kazi yako hapa Imeisha.

Wakili wa Serikali: Lingine nini lilijitokeza baada ya mazungumzo yake

Shahidi: akaniambia nimkabidhi Khalfani Bwire Yake majina, Khalfani BWIRE akasema huyu Sabaya ni Mtu Mdogo sana Nitamchezesha. Baada ya pale Mwenyekiti akaniambia kazi Ndiyo inaanza rasmi kuanzia sasa hivi nitakuwa na Kulipa Mshahara

Wakili wa Serikali: ilikuwa ni Majira ya saa ngapi

Shahidi: Takribani saa 4 usiku

Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama wewe baada ya yale Mazungumzo Ulielekea wapi

Shahidi: alisema wewe utapewa Chumba utalala hapa baada ya muda kuwa Umekwenda

Wakili wa Serikali: kingine

Shahidi: ilibidi nilale kwa sababu nisingepata Usafiri wa Kwenda Arusha

Wakili wa Serikali: nini kilifuatia

Shahidi: Kesho yake Asubuhi alinipatia TSh Laki Mbili kwenye namba yangu ya 0754916666 kutoka Airtel Money yenye namba 0784 779944.

Wakili wa Serikali: baada ya hapo Ulielekea wapi

Shahidi: Nilirudi Arusha kuendelea na Kazi zangu za Shambani

Wakili wa Serikali: Ni wakati Mwingine upi tena Ulikuja kuwasiliana tena na Mwenyekiti

Shahidi: hatukuwasiliana tena kwa sababu tarehe 25 August 2020 nilikamatwa na Askari wa Jeshi la Polisi

Wakili wa Serikali: Ulikamatiwa wapi

Shahidi: Makumira, Wilaya ya Arumeru nikiwa napanda CRDB, USA RIVER

Wakili wa Serikali: ulikuwa unapelekea CRDB pesa za Nini?

Shahidi: Nimetoka Kuuza Mazao Shambani

Wakili wa Serikali: Mazao gani

Shahidi: Karoti

Wakili wa Serikali: Ulikuwa umewauzia watu gani

Shahidi: Watu wa Mount Meru, wao walikuwa wanapeleka Game site huko Ngorongoro

Wakili wa Serikali: ulikuwa na Kiasi gani

Shahidi: Dollar za Kimarekani 1100 na TSh Millioni Moja Laki Moja na Kumi na Saba Pamoja na Euro 240

Wakili wa Serikali: baada ya Kumatwa nini Kilifuata

Shahidi: Nilikamatwa nikapakizwa Kwenye gari ni kapeleka Kituo Kikuu cha Arusha

Baada ya Lisa Moja Nilienda Kupekuliwa Nyumbani kwangu

Na Baadae Kusafirisha Kuletwa Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama zile pesa zako zilikuwa wapi

Shahidi: zilikuwa Mikono Mwa Askari pamoja na Simu zangu

Wakili wa Serikali: ilikuwaje hizo fedha

Shahidi: walinipekua kutoka katika mifuko yangu wakasema ni Noti bandia

Wakili wa Serikali: walipokukamata walikueleza wanakukamata kwa Makosa gani

Shahidi: Kwamba Nina tuhuma za kujihusisha Kula njama za kufanya Vitendo Vya ugaidi

Wakili wa Serikali: tueleze sasa Ulipofikishwa Dar es Salaam nini kilikusibu

Shahidi: Baada ya kufikishwa kituo cha polisi Dar es Salaam nilifanyiwa mahojiano na afande Mahita

Wakili wa Serikali: baada ya Mahojiano

Shahidi: Niliweka lockup Mpaka nilipofikishwa Mahakamani Kisutu

Wakili wa Serikali: Mahakamani Kisutu Ulipofikishwa ulifikishwa kwa sababu zipo

Shahidi: nilifungukiwa mashitaka Mbalimbali ikiwemo Kushiriki Vikao Vyakutenda Mambo ya kigaidi, Kula Njama za kutenda ugaidi, Kesi ya Utakatishaji wa Fedha

Wakili wa Serikali: Eleza Mahakama sasa Kwa kuanza na Khalfani Bwire we ulikutana naye wapi kabla ya Kuunganishwa naye

Shahidi: Nilikutana naye akiwa Keys Hotel na Aishi Hotel akiwa na Freeman Mbowe

Wakili wa Serikali: VIPI kuhusiana na Mohammed Ling'wenya

Shahidi: huyo sifahamu nilikutana naye Mara ya Kwanza Gerezani

Wakili wa Serikali: VIPI kuhusiana na Adam kasekwa

Shahidi: huyo simfahamu pia

Wakili wa Serikali: baada ya kuwa umeunganishwa kwenye kesi hiyo Mahakama ya kisutu ulipeleka wapi

Shahidi: Nilipelekwa Gereza la Ukonga

Wakili wa Serikali: ulikuwa na akina nani

Shahidi: kila mtu alikuwa na wing yake, Nilikuwa na Khalfani Bwire na baadae kaongezeaka Mtu anaitwa a Khalid Athuman na Baadae akaongezeka Mohamed Ling'wenya akitokea Segerea

Wakili wa Serikali: Umekuwa kwenye kesi ile kwa muda gani

Shahidi: Kwa Miezi 11

Wakili wa Serikali: Nini kilitokea Shahidi: aliletwa Mheshimiwa Mbowe Siku ya 26 July 2021 alitukuta tukiwa na Khalfani Bwire, akasema Poleni sana Nimekuja kuwatoa.

Wakili wa Serikali: Baada ya Kauli hiyo nini Kilitokea

Shahidi: Asubuhi watu wa Magereza walikuja Kusema tujiandae tunaenda Mahakamani Kesho yake 27 July 2021 tulipelekwa Kisutu Mbele ya Hakimu Mzee Simba Mimi, Khalid Athuman (Mshitakiwa 05) na Gabriel Muhina (Mshitakiwa wa 6)

Mwanasheria akasema bada ya Upelelezi, Sisi hatuhusiki kwa hiyo tumefutiwa mashitaka kwa kifungu kidogo Baada ya pale niliondoka kutoka Mahakamani kwenda kwa Mdogo wake Kitunda Kesho yake nikarudi Mahakamani Kwa Mwendesha Mashitaka Kuuliza Vitu vyangu

JAJI: ni sehemu ya Ushahidi wenu kwamba alienda Mdogo

Wakili wa Serikali: Hapana Mheshimiwa

Shahidi: Kesho yake nilipoenda Kisutu Kuuliza Utaratibu wa fedha zangu wakanielekeza niende Central Police Dar es Salaam Nikaenda Kuonana na Inspector Swila akaniandika Maelezo baada ya Kuniandika a maelezo akanipa Vitu Vyangu

Wakili wa Serikali: Umemtaja Mtu anaitwa Freeman Mbowe, Khalfani Bwire, Mohamed Ling'wenya, Just unaweza Kuwatambua

Shahidi: Ndiyo, wapo hapa mahakamani

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba sasa awatambue Hapa Mahakamani

JAJI: Utetezi

Kibatala: Hatuna Pingamizi

SHAHIDI anatembea anaenda Kumtaja Kila Mmoja kwa Jina Lake

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji siye ni hayo tu

JAJI: upande wa Utetezi

Jaji: mkizingatia ni Muda wa Mapumziko

Kibatala: tunaweza za Kushauriana nao?

Jaji: sawa Kibatala" tunapendekezo kwamba tukuombe Tu-break Kwa Dakika 30

Jaji: Saa 8:25 tutarudi tena Kuendelea

Jaji anatoka.

