Live Bunge TV: Maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu Leo

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,499
113,608
Wanabodi
Leo ni Alhamisi, nakuletea Live kutoka Bunge TV kupitia TBC, Kipindi cha Maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu Leo, ambaye jana amefanywa ni Bwana mdogo, kwa kupewa amri na Bwana mkubwa mmoja.

Spika ametangaza Waziri Mkuu hatapokea maswali, atatangaza jambo mahsusi

Waziri Mkuu kaanza kwa kumpongeza Spika, Dr. Tulia kwa kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge la IPU akiwa ni Mwanamke wa kwanza na mwafrika wa kwanza kuwa nafasi hiyo.

Waziri Mkuu ametangaza, serikali imeridhia rasmi Sera Mpya ya elimu na mitaala mipya ya elimu.

Waziri Mkuu amesema sasa mitaala ya elimu yetu inajikita kwenye utoaji wa elimu inayo zingatia kuwajengea ujuzi wa stadi za soko la ajira.

Mabadiko makuu ya kwanza, elimu ya darasa la Saba sasa mwisho ni mwaka 2026, kuanzia 2027 hakuna darasa la 7, elimu ya msingi mwisho darasa la 6, kisha unakwenda straight sekondari, elimu ya lazima ni mpaka form 4!.
Nani kama Mama?.

Hili likitekelezwa, hata ile hoja yangu ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2030, ndio mwanzo wa mwisho wa CCM! Wajinga karibu wote watakuwa wamemalizika! sasa utabadilika!.
2030 ni CCM tena!, ni CCM milele!.

Kwa vile muda unaruhusu, Spika ameruhusu maswali kwa Waziri Mkuu kuhusu hoja iliyopo mezani, Mbunge wa Mlalo, Mhe. Shangazi, akampiga swali.

Mhe. Shangazi ameuliza Shule za umma ziko chini ya Tamisemi, shule binafsi ziko chini ya nani?.

PM amejibu elimu yote ya umma na binafsi inaratibiwa na kusimamiwa na serikali, idara ya kudhibiti ubora wa elimu inazikagua Shule binafsi, ila pia serikali imewaruhusu wenye Shule binafsi kujiundia chombo chao.

Mbunge wa Sikonge, Mhe. George Kakunda, aneuliza sera ya elimu iliyohuishwa mwaka 2014, ilishindwa kutekelezeka kutokana na kutokuwepo mabadiliko ya sheria ya elimu!, leo tunakuja na sera mpya bila sheria mpya ya elimu, ni lini serikali italeta sheria mpya ya elimu itakayo endana na sera mpya ya elimu?.

Waziri Mkuu amejibu mabadiliko ya sheria ya elimu yanakuja, mchakato unaendelea.

Kipindi cha maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu kimekwisha.
Bunge linaendelea kwa maswali ya kawaida.
Asanteni kulifuatilia hili.

Thanks

Paskali
 
PM kaanza kwa pongezi kwa Dr. Tulia kuchaguliwa kuwa Spika wa IPU akiwa ni mwafrika wa kwanza.
P
 
Sasa mitaala ya elimu yetu ni kujikita kwenye utoaji wa elimu inayo zingatia kuwajengea ujuzi wa stadi za soko la ajira.
P
 
Mabadiko makuu ya kwanza, elimu ya darasa la Saba sasa mwisho ni mwaka 2026, kuanzia 2027 hakuna darasa la 7, elimu ya msingi mwisho darasa la 6, kisha unakwenda straight sekondari, elimu ya lazima ni mpaka form 4!.
Nani kama Mama?.
P
 
Mabadiko makuu ya kwanza, elimu ya darasa la Saba sasa mwisho ni mwaka 2026, kuanzia 2027 hakuna darasa la 7, elimu ya msingi mwisho darasa la 6, kisha unakwenda straight sekondari, elimu ya lazima ni mpaka form 4!.
Nani kama Mama?.
P
Pascal nakuheshimu sana .

This is very low from you.

Hiyo statement ya nani kama mama inahusikaje hapo wakati ni wazi mfumo wa madarasa mengi na kukaa miaka mingi shule haukua na tija na mitaala ilipitwa na wakati?
 
Kwa vile muda unaruhusu, Spika ameruhusu maswali kwa Waziri Mkuu kuhusu hoja iliyopo mezani, Mbunge wa Mlalo, Mhe. Shangazi, akampiga swali.
P
 
Back
Top Bottom