Matani

Na wewe HC dada wako ni mbaya mpaka hahitaji mask wakati wa Halloween.
Castomoshi- kwenu ni masikini, wanene na hamna akili mpaka herufi pekee mnazozijua ni K.F.C
Swahilian- Wewe ni mnene mpaka ukienda kupima ktk scale inakuambia hapana mmoja mmoja tafadhali!:whoo:
Na wewe Lizzy dawa yako ipo jikoni!:gossip:

yaani we ni mjinga siku uliyoenda airport uli book ndege ya pick up body
 
Hashy: mwone kwanza..ndo maana demu wako ni mnene mpaka badala ya kuvaa pencil jeans yeye huvaa marker-pen jeans!!!
Aspirin: wewe ni mjinga mpaka ulienda driving school boarding..


kaka una maneno mengi kama uriruka stage za makuzi, mwangalie mashavu yalivomshuka kama kiwango cha soka bongo, na ndio maana kwenu kunaitwa changanyikeni mzurure.....mwisho wa upepo watoto wanaendesha tairi hadi saa sita za usiku
 
Na ujanja wako wote bado unavaa chupi ya kizamani yenye maandishi ya 007 ambayo ukiigeuza inakuwa LOO
 
Mwanakijiji: Umezoea kuendesha pikipiki mpaka mara yako ya kwanza kuendesha gari ulitoa mguu nje wakati unakata kona!!!
Hashy: nyinyi TV yenu ni ndogo mpaka iko na scrollbars..
Bucho: Wewe ni mwizi mpaka ukishikilia shilingi hamsini Nyerere anabaki na vest peke yake...
Ivuga: Mwangalie kwanza..unamatege na demu wako ana miguu pinde mpaka mkisimama pamoja mnaspell; "OX"
Njiwa: ndo maana mg'ombe wenu ni mzee mpaka anatoa maziwa mgando..
Gang Chomba: Nyinyi kwenu ni maskini mpaka mnakunywaga chai na vifuniko vya bic...lol!
ChiefmTz: Babu yako ni mzee mpaka chawa za kichwani kwake zi hutembea na bakora..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom