Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,606
- 29,755
Niwapongeze CHADEMA kwa kuandaa maandamano haya muhimu. Mimi huwa nadeclare interest mara zote kwamba ni mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi. Sijawahi kuwa nje ya chama hiki asilani. Lakini kuna wakati mnauguza mgonjwa na haponi hivyo mnaomba Mungu amtwae kumpunguzia mzigo. Mgonjwa hakimbiwi
Kuhusu maandamano naamini kupitia CHADEMA ninajifunza jambo moja kubwa nalo ni UTHUBUTU, UMAKINI na UJASIRI.
Tunaweza kujitia upofu kwa kuanza kumpongeza Samia kwa kuruhusu maandamano. La hasha! Tunapaswa kuienzi Katiba ambayo imetoa haki ambazo watawala wamekuwa wakizitoa kama hisani. Rais anawajibika kwa Watanzania na siyo chama chake pekee.
Kwa minajili ya nchi kusonga mbele ni lazima sana tukubali kuwa tofauti zetu ni kwa minajoli ya kujenga na siyo kubomoana na kutafutana kama magaidi.
TUnashuhudia chawa wakitamba huku wakifanya uhalifu wa charracters assassinations kwa wenye maoni na mtazamo tofauti na watawala. Tumeona namna ambavyo watawala wakitumia hazina ya nchi kujenga taswira zao badala ya kutimiza ahadi na malengo mtambuka ya nchi.
Leo, Samia anaongoza Taifa ambalo limejaa hofu na uoga mkuu. Watu wanaogopa kukosoa pale mambo yanapokwrnda vibaya kwa hofu ya kushughulikiwa. Taasisi kama vile TRA, Polisi, TISS, DPP na mhimili wa Mahakama vimekuwa ni vyombo vinavyotumika kukandamiza hoja na fikra kinzani. Tanzania ya Samia na kabla ya Samia imekuwa na utamaduni wa kuwapa jina baya wale wambao hawaendani na fikra za watawala.
Karibia asilimia 99% ya watumiaji wa JamiiForums tumekuwa salama muda wote kwa kutumia majina bandia ili tuweze kutimiza haki yetu ya kikatiba ya kutoa maoni na kujumuika na wengine kutumia haki hiyo. Tumeona namna ambavyo mwanzilishi wa JamiiForums ndugu Maxence Melo alivyosulubiwa mahakamani kwa sababu ya kulinda uhuru wa maoni kwa kutotoa taarifa za mtumiaji wa JF ambaye alitoa taarifa iliyoisaidia serikali kung'amua wizi wa mafuta ghafi bandarini. Badala yake serikali ikaamua kutumia nguvu zake zote kutaka kumshughuulikia mtoa taarifa badala ya kuzifanyiakazi taarifa hizo.
Hivyo tunavyojisahau leo kwa kumpongeza Samia kuwa amekuwa mwanademokrasia kwa kuruhusu maandamano ni sawa na kujiingiza kwenye mtego wa kifo cha demokrasia.
Tutakuwa na neno la kumshukuru na kumpongeza Rais Sania pale atakapo ataridhia mchakato wa akatiba Mpya ya Wananchi na kuheshimu kanuni ya wananchi ndiyo wenye nchi.
Kuhusu jeshi letu la Polisi, hatuna cha kuwapongeza kwa sababu wao wanafuata amri. Wale wale waliokuwa wanawapiga risasi za moto waandamanaji ndiyo hao hao walioongoza kulinda maandamano ya tarehe 24 January 2024. Hivyo polisi wanafuata amri huku wakiweka kando utashi wao wa utii kwa Katiba na Sheria.
Ninatoa kongole kwa Jeshi letu la Wananchi kwa kutoshiriki mazonge ya kisiasa kama ambavyo Mkuu wa Mkoa alivyowataka washiriki.
Ninakubali kwamba, safari bado inaendelea kuutafuta uhuru wa kweli wa Tanzania (Tanganyika). Hatua elfu moja huanzia na moja.