MJADALA: Je, kuna uwazi wa hatua zinazochukuliwa dhidi ya Wabadhirifu wa mali za umma wanaobainishwa katika Ripoti za CAG?

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
626
938
4 (2).jpg

Tarehe 29 Machi, 2023 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alipokea Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na TAKUKURU kwa mwaka 2021/2022. Ripoti hiyo imeibua ubadhirifu katika sekta mbalimbali za umma na kuibua mijadala miongoni mwa wananchi.

Je, ungependa kufahamu ni hatua gani huchukuliwa dhidi ya wabadhirifu baada ya kusomwa kwa Ripoti ya CAG? Unadhani hatua hizo zinatosha kumaliza ubadhirifu wa Mali za Umma?

Kwa haya na mengine mengi ungana nasi katika Mjadala Maalum na Wadau leo Alhamisi, Aprili 20, 2023, kuanzia Saa 11 jioni hadi saa 2 usiku kupitia Twitter Spaces.

Mjadala umeanza. Karibuni!

MDAU #JFSPACES:
Huu ubadhirifu haujaanza leo, ni Miaka sasa. Mijadala imekuwa hii hii, hazichukuliwi hatua za kukomesha, kiufupi wanaoiba walishaona hakuna wa kuwafanya kitu maana huu wizi ni wa kimfumo haibi mtu mmoja ni 'chain' ya vigogo, sasa hawachukui hatua maana wataumbuana. Kiufupi nchi inaliwa.

MDAU #JFSPACES: Kwa upande wangu lawama zangu zote nazielekeza kwa TAKUKURU, wao ndo walaumiwe kwa sababu CAG akitoa ripoti yake wao ndio ingetakuwa wawe wa kwanza kuwakamata wahusika wa kashfa hizo na kuwapeleka mahakamani, na kama hawana uwezo huo wa kisheria ningeomba Bunge litunge Sheria ya kuwawezesha kufanya hivyo

MDAU #JFSPACES: Wabadhirifu watachukuliwa hatua? Kwanza walitakiwa waone aibu wenyewe kisha wajiuzulu, halafu Serikali iwapeleke Mahakamani. Watu wenyewe hata aibu hawana na wametia hasara nchi

MDAU #JFSPACES: Wabadhirifu Washitakiwe na kuhukumiwa kifungo zaidi ya Miaka 30, wafilisiwe Mali na account zao kufungwa na fedha zote zirejeshwe Serikalini. Wavuliwe Vyeo na nyadhifa zao, wanyang'anywe hati za kusafiria

MDAU #JFSPACES: Uwazi na sio uwazi tu, wabadhirifu wengine hakuna hatua zozote wanazochukuliwa mwishowe wanatujibu kwa kiburi. Wananchi kwenye shida zetu tukilalamika wanajua hakuna wakuwafanya kitu. Pesa ya Serikali haina mwenyewe

MDAU #JFSPACES: Uzuri ni kwamba kwa CCM ni kulindana na kuhamishwa Wizara. Ndio uwajibishwaji wa Serikali, hakuna lingine

AIDAN EYAKUZE, Mkurugenzi Mtendaji, Twaweza East Africa
AIDAN EYAKUZE (Mkurugenzi Mtendaji, Twaweza East Africa): Sisi Wananchi tuna wajibu wa kufuatilia Ubadhirifu unaotokea pale tunapokuwa karibu na maeneo husika, mfano Serikali za Mtaa tunaweza kuwa tunaona kinachoendelea lakini hatuchukui hatua Tunaacha majukumu hayo kwa Serikali ichukue hatua, tusijifanye wanyonge, sauti ya Wananchi ni kubwa, inaposikika inakuwa rahisi

Taifa au Nchi inamilikiwa na Wananchi, hivyo kwa kuwa wanatutumikia sisi ndio maana lazima tuwakague kuona matumizi yao yamelengwa kile tunachokitaka sisi, ndio maana CAG anakuwepo kukagua

CAG anaporidhia kuwa matumizi ya Fedha yapo vizuri anatoa hati safi na kama ikiwa kinyume na anatoa hati chafu Aidha, CAG hana Mamlaka ya kisheria kukamata au kushtaki Mtu au Taasisi kwa kuwa kuna vyombo vingine vyenye majukumu hayo kama DPP na TAKUKURU Ninavyoelewa CAG anapowasilisha mapungufu kupitia ripoti zake ni jukumu la vyombo vingine kuchukua nafasi kuanzia hapo

