Status
Not open for further replies.
Nyie UKIWA mkoje lakini, si mmesema rais wenu ni Lowasa sasa inakuwaje mnaanza kumpangia kazi rais wetu magufuli?
 
  • Thanks
Reactions: nao
Mi nahisi muhimu awali ya yote ni katiba tu...labda pengine alitazame kwa jicho kavu! Kesho asubui nahamia ccm.
 
Binafsi cjakuelewa vzr mtoa uzi unataka waziri wa typ gan kama mwakyembe, muhongo hadi january unawaona bado wanaweza kama muhongo em tengeneza cabinet ukiassume kama lowassa na cdm angepita.......
 
Autangazie UMMA wa watanzania kuwa hakushinda kihalali bali Lubuva na Kikwete walimbeba kibabe na kumtangaza mshindi.

Kwa kuwa umetumwa hapa ama umejituma na pengine utapeleka mrejesho, mwambie wazi miongoni mwa Marais walioingia records Za kukosa uhalali wa kuongoza Tanzania na wananchi wake ni yeye POMBE!

Mwambie, taifa hili linaumwa, lina huzuni kubwa na kuomboleza kwaajili ya udhalimu wa kutisha uliofanywa na Tume ya uchaguzi kwa maagizo ya Kikwete na ccm yao.

Mwambie, usione huu ukimya ukadhani sisi watanzania ni mapompompo na mazuzu!

Mwambie, tunakwenda madhabahuni mwa Mungu kumlilia ili kama huyu Mungu tunaemwabudu Yupo, Hakika haitochukua Muda sote tutakuwa mashuhuda!

Mwambie, tunaenda kumuuliza Mungu hivi yeye Ndio Mkuu au Lubuva ama Kikwete hata waweke mteule wao?

hapa inabidi nimtume mwingine akamwambie
 
Hapo kwa January Makamba sikubaliani na wewe,kutokana na yeye pamoja na Waziri mwenzeka katika wizara ya teknolojia na mawasiliano kushindwa kuithibiti mitandao ya simu ambayo mpaka sasa hupanga gharama za mawasiliano itakavyo yenyewe na hatujawahi kumsikia akikemea wala kuichukulia hatua zozote mitandao hii. mfano baada ya kupunguza mb hadi kufikia mb8 na kuona hakuna anayewagusa wamepunguza hadi kufikia mb 1 kwa bei ileile na kwenye wizara bado wapo hawahawa na wala hawasemi chochote, Leo hii unampa sifa kuwa ana uwezo wa kuongoza, labda katikati ya vipofu lkn si kwa watu wenye macho yanayoona. hivyo hata huo utendaji wake hakujidhihirisha dhahiri kwenye masuala ya kiutawala, labda kama ni kwenye mikakati ya kampeni za Chama chake
 
Mkuu ungesona mpaka mwisho, nimesema makamba kwa sasa awekwe kando kutokana na kundi lililo nyuma yake, anawaza madaraka makubwa mnoo

Tusubiri baraza lake litakuwaje tusiwe na mchecheto,

Tatizo sio watu tatizo wanafanya kazi na nani?
 
huna akili utampangiaje rais utaratibu wake wewe nani usilete chuki binafsi



mmm yamekuwa hayoi tena mbona alikuja kutuomba urais....hahaha saizi zile stori za kusimamishwa na wananchi njiani zimekwisha etu mkae na manguo yenu ya kijani mtapigwa
 
Imekuwa kawaida kila serikali ikiingia madarakani au wizara kupata waziri mpya, lazima wanunue magari mapya ya mawaziri wakati yaliyopo ni mazima.Magufuli komesha tabia hii kuepeuka matumizi yasiyo ya lazima. Waziri asiyetaka kutumia gari la zamani ampishe mwingine mwenye uzalendo. Kuna tetesi mawaziri huogopa kutumia magari waliyoyakuta kwa imani za kishirikina. Kwamba waliotangulia walienda nayo Bagamoyo nk.Tabia hii ife kabisa. Tena Magufuli aweke "wanted" kabisa hakuna kununua gari mpya ndani ya miaka miwili.

Magari ya waliokuwa mawaziri yarudishwe yakiwa katika ubora wake, likirudishwa gari bovu waziri husika akatwe mafao yake litengenezwe!
 
Binafsi cjakuelewa vzr mtoa uzi unataka waziri wa typ gan kama mwakyembe, muhongo hadi january unawaona bado wanaweza kama muhongo em tengeneza cabinet ukiassume kama lowassa na cdm angepita.......

mkuu soma aya ya mwisho, nimeeleza vemaa
 
Mkuu akisanye Pia Kodi sana sana tuu haswa kwa wafanyabiashara wakubwa na wale waliokuwa wanakwepa Kodi hili ndo Liwe La Kwanza Kabisa

Kukusanya Kodi peke take haitoshi. Effective use of resources required and is of Paramount importance
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom