Game Theory
Platinum Member
- Sep 5, 2006
- 8,545
- 835
- Thread starter
- #61
tuWanabodi hata mimi namfahamu vizuri huyu kijana Nyaga Mawalla.
Kitu ambacho nataka mfahamu jamaa ni Genius!. Ni genuine genius katika fani ya sheria.
Nilimtangulia madarasa kibao Ilboru alikuwa ni kichwa cha ukweli kama sikosei jamaa atakuwa ametoka na poiti 7 O-Level na point 3 A-Level.
Alijiunga UD kuchukua sheria nilimuona akichangia kile kipindi cha 'Kiti Moto' alishuka na nondo za kufa mtu nikazidi kuthibitisha ni kichwa mbaya!.
Mimi nilisoma kitu kingine kabla sijatua UD kufanya sheria. Japo kusoma sheria chuo chochote humu nchini unapata digrii yako yako ya sheria yenye hadhi sawa, lakini wanaosomea UD wanateseka zaidi, kwanza wanaipiga kwa miaka 4 wakati wenzao ni miaka mitatu tuu. Cha pili UD hakuna kupata Ist class wakati vyuo vingine ni Ist class za kumwaga.
Moja ya matatizo makubwa kabisa ya kusoma sheria ni kukremu makesi zaidi ya 500 na kuwa na kumbukumbu rasmi ya majina na maudhui ya kesi hizo wenyewe wakiita sightation.
Sasa huyu Nyaga na mwanafunzi mwenzake mwingine akiitwa Baimu, walizukusanya kesi zote muhimu za kusomwa na wanafunzi wa sheria wa UD na kuzicompile pamoja katika bonge la mkitabu wakaliita 'BAIMU & MAWALLA'. Ukishalipata hilo buku, wewe sio lazima kwenda maktaba unless ni kwa information quest.
Ndipo kuna lecture mmoja akaniibia kuwa baada ya first class ya Prof. Asha Rose Migiro, Prof. Palamagamba Kabudi na Prof. Hamoud Majamba, Ist class nyingine ilikuwa iwe ni ya Nyaga Mawalla ili walimbania tuu na mpaka leo UD wabaendelea kubania hizo Ist Class!,
Sasa ninaposikia mambo anayofanya na hiyo fani yake ya sheria nazidi kumkubali.
Watanzania tuna tatizo na kukubali mafanikio ya wenzetu. Kwani Billy Gate alianzaje?. Hamuamini kuwa Nyaga ndio Billy Gate wa Tanzania?. Kama Billy Gate original amekuwa bilionea wa dunia kwa kugundua microsoft, kuna tatizo gani Nyaga kugundua hiyo program ya Brella?. Tena ikifanikiwa TRA watamtumia kuwatengenezea ile ya kuhakikisha kila mtu analipa kodi. Ile Asycuda++ haisaidii kitu?.
Pasco
I cant knock the man's hustle ndio maana utaona kwenye ile thread ya BRELA my criticism wasnt on Mawalla bali on BRELA kununua software at 1 million usd ambayo has not worked!
maybe invisible ailete ile thread hapa siasa ukasoma mtiririko wake
Hilo la hizo idadi za 1st UD sina data lakini kuzipata sio kazi kubwa
all in all I wouldnt wanna put Mawalla & Co in the same category as DOWANS kwa sababu hawa ni hustlers ila tatizo langu ni watu wa serikali ambao hawafanyi proper checks kama PPA ilifuatwa etc