PETER KAZUNGU
Ukiangalia ripoti ya CAG ni kama vile Nchi imepigwa ganzi, vitu vinaenda tu na hakuna hatua zinazochukuliwa Kuna Walimu ambao wana levo ya Shahada maslahi yao ni duni tofauti na Wanasiasa ambao wanalipwa fedha nyingi, unadhani huyo mtu kama Mwalimu anaweza kuwa na nguvu ya kumhoji mtu anayelipwa mamlioni ya shilingi!

Tupo katika Nchi ambayo Wanasiasa wanadharau taaluma kama Walimu au Madaktari, wanafanya hivyo kwa kuwa wanawazidi kipato watumishi wengi wa ngazi ya chini Watanzania tumeumia kiasi kwamba hatujui cha kufanya, mambo yanaendelea kwa kuwa ni kama tumepigwa ganzi

TOXICBOE
Nimeona ACT Wazalendo wamechukua hatua ya kulaani kilichoandikwa katika Ripoti ya CAG ambao nao walizuiliwa. Ninachoona Bunge linatakiwa kuwa na nguvu kweli ya kuichukulia hatua Serikali Sioni kama Wananchi hata tukisema tuandamane kama tutakuwa na nguvu hiyo, zaidi tutazuiwa na Mamlaka

wa nafasi ilivyo sasa Wananchi wengi wa Tanzania ni kama hawajali kinachoendelea kuhusu Ripoti ya CAG Watu wengi wapo bize kufuatilia mambo mengine kama Michezo na Siasa

RENATHA ANDREAS
Watanzania wengi hatuna ufahamu wa kinachoendelea, pia hatuna mifumo inayoweza kuwawajibisha viongozi, ili ikitokea umetumia vibaya fedha za umma basi utawajibishwa

Tunakoelekea tutakuwa hatuna hata muda wa Mijadala kuhusu masuala kama haya, kizazi kinachohoji kinaweza kuondoka kwa kuwa hakutakuwa na hatua zinazochukuliwa Tutabaki na vijana au kizazi ambacho kinafuatilia mambo ya burudani kama mpira n.k ndio maana inafika hatua naona kuna umuhimu wa kuwa na Katiba mpya

Elimu ya uwajibikaji inatakiwa kutolewa, watu wanatakiwa kuwa na uwezo wa kuhoji na siyo kuacha vitu vinaenda kama ilivyo sasa Inatakiwa Watu wawe wanaziogopa Fedha za umma na si kushindana kuzitafuna kama ilivyo sasa

JAPHET LEMA
CAG anapotoa ripoti yake si kwamba anapita katika ofisi zote bali anachukua baadhi Hivyo inapotokea mwaka huu kuna kazi haijamalizika, anaweza kutorudi katika ofisi ileile na maana yake ni kuwa jambo hilo litakuwa limeisha juujuu

Hatuna uwazi kuhusu masuala ya Fedha za Umma na kuna changamoto kubwa kuhusu Mifumo ya Uwajibikaji katika Taasisi zetu za Umma ni nadra kusikia baada ya CAG kupita kama kuna Watu wameshikana mashati kuulizana nini kimetokea, hatuwezi kuhojiana

Mara zote Ripoti ya CAG inapowasilishwa inaambatana na Ripoti ya TAKUKURU ambayo haipati nafasi kubwa ya kuchambuliwa katika jamii Hata kwenye Bunge licha ya kujadili ripoti huwa hatusikii kama kuna vitu vimefanyika kuchukua hatua badala yake tunasikia tu imejadili na imepita hivyohivyo

Katika ubadhirifu wote mkubwa unaosikia kutoka kwa CAG lakini Taasisi kama PPRA ipo na hakuna ambacho inafanya, Taasisi kama TAKUKURU wanafanya nini kutokana na kinachoripotiwa na CAG Kuna haja ya kuchunguza Taasisi zilizoundwa kuchunguza na kuziba njia za Ubadhirifu wa Fedha, tuone kama zinafanya kazi inayotakiwa

