Max Melo kajitolea kutulinda, sisi tumeshindwa kumlinda, lakini vifungu hivi vinawapa nguvu polisi

Wasalaam wana JF,

Kwanza nimesikitishwa sana na kusumbuliwa na kushikiliwa kwa Melo kwa kile kinachoitwa kushindwa kutoa taarifa za baadhi ya wanachama kwa jeshi la polisi.

Melo ni shujaa maana anatupigania sana na ameendelea kutupigania na anasumbuliwa kwasababu yetu sisi lakini ni ukweli ulio wazi sisi tumeshindwa kumpigania au kuipigania JF hata mara moja...

Hakuna anayejua ni data za kina nani zinahitajika lakini ni ukweli ulio wazi sisi wanajf baadhi yetu tumekuwa tukiutumia mtandao huu vibaya na kweli JF admin wamekuwa wakifanya kazi kubwa kuturudisha kwenye mstari lakini wengine tumekuwa tukiwaona wao wabaya au kutuonea.

Pengine Melo anasumbuliwa kutokana na baadhi ya maandishi yetu hasa ya uongo, uchonganishi na matusi kwa viongozi au kwa Umma..., Lakini kwakuwa ni wajibu wake kulinda usiri wetu inabidi achukue mzigo wa kutulinda.. Ni wazi kuna baadhi ya mabandiko hapa yetu yanakuwa ni ya uongo, uchochezi japo mods hujitahidi kuyafuta lakini mengine yanakuwa yameshasababisha madhara na kusambaa...

Hawa mods wa JF akiwemo Melo hufanya kazi kubwa ya kutuweka kwenye mstari lakini tumekuwa viburi lakini tunasahau kuwa cyber crime act inawabana JF na wao ndio huwa wa kwanza kusumbuliwa tunapohitajika...

Ni lazima tuwe na huruma kweli kwa Melo na JF kwa kutoandika uongo au mambo tunayo yaona hayafai au yanavunja sheria za nchi na bahati mbaya mods wanapokuja kuyafuta yanakuwa tayari yameshazagaa na wengi wananukuu chanzo ni JF na tumekuwa tukitumia neno "tetesi" kusambaza uongo hadi inafikia baadhi ya taasisi kutuhumu JF moja kwa moja.

Ni vyema watu tukafahamu sisi ni sababu ya Melo kusumbuliwa na inasikitisha yeye anasumbuliwa kwasababu yetu na anatupigania lakini sisi hatumpiganii tunasubiri madhara yakishatokea ndio tunaanza kuongea.... Mfano watu wakipigwa ban kwa kukiuka sheria wataanza kusema eti oooh emenunuliwa oooh anabana uhuru oooh anatumika na serikali...

Melo ameendelea kutupigania bila kujali kashifa na matusi yetu tunayomtukana wanapokataa JF kutumika kuvunja sheria, leo hii anasumbuka kwakuwa sisi tumeshindwa kumlinda maana tunasahau kuwa yeye ana beba dhamana yetu...

Nilishasema sehemu kama JF wataona kuna kila sababu ya kufuta id yangu kwakuwa imekuwa ikisababisha usumbufu usio wa lazima ni bora waifute kuliko siku moja JF ikifungwa...ni bora nikaisoma JF kama mgeni kuliko kuwa sababu ya JF kufungiwa au wamiliki wake kusumbuliwa.

Lakini wana JF tunasahau kuwa haya ni matokeo ya cyber crime act (2015) ambayo imewapa nguvu kubwa sana jeshi la polisi kuomba taarifa ya mtu yeyote kutoka taasisi yeyote ile na anapokataa wao huiandikia mahakama kumshurutisha kutoa taarifan hivyo ni wazi Cyber crime act ina wapa nguvu sana polisi....

Tusome baadhi ya hivi vipengele vinavyo toa nguvu kwa jeshi la polisi kwenye sheria hii ya mitandao.

View attachment 446122
View attachment 446123
View attachment 446124

View attachment 446125
View attachment 446127
Peleka hivyo vifungu vyako vya kijinga huko lumumba
 
Kwa hali hii ni bora vyombo vyote vya habari vifutwe turudi enzi zile za kudumisha fikra sahihi za mwenyekiti wa CCM.
 
CCM acheni unafiki kujifanya mnalia machozi ya mamba, nyie ndio mlioichongea JF kwa hao polisi.
 
Sheria inasema a person committing or suspected ndio search inaweza fanyika kwenye computer system yake. Tena kwa kufuata utaratibu wa sheria zingine hapa nadhani wanazungumzia criminal procedure act. Na utaratibu wa sheria hiyo kwa kuwa Max sio suspect ina maana wanafanya mambo kinyume na sheria kama article 38 (4)

upload_2016-12-14_14-48-10.png



Embu jiulize treatment anazopewa Max yeye ndiyo suspect au kavunja sheria; binafsi ni shabiki wa sheria ya cyber crime lakini isitumike kufanya unyanyasaji.
 
Uvccm ni lazima mshabikie, lakini usisahau hata Lizaboni aliwakashifu baadhi ya viongozi kama Nchimbi, Lukuvi, Membe n.k
weee!! Jamaa nazikubali sana comments zako,hata mimi nashangaa leo hii uvccm nao wanalialia au zile buku 7 zitakuwa zimefika mwisho maana JF muda c mrefu itakuwa imezimwa moja Kwa moja
 
Kila mtu JF Forums angekua anaandika Kuisifia Serikali kama Gazeti la Uhuru Jamii Forums ingepewa tuzo na Stahiki zote kama tunavoona kwa "Bwana Yule" ambae ni Mpinzani pekee anaelindwa na kupigiwa saluti na Polisi wa nchi hii lakini tatizo ni kwamba 80% ya yanayoandikwa humu ni ya Kukosoa Serikali na hapo ndipo tatizo linapoanzia.
Hamna mahali popote Duniani kila mtu ataridhishwa na Serikali iliyopo.
Wenye akili wanasikiliza na wanafanyia kazi malalamiko ya wananchi na Kuwaletea Maendeleo, Wapumbavu wamekazana usiku na mchana kuwaziba midomo. Nauliza tusipowakosoa mkajua mnakosea wapi, Mtajuaje mnakosea wapi na tunachokitaka na njia za kutufikisha huko tunapotaka kufika??
 
Yaani baada ya kumaliza kuusoma huu uzi, kwa mbaaaali kakapita kasauti ka mzee wa kupiga mbizi, "Watanzania fanyeni kazi, siasa hadi 2020"....khaaaa!!
 
Back
Top Bottom