Jaji amerudi

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021, inatajwa

Jamhuri Kolamu yao ipo Vile vile

Upande wa Utetezi Kolamu yao Ipo Vile vile

Utetezi: wanaomba wanamtambulishe na wamjumuishe Wakili Nashon Nkungu Kwa sababu alikuwa Mahakama Kuu kwenye kesi Nyingine Asubuhi ya Leo.

Jaji: Sasa tulikuwa tumebakiza Upande wa Cross examination na ningependa Kuanza na wakili wa Mshitakiwa namba Moja

MTOBESYA: Nitakuwa sahihi nikisema kwamba katika Ushahidi wako hukutoa uthibitisho Wako wako kwamba Ulikuwa Ukifanya kazi kwa Ole Sabaya

Shahidi: Siyo sahihi

Mtobesya: Mwambie sasa Mheshimiwa Jaji ni uthibitisho upi Umetoa Mbele ya Mahakama hii

Shahidi: Muulize Mheshimiwa Mbowe ndiyo atakwambia kama nilikuwa nafanya kazi.

Jaji: Mbowe siyo shahidi

Jaji: labda Wakili urudie swali

Mtobesya: Ni sahihi Kwamba umesema ulikuwa unafanya kazi na Ole sabaya

Shahidi: sahihi

MTOBESYA: ni sahihi sasa kwamba Hukutoa chochote Mahakamani Kuthibitisha

Shahidi: Ndiyo sikutoa

Mtobesya: Umesema katika Ushahidi Wako kuwa ulikuwa unasafikiri Kutoka Longido kuja Moshi na kutoka Arusha Kuja Moshi ulikuwa unatumia Usafiri gani

Shahidi: Usafiri wa Umma

MTOBESYA: Ni matumaini yangu kuwa Ulipanda Basi la Umma unapewa Ticket

Shahidi: inategemea na hilo Basi

MTOBESYA: Mwambie Sasa Mheshimiwa Jaji kwamba wewe hukutoa Ticket

Shahidi: Si kutoa Ticket kwa sababu nilipandia Njiani.

MTOBESYA: kwa hiyo nipo sahihi kwamba huku safiri kwa sababu hukutoa Ticket wala Uthibitisho Wako wowote hapa Mahakamani

Shahidi: Siyo sahihi, Siyo lazima uwe na Ticket kuthibitisha.

Mtobesya: Okey Tunashukuru

Mtobesya: Tangu Ukutane na Mbowe Mpaka Unakutana na Inspector Swila ni Muda umepita

Shahidi: Umeuliza Swali siyo Sahihi

JAJI: ukuliza na Mawakili wa Serikali Wamenyamaza na Mahakama haijaingilia Ujue hilo swali ni sahihi, utatakiwa ujibu. kama hufahamu Shahidi Jibu sifahamu.

Mtobesya: Tangu huyo unayemuita Mbowe Mkutane ni Muda gani umepita

Shahidi: Mwaka moja na Nusu

Mtobesya: Kuna lolote alikuachia afande Swila baada ya kukuandika Maelezo

Shahidi: Hakuna aliloniachia baada ya Kuandika Maelezo akanipa Vitu vyangu nikaondoka

Mtobesya: kwa hiyo swila hakukwambia kwamba Siku Moja Maelezo yako anayoandika yatatumika kama Ushahidi

Shahidi: Hakuniambia

Mtobesya: alichokiandika Alikupa ukakisoma

Shahidi: Ndiyo alinipa nikasoma

Mtobesya: Ukajiridhisha Kwamba ulichokisema ni sahihi

Shahidi: ni sahihi, Ndiyo

Mtobesya: Hakuna Wakati alikwambia kuwa Umpatie kila kitu, umwambie unakijua

Shahidi: Hapana

Mtobesya: Unauhakika ulichoandika ndicho Ulichosema Leo Mahakamani

Shahidi: Ndiyo hichohicho

Mtobesya: Kwa Bahati nzuri sisi Mawakili wa Utetezi tuna nafasi ya Kupewa Nyaraka za Maelezo mliyoandika Mheshimiwa Jaji naomba nipewe Original Document ya hii, Na Msingi wangu wa Kuomba Ni Kifungu cha 164 cha Sheria ya Ushahidi

