The Boss
JF-Expert Member
- Aug 18, 2009
- 49,111
- 115,906
Kama kuna Rais Mmarekani aliwahi kukejeliwa basi hakuna aliemzidi Ronald Reagan.
Nakumbuka hata Nyerere katika hotuba zake aliwahi sema kuhusu Reagan."jitu kimekaa Tu pale linawakilisha maslahi ya mabeberu" hata halina akili".
Nyerere alikuja kuongea haya baadae Sana miaka ambayo tayari Marekani washabadilisha Sana Marais.
Sababu kubwa Sana ya kukejeliwa Kwa Ronald Reagan ilikuwa sababu Ronald Reagan hakuwa "traditional" Rais kama wengine ...waliokuwa na CV zilizoshiba zinazo onesha uhodari wao walikopita.
Ronald Reagan alikuwa muigizaji wa filam Hollywood kabla ya kuingia siasa...alishinda Ugavana...kabla ya scandal kubwa Sana kumkumba Rais Jimmy Carter akiwa madarakani kule Iran...ndo Ronald Reagan akagombea Urais akashinda.
Ronald Reagan alikuwa anaonekana kama kibaraka Tu wa kundi lililokula njama za kuhakikisha Jimmy carter anashindwa Urais....kejeli zilikuwa nyingi sana na kejeli ziliendelea hata alipomaliza Urais cha ajabu ukiangalia mafanikio Reagan anatajwa kama mmoja wa Marais waliofanikiwa Sana kuindeleza USA alibadili sheria nyingi
Sana .. kiuchumi alifanya mabadiliko makubwa Sana yeye na Margaret Thatcher wa Uingereza ndo waasisi wakubwa wa Sera za kuitoa serikali Kwenye biashara za kila siku na kuacha private sector zishike biashara hizo... Margaret Thatcher nae alipingwa mno huku jinsia yake nayo ikiguswa ..alikuja kusifiwa baadae Sana Akiwa keshatoka Madarakani.
Samia kuwa Rais wa kwanza mwanamke... katika Taifa lenye mfumo dume sugu .. Taifa lenye ushirikina sugu wa kuanzia kuua albino hadi wa kukesha makanisa ya maombi..usitegemee atapata safari yenye Urais wa chochote atakacho fanya...stereo types zitafanya baadhi wahoji kila kitu na wasiamini chochote.
Wapo wanaotaka waziwazi wasikie Kikwete anasemaje ndo waamini Samia ana maamuzi sahihi...kwao Kikwete au Kiongozi wa kiume yeyote level ya Urais ndo "kigezo" cha kuwa Samia kafanya sahihi au la ...mfumo dume unafanya kiongozi wa upinzani asihoji akili za mwanaume mwenzie mwenye PhD ambae ni waziri husika lakini anaenda moja Kwa moja kumshambulia Rais na akili ya Rais huku akijua Rais sio Mtaalam wa mikataba...hata hao kina Kikwete na Magufuli ama Kwa kushauriwa sahihi au la walisaini mikataba iliyokuja kuleta shida mbele ya safari...lakini Mradi Rais ni mwanamke na wanaomkosoa wanachapa Hadi vibao na fimbo wake zao basi Rais lazima atatukanwa hadi akili yake.
Ronald Reagan alitukanwa Kwa kupenda sherehe white house za kila mara ... Wengine walimuona ni "muigizaji Tu kutoka Hollywood" anaepewa maelekezo na "wajuzi".
Lakini hata hao wajuzi walikuja kukubali very late kuwa Reagan alikuwa Rais alieweza fanikisha Mengi mno kuliko Marais walionekana "wajuzi" kumzidi.... kuanzia kuiangusha Russia...na kumaliza cold war Hadi kuitoa Serikali kwenye biashara na kuacha sekta binafsi inawiri.
Mmoja wa wasaidizi wake alieonekana kama mjuzi kumzidi George H Bush alipokuja kumrithi alifanikiwa Jambo moja Tu kukamilisha la kumaliza cold war na kuiunganisha German...lakini alishindwa vibaya mno kwenye uchumi Hadi akaibuka jamaa anaitwa Bill Clinton akaja kuchukua Urais.
Sometimes Urais ni zaidi ya akili na ujuzi, sometimes Urais au uongozi ni "baraka tu" wakristo wanaita "Kibali" Mungu anakupa.
Tuache fitina na kejeli..na kumshambulia Kwa jinsia yake.
Tusije kuja kumthamini very very late...