Maoni ya wadau wa JamiiForums juu ya kusitishwa kwa Bima ya TOTO AFYA KADI

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
626
938
1678802578582.png

Mnamo Machi 13, 2023 NHIF ilitoa taarifa rasmi kutangaza kusitisha Huduma ya Toto Afya Kadi ili kupisha Maboresho ya huduma hiyo na kuwataka Wazazi kusajili Watoto kama Wategemezi kupitia Vifurushi vingine vya Bima ya Afya au Shule wanazosoma, soma: NHIF yafuta Bima ya Afya kwa watoto "Toto Afya Kadi".

Je, Una maoni gani kwa NHIF na Serikali baada ya tangazo hilo?

Ili kupata nafasi ya kupaza sauti yako katika mjadala huu tafadhali jiunge nasi katika Mjadala wa TwitterSpace ya JamiiForums itakaofanyika tarehe 15/03/2023 kuanzia saa 12:00 jioni mpaka saa 02:00 usiku.

Pia, unaweza kuandika maoni yako kwenye uzi huu ambayo yatasomwa siku ya mjadala.

Karibuni.
===

Mjadala umeanza

BAADHI YA HOJA ZILIZOIBULIWA NA WADAU WA JFSPACE

ANGELA MZIRAY (Meneja Uhusiano NHIF) aanza kwa kutoa ufafanuzi
ANGELA MZIRAY (Meneja Uhusiano NHIF): Kwanza niweke wazi kuwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) haujasitisha Huduma ya Watoto Kilichofanyika ni maboresho ya mfumo ambao ulikuwa unawaingiza Watoto katika huduma kwa hiyari ambao ulikuwa ukifanyika awali Sensa iliyofanyika hivi karibuni ilionesha kuwa Watoto chini ya umri wa miaka 18 wapo Milioni 31, kwa kuwa tunahitaji Watoto wapate Bima za Afya, lakini kwa uzoefu ambao tumeupata baada ya tathmini kwa kipindi cha miaka 7 watu wanaojiunga ni wachache tofauti na takwimu zilizopo.

Kwa miaka saba iliyopita takwimu zinaonesha ni Watoto zaidi ya 210,000 ndio wamejiunga katika huduma ya Bima ya Afya, hivyo imetufanya kuongeza nguvu ya kuwezesha Watoto kuongezeka Hata sasa, Watoto wanaendelea kusajili lakini katika utaratibu tofauti, mfano wanasajiliwa kwa kupitia Wazazi wao wakiingia kama wategemezi wa Wazazi wao au kupitia Shule.

NHIF tuliona utaratibu wa kumuingiza Mtoto mmojamoja unaweza kuchukua muda kwakuwa ni wa hiyari na kuna idadi ndogo ya Watoto ambao wanatakiwa kuandikishwa na kupata huduma Idadi ya Watoto 210,000 sio takwimu nzuri ukilinganisha na idadi ya takwimu halisi ya wanaotakiwa kupata huduma ya Bima ya Afya.

Suala si kiwango kidogo cha malipo ambacho kilikuwa kinalipwa, bali Watoto wanatakiwa kuingia kwa wingi na ndio maana hata katika utaratibu wa kuingia kwa njia ya shule kiwango wanachotakiwa kulipa ni kilekile, lengo ni kuwafikia Watoto Milioni 31.

Watoto wakiingia kama kundi inakuwa rahisi hata kuboresha huduma ambazo watazipata, kuna manufaa mengi ambayo wanaweza kuyapata kupitia utaratibu huu mpya, pia inawajengea Watoto ufahamu kuwa Bima ya Afya ni suala la msingi.