Mawakili wa Serikali Hatuna Pingamizi Mheshimiwa Mtobesya anatembea Kumfuata Shahidi alipo

Mtobesya: pitia Nyaraka hii Kama ndiyo Swila aliyoyaandika na Kama Ulikubali kuwa sahihi

Shahidi: Haya Ndiyo Maelezo yangu ya Kwanza

Mtobesya: Unaweza Kusoma?

Shahidi: Ndiyo

Mtobesya: Soma tarehe kisha soma Mtu aliyeandika ni nani

Shahidi: Ndiyo haya

MTOBESYA: naomba Nikuulize kuhusu hii Statement yako dhidi ya Ulichokisema Leo 1. Nionyeshe kwenye hiyo Statement sehemu ilivyoandikwa kwamba huyo uliyemuita Mheshimiwa Mbowe kuwa yule alikuwa Mlinzi wake na Msiri wake

Wakili wa Serikali: OBJECTION Kwa Mujibu wa Kifungu cha 154 anatakiwa a Muonyeshe Shahidi hicho analichokisoma, yeye amefanya Vice versa

Mtobesya: Sijapata Msingi wa Objection ya Ndugu yangu Robert Kidando Nilianza Kutengeneza Msingi kwa Kuuliza Je alichokisema hapa ndiyo kilichopo kwenye Statement, Sasa Kama anataka twende hivyo tutaenda

Jaji: Hapana tuwasaidie Wateja wetu

Wakili wa Serikali: Provisory Mstari wa Nne ndiyo inakataza

JAJI: tueleze Nyie Mmelewa nini

Wakili wa Serikali: Maamuzi ya Kifungu Hichi Yametolewa Uamuzi na Mahakama ya Rufaa katika kesi ya Lilian Otesi Vs Jamuhuri, namba 77 katika Rufaa ya Jinai ya Mwaka 251 Mwaka 2008 katika Mahakama Ya Rufaa. Katika kesi hii Ukurasa wa 25 Mahakama ilisema yafuatayo; Kinachozungumzwa pale ni sawa na Kifungu namba 154 cha Sheria ya Ushahidi Kama Kilivyo gawanyika Maeneo Mawili Eneo la kwanza, Shahidi anaweza Kudodoswa kupitia Maelezo yake aliyoyaandika Nyuma Eneo la Pili anaweza Kuhojiwa kuhusu Maswala yake hayo hayo bila Kumuonyesha Maelezo yake Lakini kama anadhamiriwa kumpima Mkanganyiko wake shahidi, Kuna Utaratibu unaotakiwa Kufuatwa. Na hivyo kabla ya a kuthibitisha amuelekeze kwanza, Tofauti na Yeye kaenda na Kumfuata

Mtobesya: Rafiki yangu anarejea Vifungu viwili Tofauti Walitaka hayo ningefika huko kwa sababu hata a kesi ya Alberto Mendez imejadili hayo na Mimi nilikuwa ni sehemu ya Ile kesi. Kwa hiyo nafahamu ninachofanya.

Wakili wa Serikali: kifungu 164 hakisimami Pele yake, Kusimama kwake kunatemegea Kifungu cha 154 Na huo ndiyo Msimamo wa Mahakama

Mtobesya: Tusaidiane Mheshimiwa Jaji dhumuni la Kifungu cha 164 ni Kumchanganya (contradict) Shahidi

Wakili wa serikali: Mimi nilikuwa nimeanza Kwenye kifungu cha 154,Sikuwa nimefika huko

Jaji: wao wanasema Wana hukumu ambayo wanaweza Kutu Supply, nafikiri ni Vyema basi tuweze Kuona tu

Mtobesya: hili swala linaweza Kuibuka tena Mbeleni tunaomba Liwe Cleared kabisa na Mahakama

Wakili wa Serikali: tunaomba Dakika 15

Jaji: sawa tunaahirisha Kwa Dakika 15

Unaachiwa huru kwa masharti ya kuja kutoa ushahidi wa uongo Tangu lini Machame ikawa Wilaya ya Moshi.

