Max Melo kajitolea kutulinda, sisi tumeshindwa kumlinda, lakini vifungu hivi vinawapa nguvu polisi

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
51,956
41,427
Wasalaam wana JF,

Kwanza nimesikitishwa sana na kusumbuliwa na kushikiliwa kwa Melo kwa kile kinachoitwa kushindwa kutoa taarifa za baadhi ya wanachama kwa jeshi la polisi.

Melo ni shujaa maana anatupigania sana na ameendelea kutupigania na anasumbuliwa kwasababu yetu sisi lakini ni ukweli ulio wazi sisi tumeshindwa kumpigania au kuipigania JF hata mara moja...

Hakuna anayejua ni data za kina nani zinahitajika lakini ni ukweli ulio wazi sisi wanajf baadhi yetu tumekuwa tukiutumia mtandao huu vibaya na kweli JF admin wamekuwa wakifanya kazi kubwa kuturudisha kwenye mstari lakini wengine tumekuwa tukiwaona wao wabaya au kutuonea.

Pengine Melo anasumbuliwa kutokana na baadhi ya maandishi yetu hasa ya uongo, uchonganishi na matusi kwa viongozi au kwa Umma..., Lakini kwakuwa ni wajibu wake kulinda usiri wetu inabidi achukue mzigo wa kutulinda.. Ni wazi kuna baadhi ya mabandiko hapa yetu yanakuwa ni ya uongo, uchochezi japo mods hujitahidi kuyafuta lakini mengine yanakuwa yameshasababisha madhara na kusambaa...

Hawa mods wa JF akiwemo Melo hufanya kazi kubwa ya kutuweka kwenye mstari lakini tumekuwa viburi lakini tunasahau kuwa cyber crime act inawabana JF na wao ndio huwa wa kwanza kusumbuliwa tunapohitajika...

Ni lazima tuwe na huruma kweli kwa Melo na JF kwa kutoandika uongo au mambo tunayo yaona hayafai au yanavunja sheria za nchi na bahati mbaya mods wanapokuja kuyafuta yanakuwa tayari yameshazagaa na wengi wananukuu chanzo ni JF na tumekuwa tukitumia neno "tetesi" kusambaza uongo hadi inafikia baadhi ya taasisi kutuhumu JF moja kwa moja.

Ni vyema watu tukafahamu sisi ni sababu ya Melo kusumbuliwa na inasikitisha yeye anasumbuliwa kwasababu yetu na anatupigania lakini sisi hatumpiganii tunasubiri madhara yakishatokea ndio tunaanza kuongea.... Mfano watu wakipigwa ban kwa kukiuka sheria wataanza kusema eti oooh emenunuliwa oooh anabana uhuru oooh anatumika na serikali...

Melo ameendelea kutupigania bila kujali kashifa na matusi yetu tunayomtukana wanapokataa JF kutumika kuvunja sheria, leo hii anasumbuka kwakuwa sisi tumeshindwa kumlinda maana tunasahau kuwa yeye ana beba dhamana yetu...

Nilishasema sehemu kama JF wataona kuna kila sababu ya kufuta id yangu kwakuwa imekuwa ikisababisha usumbufu usio wa lazima ni bora waifute kuliko siku moja JF ikifungwa...ni bora nikaisoma JF kama mgeni kuliko kuwa sababu ya JF kufungiwa au wamiliki wake kusumbuliwa.

Lakini wana JF tunasahau kuwa haya ni matokeo ya cyber crime act (2015) ambayo imewapa nguvu kubwa sana jeshi la polisi kuomba taarifa ya mtu yeyote kutoka taasisi yeyote ile na anapokataa wao huiandikia mahakama kumshurutisha kutoa taarifan hivyo ni wazi Cyber crime act ina wapa nguvu sana polisi....

Tusome baadhi ya hivi vipengele vinavyo toa nguvu kwa jeshi la polisi kwenye sheria hii ya mitandao.

upload_2016-12-14_15-50-58.png

upload_2016-12-14_15-51-37.png

upload_2016-12-14_15-52-4.png


upload_2016-12-14_15-52-48.png

upload_2016-12-14_15-53-29.png
 
19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom