Maoni kwa Wizara mbalimbali yaliyotolewa na Wadau wa Twitter Space ya Jamiiforums Januari 26, 2023

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
626
938
Awami.png

Jamiiforums kupitia ukurasa wake wa Twitter imeandaa space ambayo itatoa fursa ya dakika 2 kwa Wananchi kutoa maoni au (kupaza sauti yao) kuhusu suala lolote linalowagusa katika Wizara yoyote hapa nchini.

Mjadala huu unatarajiwa kuongozwa na Mwandishi wa Habari Sammy Awami

Ili kupata nafasi hii tafadhali jiunge nasi katika Mjadala kupitia TwitterSpace ya JamiiForums, Alhamisi hii, Januari 26, 2023, kuanzia Saa 12 Jioni hadi 2 Usiku.

Aidha, unaweza kuandika maoni yako hapa na tutayasoma kwenye twitter spaces siku ya mjadala.

Kujiunga na mjadala huu tafadhali gusa link hii hapa chini:


Updates
- Mjadala umeanza saa 12:00 Jioni

BAADHI YA MAONI YANAYOTOLEWA NA WADAU MBALIMBALI
MDAU wa JFSPACES: Wizara ya Teknolojia na Mawasiliano na Wizara ya Mambo ya Ndani Kuna utapeli mkubwa unaoendelea katika Mitandao ya Kijamii. Watu wanatapeliwa, ukiripoti Polisi hakuna hatua yoyote inayochukuliwa.

Na hata kama una Ushahidi wa kusaidia Watumiaji kukamatwa hawautaki, jambo ambalo linaturudisha nyuma sisi Vijana tulioamua kutumia platform hii kama sehemu ya kupambana na Umasikini.

MDAU wa JFSPACES: Wizara ya Elimu ibadili Silabasi kuendana na hali ya Maisha ya sasa. Watoto wafundishwe Vitu ambavyo vitakuja kuwasaidia hata kama Serikali itakuwa na uhaba wa Ajira basi Elimu waliyoipata iwasaidie kujiajiri wenyewe.

Watoto wanapoteza Miaka mingi Shuleni kusomea vitu ambavyo wakimaliza Elimu haviwasaidii chochote.

MDAU JFSPACES: Wizara ya Ulinzi na Usalama. Mahabusu zenu ni chafu mno. Zinatia huruma na kukatisha tamaa. Ukipelekwa huko lazima utoke na Magojwa.

MDAU JFSPACES: Wizara ya Habari na Mawasiliano; hakika gharama za vifurushi vya Intaneti vinatuelemea kwa tunaotumia Mtandao Kujisomea na kufanya Biashara. Punguzeni hizo gharama tafadhali.

MDAU JFSPACES: Jambo langu kubwa ni utaratibu wa Usahili unaowalazimu Waombaji kwenda Dodoma au Dar es Salaam, nadhani wangeharakisha mchakato wa kuruhusu Usahili kufanyika mahali popote.

MDAU #JFSPACES: Mimi nitoe langu kupitia Wizara ya Nishati. Waweke mipango mkakati ili kupunguza foleni kutoa huduma kwa uharaka kuwapa watu 'Control Number' ili kupata huduma kwa uharaka.

Jingine kwa upande wa maji wajitahidi kupunguza vikwazo. DAWASCO wanakwambia hawawezi kukuletea maji laiti ikiwa zaidi ya mita 50, sasa hapo hatumpi mteja haki. Wao walitakiwa wafanye 'tattooing' ni gharama gani mtu anatakiwa kulipa ila si kumfanya mteja atoe gharama mara mbili.

MDAU SPACES: Mapendekezo kwenye Wizara ya Elimu, sioni kama Serikali ina nia ya kubadili Elimu ya Tanzania Wanafunzi wanasoma masomo mengi yasiyo na tija, wanasoma Binadamu wa kwanza alikuwa Nyani vitu ambayo havina tija. Kuna ulazima gani mtu kusoma masomo 9?

MDAU SPACES: Maoni yangu yaende Wizara ya Elimu na Serikali Kuu, ningependa kupata majibu Mwalimu anachukuliwaje Tanzania hii? Hii ni kada ambayo inachukuliwa kinyonge wakati sisi ndio tumepewa jukumu kubwa la kuiandaa Tanzania ya Kesho.

Mdau JFSPACES: Wizara ya Nishati: Kuunganishiwa Umeme bado kuna changamoto ya Rushwa. Saveya hafiki eneo lenye Nyumba inayopaswa kuunganishiwa Umeme (site) mpk Rushwa itolewe Wanadai kiasi cha Fedha kama (rushwa) kati ya sh laki moja mpk mbili.