Sisi kama Taasisi ya Serikali lengo la maboresho ya TOTO AFYA KADI ni kupata huduma bora, hakuna kitu kingine chochote ambacho kimejificha nyuma ya maboresho hayo. Hatulazimishi Wazazi kulipia bima, lakini lengo ni kuwafanya Watoto wapate Huduma ya Bima iwe ni kwa kutumia utegemezi wa Mzazi au kupitia Shuleni

MDAUJFSPACES: Hizi tozo zinazotolewa kwenye mambo tofauti tofauti mfano Tsh. 20 au kiasi kingine chochote kidogo kama tunavyochangia vitu vingine, kwanini tusiichangie NHIF ili kuwa na uhakika wa Uchumi wao ambao naamini inawezekana ndio umesababisha tufike huko tulikofika.

MDAUJFSPACES: Wanachofanya #NHIF ni kama dharau kwa Watanzania. Wanapotaka Wazazi wakate vifurushi vya lazima kwani wamewapa pesa za kulipia hiyo huduma? Wanatakiwa kuona aibu kuwa katika kundi la Watoto Milioni 31 wao wamewasajili Watoto 210,000. Wanatakiwa kujiuliza hilo wanapofeli, kwani kuna mtu ambaye hajui umuhimu wa Afya?

MDAUJFSPACES: Nilitegemea kuona Taasisi kubwa kama #NHIF ingekuja na mpango mkakati wa miaka 10 ambao unaweza kuwa na neema nzuri kwa Watanzania na wao pia Hiki kinachofanyika ni kinyume kabisa na maslahi bora ya Mtoto, natambua umuhimu wa bima na kazi yenu lakini sidhani kwa mfumo huu mlioubuni lengo ni kuwakandamiza Watoto ili nyie mfikie Malengo yenu

MDAUJFSPACES: NHIF wanatakiwa kuelewa dhana ya kushirikishana kuliko kufanya maamuzi wao wenyewe Hili suala wanalosema wanaboresha si maboresho bali wanafuta hiyo huduma, kwa kuwa sasa ni kama imekuwa ngumu zaidi kujisajili kutokana na aina ya gharama Tunapoelekea Wazazi watarejea kwenye matumizi ya dawa za kienyeji!

MDAUJFSPACES: Vifurushi vilivyopo ni gharama sana, kama mtu ameshindwa kulipa Tsh. 50,400 anawezaje kulipia Vifurushi vya juu, nadhani Serikali itafakari upya na kuona namna gani ya kutatua changamoto hii.

MDAUJFSPACES: Waziri wa Afya aliwahi kusema watu wengi wanajiunga kwenye Mfuko wa Bima wakiwa tayari wanaumwa, ukweli sio kwamba wanashindwa kujiunga mapema tatizo kubwa ni wao NHIF wameshindwa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kujiunga na Bima.

MDAUJFSPACES: Kimsingi, Huduma za Afya ni Jukumu la Serikali kwa wananchi wake Kusema tu Watoto 200,000 wamesababisha Mfuko kuyumba sio kweli. Ningeshauri tu wangerudi nyuma na kuangalia njia nzuri ya kufanya watu wengi wajiunge na sio kuondoa huduma ili kushawishi watu wanachama zaidi kujiunga.

MDAUJFSPACES: Bima ya Vifurushi ni hatari mno, huduma nyingi hazipo unalipia. Wenye Bima za utumishi wa Serikali ndio wanapata huduma zote, yaani tumeingia mateso makali mno mno. Watu Maskini hawataweza kulipia Bima yote na tutashuhudia mengi mno huko Hospitali.

JFMDAUSPACES: Kama 50,400 ilikuwa ndogo wangeongeza gharama kuliko kuifuta kabisa. Ni lini viongozi wetu watakaa na kutunga Sheria na maamuzi ya kuwanufaisha Wananchi? Licha ya Tozo zote hizi bado wameshindwa kuhudumia Bima za Watoto kweli?

MDAUJFSPACES: Haya Maboresho ni danganya toto. Kwani kuifanya maboresho ni lazima usitishe huduma husika? Wekeni wazi kuwa mmeamua kusitisha huduma hiyo na kuanzisha utaratibu mpya wa Vifurushi. Kutumia Lugha tamu kwenye Habari mbaya ni ubabaishaji.

