Marekani hakuna Rais daktari, CPT, Engineer wala Advocate? Kwanini hawapendi kusoma?

Niulize swali hapa:
Kuna elimu inaitwa Egyptology, yaani elimu kuhusu Egypt. Elimu kuhusu Marekani, inaitwaje? Americanology? Watu waliosomea mambo ya taifa la Marekani, discipline yao inaitwaje?
 
Marekani ambayo kabla kupata uhuru mwaka 1776 , ilitawaliwana Uingereza na wakapata Rais wa kwanza George Washington.
Tangu wapate uhuru, haijawahi kutokea Rais yeyote , awe msomi wa chuo, daktari wa hospitali[MD] au wa falsafa phD,au mjuzi wa hesabu [CPA] ambaye amewahi kujinasibu na prefix ya cheo chake.

Je, ni ulimbukeni kutumia phD, CPA, Advocate kwenye majina ya marais? Je, haya majina wanayojipa kwenye vyeo vyao yana-reflect maendeleo kwenye nchi zao?

OBAMA [Profesa wa Sheria]

LIST YA MARAIS WOTE WA MAREKANI.

  1. George Washington (1789-1797)
  2. John Adams (1797-1801)
  3. Thomas Jefferson (1801-1809)
  4. James Madison (1809-1817)
  5. James Monroe (1817-1825)
  6. John Quincy Adams (1825-1829)
  7. Andrew Jackson (1829-1837)
  8. Martin Van Buren (1837-1841)
  9. William Henry Harrison (1841)
  10. John Tyler (1841-1845)
  11. James K. Polk (1845-1849)
  12. Zachary Taylor (1849-1850)
  13. Millard Fillmore (1850-1853)
  14. Franklin Pierce (1853-1857)
  15. James Buchanan (1857-1861)
  16. Abraham Lincoln (1861-1865)
  17. Andrew Johnson (1865-1869)
  18. Ulysses S. Grant (1869-1877)
  19. Rutherford B. Hayes (1877-1881)
  20. James A. Garfield (1881)
  21. Chester A. Arthur (1881-1885)
  22. Grover Cleveland (1885-1889)
  23. Benjamin Harrison (1889-1893)
  24. Grover Cleveland (1893-1897)
  25. William McKinley (1897-1901)
  26. Theodore Roosevelt (1901-1909)
  27. William Howard Taft (1909-1913)
  28. Woodrow Wilson (1913-1921)
  29. Warren G. Harding (1921-1923)
  30. Calvin Coolidge (1923-1929)
  31. Herbert Hoover (1929-1933)
  32. Franklin D. Roosevelt (1933-1945)
  33. Harry S. Truman (1945-1953)
  34. Dwight D. Eisenhower (1953-1961)
  35. John F. Kennedy (1961-1963)
  36. Lyndon B. Johnson (1963-1969)
  37. Richard Nixon (1969-1974)
  38. Gerald Ford (1974-1977)
  39. Jimmy Carter (1977-1981)
  40. Ronald Reagan (1981-1989)
  41. George H. W. Bush (1989-1993)
  42. Bill Clinton (1993-2001)
  43. George W. Bush (2001-2009)
  44. Barack Obama (2009-2017)
  45. Donald Trump (2017-2021)
  46. Joe Biden (2021-present)
MADAKTARI WALIKUWA HAWA.
1. James Madison
2. William Henry Harrison
3. Andrew Johnson:

MAWAKILI/WANASHERIA

1. Barack Obama: Obama alipata digrii yake ya sheria kutoka Shule ya Sheria ya Harvard na alifanya mazoezi ya sheria huko Illinois kabla ya kuingia katika siasa. Aliwahi kuwa Rais wa 44 wa Merika kutoka 2009 hadi 2017.

2.Bill Clinton: Clinton alipata digrii yake ya sheria kutoka Shule ya Sheria ya Yale na alifanya mazoezi ya sheria huko Arkansas kabla ya kuingia katika siasa. Aliwahi kuwa Rais wa 42 wa Merika kutoka 1993 hadi 2001.

3.
Gerald Ford: alipata digrii yake ya sheria Yale Law School and practiced law in Michigan kabla ya kuingia kwenye siasa . Alikuwa raisi wa 38 US tangu 1974 to 1977.

4. Richard Nixon: alipata digrii yake ya sheria Duke University Law School and practiced law in California kabla ya kuingia kwenye siasa. He served as the 37th President of the United States from 1969 to 1974.

5. Franklin D. Roosevelt: Roosevelt alihudhuria Shule ya Sheria ya Columbia lakini hakumaliza shahada yake ya sheria. Alifanya sheria kwa muda mfupi kabla ya kuingia kwenye siasa. Aliwahi kuwa Rais wa 32 wa Merika kutoka 1933 hadi 1945.