Mdau JFSPACES: Kwenye Bima ya Afya, ifikirie Watu ambao hawajaoa au kuolewa kuwa na uwezo wa kuweka wategemezi wao Kama ndugu zao wa Damu au Watu wowote itakavyoonekana inafaa. Unakuwa na Bima kubwa lakini huna Mume/Mke lakini una Wadogo wanakuangalia wewe nafasi zinapotea.

Mdau JFSPACES: Wizara ya Fedha ipunguze riba kwenye Benki za Biashara Kwa sababu hali iliyopo sio ya kumwinua Mwananchi awe Mfanyabiashara mkubwa zaidi ya kufilisika Pia Serikali iweke angalau hata muda wa Miaka miwili Kwa mkopaji kuanza kulejesha mkopo wake.

MDAU SPACES: Salamu zangu kwa Wizara ya Afya, suala la Bima, kuna Wagonjwa wanaenda Hospitali kupata huduma lakini wakienda Duka la Dawa kwenye Vituo wanakosa Dawa na wakienda Duka la Dawa la nje ya Hospitali, Dawa zipo Hivyo tuanze kuboresha Bima iliyopo kwanza.

MDAU SPACES: Salamu zangu kwa Serikali, Sisi Diaspora tulioko nje tunataka kuwa sehemu ya ujenzi wa Nchi, lakini hatupati hiyo nafasi Ni kama Serikali inatuogopa, nataka kujua nini kinakwamisha mchakato wa Uraia Pacha?

MDAU JFSPACES: Ianzishwe Wizara maalumu ya Diaspora na itambue Watanzania wote popote walipo Pia, isaidie ambao wanataka kuwekeza Nyumbani kwa kuwafanyia michakato ya kumiliki Ardhi na kulindiwa vitega Uchumi vyao. Hapa Serikali itapata Remittances na Kodi kwa miradi.

MDAU JFSPACES: Kwa upande wangu mimi, Serikali inatakiwa kuwapatia Vyeti vya Kuzaliwa Wananchi kwa urahisi Ucheleweshwaji wa Vyeti hivi unaleta changamoto muda ambao anahitaji na wekeni kiwango cha thamani kwa urahisi.

MDAU JFSPACES: Wabungwe wetu kila baada ya miaka mitano wanalipwa maslahi yao yote. Wale wanaolipwa laki tatu wanazungushwa, wengine wanakufa wakiwa hawajapata stahiki zao Kwa nini hao wanaolipwa kidogo wasilipwe haki zao mapema kama inavyokuwa kwa Wabunge

MDAU JFSPACES: Salamu zangu zinaenda Wizara ya Mazingira, suala la utoaji leseni za sehemu za Starehe likoje? Kuna kelele kubwa za muziki kwenye Bar zinazofunguliwa katika maeneo ya makazi ya watu.

Pili, kwenye Wizara ya Uchukuzi, Suala la Usafiri kwenye Daladala za Mbagala limekuwa kero, ikifika Usiku zinabadili nauli kutoka nauli ya kawaida na kuwa 1000 bila kufuata taratibu.

MDAU JFSPACES: Nashauri mafunzo kama ya kujiokoa kwenye majanga mfano yale ya moto yaanze kutolewa kuanzia watoto wakiwa na umri mdogo, kusubiri kila majanga yanapotokea kuwategemea Zimamoto inakuwa si sawa.

MDAU JFSPACES: Serikali ingilie kati kuhusu ugumu wa maisha kwa kutoa ajira kwa vijana wengi waliomaliza Vyuo katika fani mbalimbali Kwani hao ndio nguzo za kukwamua maisha ya familia zao.

MDAU JFSPACES: Nawapongeza Wizara ya Afya, wanajitahidi kufanya kazi nzuri, lakini kitu kinachoniuma ni maslahi yao kuwa duni Kama tunataka kufanya mapinduzi na mageuzi ni vizuri kuangalia nguvu kazi ambayo inapatikana kwa Watu waliopo kwenye Sekta kama hizo.

MDAU JFSPACES: Wizara ya Wanawake, Jinsia na Makundi Maalum, kuna utaratibu wa ovyo wa uanzishaji Nyumba na Taasisi za Imani.

Siku za hivi karibuni Tanzania imekuwa na idadi kubwa ya Manabii na Wahubiri, wanawalisha maneno au imani ambayo inawaathiri, tunatengeneza Taifa ambalo imani inaweza kuwapeleka Watu kuwa masikini zaidi.

MDAU JFSPACES: TAMISEMI kuna changamoto kubwa, ukiangalia Ripoti za CAG bado ubora wa kile kinachotakiwa kifanyike upo chini Muhimu wawe wanafuatilia matumizi ya Fedha, kunatakiwa kuwe na wito wa Uwajibikaji. Tunapoteza Fedha nyingi kutokana na kukosekana kwa Uwajibikaji.

MDAU JFSPACES: Kuna hospitali zinachagua Bima ya Afya, hii inasababisha Watanzania wengi kutopenda kuingia kwenye Bima ya Afya kutokana na aina ya huduma ambazo zinapatikana hospitalini.

MDAU JFSPACES: Kuna hospitali zinachagua Bima ya Afya, hii inasababisha Watanzania wengi kutopenda kuingia kwenye Bima ya Afya kutokana na aina ya huduma ambazo zinapatikana hospitalini.

MDAU JFSPACES: Ukimnyima Mtu Elimu umemfanya kuwa Masikini kwa kuwa unakuwa umemnyima Maarifa na Ufahamu Wizara ya Elimu inatakiwa kutengeneza Mifumo ya kuwakomboa Watu wake, Dunia inabadilika, tusiwe na vijana wanaohitimu masomo lakini hawawezi hata kuandika barua ya kazi.

MDAU JFSPACES: Vijana wengi wa Shuleni hawatengenezewi Mazingira ya kuwa Watawala bora Mifumo ni ileile lakini wanaohusika kuisimamia ndio ambao wameshindwa kubadilika kwenda na muda. Hiyo inasababisha vijana wengi kukosa dira wanapokuwa sehemu za maamuzi.

MDAU JFSPACES: Natamani Wizara ya Elimu ingepiga marufuku Shule za Bweni kwa kuwa Shule nyingi hazina uangalizi mzuri Kuna watoto wengi wanaharibika kitabia hasa kuanzia ngazi ya Shule za Msingi licha ya kuwa Viongozi wa Shule wanasema wanaweka uangalizi
 
Maoni yangu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Wizara ya Nishati

Mimi nashauri tungeanzisha wizara ya mafuta na gesi (Ministry of Oil and Gas). Wizara ya nishati igawanywe mara mbili kuwa wizara ya mafuta na gesi (Ministry of Oil and Gas) na wizara ya nishati (Ministry of Energy).

Wizara ya nishati (Ministry of Energy) ishughurikie usambazaji na uzalishaji wa umeme kutoka vyanzo mbalimbali mfano maji, gesi, joto ardhi, upepo, jua, mawimbi ya bahari n.k. TANESCO iwe chini ya Wizara ya nishati. Ateuliwe waziri wa nishati muda wote awaze umeme tu ili kuharakisha na kuboresha uzalishaji na usambazaji wa umeme Tanzania.

Wizara ya mafuta na gesi ishughurikie mambo ya utafutaji wa mafuta na gesi (exploration), uzalishaji wa mafuta na gesi (production), usafishaji wa mafuta na gesi (refining), usambazaji wa mafuta na gesi (distribution), uuzaji wa mafuta na gesi (marketing), uingizaji mafuta kutoka nje ya nchi (import), na uuzaji wa gesi nje ya nchi (export), pamoja na conservation of petroleum, natural gas, petroleum products, and liquefied natural gas Tanzania. TPDC, PURA na EWURA ziwe chini ya wizara ya mafuta na gesi (Ministry of Oil and Gesi). Ateuliwe waziri wa mafuta na gesi aharakishe na kuiboresha sekta ya mafuta na gesi nchini. Waziri huyo akiwa ofisini kwake awaze mambo ya gesi na mafuta tu, hakika tutapata matokeo kama ya Qatar.

Maeneo muhimu ambayo ningependa hii wizara ihusike nayo ni haya yafuatayo.

1. Utafutaji (Exploration) wa rasilimali za mafuta na gesi asilia (methane na helium)

2. Uzalishaji, usambazaji, na uuzaji wa rasilimali za mafuta na gesi aina zote.

3. Viwanda vya kusafisha mafuta, vilainishi vya mashine, na viwanda vya kuchakata gesi asilia, gesi za vimiminika (LNG na LPG).

4. Matumizi ya gesi asilia kama malighafi ili kupata bidhaa zenye thamani kama mbolea, kemikali, plastics, mafuta n.k; Matumizi ya gesi asilia majumbani, viwandani, kwenye magari nk.

5. Mipango, uendelezaji na udhibiti na usaidizi kwa sekta zote zinazoshughulikiwa na Wizara ya mafuta na gesi (Ministry of Oil and Gas).

6. Mipango, maendeleo na udhibiti wa huduma za mafuta na gesi.

7. Usimamizi wa Sheria mbalimbali zinazohusu Petroli na Gesi Asilia

Ninahisi ikiwa hivi tutaipunguzia wizara ya nishati mzigo, na tutaongeza ufanisi na ukuaji katika sekta ya mafuta na gesi Tanzania.
 