MDAUJFSPACES: Hivi NHIF mlishindwa nini kutoa taarifa kuwa ifikapo tarehe fulani, Huduma za Toto Afya Kadi zitakoma na mbadala wake utakuwa ni kupitia Bima za Wazazi ili watu wajiandae? Hamuoni ni kama mnawatesa Watu na kuwapa Msongo wa Mawazo? Mungu anatutaka tutii Mamlaka lakini si kwa vitu kama hivi.

MDAUJFSPACES: Hili inapaswa tulikatae kwa vitendo, tuwahukumu hawa watu kwa namna yoyote ile Mtoto ndio kila kitu, bora wafute Bima kwa wote lakini sio Mtoto, tulipumzika matibabu ya Watoto lakini leo mzigo wa matibabu una rudi upya kabisa.

MDAUJFSPACES: Hii ni 'Plan B' ya kulazimisha watu wajiunge na Bima ya Afya na sio jambo baya, kitu ambacho sijakielewa kwanini wamtese Mtoto na mzunguke hivyo? Mnataka kuniambia Mtoto chini ya miaka 5 yupo Shule gani? Hii kadhia ipate majibu haraka tafadhali kabla Watoto wasio na hatia hawajateseka au kupotea.

MDAUJFSPACES: Mimi ni 'Single Mother' nalea mwanangu kwa tabu mno na ana Pumu, wakati mwngine inamjia nikiwa sina ata nauli ya kumpeleka Hospitali, Bima hii ilikua mkombozi kwa mwanangu. Mimi nikiumwa napambana na Antibayotiki. Ona sasa wameitoa.

MDAUJFSPACES: Sasa mbona watasababisha Watoto wengi wakose huduma ya Bima kwa sababu Shule nyingi hazina huduma hiyo na Wazazi waajiriwa tu ndio wanauwezo wa kusajili Watoto kama wategemezi. Je, kwa sisi ambao sio Waajiriwa tutafanya nini kwa Watoto wetu?

MDAUJFSPACES: Warejeshe Toto Afya Kadi kwa mfumo wa zamani, kwani kwa mfumo huu wa maboresho watoto wengi chini ya miaka 5 ambao hawasomi watakosa huduma za Afya kutokana na umasikini wa kipato cha wazazi wao.

MDAUJFSPACES: Hakuna kitu muhimu kama 'Early Childhood Development'. Tusipokuwa makini tutatengeneza kizazi chenye Afya ya kusuasua. Huu ni ukatili mkubwa sana kwa Watoto. Kama mzazi hana Bima ya Afya na Mtoto hajafikia umri wa kuanza shule maana yake hana haki ya kuwa na Bima ya Afya.

MDAUJFSPACES: Kulazimisha wazazi wajiunge ni Ujangili, wengi hawana uwezo ndio maana
huwalipia Watoto wao. Serikali ikemee hii mara moja kwani ni kuwanyima Watoto haki yao ya msingi hasa wale wasiofikia umri wa Shule.

MDAUJFSPACES: Watuambie kwenye hizo takwimu za Shule 280 zenye Wanafunzi wenye Bima ya Toto Afya Kadi ni ngapi za Serikali na ngapi za Binafsi Inaonesha wamefanya Utafiti kwenye Shule za Binafsi ambazo nyingi ziko maeneo ya Mjini tofauti na maeneo ya Vijijini ambapo kuna kundi kubwa

ANGELA MZIRAY (Meneja Uhusiano NHIF) anafafanua tena
ANGELA MZIRAY (NHIF): Wote tunafahamu Matibabu ni gharama na kutokana na Teknolojia, gharama zinazidi kuongezeka Tutafakari kwa pamoja kama Watoto watakuwa wengi wanaoweka hizo Tsh. 50,400 na mfuko unakuwa na uwezo mkubwa wa kuwahudumia.

Hatuwalazimishi wazazi kujiunga kwenye Mfuko wa Bima, nia ya Mfuko ni kwamba tuangalie tunaweza vipi kusaidia Mfuko uweze kutoa huduma Tuangalie ukweli halisi, sasa hivi Wanafunzi wanapata matibabu kwa kadi za Tsh. 50,400 lakini bado wanaojiunga kwa hiyari ni wachache.