Jaji bado hajarejea mpaka sasa

Jaji Kaingia

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 imetajwa

Robert Kidando: Kolamu yao Ipo Vile vile na anasema wapo tayari Kupokea Maelekezo ya Mahakama

Jaji: Muda Mfupi wakati wa Dodoso na Upande wa Utetezi, Upande wa Utetezi waliomba Mahakama iruhusu itoe Maelezo yaweze Kutumika kwa Nakala halisi p4 Baada ya Mawakili wa Utetezi Kusimama Upande wa Serikali Walisimama na Kusema Utaratibu haukufuatwa

Jaji: Baada ya hapo pande zote zilisema kuna Maamuzi nikaomba Maamuzi hayo

1. Nyaraka inatakiwa itolewe, hilo limeshafanyika

2. Nyaraka hiyo inapaswa Isomwe Katika Maeneo anayotaka Kumuuliza Maswali Ili Kumcontradict

Jaji: Mahakama hii inasema Kwakuwa huo ndiyo Utaratibu basi Unatakiwa Ufuatwe na Kuendelea na Shughuli Wakili wote wanasimama na Kushukuru ishara ya Kukubaliana Maamuzi ya Jaji.

Mtobesya: Anarudi kwa Shahidi na anaomba Mahakama Impatie tena Nyaraka anaweza kuisoma Shahidi anaanza Kusoma Alishawahi KUWA Msaidizi wa Katibu wa CCM Longido Amesomea Hotel Management Alishawahi Kufanya kazi na Sabaya kama Msaidizi wake Na aliacha kazi kwa Sabaya kwasababu alitaka Kurudi Longido na alienda kwa ajili ya Kumfuata Mchumba wake Anarudia kuwa alipigiwa simu na Freeman Mbowe, Kwamba alifuatwa Longido. "Freeman aliniambia kuwa nilitumia Elfu 50 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Hai Mama Helga na kumtomgoza

Shahidianaendelea kusoma: Nilishangaa Sana Kwamba alijuaje kwa sababu ilikuwa ni kweli nilimtomgoza Alinipigia Simu Tukutane Moshi Alinipigia niende Keys Hotel Na Siku Nyingine tulienda Aishi Hotel

Mtobesya: Soma eneo linalosema Mimi nilikwenda Kwa Kutumia Nauli yangu. Umeona?

Shahidi: anapekua

Shahidi: Mimi nilikwenda Kwa Kutumia Nauli yangu, na Nilipofika alikuja Kunichukua

Mtobesya: Eleza Mahakama Kwamba huyo Mlinzi alikuwa Diwani wa Kiboriloni

Shahidi: Nilisema

MTOBESYA: elezea Sasa hapo Katika Maandishi yako humo kuna Mlinzi anaitwa Bwire

Shahidi: Mheshimiwa Jaji MI Leo nilikuwa nafafanua.

Mtobesya: hakuna mahala Kwenye Statement inaonyesha kuna Mlinzi anaitwa Bwire

Shahidi: Statement Haionyeshi

Mtobesya: kwenye Statement yako kuna sehemu inasema Baada ya Kukutana Mara ya Pili, kwamba Ulimtajia Majina huyo Mbowe watu wanaotembea na Sabaya?

Shahidi: Majina hayajaandikwa hapa kwenye Statement

Mtobesya: Ulipokutana Mara ya Tatu ulisema Ulimtajia pia Majina, hayo Majina yapo kwenye Maelezo Yapo?

