Maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu: Gesi ya Mtwara - Pinda afanya Live Briefing Bungeni!

Ili la serikali kufanya siri mikataba ya taifa ni tatizo bunge linatakiwa kujua mikataba yote ya serikali. Bunge ndiyo chombo kinachotuwakilisha sisi wananchi.
Nimewaona wabunge kadhaa wa opposition wakilitaka bunge kutimiza wajibu wake wa kuisimamia serikali. Sasa wabunge hawa wasioruhusiwa hata kuona mikataba inayoingiwa na serikali wanayopaswa kuisimamia sijui wataisimamia vipi!
 
hiyo mikataba ni ya siri kwa manufaa ya nani?hakika usiri huu ndio unaowakosesha imani watanzania kwa chama tawala
Usiri katika mikataba, hauepukiki, japo kwa lugha ya Kiwahili huitwa siri, sio kila siri ni siri, nyingine ni faragha, na nyingine ni binafsi zote zinaitwa siri.
Secrets-siri
Confidential-siri
Classified-siri
privacy-siri

Usiri wa mikataba ni confidential na sio secret!. Lengo la usiri huu ni kuzuia classified information za makampuni zisiingie kwa washindani wako wa kibiashara unfairly hivyo kuangamizwa/kushindwa.
Pasco.
 
mkuu the big show, hapa jf, zaidi ya kubadilishana mawazo, pia tunaelimishana, kuelekezana na kusaidiana!, kwa mujibu wa kumbukumbu yangu kwa somo la mwandiko term ya pili darasa la kwanza, majina ya watu na taasisi huandikwa kwa kuanzia na herufi kubwa!.
P.

madam umekielewa hicho nilichokiandika hivo vingine its not a big deal,thats why kuna typing errors,,

wakati mwingine tukiwa nyuma ya keyboard huwa tunaandika kwa hasira sana na mihemko mikali,nadhani unatambua hilo..
Kuhusu hiyo tume kuvunjwa hebu nithibitishie kwanza pasco..!
Hasira zetu tutadhihirisha hivi punde,stay tuned...!
 
ili la serikali kufanya siri mikataba ya taifa ni tatizo bunge linatakiwa kujua mikataba yote ya serikali. Bunge ndiyo chombo kinachotuwakilisha sisi wananchi.

hivi hzi akili leo umeziokota wapi?,what a point from gamba's side
 
usiri katika mikataba, hauepukiki, japo kwa lugha ya kiwahili huitwa siri, sio kila siri ni siri, nyingine ni faragha, na nyingine ni binafsi zote zinaitwa siri.
Secrets-siri
confidential-siri
classified-siri
privacy-siri

usiri wa mikataba ni confidential na sio secret!. Lengo la usiri huu ni kuzuia classified information za makampuni zisiingie kwa washindani wako wa kibiashara unfairly hivyo kuangamizwa/kushindwa.
Pasco.


thats why mkapa kawaambia ya kwamba,mipango ya maendeleo haina haja ya kufanya faragha,wananchi watataka kufaham ukweli na uhalisia pasco..!
Na hiyo faragha inayozungumziwa ina mipaka yake,chombo chetu kama bunge kina haki ya kuisimamia serikali katika vipengele mbali mbali,iweje mikataba hiyo ifanywe siri hadi kwa wabunge??
Mwaka huu mbivu na mbichi itajulikana nakuambia.
 
PM hajawa mkweli.

Makampuni mengi, hasa yaliyo kwenye sekta ya nishati na madini wanataka sana mikataba iwe wazi. Na hii ni kwa sababu huko wanakotoka wanatakiwa wawe transparent. Lakini kwa sababu wanazojua wenyewe wakubwa wa CCM wamekuwa wanang'ang'ania mikataba iwe siri. Kwa hili watanzania tunaingizwa mjini mchana kweupe. Na nadhani mikakati ya kudai uwazi wa mikataba sasa ujumuishe wanaharakati wa nchi zilizotoka haya makampuni. Mfano kuna makampuni toka Norway na UK. Wanaharakati wa Tanzania waanze kuwahusisha asasi za huko ili makampuni hayo yaweke mambo hadharani. Kuna ulaghai mkubwa kwenye hii mikataba.

Na huko tuendako, mikataba yote lazima ijulikane kwa jamii inayozunguka hizo rasilimali. Haiwezekani, kwa mfano, uchimbe Tanzanite, lakini wananchi wa Mererani hawajui chochote kuhusu mkataba wa uchimbaji madini? Hii ni fedheha na viongozi wetu waone aibu ya kutetea hii fedheha. Waafrica tunadharauliwa kwa upuuzi wa namna hii, tunatumia nguvu kubwa kufunika wizi wakati huo huo tunazidi kuomba chakula toka kwa mtu tuliyomruhusu atuibie! Very wrong.

