Mazishi ya Advocate Nyaga Mawalla utata mtupu

Nduka Original

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
1,012
816
Mpaka sasa mwili wa marehemu Advocate Nyaga Mawalla umehifadhiwa Nairobi Hospital huku vikao vikiendelea marehemu azikiwe wapi. Mvutano uko kati ya will aliyoacha marehemu na baba mzazi wa Nyaga ambaye pia ni wakili wa mstaafu Advocate Juma Mawalla.

Will aliyoacha marehemu ambayo inatunzwa na bi Fatma Karume wa Imma Advocate inasema kama ifuatavyo:

1. Kama nikifa nchini Tanzania basi mwili wangu uzikwe Momella kwenye nyumba yangu
2. Kama nikifa nje ya nchi basi nizikwe in any public cementary

Ila mzee Mawalla sasa yeye anataka will itenguliwe ili mtoto wake akazikwe kijijini Marangu. Mpaka jana vikao vimekuwa vikiendelea baina ya mzee Mawalla na mawakili wengine maarufu kama Advocate Maro na Ngimariyo ambao inasemakana walikuwa groomed na Advocate Juma Mawalla.

GOD BLESS YOU ALL.

Arusha. Utata umegubika mazishi ya Wakili maarufu nchini, Nyaga Mawalla baada ya wakili wa kujitegemea ambaye pia ni mtoto wa Rais wa zamani wa Zanzibar, Fatma Karume kuwasilisha wasia wa marehemu kwa wazazi wake ambao alitaka azikwe kwenye shamba lake la Momela, wilayani Arumeru, mkoani Arusha.

Hata hivyo, wasia huo unadaiwa kupingwa vikali na baba mzazi wa marehemu, Juma Mawalla huku akitoa sharti la kutohudhuria mazishi ya mwanaye iwapo akizikwa sehemu tofauti na Kijiji cha Marangu.

Mawalla, alifariki hivi karibuni baada ya kujirusha kutoka ghorofani akiwa Nairobi, Kenya alipokwenda kutibiwa.

Taarifa za awali zinasema kwamba Mawalla aliamua kujiua kutokana na kusumbuliwa na msongo wa mawazo, inadaiwa enzi zake za uhai alikuwa na uhusiano mbaya na baba yake.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka kwa mmoja wa mawakili wa kujitegemea mjini hapa, siku chache baada ya kifo cha wakili huyo, Karume alifika Kilimanjaro kuwasilisha wasia alioucha marehemu.

Ilidaiwa binti huyo ambaye anatajwa kuwa karibu na marehemu enzi za uhai wake, alikutana na baba yake mzazi na kuusoma.

Hata hivyo, chanzo hicho kilidai kuwa pendekezo hilo la marehemu lilipingwa vikali na baba yake na kusema iwapo mtoto wake atazikwa Momela, hatahudhuria mazishi hayo.
Imeelezwa kipindi cha miaka miwili, wakili huyo hakuweza kuongea na baba yake hadi alipofariki, kutokana na uhusiano mbaya waliokuwa nao.

Hata hivyo, wakili huyo alisisitiza kuwa, chanzo cha uhusiano mbaya baina yao ni kutokana na mzee Mawalla kumwonya mwanaye kuhusu biashara anazofanya baada kupokea malalamiko mbalimbali kutoka kwa watu, maofisa usalama na baadhi ya polisi nchini waliokuwa wakifika kijijini mara kwa mara kumsemea. Mmoja wa mawakili wa Kampuni ya Mawalla Advocates, Lemy Bartholomew alipoulizwa kwa njia ya simu na gazeti hili kuhusiana na taratibu za mazishi, alisema ni mapema kuzungumzia suala hilo kwa sababu kuna vikao vya familia vinaendelea.

Wakili huyo alisema baada ya vikao hivyo, ndipo uamuzi utakapojulikana iwapo atapozikwa shambani kwake au nyumbani kwao kijijini Marangu.

SOURCE: Mwananchi
 
kazi ipo, lakini nadhani vikao vinavyoendelea watapata mwafaka, poleni wafiwa, R.I.P, nyaga,
 
kumbe alijua atajiua eeh! basi azikwe pale alipoagizwa maana mila za kichaga nazo ngumu kwelikweli.
 
Si nilisoma humu, huye marehemu alikuwa hapatani na babake, na alienda kumuomba msamaha mzee akatoa nje, sasa why anataitaka maiti aizike? Halafu ni kutaka kuanzisha mvutano usiokuwa na maana, nini maana ya kuandika wosia?
 
Arusha. Utata umegubika mazishi ya Wakili maarufu nchini, Nyaga Mawalla baada ya wakili wa kujitegemea ambaye pia ni mtoto wa Rais wa zamani wa Zanzibar, Fatma Karume kuwasilisha wasia wa marehemu kwa wazazi wake ambao alitaka azikwe kwenye shamba lake la Momela, wilayani Arumeru, mkoani Arusha.

Hata hivyo, wasia huo unadaiwa kupingwa vikali na baba mzazi wa marehemu, Juma Mawalla huku akitoa sharti la kutohudhuria mazishi ya mwanaye iwapo akizikwa sehemu tofauti na Kijiji cha Marangu.

Mawalla, alifariki hivi karibuni baada ya kujirusha kutoka ghorofani akiwa Nairobi, Kenya alipokwenda kutibiwa.

Taarifa za awali zinasema kwamba Mawalla aliamua kujiua kutokana na kusumbuliwa na msongo wa mawazo, inadaiwa enzi zake za uhai alikuwa na uhusiano mbaya na baba yake.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka kwa mmoja wa mawakili wa kujitegemea mjini hapa, siku chache baada ya kifo cha wakili huyo, Karume alifika Kilimanjaro kuwasilisha wasia alioucha marehemu.

Ilidaiwa binti huyo ambaye anatajwa kuwa karibu na marehemu enzi za uhai wake, alikutana na baba yake mzazi na kuusoma.

Hata hivyo, chanzo hicho kilidai kuwa pendekezo hilo la marehemu lilipingwa vikali na baba yake na kusema iwapo mtoto wake atazikwa Momela, hatahudhuria mazishi hayo.
Imeelezwa kipindi cha miaka miwili, wakili huyo hakuweza kuongea na baba yake hadi alipofariki, kutokana na uhusiano mbaya waliokuwa nao.

Hata hivyo, wakili huyo alisisitiza kuwa, chanzo cha uhusiano mbaya baina yao ni kutokana na mzee Mawalla kumwonya mwanaye kuhusu biashara anazofanya baada kupokea malalamiko mbalimbali kutoka kwa watu, maofisa usalama na baadhi ya polisi nchini waliokuwa wakifika kijijini mara kwa mara kumsemea. Mmoja wa mawakili wa Kampuni ya Mawalla Advocates, Lemy Bartholomew alipoulizwa kwa njia ya simu na gazeti hili kuhusiana na taratibu za mazishi, alisema ni mapema kuzungumzia suala hilo kwa sababu kuna vikao vya familia vinaendelea.

Wakili huyo alisema baada ya vikao hivyo, ndipo uamuzi utakapojulikana iwapo atapozikwa shambani kwake au nyumbani kwao kijijini Marangu.

SOURCE: Mwananchi
 
SERENGETI District Council said it was shocked by the untimely death of the Arusha -based Advocate Nyaga Mawalla and pledged to sustain all development projects that he had supported in the district.

"We are also thinking of naming one of our streets Nyaga as a way of remembering our friend who for sure has significantly contributed to the development of Serengeti District," Serengeti District Council Chairman Mr John Ng'oina said.

He cited tourism and conservation as some of the sectors that the late Mawalla had considerably made vibrant in the district whose large part is made up of a variety of beautiful fauna and flora that form a large part of the Serengeti's ecosystem.

"His contribution on the establishment and the development of Ikona Wildlife Management Area (MWA) in our district is huge to date, " Mr Ng'oina told the ‘Daily News' on Wednesday morning.

The wildlife rich WMA is considered as a role model in the country's conservation sector and Serengeti officials say it has increased direct benefits to the local communities, who in the past relied mainly on poaching for a living. Figures available indicate that the late Mawalla donated around 400m/- for the development of the WMA between 2008 and 2012.

The WMA also lures millions of shillings from serious local and foreign investors, who have invested in the booming tourism sector in western Serengeti. According to the council chairman, the late Nyaga has also been in the frontline to support ongoing plans to construct an international airport in Mugumu through his firm of Mawalla Trust Ltd.

Construction of the airport is meant to transform Mugumu into a tourist hub, according to Serengeti leaders. The late Mawalla has, in connection to the education sector, helped the construction of four laboratories in various public secondary schools of Serengeti district.

"He promised to support construction of 21 laboratories in our district and already he supported four and this is a huge support on the development of education sector," Mr Ng'oina said. Mawalla passed away last weekend at a hospital in the Kenyan capital of Nairobi, where he was admitted for a longstanding heart attack. He was about thirty years old.
SOURCE: Daily News
 
Madhara ya kutokufuata wosia ni kwamba inawezakutokea siku members fulani wa familia wakadai mwili ufukuliwe ukazikwe kwingine.

Kama amesema akifia nje ya nchi azikwe hukohuko na yeye ameenda "kujiua" nje ya nchi. Yawezekana anajua zaidi sababu za kufanya hivyo. Itakuwa busara sana kuheshimu will yake. Actually hiyo ndiyo essence ya kuwa na will.
 
Mademu wa marehemu wanasemaje kuhusu wosia walioachiwa walete hata wa mdomo tu ili tuwe na choice maana sasa mnatuchanganya. Mama wa marehemu kama yupo ningependa kusikia kauli yake pia
 
Mademu wa marehemu wanasemaje kuhusu wosia walioachiwa walete hata wa mdomo tu ili tuwe na choice maana sasa mnatuchanganya. Mama wa marehemu kama yupo ningependa kusikia kauli yake pia

Huyu mtu ni milionea. Anajua wazi kuwa hata akifia popote duniani swala la gharama ya kusafirisha mwili sio tatizo. Kwahiyo kama amesema akifia nje ya nchi azikwe hukohuko kwenye maziko ya umma, basi alikuwa na maana yake. Na kuonyesha msisitizo hata will yake hajaiweka kwenye kampuni yake ya sheria, amepeleka kwa mwanasheria wa kampuni nyingine.

Watu wanaoweza kuongea na mzee inabidi wakae nae chini kwa utulivu wamuombe akidhi matakwa ya mwanawe.
 
Back
Top Bottom