Sheria zetu hazimpi nguvu Mwananchi wa kawaida kuchukua hatua dhidi ya Kiongozi au Viongozi ambao wanatajwa kwa Ubadhirifu kwenye Ripoti ya CAG Kitu kingine hali ya Rushwa Tanzania imetajwa kuwa kubwa, tulimsikia hata Rais akizungumzia manunuzi ya Ndege jinsi malipo yalivyokuja makubwa mara mbili ya uhalisia

LUDOVICK UTOUH (Mkurugenzi Mtendaji Wajibu Institute)
Uwazi wa Ripoti ya CAG hautoshelezi ingawa upo, tumeona Serikali inachukua hatua Mfano Mwaka 2022, Manispaa ya Arusha ilituhumiwa katika Ripoti ya CAG na Waziri Mkuu akachukua hatua hadharani

Sisi Wajibu tungependa kuona hatua zaidi zinachukuliwa Wapo wanaodai hatua hazichukuliwi, si kweli. Mfano Mwaka 2023 baada ya ripoti kutoka tumeona Rais anaagiza waliotajwa kwenye Ripoti ya CAG wachukuliwe hatua

Sheria inamtaka CAG akikutana na muamala wenye dalili za Rushwa, anatakiwa kuwasilisha mara moja kwa Mamlaka husika Hana ulazima wa kusubiri hadi wakati wa kuwasilisha ripoti yake

CAG akishawasilisha alichokiona kwa DPP au TAKUKURU hana Mamlaka ya kuwaelekeza nini cha kufanya Mara nyingi waliotajwa kwenye ripoti ya CAG wamekuwa wakichukuliwa hatua hata kama hawajapelekwa Mahakamani, baadhi wamekuwa wakishushwa vyeo na wengine kuhamishwa vitengo Si rahisi Mtu yuleyule kurudia kufanya kitu kilekile na kurejea katika ripoti kadhaa bila kuchukuliwa hatua

Tunaopigia kelele kuhusu Uwajibikaji tunatakiwa kujipongeza kwa kuwa tunaona kilichotokea kwenye Ripoti ya CAG na tunasisitiza Mamlaka kuwajibika

Vyombo vya Utawala vinapeana taarifa na vinatakiwa kufanya kazi yao ipasavyo kwa mujibu wa Sheria kuhusu Ripoti ya CAG Hatutakiwi kuingia Mitaani kwa kuwa kuna Utaratibu ambao lengo lake ni kuhakikisha atakayetuhumiwa Sheria ifuate mkondo na si kuchukua sheria mkononi

Wakala wa Ndege za Serikali ndio alinunua ndege na kukabidhi wa Air Tanzania, walianza kuwa na hasara kubwa ikawa inaenda inapungua Watanzania tuwe wadadisi, hali ya biashara ya ndege ina changamoto Duniani kote, mfano ni Kenya, SouthAfrica kote mashirika yao ya ndege yanachechemea Sisi tunatakiwa kuipongeza Air Tanzania kwa hatua iliyonayo, iendeleaa kubana matumizi na kujipanga zaidi licha ya kuwa inapata hasara

Siridhishwi na hatua za uwazi zinazochukuliwa dhidi ya wahusika wanaotajwa na kuhusishwa na wizi au upotevu wa mali za umma katika Ripoti ya CAG.

OMAR KIURE (Mkurugenzi Mtendaji Kiure Engineering LTD)
Sheria inaeleza kuwa miradi ya chini ya Tsh. Bilioni 10 inatakiwa kukabidhiwa kwa Mkandarasi mzawa lakini hilo halitekelezeki Tumekuwa tukiona matukio ya wakandarasi wengi wageni wakipewa hadi miradi ya Tsh. Milioni 300

Kuna umuhimu wa Ripoti ya TAKUKURU iwekwe wazi kama inavyowekwa ya #CAG ili tuweze kuona tulipofika na mwendelezo wetu katika mapambano dhidi ya Rushwa

Upigaji wa Mali za Umma, Rushwa na Wizi imekuwa ni kama fikra ya Kisasa lakini ni fikra potofu na ambazo zinaweza kutupeleka pabaya kama Nchi. Haiwezekani wawekezaji kuja wakati wanajua sifa yetu ni mbaya hata kama tuna mali watatuacha na hawatakuja

TITO MAGOTI
Baada ya Ripoti ya CAG tulitarajia kuwa na hatua ya Watu kujiuzulu, kuchukuliwa hatua lakini inawezekana huwa tunajisahau kuwa tuko wapi, ni kwa sababu mifumo yetu haina nafasi ya uwajibikaji huo

(Tanzania) tumepoteza utambulisho wetu, kama vile kuwa waadilifu, mfano mtu anapopewa majukumu ya kazi ya umma anatakiwa kuwa mwadilifu n.k Hatuna mwenendo mzuri kama Taifa jambo ambalo limesababisha tumekosa Uwajibikaji

Wanasiasa wanaweza kutumia nguvu na silaha yoyote kubomoa njia au nyenzo inayoweza kuhoji mambo yanayohitaji uwajibikaji Mfano Mjadala kama huu unaweza kushambuliwa kwa propaganda au kupandikiza Watu na njia nyingine zote ili tu wabaki na kile wanachoona kinawabeba wao
 
Huu ni mjadala muhimu sana, nausubiri kwa hamu nipate kufahamu hatua zinachokuliwa, na ikiwezekana tupate na mifano kabisa kuwa fulani alipata adhabu hii baada ya kutajwa kwenye ubadhilifu wa ripoti ya CAG mwaka fulani.

Tunalipa kodi, tozo halafu kuna watu wanafuja lazima tujue wanafanywa nini au watafanywa nini?
 
Nishafika hapo mjini Twitter, nasubiri mjadala huu kwa hamu kubwa sana
 
Ukurupukaji wa maamuzi jukwaani na kushangiliwa siyo sahihi kuna watu wanaumizwa kwa ajili watu kutafuta misifa. Sheria na taratibu zifuatwe. Maza yuko vizuri, kazi iendelee.
 
Hatua zinazochukuliwa ni nyepesi, na za kiuoga, zisizoelekezwa kutibu tatizo, bali ni kama kulipooza tu ndio maana haya madudu yamekuwa yakijirudia kila mwaka.

Tumeshazoea kuwa taifa la kupoteza pesa za walipakodi bila wahusika kuchukuliwa hatua zozote za maana na mamlaka kwasababu ya kulindana.
 
Nani wa kumfunga paka kengele?

Kama mwizi ndio mkamat wezi, Je unadhani wezi wenzie hawatamtaja mbele ya Hakim ambaye naye mwizi?
 
Inawezekana huu ubadhirifu ni chain, ukichukua hatua kwa aliyetajwa, utajikuta anayechukua hatua naye yupo, hata kama ni kwa mbali lakini mgao ulimfikia, inabidi tuwaze hivi maana sijawahi kusikia ripoti ya CAG isomwe hatua kali zikafuata.
 
Hakuna, na hata nikipewa mimi wadhifa na serikali nitaiba sanaaa
 
Usiulize, polisi waliwajibu ACT-Wazalendo kuwa tayari rais amekwisha chukua hatua dhidi ya waliotajwa.
 
Tarehe 29 Machi, 2023 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alipokea Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na TAKUKURU kwa mwaka 2021/2022. Ripoti hiyo imeibua ubadhirifu katika sekta mbalimbali za umma na kuibua mijadala miongoni mwa wananchi.

Je, ungependa kufahamu ni hatua gani huchukuliwa dhidi ya wabadhirifu baada ya kusomwa kwa Ripoti ya CAG? Unadhani hatua hizo zinatosha kumaliza ubadhirifu wa Mali za Umma?

Kwa haya na mengine mengi ungana nasi katika Mjadala Maalum na Wadau leo Alhamisi, Aprili 20, 2023, kuanzia Saa 11 jioni hadi saa 2 usiku kupitia Twitter Spaces.

Mjadala umeanza. Karibuni!

MDAU #JFSPACES:
Huu ubadhirifu haujaanza leo, ni Miaka sasa. Mijadala imekuwa hii hii, hazichukuliwi hatua za kukomesha, kiufupi wanaoiba walishaona hakuna wa kuwafanya kitu maana huu wizi ni wa kimfumo haibi mtu mmoja ni 'chain' ya vigogo, sasa hawachukui hatua maana wataumbuana. Kiufupi nchi inaliwa.