FJM

Yaani mifumo yetu, taasisi zetu (likiwemo Bunge) na sisi wenyewe ni dhaifu kiasi hicho mpaka tuombe msaada wa wanaharakati wa nje! Hii ni aibu. Tunapaswa kuona hiyo mikataba, haiwezi kufanywa siri hata kwa wawakilishi wetu. Mbona nchi zingine inafanyika na kama ulivyosema huko huko yanakotoka hayo makampuni na wawekezaji!
 
  • Thanks
Reactions: FJM
madam umekielewa hicho nilichokiandika hivo vingine its not a big deal,thats why kuna typing errors,,

wakati mwingine tukiwa nyuma ya keyboard huwa tunaandika kwa hasira sana na mihemko mikali,nadhani unatambua hilo..
Kuhusu hiyo tume kuvunjwa hebu nithibitishie kwanza pasco..!
Hasira zetu tutadhihirisha hivi punde,stay tuned...!
Kuandika majina ya watu kwa herufi ndogo sio typing error!, ni negligency kama sio ignorance!,
Tume haiwezi kuvunjwa kwa sababu haikuwahi kuwepo, kilichofanyika ni kutangaza kuwa ule mpango wa kuunda tume, sasa haupo tena!, umekufa kwa sababu mgogoro umeishamalizika rasmi!.
Pasco.
 
Ivi mikataba ya inchi inakuwaje siri ata kwa wawakilishi wa wananchi
serikali ni ya wananchi na imewekwa na wananchi sasa inapoingia mkataba kwa niaba yetu why tusijulishwe kilichomo
ningependa nipate yaliyomo kwenye mkataba wa bandari ya bagamoyo na lile bomba la gesi nahisi tumepigwa big time
 
serikali ya TZ inafanya kila jambo / kitu ni siri. hata sura ya Lulu wakati anaachiwa kwa dhamana TBC walifanya kuwa siri..eti waliziba uso wa Lulu wakati yuko kwenye mchakato wa kutoka mahakamani! mwee...tuna kazi kweli!

Raslimali tunaambiwa ni mali ya watanzania ila mikataba ni siri..hata sielewi. halafu wewe
Pasco unatuambia eti lazima mikataba iwe siri eti kwa sababu ndani ya mikataba kuna information za makampuni ambazo makampuni hayataki washindani wao wazione. hiyo sio kweli, kwa sababu mikataba yote inatengenezwa kutokana na sheria za nchi zinazohusu raslimali husika. mathalani mikataba ya madini inatengenezwa kwa kutumia Sheria ya Madini ya Mwaka 2010. mikataba ya gesi inatengenezwa kwa kutumia PSA (Production Sharing Agreements). sasa kichekesho ni hiki: sera ya gesi haijakamilika maana ikikamilika sera ndio serikali inatengeneza sheria ya gesi ambayo mpaka sasa haipo. hizo PSA zimepitwa na wakati na hazizingatii maslahi ya watanzania. mwaka jana Prof. Muhongo aliiagiza Bodi mpya ya Wakurugenzi ya TPDC kupitia upya mikataba yote 26 ya gesi. ripoti tayari amekabidhiwa...na kuna mapungufu makubwa mno yanayoonesha watanzania hatunufaiki ipasavyo na raslimali yetu ya gesi. sasa kimbembe kinakuja Prof ameshauriwa asiipige chini hiyo mikataba kwa madai eti wawekezaji watakimbia na kwenda kuwekeza nchi zingine kama Msumbiji ambako kuna gesi nyingi! ..upuuzi mtupu!

To make a long story short ni kwamba wawekezaji hawataki mikataba iwekwe wazi kwa sababu watanzania watajua unyonyaji uliomo katika mikataba hiyo. na viongozi wa serikali hawataki mikataba iwekwe wazi kwa kuwa walishalipwa 10% na wawekezaji, na ndo kama hayo ya mabilioni ya Uswisi. kimsingi wanataka watanzania tuishi kama mazezeta kila jambo tusihoji bali tuwe tunaimba pambio la NDIO MKUU..NDIO MKUU! thanx wanamtwara wameimba kinyume..HAPANA MKUU..HAPANA MKUU!
 
kuandika majina ya watu kwa herufi ndogo sio typing error!, ni negligency kama sio ignorance!,
tume haiwezi kuvunjwa kwa sababu haikuwahi kuwepo, kilichofanyika ni kutangaza kuwa ule mpango wa kuunda tume, sasa haupo tena!, umekufa kwa sababu mgogoro umeishamalizika rasmi!.
Pasco.

