Matangazo ya DAWASCO hayana akili

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,888
2,772
Nimeshayasikia kama matatu hivi. yote ni ya kufikirika tu, hakuna la ukweli hata moja. Eti wakwe wanakuja wataogea nini? lingine jamaa hajaoga siku tatu, anaishi sinza anataka kuomba maji tegeta. lingine mke anamkimbia mumewe kisa hakuna maji. na mtoto nguo zake chafu hadi rangi imebadilika. kifupi DAWASCO hawana watu wa kuwatengenezea matangazo yao-wanabuni tu. hawana watu makini wa masoko. Hivi wanataka tuamini kuwa tunaishi katika ulimwengu ambao hakuna chaguo lingine isipokuwa wao tu? Kwani wakazi wa tabata, ubungo, kimara, etc. wanaishije? wanataka tuamini kuwa kila nyumba tanzania hii inategemea maji yao? Ningeandika mengi sana ila kwa huo muhtasari inatosha. DAWASCO wajipange, na matangazo yao yaendane na mazingira halisi wala si ya kubuni kama wanavyofanya.
 
It is true Mziwanda. Matangazo yanakosa mantiki. Nadhani DAWASCO waji-address kwanza kwenye suala la kuwapa wananchi walio wengi maji salama ya kunywa. Kuna watu kibao hapa mjini hawajaona hata tone moja la maji kwenye bomba zao. Mahali pengine vishoka wamejiunganishia maji kienyeji na DAWASCO wanawajua wamenyamaza. This is ridiculous!!! Wajipange upyaaaaaa!!!!
 
Tangazo lingine, hakimu anahukumu kesi ya mteja wao - hukumu faini na kifungo.

Hakuna uhusiano mzuri kati yao na wateja wao - hali ambayo ingewasaidia kuongeza wateja na kukusanya madeni 'smoothly'
 
Yule Meneja mauzo wao Bw.Raymond Mndolwa anaongea kwa MKWARA sana Redioni,Matangazo wamerokodiwa na watu wa Radio Tumaini tutegemee nini...
 
kunatakiwa kuwe na tangazo la watu wasiopata maji kutoka kwenye bomba zao, kuelimisha watu wafenyeje ili kupata huduma hizo.
 
Inabidi wajipange upya. Na huyo kaaya aangalie watendaji wake vizuri. Nadhani huwa anayapitia hayo matangazo pia
 
Yaani hawa DAWASCO kwa kweli matangazo yao hayana uwiano na huduma zao hapa mjini... Kwanza Huduma zao hazijafika kwenye maeneo yote..... Wanapaswa kwanza kuhamasisha watu wapende huduma yao kwa kuwa fast kuwaunganishia watu maji.....
Hawako na ushindan mkubwa, na urasimu ni mwingi ndo maana watu wenye uwezo wao huona ni afadhali kuchimba kisima chako........
 
Hujawahi kusikia RAP Katuni ya Inspector, sasa Dawasco nao wamekuja na Advert Katuni au sio? let them do what they do it is FREEDOM OF SPEECH and also their way of sendin the msg to their costumers.
 
Mlipe bili zenu hizo na sisi wakazi wa Kimara tunao pata maji kwa wiki mara 1 tuwe tunapata sawa kama mnao ishi Masaki na kwingineko uzunguni.
Mnatuboa sana lipieni ankra zenu hizo maji kwenu huko yanamiminika sie hata tone tu taabu ndoo tunanua 500/= kwa ajili yenu.
 
Sio tu hayana akili, bali pia hayana maadili. Mtoto anamkataza baba kumuita mwanae kisa maji. Tanzania hatujafika huko, wasitake kutuharibia watoto. Wajipange watoe huduma inavyostahili.
 
ni lazima ujumbe umefika mahala pake, hilo ndo lengo la matangazo ya biashara. swala la wapi tangazo limetengenezwa sio issue hapa au kuna sehemu mnataka kuwaelekeza sawasco wakatengeneze hayo matangazo mnayoyataka? kalipie maji kama untumia maji yao.
 
DAWASCO wanaboa kwa kweli..
JF members wote ikiwa ni pamoja na mimi mwenyewe, nawaomba wafikirie upya matangazo yao, na la msingi zaidi ni huduma zao za maji (ziwe huduma bora)........
 
Matangazo lazima yawe na vitu vitatu. Kingreza wanasema rational, emotional & fear appeal. Ss sijui dawasco wapo wapi hapo. Ujumbe umefika ndio ila tunawachukuliaje? Au kwa vile ni monopoly ndio wafanye wanavyojisikia?
 
Yule Meneja mauzo wao Bw.Raymond Mndolwa anaongea kwa MKWARA sana Redioni,Matangazo wamerokodiwa na watu wa Radio Tumaini tutegemee nini...

Wala sio Radio tumaini, Kuna mdada mmoja wa radio one anasauti ya kukwama kwama ndo anasikika sana. Yaani kila nikisikia tangazo lao lazima nibadili station. Wana boooooaaaaaaa sana.
 
Back
Top Bottom