plus_ix
JF-Expert Member
- Jul 10, 2022
- 561
- 1,390
Habarini wana JF. Moja kwa moja kwenye mada kama kichwa hapo juu kinavyojieeleza.
Huyu ni mtoto wa jamaa angu nimeona niandike kwaajili yake, labda tutapata msaada humu ndani maana binafsi nimeshindwa.
Nina mtoto kwa sasa ana umri wa miaka kumi na nne (14) yupo kidato cha kwanza lakini kwa mwenendo wake naona hata kidato cha pili hatoboi, dogo ana matukio ya ajabu sana na tumejitahidi kwa kila njia lakini imeshindikana ntaweka matukio yake kiufupi.
Mwanzo kabisa wakati yupo darasa la tano alikimbia nyumbani hapa, alitoka Pugu mpaka kinyerezi kwa mguu kwa madai hakupendi. Tulijua ni kwa sababu ya utoto tulimtafuta kama siku mbili na kwa msaada wa polisi tulimpata tukapiga kidogo tukaacha.
Akakaa sawa akanza tutesa na tabia ya udokozi wa hela ndogondogo na anakopeleka ni kwenye play station tukamshika tena tukapiga kwa kuhofia ataanza kudokoa hela kubwa kubwa lakin nikama ndo tulikuw tunachochea moto.
Baada ya hapo matukio ni mengi sana hapa katikati ila kwa hili alilofanya kipindi hiki ni hatari zaidi. Ameanza kidato cha kwanza vizuri na kwa matokeo mazuri tu ya shule ya msingi kuanzia mwezi wa 1 mpaka mwezi wa sita matokeo yalikuja mabovu sijawahi ona. Somo alilofaulu sana alikuwa na arobaini nalo ni Kiswahili hayo mengine ni 14, 4.
Aisee ndio kuchukua maamuzi kwenda shuleni kukuta taarifa mtoto ni mtoro sugu, siku alizoingia darasani zinahesabika na kila siku anapewa hela ya shule. Ndio kufatili kwa makini kumbe anashinda chimbo na jamaa yake ambao wanaacha begi na nguo za shule kwa huyo jamaa, wanavaa nguo za nyumbani waneenda ps muda wa kurudi shule wanapitia kwa jamaa anavaa kama alivyoondoka asubuhi na kurudi nyumbani.
Basi hapa tulimkamata, tulipiga sana nusu kuua mpaka Mwalimu Mkuu aliingilia kati akasema hapa amenyoka. Tukampa mwalimu wa kumfatilia walivofungua shule kama wiki mbili tu hivi nikaitwa shuleni kwamba mwanao amekodi wahuni wa mtaani waje kumpiga mwalimu.
Aisee hapa nilipatwa na hasira sana, nilimpiga kiganja kimoja cha maana ndio nikamwambia jieeleze, ndio kuniambia wale wahuni aliwanunulia packet tatu za sigara akawapa na hela ya bangi ili waje kumpiga mwalimu!
Nilikuw najiuliza huyu ni mtoto wa namna gani licha ya mimi utotoni kuwa mtundu lakini kwa huyu mtoto ni zaidi. Mwezi wa 11 nilimpa hela apeleke shule, yeye akala ile hela na alivyogundua nimejua hajapeleka hela shuleni akaja nyumbani akaingia chumbani kwangu akapekenyua hela akabeba elfu hamsini akakimbia, hajalala nyumbani siku mbili, tukamtafuta tukampata.
Tulimpa kipigo kikali, nina jamaa angu polisi nikampigia simu aje amchimbe mikwara, jamaa kweli alikuja mpaka nyumbani na gari ya polisi na badhi ya askari na kule kwenye gari kulikuwa na waharifu waliopigwa na wananchi wamechakaa damu wanapelekwa hospitali nikasema mbebeni na huyu kwa lengo la dogo aogope ajue kichapo kilivyo huko njee na biti za polisi.
Walizunguka nae wakamrudisha jioni hapa alikuwa mpole balaa mpaka kilichotokea hiki sasa mpaka hapa naandika huu uzi huyu mtoto kaiba laki moja na kakimbia toka jana.
Naombeni mnisaidie mbinu gani ni itumie kwa huyu mafia ili akae sawa, kama ni kipigo nimepiga mnoo, ushauri kapewa mpaka na wachungaji lakini bado.
Naona hili nisikio la kufa.