Kero yangu ni kwa Wizara inayohusika na maji hasa mkoa wa Dar es Salaam.

Wizara na serikali ilidai imezindua visima vya maji na kudai kwamba kero imeisha lakini uhalisia sio kabisa.

Bado maeneo mengi ya Dar hatupati maji inavyotakiwa.

Ni kawaida sana kukosa maji hata siku nne au zaidi.

Wakazi wa Ubungo, Kimara tunawaomba sana mtutatulie adha hii kwa vitendo.
 
Tupo tunasubiri Mjadala uanze. Fanyeni kizungu basi ianze saa 12 kweli. Naomba mnifikishie ujumbe wangu
 
Wizara ya Elimu, tuendane na Mabadiliko ya dunia halisi. Muda wa kufanya mapinduzi katika Mitaala yetu ni sasa. Tubadilike!
 
Wizara ya nishati.

Kuunganishiwa umeme bado kuna changamoto ya rushwa. Saveya hafiki eneo lenye nyumba inayopaswa kuunganishiwa umeme (site) mpk rushwa itolewe. Wanadai kiasi cha fedha kama (rushwa) kati ya sh laki moja mpk mbili.
 
Wizara ya Fedha upunguze riba kwenye mabenki ya biashara Kwa sababu hali iliyopo sio ya kumwinua mwananchi awe mfanyabiashara mkubwa zaidi ya kufilisika. Pia serikali iweke anagalau hata muda wa Miaka miwili Kwa mkopaji kuanza kulejesha mkopo wake.Asanteni sana
 
Maoni yangu kwenye Wizara ya Afya kuhusu Bima ya Afya, wizara ifikirie watu ambao hawajaoa au kuolewa kuwa na uwezo wa kuweka 'wategemezi' wao mfano ndugu zao wa damu au watu wowote itakavyoonekana inafaa.

Unakuta una bima yenye uwezo wa wewe kuongeza wategemezi lakini unalazimishwa wawe watoto au mwenza wako, maisha yetu Watanzania tunayajua vipi kwa ambao hawana wenza/ watoto lakini wana ndugu wa damu (kaka/dada) wanaomtegemea yeye? Nafasi hiyo ipotee wakati angaweza kuitumia vilivyo ikawa msaada mkubwa kwake?!
 
Ianzishwe Wizara maalumu ya Diaspora na itambue Watanzania wote popote walipo na wanafanya nini.Pia isaidie Watanzania ambao wanataka kuwekeza nyumbani kwa kuwafanyia michakato ya kumiliki ardhi na kulindiwa vitega uchumi vyao. Hapa serikali itapata Remittances na Kodi kwa miradi itakayo anzishwa.
 
Maoni kwa Wizara ya Habari, watu wana uhuru wa kujieleza na kutoa maoni yao kikatiba, lakini pia serikali imekuwa msemaji mzuri wa kuwa watu wako huru kutoa maoni yao, na kukosoa pale wanapoona hapaendi sawa lakini mtu akifanya hivyo tunasikia kapoteza kazi, na wengine kushikiliawa na Polisi, Wizara isimamie haki hii ya kikatiba na waache watu watoe maoni pamoja na kukosoa bila kutisha watu
 
unazungumzia wizara wau wazara .
tunacho taka sasa waziri yoyote asiwe mbunge ni kutoka taasisi za wizara na sio mwanasiasa
 
Hoja yangu ni Wizara ya Mambo ya ndani.

Je hoja ya ukomo wa upelelezi imefikia wapi?

Wananchi tunaenda vituo vya polisi kulalamika mambo mbali mbali ambayo yananakiliwa (recored) lakini unakaa miezi zaidi ya minne hakuna mrejesho.. zaidi ya kuambiwa bado endelea kusubiri?
 
Nalia na Wizara ya kazi. Aisee mmezidi na hivi vibali vya kazi kwa wageni. Hamna uchungu kusema watanzania wajiajiri huku vibali vinatolewa kiholela. Nafasi ambazo zilikuwa zimeshikwa na wazawa tangia 2021 zimerudi kuwa za wageni. Hizo succession plans huwa za kazi gani?
 
Wizara ya Elimu mko dunia gani?? Wanafunzi wanakaririshwa tu hawapati maarifa na life skills na mnajifanya eti ni Competence Based Curriculum. Tunamaliza mwezi wa kwanza vitabu vya kiada bado....halafu lazima Wizara mregulate hizi international schools. Tunatamani na sisi watoto wetu wasome Cambridge system waweze kucompete globally siyo nationally. Mtoto hata wa Form 6 hawezi kujielezea vizuri kwa kiingereza na ana Division 1 ya one digit! Tembeleeni Zimbabwe mjifunze. Elimu ni basic need na iwe elimu bora.
 
Back
Top Bottom