6 Thomas Jefferson: Jefferson pia alikuwa mwanasheria kitaaluma. Alilazwa katika baa ya Virginia mnamo 1767 na akafanya sheria kwa miaka kadhaa kabla ya kuingia kwenye siasa. Jefferson aliwahi kuwa Rais wa tatu wa Merika kutoka 1801 hadi 1809.

7. James Madison: Madison alipata elimu yake ya kisheria kutoka Chuo cha William na Mary na alifanya sheria huko Virginia. Alikuwa mmoja wa waandishi wa msingi wa Katiba ya Merika na aliwahi kuwa Rais wa nne wa Amerika kutoka 1809 hadi 1817.

8. James Monroe: Monroe alisoma sheria chini ya Thomas Jefferson na kufanya sheria huko Virginia. Aliwahi kuwa Rais wa tano wa Merika kutoka 1817 hadi 1825.

9. John Quincy Adams: Adams alikuwa mwanasheria aliyeelimishwa na Harvard ambaye alitekeleza sheria kabla ya kuingia kwenye siasa. Aliwahi kuwa Rais wa sita wa Merika kutoka 1825 hadi 1829.

10. Andrew Jackson: Jackson alianza kusomea sheria katika ujana wake na alilazwa katika baa ya North Carolina mwaka wa 1787. Alifanya mazoezi ya sheria huko Tennessee na aliwahi kuwa Rais wa saba wa Marekani kuanzia 1829 hadi 1837.

11. Abraham Lincoln: Lincoln ni mmoja wa wakili-marais maarufu katika historia ya U.S. Alifanya mazoezi ya sheria huko Illinois na aliwahi kuwa Rais wa 16 wa Merika kutoka 1861 hadi 1865.

12. Franklin Pierce: Pierce alihudhuria shule ya sheria katika Chuo cha Bowdoin na alifanya mazoezi ya sheria huko New Hampshire. Aliwahi kuwa Rais wa 14 wa Merika kutoka 1853 hadi 1857.

13. Benjamin Harrison: Harrison alisomea sheria katika Chuo Kikuu cha Miami na kufanya mazoezi ya sheria huko Indiana. Aliwahi kuwa Rais wa 23 wa Merika kutoka 1889 hadi 1893.

14.Rutherford B. Hayes: Alisoma Harvard Law School na kufanya kazi Ohio. Alikuwa raisi wa 19 wa Marekani toka 1877 mpaka 1881.

15. William Howard Taft: Alisoma chuo cha Yale akifanya kazi huko Ohio. Alikuwa raisi wa 27 tangu 1909 to 1913 na baadae akawa jaji mkuu wa Marekani .

16. Calvin Coolidge: Alisoma Law na kuwa wakili huko Massachusetts. Alifanya kazi za uwakili kabla ya kuingia kwenye siasa na kuwa raisi wa 30 tangu 1923 to 1929.

17. Woodrow Wilson: Wilson alisoma shule ya sheria kwa vitendo Chuo kikuu Virginia na kufanya kazi ya uwakili,alikuwa raisi wa 28 wa marekani toka 1913 mpaka 1921.

18. Chester A. Arthur: Arthur practiced law in New York City before entering politics. He served as the 21st President of the United States from 1881 to 1885.

19.Grover Cleveland: Cleveland studied law and was admitted to the bar in 1859. He practiced law in New York and served as the 22nd and 24th President of the United States from 1885 to 1889 and again from 1893 to 1897.

20. Chester A. Arthur: Alikuwa wakili New York City kabla hajaingia siasani. Akawa raisi wa 21wa Marekani toka 1881 mpaka 1885.

Hao wote, madaktari, CPA, MAprofessor na Mawakili hawatumii tittle zao, kwanini Afrika ?

Kwanini Maraisi wa kisasa , hasa Afrika wanapenda recognition ya udaktari ?
Ongezea hapo kwa huyu mzee wa upinde pope Francis yeye hana elimu? Mbona kwenye articles za kina Bagonza kutwa kuna (PhD), huku kwetu elimu inaondoka mdogo mdogo vijana wanafakamia maphd na uwakili kwaajili ya title si ilmu bwanshee
 
Dr John pombe Joseph magufuli

Napenda Sana kulitamka hvyo
Angekuwepo hadi leo, ningemshauri sana aliondoe hilo jina lenye herufi P, pamoja na kwamba ni la wahenga wake.
Kumbe haya majina kwenye ulimwengu wa roho, yanabeba mambo mazito sana
Majina kama
Shida'
Tabu
Mateso
Nyanzala (njaa)
Malimi (ukame)
Si majina ya kuwapa watoto, hata kama mwenye jina aliwahi kuwa Rais wa dunia nzima
I like chagga people names
Eli........
Elibariki
Elisante, n.k.
Eli-===God
Halafu wakipata fedha tunaaza kupiga kele kwamba wanaiba; hawaibi ni Mungu
 
Haya mambo yalianza Kikwete, kuitwa Ndugu Jakaya Kikwete kwenye karatasi ya huku jirani yake kuna Dr Wilbroad Slaa na Prof Ibrahim Lipumba sijui na nani huko akaona msinitanie.

Aliamua kununua hiyo hadhi, sasa ni mwendo mdundo.
 
Familia pekee mbili za Marekani zilizaowahi kushika Urais wa Marekani mara mbili

2. John Adams (1797-1801)
6. Andrew Jackson (1829-1837)

41. George H. W. Bush (1989-1993)
43. George W. Bush (2001-2009)
Familia Mbili zilizoshi/Zitazoshika urais Tanzania :
1. Ali Hassa Mwinyi- Rais wa Tanganyika
2. Hussein Mwinyi- Rais wa Zanzibar
1. Abei Karume
2. Karume JR.
1. Samia Suluhu.
2................Hafith Hassan 2030-35[Zanzibar]
 
Wakatoliki kaa nao mbali.
Mapadri wengi wana digrii si chini ya tatu . Ukiona ana phD hiyo ana digrii nne,akaamua kupiga masters na phD.
Kwa mambo ya elimu CATHOLIC ndio bora duniani.
Marekani yenyewe tangu imeanza kujitawala, Marais wakatoliki ni huyu Biden ndo wa pili,wa kwanza ni yule aliyeuawa JF Kennedy ndo alikuwa wa Rais mkatoliki wa kwanza. Sasa sijui labda wanatamba zaidi Africa, south America na nchi chache za Ulaya na pengine nchi kubwa zaidi ni France.
 
Marekani ambayo kabla kupata uhuru mwaka 1776 , ilitawaliwana Uingereza na wakapata Rais wa kwanza George Washington.
Tangu wapate uhuru, haijawahi kutokea Rais yeyote , awe msomi wa chuo, daktari wa hospitali[MD] au wa falsafa phD,au mjuzi wa hesabu [CPA] ambaye amewahi kujinasibu na prefix ya cheo chake.

Je, ni ulimbukeni kutumia phD, CPA, Advocate kwenye majina ya marais? Je, haya majina wanayojipa kwenye vyeo vyao yana-reflect maendeleo kwenye nchi zao?

Hao wote, madaktari, CPA, MAprofessor na Mawakili hawatumii tittle zao, kwanini Afrika ?

Kwanini Maraisi wa kisasa , hasa Afrika wanapenda recognition ya udaktari ?

Hii ni hoja ya msingi sana, niliwahi kushauri Kuongezeka Ph.D za Heshima: Kuna haja TCU watoe ufafanuzi wa matumizi ya title ya Dr. kwa Ph.D za heshima na Ph.D za ukweli?
P
 
Marekani yenyewe tangu imeanza kujitawala, Marais wakatoliki ni huyu Biden ndo wa pili,wa kwanza ni yule aliyeuawa JF Kennedy ndo alikuwa wa Rais mkatoliki wa kwanza. Sasa sijui labda wanatamba zaidi Africa, south America na nchi chache za Ulaya na pengine nchi kubwa zaidi ni France.
Upo sahihi bwashee.
 
Tofauti na wengine wenzetu when it comes to maamuzi au kupata kingozi ni mfumo wa nchi rather than president. Hizi Phd ,dr ni sifa tu za kujiuza kisiasa but hazisaidii maamuzi ya nchi
Kwa Tz na za kuuza Sura ndio maana unaona watu wanazitafuta na kuzitumia, wenzetu uelewa wao mkubwa wanakupima na utekelezaji wako. Na pia siasa za uchawa hawana
 
Wako wote hao,hawaitani hivyo vyeo mitaani kama kwetu huku uswahilini utasikia wakili msomi,kwani kuna wakili hajasoma
Hilo la wakili msomi nitakupa elimu siku nyingine. Kwa hili joto la leo hapo rufiji nutakuwa hupumui na hutaelewa.
 
Kwa Tz na za kuuza Sura ndio maana unaona watu wanazitafuta na kuzitumia, wenzetu uelewa wao mkubwa wanakupima na utekelezaji wako. Na pia siasa za uchawa hawana
Hawana culture ya uchawa ( aka unafki ulio rasimishwa)
 
Ujazo vs ubora. Tusilaumu kitu, tunaochagua ni sisi wananchi kwa hiyo mambo yakienda kombo tuanze kwanza kujipa lawama sisi wapiga kura.
Tunamchagua nani, wanajichagua wenyewe.
Bila kupepesa macho mtu anasimama jukwaani, nakuamuru aletewe fulani.
Eti nikulipe mshahara nikupe nyumba gari ni halafu utangaze mbaya wangu mshindi, dhubutu.

Sent from my TECNO CK7n using JamiiForums mobile app
 
professor na Dr ni titles za kufundishia vyuoni na kwenye utafiti tu. Ukiwa kwenye Kazi za kawaida hutakiwi kutumia.
Engineer ni cheo cha makazini huko na sio kwenye siasa.

Ndio maana husikii Dr au Professor japo wenye titles hizo wapo kwenye siasa zao.
 
Back
Top Bottom