Shahidi: Hayapo

Mtobesya: Wakati Unaongozwa na Wakili Wa Serikali na huyo uliyemuita Mbowe ulimpigia Sabaya na Baadae Mbunge uliyemjulisha, Je hayo yapo kwenye Statement Yako?

Shahidi: hayapo

Mtobesya: pia wakati wakili wa Serikali anakuongoza nilisikia Majina ya Hotel na Club ulizotaja kwa Majina yake, Hizo Taarifa zipo humo kwenye Statement Yako?

Shahidi: Hazipo

Mtobesya: Wakati wakili wa Serikali anakuongoza Huyo uliyesema ni Bwire alitamka Sabaya ni Mtoto Mdogo atamchezesha, Je yapo kwenye Statement?

Shahidi: Hayapo

Mtobesya: Wakati wakili wa Serikali anakuongoza a umesema wewe unajishughulisha na Kilimo na Ukasema unavyofanya Kilimo, Je yapo hapo kwenye Statement..?

Shahidi: Hayapo

Mtobesya: Soma kwa Sauti Kuanzia Sehemu unayosema kuwa Ulikuwa Msaidizi wa Katibu wa CCM Shahidi anasoma Kuwa alikuwa Msaidizi wa Katibu wa CCM na mwanaharakati wa CCM.

Mtobesya: Wakati wakili wa Serikali anakuongoza ulisema kuwa wewe Ulishawahi kuwa Msaidizi wa CCM.

Shahidi: Hapana

Mtobesya: Je ungependa Maelezo uliyoyaongea Leo yaingie kwenye Ushahidi wako?

Shahidi: Ndiyo kwa sababu nimeongea Chini ya Kiapo ningependa yaingie kama Ushahidi

Jaji: Upande wa Serikali

wakili wa Serikali: Hatuna Pingamizi

Mheshimiwa Jaji anaandika Mahakama ipo Kimya

MTOBESYA amerudi kukaa katika Eneo lake

Jaji: kwa sababu imeombwa na Shahidi Kuwa Maelezo hayo hayajapingwa Na Mahakama, na haijapingwa na Upande wa Mashitaka basi Mahakama Imepokea Maelezo hayo Kama Kielelezo namba 1.

Mtobesya: naomba Kuendelea Mheshimiwa

MTOBESYA: Nitakuwa sahihi nikisema Kwa kipindi hicho Mpaka Unaandika Statement ulikuwa unajishughulisha na siasa

Shahidi: Siyo sahihi Kwa sababu Mimi ni Mwandishi ninayepiga Picha Siyo Mwanasiasa

Mtobesya: Kwa hiyo wewe siyo Mwanachama

Shahidi: Siyo Mwanachama Wa Chama Chochote

Mtobesya: Ni lini Uliacha kuwa Mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi

Shahidi: Sijawahi Kuwa Mwanachama wa Chama chochote Kile

Mtobesya: Hujawahi Kuwa Karibu na Viongozi wa Kisiasa

Shahidi: Nimesema kuwa nimekua karibu na Viongozi wa Serikali na Siasa

Mtobesya: Unaweza Kumtajia Mheshimiwa Jaji ni akina nani uliwahi Kuwa nao karibu

Shahidi: Mrisho Gambo, Daqaro, na Sabaya

MTOBESYA: hujawahi Kuandika Barua ukiwa Gerezani Kwa Viongozi wa Kisiasa wakusaidia kwenye kesi iliyokuweka Jela?

Shahidi: Sijawahi

Mtobesya: hujawahi Kutembelewa na Viongozi wa Kisiasa Ukiwa Gerezani?

