Status
Not open for further replies.
zaidi awe raisi wa Tanzania,awasikilize watanzania na sio kuwasikiliza ccm.
 
No 1,3,4 na 8 ni watu makini sana na wanahitaji sana ....hivyo nasikitika kukutangazia kuwa maombi yako katika namba tajwa hayatozingatiwa kabisa! Hao ni wachapakazi wazuri na wana hitajika...
 
mkuu kuna kasoro naiona hapa kuna rais na makamu wake ambaye huyu ataitwa msaidizi wa rais ,pale nairobi wana mfumo mzuri rais huambatana na makamu wake katika shughuli za kikazi mfano kukagua ,kutoa maelekezo kweli inapendeza hapa kwetu hali ipo tofauti hili mkuu tuliweke sawa

Kwa hiyo Mama Samia mara hii amegeuka samaki wa Kipare,unakula ugali kwa kuangalia picha!
 
Mimi ningependa aanze na kurudisha nyumba zote za serikali zilizofisidiwa wakati wa utawala wa Nkapa na kwa kuanzaia aanze yeye mwenyewe kurudisha pamoja na zile inazosemakana walipewa jamaa na marafiki zake. Hapo ndipo tutaona kweli anachukia ufisadi. Baada ya hapo afungue haraka mahakama ya mafisadi kama alivyoahidi na mtu wa kwanza kumshitaki awe Lowassa kwasababu wamemsema sana sana majukwaani kabla na baada ya kugombea urais. Umefika wakati sasa apelekwe mahakamani ili mahakama itamke kama ni fisadi au laa
 
1. Mheshimiwa Rais kuna vijana wengi ambao naamini katika utendaji wao lkn siamini kundi lake, na mmoja wao ni Januari Makamba. Huyu binafsi namwamini kiutendaji, ubunifu lakini kinachomsumbua ni kutaka madaraka makubwa, kundi lake lililo nyuma yake, Huyu badala ya kuchapa kazi atakuwa anawaza urais baada yako kustaafu. Kwa mtazamo wangu ungemweka kando kwa mda baada ya miaka miwili ndo uumpe majukumu.

2. Kwa kukusaidia mh Rais ni vema ukachagua mawaziri wachache ambao wengi wao hawakuwa mawaziri, sio viongozi katika chama, vijana, wenye elimu isiyo na shaka. Hawa ndio wataileta tanzania mpya ya HAPA KAZI TU.

Mh Rais ukikosea kwenye baraza la mawaziri basi jua umeuwa nchi, na hapo tutadhibitisha kuwa hakuna cha Magufuli 4 change itakuwa ccm ni ile ile.

Asantee.

nimefurahi umekubali magufuli ni Rais... dawa imeingia vizuri ..safi sana ...

pili.... Prof Anna tIbaijuka anatofauti gani na mzee wa richmond uliyekuwa ukimpigia chapuo....

nina imani baraza la Dr. Magufuli litakuwa dogo na watu wa kazi tu...
 
Pamoja na kwamba sina imani na chama chako, ila naomba unishawishi wewe binafsi katika serikali yako.
Kama ulivyojinaji kuwa serikali yako, yani Tanzania ya Magufuli itakuwa KAZI TU, basi naomba udhihirishe hivyo katika baraza lako la mawaziri.

Kabla hata sijataka kujua waziri mkuu ambaye ataendana na sura ya kauli mbiu yako, lakini nataka usituletee watu hawa ambao walikuwa mzigo kwa taifa na waliolifikisha nchi hapa ilipo chini ya aliyekutangulia pamoja na waziri mkuu wake.

1. Sopteter Muhongo.
Huyu pamoja na kwamba tunaambiwa hakuhusika moja kwa moja kwenye kashfa xa escrow lakini alikuwa kinara wa utetezi katika sakata hili. Pia ni miongoni mwa waziri wenye elimu kubwa lkn hakuwa na mkakati bunifu wa kutatua tatizo la umeme nchini zaidi ya kuiacha tanesco kwenye deni kubwa. Pia ni miongoni mwa viongozi ambao hawathamini wawekezaji wa ndani, anaamini nchi itajengwa na wazungu au wachina.

