Freyzem
JF-Expert Member
- Jun 29, 2013
- 10,052
- 24,442
Hatimae leo yamenifika kwakweli!
Nimefika hospital moja ya binafsi baada ya kujisikia sivyo ndivyo huku nikisumbuliwa na maumivu ya kifua na homa ambayo iliniibukia ghafla nikiwa katika shughuli zangu za kila siku.
Cha kushangaza baada ya kuikabidhi bima yangu kwa mtoa huruma alinijulisha kuwa mtandao wa bima inasumbua, pia akaongeza kwa kusema bima nyingi za NHIF zimefungiwa, hivyo kama nahitaji matibabu nitapaswa kuiacha kadi akae nayo kwa siku zisizojulikana (maana kaniambia kwa leo sitoweza kuichukua) ama nilipie huduma nibaki na kadi yangu!
Baada ya maongezi ya muda kiasi na yule mtoa huduma, niliamua kuondoka kwenda hospital nyingine, nako pia walitoa majibu yanayoashiria sitoweza kupata huduma kwa kadi ya NHIF, hivyo kwa kuwa nilikuwa najiona nabanwa zaidi, ilibidi nikubali kupata huduma kwa cash, ambapo nilitumia zaidi ya 100k ambayo kiukweli kama ningekuwa sina akiba nisingeweza kupata Ile huduma!
Nimeshuhudia pia wagonjwa wengine waliofika na bima zao katika hospital zote nilizoenda na wakaishia kujililia, wengine kuondoka na wengine kuhaha kupiga simu kwa ndugu/marafiki kuwakopa ili wapate huduma kwa wakati!
Kiukweli hili jambo linaumizi hasa hawa wananchi wa kawaida, watoto na wale waliokatiwa bima na ndugu zao n.k.
Serikali itoe taarifa kama kweli hizi Bima za Afya za NHIF zimezuiwa, lakini ieleze kama kweli mtandao wa bima unasumbua kiasi kwamba ni lazima mgonjwa aiache bima kwa watoa huduma kwa siku kadhaa hadi tatizo litakapoisha!
Lakini pia kama kuna mchezo unafanywa na hizi hospital ili wagonjwa watibiwe kwa cash angali wanabima, serikali ichukue hatua kali Kwa hizi hospital na vituo vya afya vinavyofanya huu mchezo!
Hili tatizo ambalo wananchi wanaumia chanzo kikuu ni serikali, isikwepe hili.