Hadi sasa zipo Shule 280 zenye Wanafunzi wanaonufaika kwa utaratibu wa Bima ya hiyari. Sisi tumeweka kiwango kidogo ili waweze kupata Huduma hata kwenye Hospitali za Binafsi

Wote tunafahamu Matibabu ni gharama na kutokana na Teknolojia, gharama zinazidi kuongezeka Tutafakari kwa pamoja kama Watoto watakuwa wengi wanaoweka hizo Tsh. 50,400 na mfuko unakuwa na uwezo mkubwa wa kuwahudumia
 
Serikali imeamua kupita mlango wa nyuma ili watu wakate bima kwa lazima.

Toto Afya ilikuwa kificho cha wengi kutokata.
 
Walisikiliza kwanza maoni ya wananchi....kwamba wanataka nini??? Au ndo walijifungia ofisini na mafile wakaja na hitimisho.
 
Huo ni ubinafsi na hatua mbaya kwa wananchi wa hali ya chini, muogopeni Mungu nyie wahusika wa huu mpango.

Sio watu wote wapo na ajira au mifumo ya kuchangia bima iweje leo hii mlete huo mpango?

Lengo ni kupunguza idadi ya wanachama kama mlivyokuwa mkilalamika kuwa mfuko unaelemewa?
mnakera saana nitarudi usiku kuendeleza hoja.
 
Ingawa bima ya toto afya ilikuwa ni elfu 50 tu ila watu wengi walishindwa kumudu gharama hizo..

sasa walipositisha ili kulazimisha watu wajiunge na bima za familia hili hawatafaulu kwanza watu wengi hawana uwezo wa kumudu mahitaji ya chakula tu leo unamlazimisha ajiunge na bima kwa gharama kubwaa hivyo.

Hawa watendaji wa NHIF wapo kwa ajili ya kuhudumia wananchi au kukusanya mapata kwa serikali.

serikali inatakiwa itenge budget ya kuongezea malipo kusaidia wananchi bima za afya pia maofisa na viongozi wa serikali wakatwe zaidi kwenye bima zao kufidia wananchi wa chini kumudu gharama za bima.
 
NHIF wanasema kuwa watoto michango ya Toto Afya ilizidiwa na matumizi kwa 600% maana watoto wengi walikuwa wagonjwa
 
NHIF wanasema kuwa watoto michango ya Toto Afya ilizidiwa na matumizi kwa 600% maana watoto wengi walikuwa wagonjwa
Yan kati ya watoto million 30 waliosajiliwa na bima ya afya n laki mbili lakin serikali imeshindwa kuwahudumia....hii serikali haiwezi kuwa serious...wakat kuna viongozi wanaenda kutibiwa nje gharama inawezafika ata million 100+..kwa mtu mmoja.
 
Yan kati ya watoto million 30 waliosajiliwa na bima ya afya n laki mbili lakin serikali imeshindwa kuwahudumia....hii serikali haiwezi kuwa serious...wakat kuna viongozi wanaenda kutibiwa nje gharama inawezafika ata million 100+..kwa mtu mmoja.
We deal na mtoto wako usichukue ujumuishi wa wengine
 
Wizara imemshinda Ummy aondolewe apishe watu wenye huruma na ubunifu kwa watanzania.

Kuna watoto ambao wazazi wao wapo nje sasa wazazi hao wanakata bima kwao zitawasaidia nini?

Hiyo NHIF iliyofilisika ndio inaenda kufa kibudu. Kibudu cha kifo cha mende miguu juu

Ndio maana Madelu anawaambia wanajuatu mambo ya usangoma
 
Je, kusajili kupitia shule au vyuoni gharama ni zile zile elfu 50 au kuna mabadiliko. Ndugu zangu kwa hali hii Twafaaaa!!
 
Back
Top Bottom