2. Lazaro Nyalandu.
Huyu ni miongoni mwa mawaziri ambao tumeshuhudia tembo wakiuliwa kwa wingi, na twiga wetu wakisafirishwa kwenda nje, hafai katika serikali yako, kwani atafanya kazi ya mazoeaa ya serikali ya awamu ya 4.

3. Mwigulu Nchemba.
Pamoja na kwamba hakukaa kwenye wizara ya fedha kwa mda mrefu, lkn ni miongoni mwa vijana ambao hawana adabu katika taifa hili. Ni mmoja wa wanasiasa wachanga ambao hajali matamshi yake mbele ya umma, haangalii baada ya hapa athari zake zitanipeleka wapi, sio mstaarabu.

4. Willium Lukuvi.
Huyu kwa mwendo wa kasi inayohitajika nchini hatufai, utendaji wake hauto tofautiana na wa awamu ya 4, hana jipya ndani ya serikali yako.

5. Shukuru Kawambwa
Huyu ni moja ya mawaziri walioshusha thamani ya elimu yetu. Sio mbunifu. Fedha za fidia za rada mpaka leo hatujui matumizi yake yalienda wapi, hatufai kabisaa.

6.Hawa Ghasia.
Huyu mama bado uchama umemkaa kichwani kuliko maslai ya taifa. Hayupo active katika utendaji wake.

7. Jumanne Maghembe.
Huyu ni moja ya mawaziri ambao ndio chanzo cha huduma mbovu za elimu na maji. Elimu yake ni kubwa lkn haina msaada kwetu.

8.Harrison Mwakyembe.
Huyu kinachompa sifa ni lile sakata la richmond ambalo tunamwona kama shujaa. Lakini kiukweli hafai hata kuwa mwenyekiti wa kijiji. Sijaona mafanikio yake katika wizara alizozisimamia, ni mzigo ana asili ya mtandao ambao ni chanzo cha utendaji mbovu nchini. Ni mafya wa kisiasa

9. Magreth Sitta
Mama huyu tangu zama ni outdated, haendani na kasi ya dunia, yupo nyuma na mda, hafai katika serikali yako.

10. Sofia Simba
Hana tofauti na Mama sitta, tena huyu uchama na mtandao wa uongozi umemjaa kichwani, hafai katika serikali yako.

11. Andwer Chenge
Najua huyu unamfahamu vema

12. Anna Tibaijuka
Najua unamfahamu vizur

13. Willium Ngeleja
Najua wamfahamu vzr

NB.
1. Mheshimiwa Rais kuna vijana wengi ambao naamini katika utendaji wao lkn siamini kundi lake, na mmoja wao ni Januari Makamba. Huyu binafsi namwamini kiutendaji, ubunifu lakini kinachomsumbua ni kutaka madaraka makubwa, kundi lake lililo nyuma yake, Huyu badala ya kuchapa kazi atakuwa anawaza urais baada yako kustaafu. Kwa mtazamo wangu ungemweka kando kwa mda baada ya miaka miwili ndo uumpe majukumu.

2. Kwa kukusaidia mh Rais ni vema ukachagua mawaziri wachache ambao wengi wao hawakuwa mawaziri, sio viongozi katika chama, vijana, wenye elimu isiyo na shaka. Hawa ndio wataileta tanzania mpya ya HAPA KAZI TU.

Mh Rais ukikosea kwenye baraza la mawaziri basi jua umeuwa nchi, na hapo tutadhibitisha kuwa hakuna cha Magufuli 4 change itakuwa ccm ni ile ile.

Asantee.

Kuna mkono wa J.Makamba katika post hii.J. Mkamba hufai popote pale labda kitengo cha propaganda cha CCM. Tatizo ni Uwaziri Mkuu hapa
 
nimefurahi umekubali magufuli ni Rais... dawa imeingia vizuri ..safi sana ...

pili.... Prof Anna tIbaijuka anatofauti gani na mzee wa richmond uliyekuwa ukimpigia chapuo....

nina imani baraza la Dr. Magufuli litakuwa dogo na watu wa kazi tu...