Shahidi: sijawahi

Mtobesya: Ulikutana na Mheshimiwa Mbowe Gerezani tarehe ngapi

Shahidi: Tarehe 26 07 2021

MTOBESYA: Maelezo yako umeandika Lini

Shahidi: Siku Mbili baada ya Kutoka Gerezani

Mtobesya: na Umesema wakati Umefika Mahakamani Kisutu Siku hiyo, mlielekezwa nini Siku hiyo

Shahidi: Baada ya Upelelezi Kukamilika tumeonekana hatuna hatia tena

Mtobesya: Unakumbuka Namba ya Kesi Uliyokuwa umeshitakiwa nayo

Shahidi: sikumbuki Mtobesya: Naweza Kusema Kesi namba 63 ya Mwaka 2020

Shahidi: Sahihi

Mtobesya: Unakumbuka Mashitaka uliyoshitakiwa nayo wewe Binafsi

Shahidi: Kushiriki Vikao Kula Njama za kutenda Vitendo Vya ugaidi na Utakatishaji

Mtobesya: Kwa Niaba ya Mshitakiwa wa Kwanza naomba tuishie hapa

Mheshimiwa Jaji naitwa John Mallya

Mallya: shahidi Nina Mswali Machache, Jibu kwa Sauti

Mallya: Diwani analipwa TSh ngapi

Shahidi: sifahamu

Mallya: Diwani analipwa posho TSh Ngapi

Shahidi: sifahamu

Mallya: Kwa ufahamu wako wewe Sabaya alikuwa anakulipa Kutoka Mfuko gani

Shahidi: sifahamu

Mallya: Kwa hiyo wewe hukutaka kabisa Kujua kama anaiba au anatoa wapi

Shahidi: sikujua Mallya: alikuwa anakulipa TSh ngapi

Shahidi: Laki tatu

Mallya: Kwa Picha au Kwa Mwezi

Shahidi: Kwa Mwezi

Mallya: Mheshimiwa naomba Kielelezo namba D1

Mallya: Soma Hapo Mwanzoni Shahidi: nilianza Harakati za Kisiasa na Kuwa Msaidizi wa Katibu wa CCM

Mallya: Umemtaja Mrisho Gambo alikuwa Chama Gani

Shahidi: CCM

Mallya: Sabaya alikuwa Chama gani

Shahidi: CCM

Mallya: Daqaro Mkuu wa Wilaya Alikuwa Chama gani

Shahidi: Mkuu wa Wilaya hana Chama

Mallya: Unasema Sabaya alikuwa Diwani wa Chama gani

Shahidi: CCM

Mallya: halafu Magufuli akamteua kuwa Mkuu wa wilaya

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa mKuu wa Wilaya hana Chama ila Magufuli alimteua Sabaya wa CCM

Shahidi: Ndiyo alimteua akiwa CCM

Mallya: hapa karibu Umesikia kabla ya Sabaya kufungwa Miaka 30 aliomba Mahakama impungzuie Adhabu sababu anamchumba, Wewe Umesema Sabaya alikuwa na Mke

Shahidi: Mimi najua Sabaya alikuwa na Mke

Mallya: Kwa hiyo Kule Kadanganya Mahakama

Shahidi: sijui yeye sasa

Mallya: nimesikia Ulimtajia Mheshimiwa Freeman Mbowe, Sylvester Nyegu

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Umesikia Kuwa Mahakama Imemfunga Kwa Makosa ya Ujambazi Arusha

Shahidi: Ndiyo nimesikia

Mallya: Soma Statement yako hapo Mlipokuwa Mwishoni Mwa Mwaka 2017

Shahidi anasoma

Mallya: Kwa hiyo Hapa ulisema Mwishoni Mwa 2018, Mahakama ichukue lipi

Shahidi: Aliye andika atakuwa amekosea

Mallya: Soma Hapo Juu

Shahidi: Mimi nathibitisha kuwa Maelezo haya ni Sahihi

Mallya: Sasa wakati gani tujue upo sahihi hapo Umethibitisha Upo sahihi na Leo unasema tuchukue ya leo Kwamba Uliacha kazi kwa Sabaya 2017 na Leo unasema uliacha kazi 2018, Hapo Chini Maelezo uliyosaini yana maana gani

Shahidi: Yana maana ya Uthibitisho

Mallya: Mkuu wa Wilaya analipwa TSh ngapi

Shahidi: Sifahamu

Malya: Sabaya alikuwa anakulipa TSh ngapi

Shahidi: Laki tatu

Mallya: alikuwa anatoa wapi

Shahidi: sifahamu

Mallya: umesema Sabaya alikuwa anaongozana na Watu 7 au 8, Je walikuwa wanalipwa na nani

Shahidi: sifahamu, Walikuwa ni MARAFIKI zake

Mallya: wakati Unatoa Majina Mwaka 2017 na Ukaja kuyatoa tena Mwaka 2018 kwanini ulikuwa nayo.

Shahidi: walikuwa MARAFIKI zangu

Mallya: ulipokamatwa Arusha alikuhoji Afande Mahita

Shahidi: Ndiyo

Mallya: hayo aliyokuhoji umeyatoa hapa Mahakamani?

Shahidi: Ndiyo

Mallya: je umeshawahi kuyatoa hayo Maelezo kwa Maana Karatasi kwa Mheshimiwa Jaji

Shahidi: Siyo kazi yangu

Mallya: Mheshimiwa Jaji naomba ajibu swali langu

Jaji: Je aliyatoa lakini

Mallya: nataka iingie kwenye Rekodi ya Mahakama

Mallya: Ulipokutana na Mbowe Gerezani alikwambia Nimekuja kuwatoa na Kesho yake ukatoka kweli

Shahidi: Ni sahihi nilitoka

Mallya: baada ya Kufutiwa kesi ulienda Central Kufuata Vitu vyako

Shahidi: Ni sahihi, Nilienda Central kwa Inspector Swila nikatoa Maelezo, ndiyo Nikapewa vitu Vyangu

Mallya: Kwa hiyo Mahakama irekodi kuwa ulipewa Vitu Vyako baada ya Kuandika Maelezo

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Ni hayo tuh Mheshimiwa Jaji

JAJI: hujamuuliza kama alipotoka Gerezani alienda kwa MChumba wake

Mahakama KICHEKO

JAJI: Kesho tunaweza kumaliza Mapema Je tunaweza Kupata Shahidi Mwingine

Wakili wa Serikali: Bado hatuna Uhakika tulikuwa tunahangaika kumpata

Jaji: basi Jitahidini Msijiandae Kumkosa

Jaji: basi nahairisha Mpaka kesho ambapo Upande wa utetezi watamalizia Kuuliza Maswali ya Dodoso Kisha Upande wa Mashitaka watarudi kwaajili ya Re examination

Jaji: naahirisha Mpaka Kesho saa 3 kamili


Face with tears of joy
Face with tears of joy
 
Mr. Kingai tunakudai ( Mahakama) utuonyeshe vitendea kazi vya kufanyia UGAIDI, kama ni mapanga, mashoka, misumeno ya moto na utuonyeshe miti iliyopangwa kukatwa pamoja na maroli ya kusombea magogo kuja Dar, Arusha, Moshi na Mwanza kufunga barabara kama mpango ulivyokuwa umesukwa na Mh. Mbowe akiwatumia makomandoo wastaafu kina adamoo, pamoja na vipeperushi vya maandamano kote nchini na tarehe ambayo ilikuwa imepangwa na Mr. Mbowe.

Pia tuhakikishie kupitia hata ikibidi vipimo vya DNA ama finger prints kwamba ile Bunduki alitumiwa na Adamoo na ni yake ambayo alipanga kumlipua Mr. Sabaya.
 
All in all, Mbowe siyo Gaidi! Bora wangemshtaki kwa makosa yale yale ya kitoto na tuliyo yazoea tangu awamu ya tano ilipoingia madarakani ya kile kinachoitwa 'uchochezi'

Ila siyo ugaidi.
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂

Usiwapangie!!!!

Niliskia walisema "Watamlazimisha na watamnyoa"
 
Back
Top Bottom