Max Melo kajitolea kutulinda, sisi tumeshindwa kumlinda, lakini vifungu hivi vinawapa nguvu polisi

Wasalaam wana JF,

Kwanza nimesikitishwa sana na kusumbuliwa na kushikiliwa kwa Melo kwa kile kinachoitwa kushindwa kutoa taarifa za baadhi ya wanachama kwa jeshi la polisi.

Melo ni shujaa maana anatupigania sana na ameendelea kutupigania na anasumbuliwa kwasababu yetu sisi lakini ni ukweli ulio wazi sisi tumeshindwa kumpigania au kuipigania JF hata mara moja...

Hakuna anayejua ni data za kina nani zinahitajika lakini ni ukweli ulio wazi sisi wanajf baadhi yetu tumekuwa tukiutumia mtandao huu vibaya na kweli JF admin wamekuwa wakifanya kazi kubwa kuturudisha kwenye mstari lakini wengine tumekuwa tukiwaona wao wabaya au kutuonea.

Pengine Melo anasumbuliwa kutokana na baadhi ya maandishi yetu hasa ya uongo, uchonganishi na matusi kwa viongozi au kwa Umma..., Lakini kwakuwa ni wajibu wake kulinda usiri wetu inabidi achukue mzigo wa kutulinda.. Ni wazi kuna baadhi ya mabandiko hapa yetu yanakuwa ni ya uongo, uchochezi japo mods hujitahidi kuyafuta lakini mengine yanakuwa yameshasababisha madhara na kusambaa...

Hawa mods wa JF akiwemo Melo hufanya kazi kubwa ya kutuweka kwenye mstari lakini tumekuwa viburi lakini tunasahau kuwa cyber crime act inawabana JF na wao ndio huwa wa kwanza kusumbuliwa tunapohitajika...

Ni lazima tuwe na huruma kweli kwa Melo na JF kwa kutoandika uongo au mambo tunayo yaona hayafai au yanavunja sheria za nchi na bahati mbaya mods wanapokuja kuyafuta yanakuwa tayari yameshazagaa na wengi wananukuu chanzo ni JF na tumekuwa tukitumia neno "tetesi" kusambaza uongo hadi inafikia baadhi ya taasisi kutuhumu JF moja kwa moja.

Ni vyema watu tukafahamu sisi ni sababu ya Melo kusumbuliwa na inasikitisha yeye anasumbuliwa kwasababu yetu na anatupigania lakini sisi hatumpiganii tunasubiri madhara yakishatokea ndio tunaanza kuongea.... Mfano watu wakipigwa ban kwa kukiuka sheria wataanza kusema eti oooh emenunuliwa oooh anabana uhuru oooh anatumika na serikali...

Melo ameendelea kutupigania bila kujali kashifa na matusi yetu tunayomtukana wanapokataa JF kutumika kuvunja sheria, leo hii anasumbuka kwakuwa sisi tumeshindwa kumlinda maana tunasahau kuwa yeye ana beba dhamana yetu...

Nilishasema sehemu kama JF wataona kuna kila sababu ya kufuta id yangu kwakuwa imekuwa ikisababisha usumbufu usio wa lazima ni bora waifute kuliko siku moja JF ikifungwa...ni bora nikaisoma JF kama mgeni kuliko kuwa sababu ya JF kufungiwa au wamiliki wake kusumbuliwa.

Lakini wana JF tunasahau kuwa haya ni matokeo ya cyber crime act (2015) ambayo imewapa nguvu kubwa sana jeshi la polisi kuomba taarifa ya mtu yeyote kutoka taasisi yeyote ile na anapokataa wao huiandikia mahakama kumshurutisha kutoa taarifan hivyo ni wazi Cyber crime act ina wapa nguvu sana polisi....

Tusome baadhi ya hivi vipengele vinavyo toa nguvu kwa jeshi la polisi kwenye sheria hii ya mitandao.

View attachment 446122
View attachment 446123
View attachment 446124

View attachment 446125
View attachment 446127
15589488_609802089220930_1340586433250883118_n.jpg
 
Ebu tusaidie na Article 18(1),(2) za katiba ya JMT ya mwaka 1977 na marekebisho yake...
na tueleze unaelewa nn kuhusu supremacy of the constitution
18.-(1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru
kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta,
kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo
chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa
mawasiliano yake kutoingiliwa kati.
(2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu
matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu
kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala
muhimu kwa jamii.

Angalia hayo maneno " Bila ya kuathiri sheria za nchi" halafu tafuta tafsiri ya kisheria nadhani utakuwa amewasaidia wengi
 
18.-(1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru
kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta,
kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo
chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa
mawasiliano yake kutoingiliwa kati.
(2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu
matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu
kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala
muhimu kwa jamii.

Angalia hayo maneno " Bila ya kuathiri sheria za nchi" halafu tafuta tafsiri ya kisheria nadhani utakuwa amewasaidia wengi
Maana yake ni kua that right is not absolute it is subject to other rules and regulations,
 
Huo mswada ukifika mezani kwangu nitausaini hapohapo bila kuchelewesha
Hii ngoma ilipitishwa zama za JK na wala si JPM Uyu wa sasa anafanya kutekeleza tuu yaliyomo ilibidi tukomae nao toka kipindi kile kabla ya kupitishwa
 
Mimi nitaendelea kusema. Hapa na kwingineko. Naona wengi wamekamatwa na Stockholm Syndrome wameanza kumsifu anayewadhuru. Sheria ndiyo kandamazi sio matamshi ya watu.
 
Hii ngoma ilipitishwa zama za JK na wala si JPM Uyu wa sasa anafanya kutekeleza tuu yaliyomo ilibidi tukomae nao toka kipindi kile kabla ya kupitishwa
Kweli kabisa. JPM alisema akiletewa ataisaini kwa kuwa alishaisoma tangu enzi za JK. Na alisema haoni haja kwanini inachelewa kupitishwa.
 
Wachache wanajitungia Sheria kujilinda na kuwakandamiza waliowengi. Ulafi wa madaraka upo wa aina nyingi tu.
 
Back
Top Bottom