bado sijaamin maneno hayo..
Haiwez kuwa kirahis ivo.
 
serikali ya tz inafanya kila jambo / kitu ni siri. Hata sura ya lulu wakati anaachiwa kwa dhamana tbc walifanya kuwa siri..eti waliziba uso wa lulu wakati yuko kwenye mchakato wa kutoka mahakamani! Mwee...tuna kazi kweli!

raslimali tunaambiwa ni mali ya watanzania ila mikataba ni siri..hata sielewi. Halafu wewe
pasco unatuambia eti lazima mikataba iwe siri eti kwa sababu ndani ya mikataba kuna information za makampuni ambazo makampuni hayataki washindani wao wazione. Hiyo sio kweli, kwa sababu mikataba yote inatengenezwa kutokana na sheria za nchi zinazohusu raslimali husika. Mathalani mikataba ya madini inatengenezwa kwa kutumia sheria ya madini ya mwaka 2010. Mikataba ya gesi inatengenezwa kwa kutumia psa (production sharing agreements). Sasa kichekesho ni hiki: Sera ya gesi haijakamilika maana ikikamilika sera ndio serikali inatengeneza sheria ya gesi ambayo mpaka sasa haipo. Hizo psa zimepitwa na wakati na hazizingatii maslahi ya watanzania. Mwaka jana prof. Muhongo aliiagiza bodi mpya ya wakurugenzi ya tpdc kupitia upya mikataba yote 26 ya gesi. Ripoti tayari amekabidhiwa...na kuna mapungufu makubwa mno yanayoonesha watanzania hatunufaiki ipasavyo na raslimali yetu ya gesi. Sasa kimbembe kinakuja prof ameshauriwa asiipige chini hiyo mikataba kwa madai eti wawekezaji watakimbia na kwenda kuwekeza nchi zingine kama msumbiji ambako kuna gesi nyingi! ..upuuzi mtupu!

to make a long story short ni kwamba wawekezaji hawataki mikataba iwekwe wazi kwa sababu watanzania watajua unyonyaji uliomo katika mikataba hiyo. Na viongozi wa serikali hawataki mikataba iwekwe wazi kwa kuwa walishalipwa 10% na wawekezaji, na ndo kama hayo ya mabilioni ya uswisi. Kimsingi wanataka watanzania tuishi kama mazezeta kila jambo tusihoji bali tuwe tunaimba pambio la ndio mkuu..ndio mkuu! Thanx wanamtwara wameimba kinyume..hapana mkuu..hapana mkuu!


Thanks a lot mkuu..
Bila shaka pasco ni kibaraka wao..
Ukweli sasa upo wazi,mafisadi hawana pa kutokea.
 
Ili la serikali kufanya siri mikataba ya taifa ni tatizo bunge linatakiwa kujua mikataba yote ya serikali. Bunge ndiyo chombo kinachotuwakilisha sisi wananchi.
​gesi kuunda kundi la nne la kugombea urais ndani ya ccm pazuri hapo ccm bana kila kiongozi ni msanii mchafu
 
Mhe. PINDA anatumia BUNGE kudanganya UMMA. Huo uchochezi wa KISIASA uliofanywa na vyama vya SIASA mbona viongozi wa hivyo VYAMA kama unawafahamu WAKAMATWE.
Watanzania wa sasa WANATAKA ile AHADI ya MAISHA bora ITIMIE kwa kutumia RASILIMALI zao.....
 
pasco,,
mbona kuna taarifa nimezipata ya kwamba hiyo kamati ya bunge ipo na itaundwa?
Nimempgia simu mbunge wa lindi,na nimeongea na ndugu magdalena sakaya wanasema hoja hiyo ya kuundwa kwa kamati/tume huru ya bunge ipo pale pale?
Au ulikuwa unataka kupotosha jamvi hili??
 
uharibifu wote huo wa kuwajibika ni Prof Muhongo na wenzake kwa kauli za dharau kwa wana Mtwara. WM anatoa matumaini - inatakiwa ratiba ya utekelezaji ili wana Mtwara waweze kufuatilia kwa karibu. Kusini ni sehemu iliyosahaulika kwa nusu karne yote
mimi ningependa kuona na master plan ya reli kutoka ntwara kwenye deepest port in east africa uelekea kaskazini magharibi ya tz sio Picha za Kabila na viongozi wetu, hiyo bandari ni mgodi, na pia reli, sio tunaiangaliaangalia drc , tunavyo fanya sasa, bila kusahau zambia na Malawi
 
Back
Top Bottom