MDAU #JFSPACES: Kwa upande wangu lawama zangu zote nazielekeza kwa TAKUKURU, wao ndo walaumiwe kwa sababu CAG akitoa ripoti yake wao ndio ingetakuwa wawe wa kwanza kuwakamata wahusika wa kashfa hizo na kuwapeleka mahakamani, na kama hawana uwezo huo wa kisheria ningeomba Bunge litunge Sheria ya kuwawezesha kufanya hivyo

MDAU #JFSPACES: Wabadhirifu watachukuliwa hatua? Kwanza walitakiwa waone aibu wenyewe kisha wajiuzulu, halafu Serikali iwapeleke Mahakamani. Watu wenyewe hata aibu hawana na wametia hasara nchi

MDAU #JFSPACES: Wabadhirifu Washitakiwe na kuhukumiwa kifungo zaidi ya Miaka 30, wafilisiwe Mali na account zao kufungwa na fedha zote zirejeshwe Serikalini. Wavuliwe Vyeo na nyadhifa zao, wanyang'anywe hati za kusafiria

MDAU #JFSPACES: Uwazi na sio uwazi tu, wabadhirifu wengine hakuna hatua zozote wanazochukuliwa mwishowe wanatujibu kwa kiburi. Wananchi kwenye shida zetu tukilalamika wanajua hakuna wakuwafanya kitu. Pesa ya Serikali haina mwenyewe

MDAU #JFSPACES: Uzuri ni kwamba kwa CCM ni kulindana na kuhamishwa Wizara. Ndio uwajibishwaji wa Serikali, hakuna lingine

AIDAN EYAKUZE, Mkurugenzi Mtendaji, Twaweza East Africa
AIDAN EYAKUZE (Mkurugenzi Mtendaji, Twaweza East Africa): Sisi Wananchi tuna wajibu wa kufuatilia Ubadhirifu unaotokea pale tunapokuwa karibu na maeneo husika, mfano Serikali za Mtaa tunaweza kuwa tunaona kinachoendelea lakini hatuchukui hatua Tunaacha majukumu hayo kwa Serikali ichukue hatua, tusijifanye wanyonge, sauti ya Wananchi ni kubwa, inaposikika inakuwa rahisi

Taifa au Nchi inamilikiwa na Wananchi, hivyo kwa kuwa wanatutumikia sisi ndio maana lazima tuwakague kuona matumizi yao yamelengwa kile tunachokitaka sisi, ndio maana CAG anakuwepo kukagua

CAG anaporidhia kuwa matumizi ya Fedha yapo vizuri anatoa hati safi na kama ikiwa kinyume na anatoa hati chafu Aidha, CAG hana Mamlaka ya kisheria kukamata au kushtaki Mtu au Taasisi kwa kuwa kuna vyombo vingine vyenye majukumu hayo kama DPP na TAKUKURU Ninavyoelewa CAG anapowasilisha mapungufu kupitia ripoti zake ni jukumu la vyombo vingine kuchukua nafasi kuanzia hapo

PETER KAZUNGU
Ukiangalia ripoti ya CAG ni kama vile Nchi imepigwa ganzi, vitu vinaenda tu na hakuna hatua zinazochukuliwa Kuna Walimu ambao wana levo ya Shahada maslahi yao ni duni tofauti na Wanasiasa ambao wanalipwa fedha nyingi, unadhani huyo mtu kama Mwalimu anaweza kuwa na nguvu ya kumhoji mtu anayelipwa mamlioni ya shilingi!

Tupo katika Nchi ambayo Wanasiasa wanadharau taaluma kama Walimu au Madaktari, wanafanya hivyo kwa kuwa wanawazidi kipato watumishi wengi wa ngazi ya chini Watanzania tumeumia kiasi kwamba hatujui cha kufanya, mambo yanaendelea kwa kuwa ni kama tumepigwa ganzi

TOXICBOE
Nimeona ACT Wazalendo wamechukua hatua ya kulaani kilichoandikwa katika Ripoti ya CAG ambao nao walizuiliwa. Ninachoona Bunge linatakiwa kuwa na nguvu kweli ya kuichukulia hatua Serikali Sioni kama Wananchi hata tukisema tuandamane kama tutakuwa na nguvu hiyo, zaidi tutazuiwa na Mamlaka

wa nafasi ilivyo sasa Wananchi wengi wa Tanzania ni kama hawajali kinachoendelea kuhusu Ripoti ya CAG Watu wengi wapo bize kufuatilia mambo mengine kama Michezo na Siasa

RENATHA ANDREAS
Watanzania wengi hatuna ufahamu wa kinachoendelea, pia hatuna mifumo inayoweza kuwawajibisha viongozi, ili ikitokea umetumia vibaya fedha za umma basi utawajibishwa

Tunakoelekea tutakuwa hatuna hata muda wa Mijadala kuhusu masuala kama haya, kizazi kinachohoji kinaweza kuondoka kwa kuwa hakutakuwa na hatua zinazochukuliwa Tutabaki na vijana au kizazi ambacho kinafuatilia mambo ya burudani kama mpira n.k ndio maana inafika hatua naona kuna umuhimu wa kuwa na Katiba mpya

Elimu ya uwajibikaji inatakiwa kutolewa, watu wanatakiwa kuwa na uwezo wa kuhoji na siyo kuacha vitu vinaenda kama ilivyo sasa Inatakiwa Watu wawe wanaziogopa Fedha za umma na si kushindana kuzitafuna kama ilivyo sasa

JAPHET LEMA
CAG anapotoa ripoti yake si kwamba anapita katika ofisi zote bali anachukua baadhi Hivyo inapotokea mwaka huu kuna kazi haijamalizika, anaweza kutorudi katika ofisi ileile na maana yake ni kuwa jambo hilo litakuwa limeisha juujuu

Hatuna uwazi kuhusu masuala ya Fedha za Umma na kuna changamoto kubwa kuhusu Mifumo ya Uwajibikaji katika Taasisi zetu za Umma ni nadra kusikia baada ya CAG kupita kama kuna Watu wameshikana mashati kuulizana nini kimetokea, hatuwezi kuhojiana

Mara zote Ripoti ya CAG inapowasilishwa inaambatana na Ripoti ya TAKUKURU ambayo haipati nafasi kubwa ya kuchambuliwa katika jamii Hata kwenye Bunge licha ya kujadili ripoti huwa hatusikii kama kuna vitu vimefanyika kuchukua hatua badala yake tunasikia tu imejadili na imepita hivyohivyo

Katika ubadhirifu wote mkubwa unaosikia kutoka kwa CAG lakini Taasisi kama PPRA ipo na hakuna ambacho inafanya, Taasisi kama TAKUKURU wanafanya nini kutokana na kinachoripotiwa na CAG Kuna haja ya kuchunguza Taasisi zilizoundwa kuchunguza na kuziba njia za Ubadhirifu wa Fedha, tuone kama zinafanya kazi inayotakiwa

Sheria zetu hazimpi nguvu Mwananchi wa kawaida kuchukua hatua dhidi ya Kiongozi au Viongozi ambao wanatajwa kwa Ubadhirifu kwenye Ripoti ya CAG Kitu kingine hali ya Rushwa Tanzania imetajwa kuwa kubwa, tulimsikia hata Rais akizungumzia manunuzi ya Ndege jinsi malipo yalivyokuja makubwa mara mbili ya uhalisia

LUDOVICK UTOUH (Mkurugenzi Mtendaji Wajibu Institute)
Uwazi wa Ripoti ya CAG hautoshelezi ingawa upo, tumeona Serikali inachukua hatua Mfano Mwaka 2022, Manispaa ya Arusha ilituhumiwa katika Ripoti ya CAG na Waziri Mkuu akachukua hatua hadharani

Sisi Wajibu tungependa kuona hatua zaidi zinachukuliwa Wapo wanaodai hatua hazichukuliwi, si kweli. Mfano Mwaka 2023 baada ya ripoti kutoka tumeona Rais anaagiza waliotajwa kwenye Ripoti ya CAG wachukuliwe hatua

Sheria inamtaka CAG akikutana na muamala wenye dalili za Rushwa, anatakiwa kuwasilisha mara moja kwa Mamlaka husika Hana ulazima wa kusubiri hadi wakati wa kuwasilisha ripoti yake

CAG akishawasilisha alichokiona kwa DPP au TAKUKURU hana Mamlaka ya kuwaelekeza nini cha kufanya Mara nyingi waliotajwa kwenye ripoti ya CAG wamekuwa wakichukuliwa hatua hata kama hawajapelekwa Mahakamani, baadhi wamekuwa wakishushwa vyeo na wengine kuhamishwa vitengo Si rahisi Mtu yuleyule kurudia kufanya kitu kilekile na kurejea katika ripoti kadhaa bila kuchukuliwa hatua

Tunaopigia kelele kuhusu Uwajibikaji tunatakiwa kujipongeza kwa kuwa tunaona kilichotokea kwenye Ripoti ya CAG na tunasisitiza Mamlaka kuwajibika

Vyombo vya Utawala vinapeana taarifa na vinatakiwa kufanya kazi yao ipasavyo kwa mujibu wa Sheria kuhusu Ripoti ya CAG Hatutakiwi kuingia Mitaani kwa kuwa kuna Utaratibu ambao lengo lake ni kuhakikisha atakayetuhumiwa Sheria ifuate mkondo na si kuchukua sheria mkononi

Wakala wa Ndege za Serikali ndio alinunua ndege na kukabidhi wa Air Tanzania, walianza kuwa na hasara kubwa ikawa inaenda inapungua Watanzania tuwe wadadisi, hali ya biashara ya ndege ina changamoto Duniani kote, mfano ni Kenya, SouthAfrica kote mashirika yao ya ndege yanachechemea Sisi tunatakiwa kuipongeza Air Tanzania kwa hatua iliyonayo, iendeleaa kubana matumizi na kujipanga zaidi licha ya kuwa inapata hasara

Siridhishwi na hatua za uwazi zinazochukuliwa dhidi ya wahusika wanaotajwa na kuhusishwa na wizi au upotevu wa mali za umma katika Ripoti ya CAG.

OMAR KIURE (Mkurugenzi Mtendaji Kiure Engineering LTD)
Sheria inaeleza kuwa miradi ya chini ya Tsh. Bilioni 10 inatakiwa kukabidhiwa kwa Mkandarasi mzawa lakini hilo halitekelezeki Tumekuwa tukiona matukio ya wakandarasi wengi wageni wakipewa hadi miradi ya Tsh. Milioni 300

LUDOVICK UTOUH (Mkurugenzi Mtendaji Wajibu Institute)
Kuna umuhimu wa Ripoti ya TAKUKURU iwekwe wazi kama inavyowekwa ya #CAG ili tuweze kuona tulipofika na mwendelezo wetu katika mapambano dhidi ya Rushwa

Upigaji wa Mali za Umma, Rushwa na Wizi imekuwa ni kama fikra ya Kisasa lakini ni fikra potofu na ambazo zinaweza kutupeleka pabaya kama Nchi. Haiwezekani wawekezaji kuja wakati wanajua sifa yetu ni mbaya hata kama tuna mali watatuacha na hawatakuja

TITO MAGOTI
Baada ya Ripoti ya CAG tulitarajia kuwa na hatua ya Watu kujiuzulu, kuchukuliwa hatua lakini inawezekana huwa tunajisahau kuwa tuko wapi, ni kwa sababu mifumo yetu haina nafasi ya uwajibikaji huo

(Tanzania) tumepoteza utambulisho wetu, kama vile kuwa waadilifu, mfano mtu anapopewa majukumu ya kazi ya umma anatakiwa kuwa mwadilifu n.k Hatuna mwenendo mzuri kama Taifa jambo ambalo limesababisha tumekosa Uwajibikaji

Wanasiasa wanaweza kutumia nguvu na silaha yoyote kubomoa njia au nyenzo inayoweza kuhoji mambo yanayohitaji uwajibikaji Mfano Mjadala kama huu unaweza kushambuliwa kwa propaganda au kupandikiza Watu na njia nyingine zote ili tu wabaki na kile wanachoona kinawabeba wao
HAKUNA WAKUCHUKULIWA HATUA WABADHILIFU WOTE NI MAKADA WA CCM
 
Back
Top Bottom