Tunajenga nchi, mabadiliko yatakuja soon
 
Dr.Magufuli tunahitaji watu ya caliber wakina Nchemba katika baraza la mawaziri... huyu jamaa anafaa hata kuwa PM
 
Kuna mkono wa J.Makamba katika post hii.J. Mkamba hufai popote pale labda kitengo cha propaganda cha CCM. Tatizo ni Uwaziri Mkuu hapa

Ni mesema makamba anapaswa kuwekwa nje miaka mi 2 kwani kwa sasa sina imani naye kutokana na kundi lake, pamoja na kuusaka urais baada ya kuwatumikia wananchi
 
Muhongo, Mwigulu, mwakyembe wanafaa sana kuwepo hao wengine hawafai wote

Mwakyembe hafai maana ndiye alinunua mabehewa mabovu akala pesa za ukarabati wa reli pia ATC na kule bandarini napo alifanya maovu mengi , lakini kwa kawaida Mwakyembe huwa ni rafiki mkubwa wa Magufuli hivyo huenda Magufuli akafumba macho na kuamua kumpa Uwaziri wa Uchunguzi tena.
 
Muhongo kichwa aliingizwa chaka nA wabongo, huyu arudi tena kwenye nishati alisimamia vema tanesco

Tatizo la Muhongo sio mwanasiasa, ila wakati wake alipiga kazi ya hatari, tena mie nitaenda mbali zaidi na kusema kama inawezekana na Masele arudi kuwa katibu mkuu wizara ya nishati.
 
Kuna harufu ya Mkono wa Makamba kuutaka U-PM kwenye post hii.Ila dogo yule hana jipya zaidi ya malingo
 
Mwakyembe hafai maana ndiye alinunua mabehewa mabovu akala pesa za ukarabati wa reli pia ATC na kule bandarini napo alifanya maovu mengi , lakini kwa kawaida Mwakyembe huwa ni rafiki mkubwa wa Magufuli hivyo huenda Magufuli akafumba macho na kuamua kumpa Uwaziri wa Uchunguzi tena.
Maovu yapi alifanya?
 
acha kujiangaisha unapigia mbuzi Gitaa tu-Muombe tu Mungu Miaka 10 iishe mapema tuangalie chama kingine.Aliweza hivyo Nyerere tu.

Kweli watu wengine wanasikitisha katika mtazamo yao. Tunaambiwa kwa miaka 54 ya Uhuru hakuna kilichofanyika ,! Ila Nyerere Aliweza! Nyerere katawala miaka 24 hii inaesabiwa wapi?
 
Ameshaanza na lakudhurura maofisini
Mwenzake naye alianza na mkwara huo huo wa kuzunguka wizara zote, masokoni na kuitisha vikao au mwenyewe kama alivyoita semina ya kagharama kubwa kule Ngurdoto eti ikiitwa semina elekezi tukadhani mambo yangekuwa mazuri kumbe ilikuwa geresha tu. Muda si mrefu mambo yakaanza kuwa hovyo na yeye akageuza upepo wa ziara zake akaanza kuzunguka nje kila siku hasa hasa Marekani. Kwanza alianza na ziara alizoziita za kujitambulisha. Sasa sijui alikuwa anajitambulisha kama balozi au Rais. Tena wakati huo alikuwa ametoka kwenye kikao cha AU ambako kwa mara ya kwanza alihutubia kwa kiswahili. Sasa cha ajabu baada ya kurudi akaanza kwenda ena kwa wale wale alio kutana nao kwenye mkutano wa AU eti kujitambulisha. Baada ya kuzunguka katika nchi mbali mbali za Afrika akijitambulisha akaanza sasa kwenda huko wanakoita ng'ambo. Baada ya hapo ikawa safari moja huanzisha nyingine. Mara leo yuko Marekani, kesho Uingereza nk mpaka sasa sijui ametiza safari ngapi mpaka anaondoka. Lets give Magufuli a benefit of doubt!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom